Thursday, August 31, 2017

31 August 2017, Tetesi za soka Ulaya michezoni leo Alhamisi

Arsenal wanafanya jaribio la dakika za mwisho kumsajili mshambuliaji wa Paris St-Germain Julian Draxler, 23, na wakimkosa watazuia uhamisho wa Alexis Sanchez, 28, kwenda Manchester City. (Daily Mirror)

Manchester City watapanda dau la pauni milioni 70 taslimu kutaka kumsajili mshambuliaji wa Arsenal Alexis Sanchez, 28, na tayari wamepeleka kikosi chake cha wansheria na madaktari nchini Chile kwa ajili ya kukamilisha usajili huo. (Independent)

Matumaini ya Manchester City ya kumsajili beki wa West Brom Jonny Evans, 29, bado ni ati ati, kwa sababu Eliaquim Mangala, 26, ambaye angehusika katika mkataba huo hataki kwenda West Brom.

Arsenal na Leicester walipanda dau la pauni milioni 25 kumtaka beki huyo, lakini maombi yao yalikataliwa. (Daily Telegraph)

Crystal palace wana matumaini ya kumsajili Eliaquim Mangala kutoka City kwa pauni milioni 23. (Sun)

Swansea wanakaribia kumsajili kiungo wa Bayern Munich Renato Sanches kwa mkopo. (Guardian)

West Ham wanapanga kumchukua Jack Wilshere, 25, kwa mkopo kutoka Arsenal. (Sun)

Baada ya kukosa mtu wa kumsaidia Victor Moses, Chelsea wanafikiria kumsajili Bacary Sagna. (Daily Star)

Mshambuliaji wa Chelsea Diego Costa, 28, anakaribia kujiunga tena na Atletico Madrid ambao wametoa dau jipya la pauni milioni 49 ambazo Chelsea wanafikiria kuzipokea. (Sun)

Chelsea bado wapo kwenye mazungumzo na Everton ya kumsajili kiungo mshambuliaji Ross Barkley, 23, huku muda ukizidi kutaradad wa kusajili wachezaji watatu wapya ambao Antonio Conte aliwataka. (Daily Telegraph)

Tottenham pia wanafikiria kumsajili Ross Barkley. (Evening Standard)

Tottenham wanaongoza katika mbio za kutaka kumsajili winga wa Leicester City Demarai Gray kabla ya dirisha la usajili kufungwa leo. (Daily Mirror)

Tottenham wanajiandaa kukamilisha usajili wa beki wa kulia wa PSG Serge Aurier, 24, kwa pauni milioni 23 baada ya wizara ya mambo ya ndani ya Uingereza kumpa kibali cha kufanya kazi. (Guardian)

Barcelona, Chelsea na Tottenham zinamnyatia winga wa Leicester City Riyad Mahrez, 26. (L'Equipe)

Chelsea wapo kwenye mazungumzo ya kina na Swansea ya kumsajili mshambuliaji Fernando Llorente, 32. (ESPN)

Everton wanafikiria kumsajili mshambuliaji wa Chelsea Mitchy Batshuayi. (FootMercato)

Liverpool wanaendeleza juhudi zao za kumsajili kiungo wa Monaco Thomas Lemar, 21, na wamepanda dau la pauni milioni 74. (Independent)

Liverpool tayari wameandaa madaktari kusafiri kwenda Paris kwa ajili ya vipimo vya afya vya Thomas Lemar, wa Monaco, iwapo makubaliano yatafikiwa baina ya timu hizo mbili. (Liverpool Echo)

Liverpool pia wapo tayari kutoa pauni milioni 75 kumsajili beki wa kati wa Southampton Virgil van Dijk, 26, ingawa Southampton wamesema hawataki kumuuza. (Times)

Meneja wa Newcastle anataka kumsajili mshambuliaji wa Liverpool Divock Origi, kuziba nafasi ya Dwight Gayle ambaye anataka kuondoka. (Express)

Fulham wamepanda dau la pauni milioni 15 kumtaka mshambuliaji wa Newcastle Dwight Gayle, 27, lakini Newcastle wanataka pauni milioni 18-20. (Daily Mail)

Newcastle wanatarajiwa kuwa na pilikapilika nyingi leo kabla ya dirisha la usajili kufungwa huku wakitaka kumsajili kwa mkopo winga wa Chelsea Kenedy, 21. (Evening Chronicle)

Tottenham na West Ham wapo tayari kupambana kumsajili kiungo wa Barcelona Andre Gomes, 24. (Daily Mirror)

31 August 2017, Bushiri awaniwa na Mwembeladu Fc

Mwadui FC imeachana na Bushiri mwishoni mwa msimu uliopita taarifa hiyo imekuwa habari njema kwa Mwembeladu inayosaka huduma ya kocha huyo kwa muda mrefu.

Ofisa Habari wa Mwembeladu, Said Mussa alisema uongozi wa timu hiyo tayari umeshafanya mazungumzo ya awali na kocha huyo.

Mussa alisema lengo la kumsaka kocha huyo ni kuona timu yao msimu huu inafanya vizuri kwa kupanda daraja.

“Dhamira yetu ni kuona tunafanya vema katika ligi yetu msimu huu, ndio maana tunakosa usingizi kwa kumsaka Kocha Bushiri kila kona ili wachezaji wetu wapate mafunzo mazuri kutoka kwake,” alisema Mussa.

Kocha Bushiri alisema ni kweli amefanya mazungumzo na uongozi wa timu hiyo na anajipanga kufanya kazi na uongozi wa timu hiyo kwa mujibu wa makubaliano yao.

Alisema ataenda kuisaidia timu hiyo kwa vile mipango yake ni kufundisha soka Tanzania bara, lakini kutokana na mipango yake yakwenda huko haijakaa vizuri ameamua kutumia muda wake aliopo hapa kuwasaidia vijana wa timu ya Mwembeladu waliokuwa na hamu ya kufundishwa na yeye.

Admit Mwanasport

31 August 2017, Watu 6 wafariki katika machimbo haramu ya madini Kusini-Mashariki mwa DR Congo

Watu 6 wamefariki katika maporomoko ya ardhi yaliotokea katika machimbo haramu ya madini Kolwezi Kusini-Mashariki mwa Jamhuri ya kidemokrais ya Congo

Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa na vyanzo vya habari  Kolezwi ni kwamba watu 6 wamefariki katika maporomoko ya ardhi ya machimbo ya madini Kolwezi, mgodi wa madini unaopatikana Kusini-Mashariki mwa Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo.

Ajali hiyo imeripotiwa kutokea Jumanne wakati ambapo wachimbaji hao haramu walikuwa wakiendesha shughuli yao nya uchimbaji madini bila ya vibali.

Taarifa hiyo iliotolewa na gavana wa jimbo la Lualaba.

31 August 2017,Makao makuu ya chama cha upinzani yachomwa moto Sierra Leone

Makao Makuu ya chama cha upinzani cha Alliance Democratic Party (ADP ) yamechomwa moto mjini Freetown nchini Sierra Leone.

Kwa mujibu wa habari,wazima moto walifika kujaribu kusaidia kuuzima moto ulioanzia ghorofa ya juu kabisa ya jengo hilo.

Kiongozi wa upinzani Mohamed Kamaremba Mansaray amekiambia kituo cha habari cha Anadolu kuwa anashuku huo moto umeanzishwa na chama tawala APC.

Bwana Kamaremba amesema kuwa bomu lenye petroli lilirushwa ndani ya ofisi yake majira ya asubuhi na kusababisha vitu vya thamani ikiwemo makaratasi muhimu kuungua.

Bwana Kamaremba amesema anaamini ni chama tawala ndio kinahusika kwani waliwahi kumchomea ofisi yake miaka ya nyuma na hakuna hatua yoyote ya kisheria iliyochukuliwa.

Kiongozi huyo wa upinzani amesema kuwa chama tawala kimefanya hivyo kutokana na yeye kupinga na kukosoa siasa zao kila mara.

Hata hivyo chama tawala kimeyakanusha mashtaka hayo na kuitaka polisi kufanya uchunguzi zaidi.

31 August 2017,Sakata la Manji imebainika anavyuma kwenye moyo

Daktari katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) iliyopo jijini Dar es salaam ameieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu namna walivyouchunguza moyo wa mfanyabiashara Yusuf Manji.

Mkurugenzi Mtendaji wa JKCI, Profesa Mohammed Janabi (51) ametoa ushahidi wa upande wa utetezi katika kesi ya kutumia dawa za kulevya inayomkabili Manji.

Profesa Janabi ameieleza Mahakama jinsi walivyoangalia vyuma vilivyopo kwenye moyo wa Manji kama vimeziba au la.

Akiwa shahidi wa kwanza wa upande wa utetezi, Profesa Janabi aliongozwa na wakili Hajra Mungula kutoa ushahidi mbele ya Hakimu Mfawidhi, Cyprian Mkeha.

Manji ambaye katika hati ya mashtaka jina lake ni Yusufali Manji, alifikishwa mahakamani hapo kwa mara ya kwanza Februari 16 akidaiwa kati ya Februari 6 na 9 katika eneo la Sea View, Upanga wilayani Ilala alitumia dawa za kulevya aina ya Heroin .

Admit Mwananchi

Wednesday, August 30, 2017

30 August 2017, Tetesi za soka Ulaya michezoni leo jumatano

Tottenham wanakaribia kukamilisha usajili wa beki wa kimataifa wa Argentina Juan Foyth, 19, kutoka Estudiantes kwa pauni milioni 8 na pia bado wanajaribu kumsajili beki wa PSG Serge Aurier, 24, kwa pauni milioni 23. (Guardian)

Liverpool wamekubali kumuuza kiungo Philippe Coutinho, 25, kwenda Barcelona kwa pauni milioni 148. (Yahoo Sports)

Jose Mourinho anataka kumsajili winga wa Leicester City Riyad Mahrez. (SFR Sport)

Arsenal huenda wakashawishiwa kumuuza Alexis Sanchez, 28, iwapo watapata dau la kuvutia. (BBC Radio 5 live)

Arsenal wamekataa dau la pauni milioni 30 kutoka Liverpool la kumtaka Alex Oxlade-Chamberlain, ambaye pia amekataa kwenda Chelsea kwa pauni milioni 40. (Evening Standard)

Raheem Sterling atabakia Manchester City na hatokuwa sehemu ya mkataba wa City kumsajili Alexis Sanchez kutoka Arsenal. (Sky)

Sergio Aguero huenda akataka kuondoka Manchester City mwezi Januari iwapo Pep Guardiola ataendelea kutomtumia. (Manchester Evening News)

Inter Milan wamepanda dau jipya kumtaka beki wa kati wa Arsenal Shkodran Mustafi, 25. (Sky Sports)

Tottenham wanafikiria kutopanda dau la kutaka kumsajili kiungo wa Everton Ross Barkley, 23, kwa sababu ni majeruhi kwa sasa. (London Evening Standard)

Arsenal wamepanda dau la kutaka kumsajili winga wa Real Madrid Lucas Vazquez. (Diario Gol)

Mshambuliaji wa Chelsea Diego Costa huenda akashangaza wengi na kujiunga na Las Palmas kwa mkopo huku akisubiri kujiunga na Atletico Madrid. (Sun)

Dau la pauni milioni 25 la Chelsea kumtaka Ross Barkley limekataliwa na Everton. (BBC)

Beki wa kati wa West Brom Jonny Evans, 29, atakataa kujiunga na Arsenal na badala yake anataka kwenda Manchester City. (Daily Mail)

West Brom wanatarajia kumsajili beki wa kati Grzegorz Krychowiak, 27, kutoka Paris Saint-Germain. (Sun)

West Brom pia wanatarajia kukamilisha usajili wa beki wa Arsenal Kieran Gibbs, 27, katika saa 24 zijazo. (Daily Mirror)

Beki wa Southampton Virgil van Dijk, 26, bado ana matumaini ya kwenda Liverpool ingawa Arsenal na Chelsea huenda nazo zikapanda dau katika saa za mwisho kabla ya dirisha la usajili kufungwa. (Independent)

Crystal Palace watamuunga mkono meneja wake Frank de Boer kwa kusajili wachezaji watatu wapya. (Daily Star)

Stoke City wanataka kumsajili kiungo wa Manchester City Fabian Delph, 27, na wapo tayari kutoa pauni milioni 12, kwa mchezaji huyo aliyenunuliwa kwa pauni milioni 8 kutoka Aston Villa miaka miwili iliyopita. (Daily Telegraph)
Meneja wa Newcastle United Rafael Benitez yuko tayari kumuuza mshambuliaji wake Dwight Gayle, 26, kwa pauni milioni 18. (Guardian)
Napoli wanataka kumsajili kiungo wa Barcelona Denis Suarez, 23. (Corriere dello Sport)
Winga Adama Traore, 21, anataka kuondoka Middlesbrough kwenda Lille. (Gazette Live)
Divock Origi huenda akaondoka Liverpool na kwenda Tottenham, kwa mujibu wa baba yake. (Sky)

30 August 2017, Tambua umuhimu wa kutompiga mkeo

KABLA HUJANYANYUA MKONO NA KUMPIGA MKE WAKO BASI SOMA MAKALA HII

Niliamka usiku baada ya kusikia kelele za mtoto wangu mkubwa wa miaka tisa. “Baba! Baba! Baba Zack hayupo katoroka! Kaondoka na nguo!” Nilistuka kutoka usingizini na kutoka sebuleni, niligonga kila chumba kumtafuta lakini hakuepo.

Watu wote waliokuepo mule ndani waliamka, ndiyo kwanza tulikua tumemaliza wiki tangu kumzika mke wangu na Zack mwenye umri wa miaka mitano alikua anampenda sana Mama yake hivyo nilijua kuna kitu.

Tulianza kazi ya kutafuta, tukiita huku na kule lakini wapi, mke wangu alikua amezikwa Kijijini hivyo hata mambo ya Polisi kulikua hakuna. Tulitafuta usiku mzima na mpaka asubuhi hatukua tumempata, kila mtu alichanganyikiwa tukihisi labda amejiua au kutoroka kutokana na kifo cha ghafla cha Mama yake.

Asubuhi tukiwaza nini cha kufanya, alikuja mtoto mmoja wa pale Kijijini na kutuambia kua maeona mtoto Kalala makaburini.

Tulikimbia ambapo hakukua mbali sana sema migombani tuliangalia kumkuta Zack katandika nguo chini kalala.

juu ya kaburi lake kalala.
Kila mtu alistuka, tulimsuta, alionekana kuchoka sana na njaa na aliponiona tu alianza kulia huku akishikilia msalaba wa kaburi la Mama yake akisema hawezi kuondoka na kumuacha Mama yake peke yake.

Tulijaribu kumbembeleza lakini wapi, hakutaka kuondoka na hatukutaka kumlazimishia.
Mtoto wangu mkubwa alienda na kukaa pembeni yake, akimuambia kuwa waondoke wamuache Mama apumzike.

Zack alimuuliza “Dada wewe humpendi tena Mama?” alimjibu nampenda na Zack alimuuliza tena, “Sasa kama unampenda mbona unamuacha huku porini peke yake..”

Watu wote walisikitika na mimi machozi yalianza kunitoka, kabla hajajibiwa alisema maneno ambayo yalinifanya nigande kwa mstuko na kushikwa na kigugumizi. “Mimi siwezi kuondoka Dada, tukimuacha Mama peke yake huku porini Baba atakuja usiku na kumpiga atamuumiza kama anavyofanyaga nyumbani.

Baba anatupenda sisi lakini hampendi Mama hivyo anampiga kila siku tukimuacha Mama mwenyewe, sasa tukimuacha huku porini si atakuja kumuua Mama na watu hawatajua, mimi sitaki Mama afe Dada nakaa nae hapahapa mpaka aamke huko chini walikomlaza ili Baba sijempiga..”
Niliumizwa na kifo cha Mke wangu lakini maneno ya mwanangu yalinifanya nijione kama shetani.

Nilianza kukumbuka namna ambavyo Zack kila siku alikua akimganda Mama yake, alikua akitaka kulala na sisi, alikua akitaka kuongozana hata kazini na Mama yake.

Sikujua sababu ya kufanya hivyo, kwani kweli nilikua namnyanyasa na kumtesa mke wangu lakini si mbele za watoto.

Mbele za watoto nilikua Baba bora na sikujua kama wanaona, nilijikuta napiga magoti kuombamsamaha lakini hakutaka kuondoka mpaka Babu mmoja alipokuja na kumuambia tutaleta Polisi wa kumlinda Mama yako.

Wewe bado mdogo, kuna hawa vijana ni Polisi watakaa na mapanga hapa watamlinda Mama yako na Baba yako hatampiga tena. Hapo ndipo alikubali kuondoka.

MOYO WANGU UNAFADHAIKA SANA KWANI MWANANGU HANIAMINI KABISA....Tafadhali SHARE hii ili wababa wajifunze kutowapiga wake zao.

Admit Uhondo planet

30 August 2017, Muuguzi afungwa kifungo cha maisha kwa kosa la kuwaua wagonjwa sita

Muuguzi nchini Ujerumani anayetumikia kifungo cha maisha kwa kuwaua wagonjwa sita, imebainika aliwaua wengine 84.

Idadi ya watu aliowaua imemwingiza katika rekodi ya mwanamke aliyefanya mauaji mengi kuliko wote nchini humo.

Mwanamke huyo, Niels Hoegel (40), alifungwa mwaka 2015 baada ya kupatikana na hatia ya kuwaua wagonjwa sita kwa kuwachoma sindano inayosababisha moyo kusimama ghafla.

Mamlaka za nchi hiyo zimekuwa zikifanya uchunguzi wa maelfu ya vifo, ikiwamo kufukua maiti za wagonjwa waliokufa chini ya uangalizi wake katika hospitali binafsi za Delmenhorst na Oldenburg ambazo amewahi kufanya kazi.

Polisi nchini humo wameliambia Shirika la CNN kuwa, wanaamini Hoegel aliua wagonjwa 36 katika Hospitali ya Oldenburg kati ya mwaka 1999 na 2001, na wengine 48 katika Hospitali ya Delmenhorst.

Pia, wanasema idadi ya watu aliowaua inaweza kuwa kubwa zaidi lakini ushahidi hautapatikana kwa kuwa miili mingi ilichomwa moto, hivyo si rahisi kugundua sababu ya kifo kwa kupima majivu.

Katika mwendelezo wa kesi zake, Hoegel amekiri kuwachoma sindano wagonjwa ili moyo ushindwe kufanya kazi naye ajaribu kuwafufua kwa kuuamsha.

Amesema alitamani kuona anamfufua mtu baada ya kumchoma sindano hiyo na kwamba, alifadhaika aliposhindwa kuwarudishia uhai.

Johann Kuehme, ofisa wa polisi katika Mji wa Oldenburg aliwaambia wanahabari jana Agosti 29 kuwa idadi hiyo ya vifo imewaduwaza.

"Mauaji huenda yasingekuwa makubwa kiasi hiki kama hospitali hizi zingechukua hatua kuchunguza vifo au kutoa taarifa kwa mamlaka kuhusu vifo hivyo ili vichunguzwe,” amesema.

Admit Mwananchi

30 August 2017, Mbunge wa Tunduma akamatwa na polisi

Mbunge wa Tunduma, Frank Mwakajoka amekamatwa na polisi akiwa katika viwanja vya Mahakama ya Wilaya ya Mbozi mjini Vwawa.

Mwakajoka amekamatwa jana Agosti 29 baada ya kufika mahakamani hapo kufuatilia kesi inayomkabili mbunge mwenzake wa Mbozi, Pascal Haonga.

Katibu wa Chadema Wilaya ya Mbozi, James Mbasha amesema mbunge huyo amekamatwa lakini hajui kosa linalomkabili.

Mbasha amesema alipata taarifa leo asubuhi kwamba mbunge huyo anatafutwa na polisi.

Katika kesi mahakamani hapo, Haonga na wenzake wawili Wilfred Mwalusanya na Mashaka Mwampashi wanakabiliwa na mashtaka mawili, kufanya vurugu na kuwazuia askari kufanya kazi yao kinyume cha sheria.

Mwendesha mashitaka wa polisi, Samwel Saro anadai jana Agosti 28 saa saba mchana, washtakiwa walimzuia askari kutimiza majukumu yake ya kumkamata Mwampashi aliyedaiwa kwamba si mjumbe halali katika uchaguzi wa mwenyekiti wa Mamlaka ya Mji Mdogo wa Mlowo.

Washtakiwa pia wanadaiwa kumfanyia vurugu msimamizi wa uchaguzi huo ambaye ni Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Mbozi, Lauteri Kanoni.

Washitakiwa walikana mashtaka mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi wa mahakama hiyo, Asha Waziri ambaye alisema dhamana iko wazi kwa kila mshtakiwa kuwa na wadhamini wawili wenye barua za utambulisho kutoka kwa watendaji wa maeneo yao watakaoweka bondi ya Sh2 milioni kila mmoja.

Washtakiwa walitimiza masharti na kuachiwa huru kwa dhamana. Kesi itatajwa Septemba 25 na washtakiwa watasomewa maelezo ya awali.

Tuesday, August 29, 2017

29 August 2017, Tetesi za soka Ulaya michezoni leo jumanne

Manchester United wamepewa matumaini na Real Madrid ya kumsajili Gareth Bale, 28. (Marca)

Manchester United watampa mkataba mpya beki wa kushoto Luke Shaw, 22, ili kuepuka asiondoke bure mwisho wa mkataba wake. (Sun)

Chelsea wanakaribia kumsajili kiungo wa Leicester City Danny Drinkwater, 27, kwa pauni milioni 40 pamoja na Alex Oxlade-Chamberlain, 24 kutoka Arsenal. (Express)

Chelsea wanakaribia kumuuza mshambuliaji wake Diego Costa, 28, kwenda Atletico Madrid kwa pauni milioni 30. (Mirror)

Liverpool bado wanamtaka beki Virgil van Dijk, 26. (Mail)

Liverpool wamethibitisha kufikia makubaliano ya kumsajili Naby Keita kutoka Red Bull Leipzig ifikapo Julai mosi 2018. (Sky Sports)

Liverpool wapo tayari kutumia pauni milioni 135 kuwasajili Virgil van Dijk na Thomas Lemar, baada ya kukamilisha usajili wa Naby Keita. (The Sun)

Mateo Kovacic ameonesha nia ya kutaka kujiunga na Liverpool na kuondoka Real Madrid. (Diario Gol)

Monaco wamekataa dau la pili kutoka Liverpool la kumtaka Thomas Lemar. (Sky Sports)

Swansea wanataka kumsajili kiungo wa Bayern Munich Renato Sanchez, 20. (Wales Online)

Manchester City wanapanga kupanda dau jingine kumtaka mshambuliaji wa Arsenal Alexis Sanchez, 28. (Goal)

Manchester City wanapanga kupanda dau jipya kumtaka beki wa kati wa West Brom Jonny Evans, 29, baada ya dau la pauni milioni 21 kutoka kwa Leicester kukataliwa. (Mirror)

Beki wa Manchester City Eliaquim Mangala, 26, huenda akajiunga na West Brom kama sehemu ya mkataba wa kumsajili Jonny Evans. (ESPN)

Meneja wa West Brom Tony Pulis anarejea Emirates na dau la pauni milioni 13 kumtaka beki Kieran Gibbs. (The Sun)

Tottenham huenda wakamkosa beki wa PSG Serge Aurier, 24, ambaye anataka kwenda Manchester United. (SFR Sport)

Sam Allardyce huenda akarejea Crystal Palace iwapo Frank de Boer atafukuzwa kazi. (Mirror)

Daktari wa timu ya taifa ya Brazil Michael Simoni amesema tatizo la mgongo la kiungo wa Liverpool Philippe Coutinho linasababishwa na msongo wa mawazo kuhusiana na hatma yake. (Sun)

Mkuu wa Juventus Beppe Marotta amesema klabu yake itapanda dau jipya kumtaka kiungo wa Liverpool Emre Can, 23, mwezi Januari. (Premium Sport)

Pepe Reina atabakia Napoli licha ya kupata nafasi ya kujiunga na Paris Saint-Germain. (AS)

Mkurugenzi wa Barcelona Robert Fernandez amesema klabu yake itasajili mchezaji mmoja au wawili zaidi kabla ya dirisha la usajili kufungwa, hii ni baada ya kukamilisha usajili wa Ousmane Dembele kwa pauni milioni 135. (Mundo Deportivo)

Juventus wanakaribia kukamilisha usajili wa Benedikt Howedes, 29, kutoka Schalke. (Gazzetta dello Sport)

29 August 2017,Sadc imejipanga kuzuia ugaidi_ Mahiga

Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Dk Augustine Mahiga amesema kikundi chochote cha kigaidi au kiharamia kitakachoingia katika moja ya nchi zilizo katika ukanda wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (Sadc) kitajuta.

Akizungumza kwa sababu kikundi hicho cha uigaidi kitashambuliwa na majeshi ya nchi zote katika ukanda huo iwapo kitaanza uchokozi.

Amesema nchi za Sadc zimeamua kujizatiti katika ulinzi kwa kuunganisha majeshi yake ili kujiweka sawa na tishio lolote la ugaidi na uharamia zikiamini uchumi wake hautaimarika kama moja ya nchi itakuwa inasumbuliwa na ugaidi.

“Wakazi wa Tanga wamebahatika kuona mazoezi ya pamoja ya majeshi ya Sadc na kujionea yalivyo imara. Naamini kundi lolote la ugaidi au uharamia litakalothubutu kuingia katika nchi yoyote litajuta,” amesema.

Balozi Mahiga amesema hayo wakati akifunga mazoezi ya pamoja ya kijeshi yaliyopewa jina la Ex-Matumbawe yaliyoendeshwa na majeshi kutoka nchi saba zilizo katika jumuiya ya Sadc yaliyofanyika mkoani Tanga na kuhitimishwa jana Agosti 28.

Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania (JWTZ), Jenerali Venance Mabeyo, amesema mazoezi ya Ex-Matumbawe yenye madhumuni ya kimkakati, utendaji kivita na ki-mbinu yamefanyika nchini kwa mara ya kwanza baada ya kuendeshwa Zambia, Lesotho, Afrika Kusini, Namibia, Angola na Zimbabwe.

Admit Mwananchi

29 August 2017, Polisi yachunguza upya kifo cha mchora katuni Naji

Polisi wa Uingereza wamesema wanachunguza tena mauaji ya mchora Katuni wa Kipalestina Naji Al-Ali.

Alipigwa risasi wakati alipokuwa akitembea kuelekea ofisini kwake jijini London Julai 1997.

Naji al- Ali anajulikana zaidi kutokana na katuni zake ambazo zilikuwa zikichapishwa katika gazeti la Kuwaiti, na mara kadhaa alikuwa akiwashutumu viongozi wa Kiarabu na utawala.

Polisi wa mji wa London wamesema wanamatumaini kwamba watu ambao hawakutaka kuzungumza wakati mauaji yalipotokea pengine sasa wataweza kuzungumza.

29 August 2017, Takukuru wachukuwe hatua dhidi ya wala rushwa_Rais Magufuli

Rais John Magufuli amewataka viongozi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) kutokuwa na kigugumizi cha kuchukua hatua pale wanapokuwa na ushahidi dhidi ya watu wanaojihusisha na vitendo vya rushwa.

Ametoa agizo hilo jana Agosti 28, alipotembelea na kuzungumza na wafanyakazi wa Takukuru katika ofisi za makao makuu ya Taasisi hiyo jijini Dar es Salaam.

“Kuna mambo mengi ya hovyo yanafanyika, tumehakiki pembejeo za ruzuku na kubaini madai ya Sh48 bilioni ni hewa, tumebaini wafanyakazi hewa zaidi ya 19,500, tumebaini kaya masikini hewa 56,000 zilizopaswa kupata fedha Tasaf, tumebaini wanafunzi hewa 5,850 waliotakiwa kupata mkopo, kuna vichwa vya treni 11 vimeletwa bila kuwepo mkataba na mengine mengi, haya yote yanafanyika kwa rushwa, nataka kuwaona mnachukua hatua stahiki,”amesema.

Taarifa ya Ikulu imesema Rais ameeleza kuwa na imani na Takukuru na amewataka wafanyakazi wake kufanya kazi kwa kuzingatia weledi, uzalendo na uadilifu, akiahidi Serikali kufanyia kazi changamoto zinazowakabili.

Monday, August 28, 2017

28 August 2017, Tetesi za soka Ulaya michezoni leo jumatatu

Liverpool wamemuulizia kiungo wa Monaco Thomas Lemar, 21, na wapo tayari kuvunja rekodi ya uhamisho ya klabu kwa kutoa pauni milioni 55. (Daily Telegraph)

Paris Saint-Germain wamefikia makubaliano ya kumsajili kwa mkopo kwanza, mshambuliaji wa Monaco, Kylian Mbappe, 18, na kuweza kukamilisha usajili wa pauni milioni 166 msimu ujao. (L'Equipe)

Manchester United wamewapa Real Madrid pauni milioni 92 kutaka kumsajili Gareth Bale. (Daily Star)

Barcelona wanamuona Marcus Rashford wa Manchester United kama mrithi wa baadaye wa Luis Suarez. (Don Balon)

Chelsea wana uhakika wa kukamilisha uhamisho wa pauni milioni 30 wa kiungo wa Leicester City Danny Drinkwater, 27, kabla ya dirisha la usajili kufungwa. (Daily Telegraph)

Manchester City wapo tayari kuwapa Arsenal pauni milioni 70 pamoja na beki Jason Denayer, ili kumsajili Alexis Sanchez, 28. (Daily Star)

Manchester City wanajiandaa kupanda dau kumtaka mshambuliaji wa Borussia Dortmund Pierre Emerick Aubameyang, iwapo watashindwa kumsajili Alexis Sanchez. (Le10Sport)

Leicester City wamepanda dau la pauni milioni 23 kutaka kumsajili beki wa West Brom Jonny Evans, 29. (BBC)

Hatma ya meneja wa Crystal Palace iko mashakani baada ya kupoteza mechi tatu za EPL. (Guardian)

Meneja wa West Ham Slaven Bilic anapambana vikali kulinda kazi yake baada ya kupoteza mechi tatu za mwanzo za EPL. (Sun)

Meneja wa Liverpool Jurgen Klopp amesema yuko tayari kumruhusu Divock Origi, 22, kuondoka kwa mkopo iwapo klabu yake itaongeza wachezaji wapya kabla ya dirisha la usajili kufungwa. (Liverpool Echo)

Beki wa Arsenal Shkodran Mustafi, 25, anajiandaa kuondoka Emirates na kwenda Inter Milan, mwaka mmoja tu baada ya kusajiliwa kwa pauni milioni 35 kutoka Valencia. (ESPN)

Stoke City wamefikia makubaliano na Tottenham ya kumsajili beki Kevin Wimmer, 24, kwa pauni milioni 15. (Sky Sports)

Mshambuliaji wa Chelsea Loic Remy, 30, ananyatiwa na Las Palmas ya Uhispania na Calgiari ya Italia. (Daily Mail)

Meneja wa Chelsea atabakia Stamford Bridge hata kama watashindwa kuongeza wachezaji wengine wapya. (Evening Standard)

Chelsea wanataka kumsajili mshambuliaji wa Swansea Fernando Llorente, 32, wakilenga kusajili wachezaji watatu wapya kabla ya dirisha la usajili kufungwa. (Independent)

Kipa wa Liverpool Simon Mignolet, 29, ananyatiwa na Napoli. (Gianluca Di Marzio)

West Brom wamepanda dau la pauni milioni 10 kumtaka kiungo wa Fenerbahce Josef de Souza, 28, na pia wamemuulizia beki wa Bournemouth Tyrone Mings, 24. (Daily Mail)

Swansea watapanda dau la pauni milioni 13 kutaka kumsajili tena mshambuliaji wa Manchester City Wilfried Bony, aliouzwa kwenda City kutoka Swansea mwaka 2015 kwa pauni milioni 28. (Daily Mail)

Inter Milan wanakaribia kumsajili Keita Balde wa Lazio kwa pauni milioni 27. (Daily Mirror)

Birmingham City wanazungumza na kiungo wa kimataifa wa Ghana Afiriye Acquah, 25, kutaka kumsajili kutoka Torino. (Sky Sports)

28 August 2017, Simba yaanza ligi kwa kugawa wiki

SIMBA imeanza mechi za Ligi Kuu Bara kwa kuweka rekodi tano za maana ambazo zimewashtua Yanga na huenda zikawachukua mechi kadhaa kujibu mapigo.

Kipigo cha mabao 7-0 ilichokitoa kwa Ruvu Shooting juzi Jumamosi, kimeifanya Simba kuongoza Ligi kwa kishindo huku ikiweka rekodi za maana.

Kwanza, Simba inakuwa timu ya kwanza kupata ushindi mkubwa zaidi katika mechi ya kwanza ya ligi katika kipindi cha zaidi ya miaka 10 iliyopita. Rekodi ya karibuni ilikuwa ikishikiliwa na Yanga ambayo iliifunga Ashanti United mabao 5-1 katika mechi ya ufunguzi ya msimu wa 2013/14.

Pia ushindi huo umeifanya Simba kuweka rekodi ya kufunga mabao mengi zaidi katika mchezo mmoja ndani ya miaka 10 iliyopita. Ushindi mkubwa wa mwisho kwa Simba ulikuwa dhidi ya Majimaji kwa mabao 6-1, hiyo ilikuwa Novemba 2015.

Simba pia imekuwa timu pekee iliyoweza kufunga mabao zaidi ya mawili katika mechi za ufunguzi wa ligi msimu huu.

Ushindi huo umeifanya pia Simba kuvunja rekodi ya Yanga kuifunga Ruvu mabao mengi ambapo ilifanya hivyo mwaka 2014 ilipoifunga kwa idadi kama hiyo ya mabao. Hata hivyo Simba bado ina kazi nzito ya kuvunja rekodi ya mabao 8-0 ambayo Yanga inaishikilia kwa kuifunga Coastal Union mapema 2015.

OKWI NAYE

Emmanuel Okwi amevunja rekodi ya Mrundi, Amissi Tambwe ambaye ndiye mchezaji wa sasa aliyewahi kufunga mabao manne kwenye mchezo mmoja. Tambwe alifunga mabao manne wakati Simba ikiifunga Mgambo JKT kwa mabao 6-0 mwaka 2013 na Yanga ilipoifunga Coastal Union 8-0.

Okwi amefunga ‘Hat Trick’ yake ya pili tangu alipoanza kucheza ligi hiyo mwaka 2009 kabla ya kuondoka na kurejea mara mbili tofauti. Hat Trick yake nyingine alifunga dhidi ya Ndanda mwaka 2015.

Mabao hayo yamemfanya Okwi kuwa mchezaji aliyefunga hat Trick ya mapema zaidi Ligi Kuu ambapo alitumia dakika 32 tu kufanya hivyo wakati wachezaji wengine wote waliomtangulia walitumia dakika zaidi ya 45.

“Hii inaonyesha ni kwa namna gani watu wamedhamiria kufanya kitu kwenye ligi, tutapambana kwa nguvu kwa pamoja na kuipa mafanikio Simba,”alisema Okwi ambaye pamoja na kufunga mabao hayo manne na kuwa kinara kwenye safu ya ufungaji bora, amesema kazi bado.

Akizungumzia sababu ya kuuingiza mpira ndani ya jezi yake tumboni, alisema: “Nimefanya hivyo kwa makusudi, mke wangu ni mjamzito na hii ilikuwa ni ishara ya zawadi kwake.”

Kocha Msaidizi wa Simba, Jackson Mayanja alisema: “Tunaendelea kufanya maboresho kwa kuimarisha safu ya ushambuliaji.”|

Katika mchezo huo, Mganda Okwi aling’ara baada ya kufunga mabao manne peke yake.

28 August 2017, Kesi ya uchaguzi kenya yaanza kusikilizwa

Mahakama Kuu nchini Kenya imeanza kusikiliza kesi ya kupinga ushindi wa Rais wa Kenya,Uhuru Kenyata, iliyotakiwa kuanza kusikilizwa jana.

Kesi hiyo ilitakiwa kuanza jana jioni baada ya kumalizika kwa hatua ya kwanza iliyofanyika juzi kwa pande zote tatu yaani upande wa NASA, Jubilee na Tume ya Taifa ya Uchaguzi na Mipaka nchini humo(IEBC) kuwasilisha mahakamani hoja zao za maandishi.

Msajili wa Mahakama hiyo, Esther Nyaiyaki akinukuliwa na gazeti la Kiingereza la Standard nchini humo bila kueleza mabadiliko hayo alisema itasikilizwa leo.

Kesi hiyo inatokana na uamuzi wa Muungano wa vyama vya upinzani NASA chini ya mgombea wake Raila Odinga kupinga matokeo ya uchaguzi wa urais wa Agosti 8, wakidai kuwa haukuwa wa haki na huru.

Odinga amepinga matokeo yaliyotangazwa Agosti 11, mwaka huu na Tume hiyo yakimtambua Rais Uhuru Kenyatta wa Muungano wa Jubilee kuwa mshindi wa kiti cha urais katika ungwe ya pili akipata kura 8, 203, 290 sawa na asilimia 54.27 huku mpinzani wake mkuu, mgombea wa Muungano wa upinzani wa NASA, Raila Odinga akIpata kura milioni 6,762,224 sawa na asilimia 44.74.

Odinga hakukubaliana na matokeo hayo hadharani na aliamua kuwasilisha stakabadhi zake mahakamani hapo ikiwa ni saa nane kabla ya tarehe ya mwisho. Baadaye, Agosti 24, mwaka huu, Rais Uhuru Kenyatta na Naibu wake William Ruto kwa upande wao, pia waliwasilisha stakabadhi zao kuhusiana na kesi hiyo.

Odinga ambaye alikuwa ni miongoni mwa wagombea nane wa kiti hicho cha urais, alilalamika pia kuwapo hujuma za Rais Uhuru Kenyatta kutumia mamlaka yake vibaya katika kuingilia mfumo wa tume hiyo.

28 August 2017, WFP kukata mgao wa chakula kwa wakimbizi Tanzania

Shirika la chakula duniani WFP limetangaza kukata mgao wa chakula kwa wakimbizi kutoka Congo na Burundi nchini Tanzania.

Kwa mujibu wa habari,shirika hilo limepunguza ugawaji wa chakula kwa wakimbizi 320,000 katika maeneo ya Mtendeli,Nduta na Nyarugusu kaskazini magharibi mwa Tanzania.

Ripoti zinaonyesha kuwa mpaka kufiikia mwezi Desemba WFP inahitaji dola za kimarekani milioni 23.6 ili kuweza kukidhi mahitaji ya wakimbizi Tanzania.

Mwakilishi wa WFP Tanzania Michael Dunford amesema kuwa endapo wafadhili hawatojitokeza kulidhamini shirika hilo basi itawabidi wakate mgao wa chakula haraka iwezekanavyo.

Tanzania ni kati ya nchi yenye idadi kubwa ya wakimbizi kutoka nchi nyingi barani Afrika.

28 August 2017, Lisu awataka Mawakili kutohudhuria mahakamani jumanne na jumatano

Baraza la Uongozi wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) limewataka mawakili nchi nzima kutohudhuria  mahakamani  Jumanne na Jumatano kama njia ya kupinga Kampuni ya Immma Advocate kuvamiwa.

Alizungumza  jana Jumapili, Rais wa TLS, Tundu Lissu alisema uamuzi huo umefikiwa juzi na kikao cha baraza la uongozi la chama hicho.

Alisemaa mawakili wote wanaotetea wananchi kwenye mahakama na kwenye mabaraza wasifanye kazi siku hiyo.

Aidha baraza hilo linafahamu kwamba wateja wao wataathirika siku hizo lakini usalama wa mawakili ni muhimu zaidi.

Lissu alisema baraza la uongozi linavitaka vyombo vya ulinzi na usalama kuwahakikishia ulinzi mawakili wa Immma Advocate dhidi ya vitisho vinavyoweza kuhatarisha usalama wao.

Pia baraza hilo linafanya jitihada za haraka za kukutana na Mkuu wa Jeshi la Polisi na Idara la usalama ili kujadiliana kuhusu shambulio hilo.

Lissu amewataka wananchi kuhakikisha wanalinda usalama,uhuru na heshima ya wanasheria na mawakili ili waweze kutekeleza wajibu wao wa kuwatetea wananchi.

28 August 2017,Mambo saba yakuzingatia kurefusha nywele

NYWELE humfanya mtu kuwa na muonekano mzuri kutokana na kuzijali, lakini muda mwingine husababisha kupoteza muonekano mzuri  na kuwa kama kichaa sababu ya kutozijali

JAMBO la kuzingatia kabla ya kuendelea kusoma na makala haya ni kufahamu kuwa ukuzaji wa nywele unakwenda pamoja na dhamira nzima ya utunzaji wake.

Ifahamike kuwa kama mtu anafuata kwa makini mbinu za utunzaji wa nywele, basi itakuwa rahisi kuzikuza nywele zake.

MAMBO SABA YAKUZINGATIA ILI KUREFUSHA NYWELE ZAKO ZIKIWA NA MUONEKANO MZURI

kuna mambo muhimu ambayo mtu anatakiwa kuyazingatia ili kuhakikisha nywele zake zinarefuka huku zikiwa na muonekano mzuri .

1. Jambo la kwanza ambalo ni muhimu kwa muhusika kuwa makini nalo, ni uchaguzi wa shampoo. Kama mhusika si mtaalamu katika kuchagua shampoo, anatakiwa kuonana na wataalamu wa urembo ili wampe ushauri juu ya aina ya nywele zake na shampoo anayotakiwa kutumia.

2. Jenga tabia  ya kupunguza nywele zake kila baada ya wiki mbili, hapa namaanisha kukata ncha. Kufanya hivyo kutasabaisha nywele zikue huku zikiwa na ubora unaotakiwa.

3. Jambo jingine la muhimu ni kupaka mafuta ambayo yanakwenda sambamba na nywele zako, kama ilivyo katika shampoo.

4.Mhusika pia anatakiwa kupata ushauri kutoka kwa wataalamu wa nywele ili kufahamu aina sahihi ya mafuta yake.

5. Vile vile stiming ni kitu muhimu kwa mhusika katika kuhakikisha kwamba nywele zake zinakuwa katika ubora unaotakiwa.

6. Jambo jingine ambalo mhusika anatakiwa kufahamu ni kuhakikisha anazichana nywele zake kwa kutumia kitana kikubwa kabla ya kumalizia kwa kitana kidogo, hii ni kila baada ya kuosha nywele zake. Kitana kikubwa kitasaidia kufungua nywele ambazo zimefungamana na kile kidogo husaidia kulainisha nywele.

7.Pia ni muhimu kuosha nywele kila baada ya siku tatu na kama mhusika akiona hana muda wa kutosha, basi afanye hivyo kila baada ya wiki moja.

Sunday, August 27, 2017

27 August 2017, Tetesi za soka Ulaya michezoni leo jumapili

Liverpool wameweka makataa ya hadi Jumatatu, kwa Barcelona wawe wamefikia bei ya Philippe Coutinho, 25. (Onda Cero)

Liverpool wanataka kukamilisha usajili wa Alex Oxlade Chamberlain, 24, kabla ya dirisha la usajili kufungwa. Chelsea pia wanamtaka winga huyo wa Arsenal. (Sunday Mirror)

Mshambuliaji wa Arsenal Alexis Sanchez, 28, imeripotiwa anaitaka klabu yake kumfanya kuwa mchezaji anayelipwa zaidi katika EPL iwapo wanataka asaini mkataba mpya. (Daily Star)

Meneja wa Arsenal Arsene Wenger hajakata tamaa ya kumsajili Thomas Lemar wa Monaco, 22, pamoja na Virgil van Dijk, 26, ingawa huenda ikawa msimu ujao. (Sun)

Arsenal wanataka kumsajili mshambuliaji wa Arsenal Marco Asensio, 21. (Sunday Express)

Paris Saint-Germain wanaendelea na majadiliano ya kumsajili mshambuliaji wa Monaco Kylian Mbappe kwa pauni milioni 166 kabla ya dirisha la usajili kufungwa, ingawa Monaco wenyewe wanataka Mbappe aende Real Madrid. (Sunday Telegraph)

Iwapo Kylian Mbappe ataondoka Monaco, klabu hiyo itataka kuziba pengo lake na Islam Slimani, 29, wa Leicester City. (Leicester Mercury)

Kiungo wa Bayern Munich Renato Sanchez, 20, ameomba kuachwa kwenye kikosi dhidi ya Werder Bremen ili ashughulikie mustakbali wake huku Chelsea na Liverpool zikimfuatilia. (Metro)

Everton wanataka kuwapiku Chelsea katika kumsajili mshambuliaji wa Leicester Jamie Vardy, kwa pauni milioni 40. (Sunday Mirror)

Tottenham huenda wakataka kumsajili mshambuliaji wa Liverpool Divock Origi, 22, iwapo Vincent Janssen ataondoka. (Sun)

Juventus wanataka kumsajili kiungo wa Barcelona Andre Gomes, 24. (Marca)

Mmiliki wa Valencia amewasili mjini Manchester kuanza mazungumzo ya kumsajili kiungo wa Manchester United Andreas Pereira, 21. (Sunday Express)

Leicester City wanataka kumsajili beki wa Manchester United Chris Smalling. (Daily Mirror)

Beki wa PSG Serge Aurier anasubiri kibali cha kufanya kazi Uingereza baada ya kukamilisha vipimo vya afya ili kujiunga na Tottenham. (Sky Sports)

27 August 2017, Vijiji 11 vyakabidhiwa fedha kwa ajili ya shughuli za kimaendeleo

Jumuiya ya Hifadhi ya Wanyamapori ya Enduimet (WMA) imekabidhi Sh99 milioni kwa vijiji 11 wilayani Longido kwa ajili ya shughuli za maendeleo ya wananchi.

Fedha hizo zimetolewa na kampuni ya uwindaji ya Shangri-la iliyopo wilayani Longido mkoani Arusha.

Imeelezwa kuwa fedha hizo zinatokana na mapato yaliyokusanywa kwa ajili ya shughuli za uwindaji katika kampuni hiyo.

Vijiji hivyo 11 vinavyounda jumuiya hiyo kwa kutoa maeneo ya shughuli za uwindaji kila kimoja kimepewa Sh9 milioni.

Mkuu wa Wilaya ya Longido, Daniel Chongolo amewaagiza watendaji wa vijiji husika kuhakikisha wanaainisha mapato na matumizi ya fedha hizo katika kila kijiji ili zijulikane zilivyotumika.

Chongolo amesema kumekuwepo ubadhirifu wa fedha za wananchi unaofanywa na watendaji wanaojali masilahi binafsi ikiwemo kujilipa posho.

27 August 2017, Kimbunga Harvey chasababisha wafungwa 4,500 kuhamishwa Marekani

Gavana wa jimbo la Texas, Greg Abbott, anasema kuwa, mafuriko ya kutisha ndio swala lake kuu la msingi, huku mvua kubwa inayoandamana na kimbunga kiitwacho Harvey, ikiendelea kutatiza mambo katika jimbo hilo.

Bwana Abbott anasema kwamba, miji miwili katika barabara inakopitia kimbunga hicho, Houston na Corpus Christi, tayari imepokea mvua zaidi ya Sentimita 50 na kiwango kinatarajiwa kuongezeka kwa mita moja zaidi, kabla ya kimbunga hicho kupungua, ifikiapo katikati ya wiki hii.

Zaidi ya wafungwa 4,500 katika gereza moja kusini mwa Houston wamehamishiwa hadi gereza lingine mashariki mwa Texas kwa sababu ya kuongezeka kwa maji ya mto Brazos ulioko karibu.

Maafisa wakuu wa jimbo hilo wamesema.
Juhudi za uokoaji, zinatatizwa na upepo mkali.

Mamia kwa maelfu ya watu wamekatikiwa na guvu ya umeme.

Kufikia sasa kifo cha mtu mmoja tu kimethibitishwa kutokea katika mji wa Rockport, huku wakuu wakionya kuwepo kwa mafuriko zaidi ya maji.

27 August 2017, Watu 27 wameuawa na wanamgambo wa Boko Haram Juma liliopita Nigeria

Watu 27 wameuwa wiki iliopita na wanamgambo wa Boko Haram katika mashambulizi tofauti.

Wanamgambo wa kundi hilo walichoma moto majumba ya rais katika mkoa wa Borno, mkoa ambao unapatikana Kaskazini mwa Nigeria.

Rais wa Nigeria ameahidi kupambana na kundi la  Boko Haram alipotoka nchini Uingereza ambapo alikuwa akipewa matibabu.

Kundi hilo limeanz akushambulia Nigeria mwanzoni mwa mwaka 2000 na kuzidisha mashambulizi yake baada ya kuuawa kwa kiongozi wake Muhammed Yusuf mwaka 2009

27 August 2017, Lema kupigwa marufuku kufanya mikutano Arusha

Jeshi la polisi mkoani Arusha, limepiga marufuku mikutano ya mbunge wa jimbo la Arusha mjini (Chadema), Godbless Lema iliyokuwa inaendelea katika jiji la Arusha ili kupisha maandalizi ya mtihani wa darasa la saba na mbio za Mwenge.

Katika barua ya Mkuu wa polisi wilaya ya Arusha, Mrakibu mwandamizi wa polisi (SSP),E.Tille ambayo imethibitisha na Kamanda wa polisi mkoa wa Arusha,(SACP) Charles Mkumbo imeeleza kuwa, Lema amezuiwa kufanya mkutano kuanzia kesho Agosti 27 hadi Septembaa mosi.

"Ofisi ya Mkuu wa polisi wilaya ya Arusha, inakutaarifu kuwa imezuia mikutano yako yeye ratiba kuanzia Agosti27 hadi Septema mosi kwa ajili ya kupisha maandalizi ya kuhitimisha mtihani wa darasa la saba na mwenge wa uhuru" ilisomeka barua hiyo na kushauri Lema kupanga mikutano kuanzia Septemba 8 mwaka huu.

Kamanda Mkumbo amesema, sababu kubwa ya kuzuiwa mikutano hiyo ni kwa kuwa wanahitajika polisi wa ulinzi na hivyo haiwezekani kupata polisi wa kulinda mikutano na pia kushiriki katika masuala ya mitihani na mwenge.

"Haya ni mambo ya kitaifa hivyo ndio sababu OCD amesitisha mikutano ya mbunge na mambo haya yakimalizika ataendelea na mikutano yake"alisema.

Akizungumza na mwananchi jana, Lema alisema anapinga polisi kuzuia mikutano yake, kwani ni ukiukwaji wa sheria na haki za mbunge.

Lema amesema sheria ya bunge kifungu cha nne fasihi ya kwanza, kinazungumzia uhuru wa mbunge kufanya mikutano jimboni kwake na kifungu cha 4(1) na (2) vinaelezea uhuru huo wa mbunge kufanya mikutano na pia ni ukiukwaji wa sheria kuzuia mikutano ya mbunge kwenye jimbo lake.

Lema amesema anaamini, kuzuiwa mikutano yake ni njama baada ya kubainika katika mikutano zaidi ya 10 ambayo amefanya katika jimbo la Arusha imekuwa na mafanikio makubwa na wananchi wa Arusha wamepata fursa ya kujua ukweli wa mambo mbali mbali.

"Hizi ni njama najua walipanga kuvuruga mikutano na kuharibu vyombo vyangu wakashindwa, wakanitakama kwa kuzidisha dakika 7 kwenye mkutano wangu mmoja nikawashinda kwa hoja sasa wameona wazuie kabisa na ikiwezekana watumie nguvu"alisema

Amesema sasa anashauriana na wanasheria wake kuona kama akubali barua ya polisi ama aendelee na mikutano kwani kimsingi, maeneo ambayo mikutano imepangwa kufanyika sio ya shule .

"Sasa kesho Jumapili nipo nje ya mji eneo la Olmoti kuna maandalizi yapi ya mwenge na darasa la saba , ntakuwa na mkutano eneo la soko la Shuma kuna mkusanyiko kila siku wa watu, nitaathiri nini huo mwenge ambao utafika kuanzia Septemba 6"amesema

Hata hivyo amesema, baada ya barua hiyo na kushauriana na mawaziri kadhaa na viongozi wa serikali, atalifikisha pia bungeni, kwani ni jambo la ajabu mbunge kuzuiwa kufanya mikutano kwasababu za mwenge na mitihani ya darasa la saba.

Amesema muda ambao umetakiwa na polisi afanye mikutano, anapaswa kuwa katika shughuli za kibunge jambo ambalo anaamini litaathiri ratiba za utendaji wa kazi zake.

Admit Mwananchi

Saturday, August 26, 2017

26 August 2017, Tetesi za soka Ulaya michezoni leo jumamosi

Tottenham wanajaribu kukamilisha usajili wa beki wa kimataifa wa Ivory Coast Serge Aurier, 24, kwa pauni milioni 23 kutoka Paris Saint-Germain kabla ya dirisha la usajili kufungwa. (Guardian)

Paris Saint-Germain wamekamilisha makubaliano na Monaco ya kumsajili Kylian Mbappe, 18, na kiungo mkabaji Fabinho, 23, kutoka Monaco. (Daily Record)

Chelsea wanapanga kuwa na mazungumzo na Everton kuhusiana na uhamisho wa pauni milioni 30 wa kiungo Ross Barkley baada ya timu hizo mbili kucheza siku ya Jumapili. (Sun)

Chelsea pia wanafikiria kupanda dau la kumtaka mshambuliaji wa Swansea Fernando Llorente, 32 ambaye anataka kucheza tena chini ya Antonio Conte. (Daily Telegraph)

Arsenal watamuuza beki Shkodran Mustafi, 25, kabla ya dirisha la usajili kufungwa iwapo watapata dau la pauni milioni 35, ambazo walilipa kumnunua kutoka Valencia mwaka jana. Juventus na Inter Milan zinamtaka beki huyo. (Daily Mail)

Meneja wa West Brom Tony Pulis yuko tayari kupanda dau la pauni milioni 30 kumsajili beki wa Liverpool Mamadou Sakho, 27. (Daily Telegraph)

Crystal Palace wana uhakika wa kumsajili Mamadou Sakho aliyecheza kwa mkopo katika klabu hiyo msimu uliopita. (Times)

Newcastle na Watford zinafikiria kumsajili mshambuliaji wa Leicester City Islam Slimani, 29. (Daily Mirror)

Arsenal huenda wakapanda dau kumtaka mshambuliaji wa Real Madrid Karim Benzima, 29, iwapo Alexis Sanchez ataondoka Emirates. (Diario Gol)

Arsenal wapo tayari kumuuza Alex Oxlade Chamberlain, 24, kwa timu itakayopanda dau la pauni milioni 35, huku Liverpool na Chelsea zikimtaka. (Daily Mirror)
Liverpool watajaribu kwa mara ya mwisho kutaka kumsajili Alex Oxlade-Chamberlain, wakitaka kuwapiku Chelsea. (Mirror)

Paris Saint Germain wamekataa dau la pauni milioni 32.4 kutoka kwa Barcelona kumtaka Angel Di Maria, 29. (AS)

Barcelona bado wanataka kumsajili Philippe Coutinho na Angel Di Maria, baada ya kukamilisha usajili wa Ousmane Dembele. (Marca)

Inter Milan inataka kuwasajili Shkodran Mustafi, 25, wa Arsenal na Eliaquim Mangala, 26, wa Manchester City. (Gazzetta dello Sport)

Manchester City na Paris Saint-Germain zitapambana kumsajili kiungo wa Porto Danilo Pereira. (A Bola)

Calgliari wanataka kumsajili mshambuliaji wa Chelsea Loic Remy. (Sky Sport Italia)

Marseille wanafikiria kumtaka mshambuliaji wa Liverpool Divock Origi, baada ya Olivier Giroud kuamua kubakia Emirates. (Mercato)

26 August 2017, Uzembe wa watumishi wa Afya wasababisha kifo cha mama mjamzito

Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Wilaya ya Manyoni mkoani Singida imewafukuza kazi Watumishi watatu wa halmashauri hiyo wakiwemo Wawili wa idara ya afya ambao wanatuhumiwa kufanya uzembe na kusabisha kifo cha mama mjazito aliyekuwa anasubiri kujifungua kwa njia ya upasuaji.

Baraza hilo limefikia uamuzi huo baada ya uchunguzi kubaini kuwa watumishi hao walikiuka kanuni za utumishi na aadili ya kazi zao.


Admit Tbc

26 August 2017, Ligi kuu Tanzania kuanza leo

Msimu mpya wa ligi kuu Tanzania bara unaanza hii leo ambapo kwenye siku yake ya kwanza viwanja saba vitawaka moto na kesho kutakuwa na mchezo mmoja utakaochezwa hapa jiji DSM.

Kaimu katibu mkuu wa shirikisho la soka hapa nchini (TFF) Wilfred Kidau amesema wanataka ligi hiyo iendeshwe kwa haki na usawa na hakuna kuipendelea timu yeyote.

Timu kumi na sita zinashiriki ligi hiyo huku kukiwa na timu mpya tatu zilizopanda daraja msimu huu ambazo ni Singida United, Njombe Mjii na Lipuli FC ya Iringa.

Enock Bwigane

26 August 2017 , Raia wauawa katika operesheni ya kijeshi Somalia

Afisa mmoja nchini Somalia ameshutumu jeshi la nchi hiyo pamoja na wafuasi wao kutoka nchi nyingine kuwaua raia tisa akiwemo mwanamke na mtoto mdogo.

Ali Nur Mohamed,Gavana msaidizi wa mkoa wa Shabelle ameviambia vyombo vya habari kuwa mauji hayo ya raia wasiokuwa na hatia yalitokea pale jeshi la Somalia pamoja na wanajeshi wengine kutoka nje,walipovamia shamba karibu na kijiji cha Bariire.

Kwa mujibu wa habari,wanajeshi hao walivamia shamba hilo siku ya Ijumaa na kuua watu tisa.

Hata hivyo makamanda wa jeshi nchini Soamlai hawakuwa na habari yoyote kuhusu operesheni ya namna hiyo.

Baadhi ya vyombo vya habari vinadai kuwa waliopoteza maisha ni watu kumi.

Afisa huyo amesema mauaji hayo yalikuwa ni ya makusudi na kuishutumu Marekani)

26 August 2017,Tshishimbi anajua_ Okwi

MCHEZAJI anayeongoza kwa kupendwa na mashabiki wa Simba, Emmanuel Okwi ametamka kwa mdomo wake kuwa kiungo mpya wa Yanga, Kabamba Tshishimbi ni fundi na anajua kazi yake.

Okwi amesema wazi kuwa kiungo huyo mpya wa watani zao, anajua soka na kumvulia kofia kwa namna alivyokipiga katika mechi ya Ngao ya Jamii juzi Jumatano pale Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam.

Straika huyo aliyewahi kucheza Yanga, alisema Tshishimbi anacheza soka la kazi, ushindani pamoja na kuburudisha na kwamba kama hiyo juzi alishuka uwanjani akiwa hayupo fiti kwa asilimia zote, hajui akiwa fiti atakuwaje kwa mpira mwingi aliowapigia Taifa.

Katika mechi hiyo ambayo Yanga ililala kwa penalti 5-4 baada ya kumaliza dakika 90 bila kufungana, kiwango cha Mkongomani huyo kimemfanya Okwi aliyewahi kuifunga Yanga mara tatu kuthubutu kutamka neno kutoka moyoni ambalo hata kocha wake, Joseph Omog alilikubali.

“Tshishimbi ana uwezo mkubwa, ameweza kucheza maeneo mengi, anajituma kuhakikisha timu yake inakuwa na mafanikio. Uchezaji wa aina yake ni wa mchezaji mwenye kuona mbali, hivyo wamepata mtu atakayewasaidia kwenye ligi na mashindano mengine,” alisema Okwi.

Mbali na Okwi, kiungo fundi wa kuchezea mpira, Haruna Niyonzima, naye alimzungumzia Tshishimbi na kumpa sifa kwamba Yanga wamepata mtu ambaye walimtafuta kwa muda mrefu.

“Nashukuru kwa kupata ushindi katika mechi yangu ya kwanza, ila nitoe pongezi kwa kiungo mpya wa Yanga Tshishimbi, alikuwa kikwazo kikubwa kwetu na pengine ndio alifanya tushindwe kupata ushindi ndani ya dakika tisini,” alisema.

Kiungo mwingine wa Simba, Mghana James Kotei naye alifunguka na kusema kuwa katika usajili ambao Yanga wameufanya msimu huu, basi Mkongomani huyo ndiye fundi na atawabeba katika mechi nyingi zilizopo mbele yao.

Friday, August 25, 2017

25 August 2017, Tetesi za soka Ulaya michezoni leo Ijumaa

Chelsea wana uhakika wa kumsajili kiungo wa Arsenal Alex Oxlade-Chamberlain, 24, kwa pauni milioni 35 kabla ya dirisha la usajili kufungwa Alhamisi ijayo. (Daily Telegraph)

Chelsea wananajaribu kufanikisha usajili wa pauni milioni 15 wa mshambuliaji wa Swansea Fernando Llorente, 32, ambaye alicheza chini ya Antonio Conte, Juventus. (Daily Telegraph)

Juventus wamewasiliana na Chelsea kumuulizia beki wa kati Gary Cahill. (Sun)

Manchester City wamekata tamaa ya kumsajili mshambuliaji wa Monaco Kylian Mbappe, 18, kwa pauni milioni 150. (Sun)

Manchester City watapanda dau la tatu la zaidi ya pauni milioni 25 kutaka kumsajili beki wa West Brom Jonny Evans, 29. (Times)

Mchezaji wa Monaco Thomas Lemar amesema angependa zaidi kujiunga na Manchester United badala ya Arsenal. (Duncan Castles)

Zlatan Ibrahimovic amekubali kupunguziwa mshahara wake kwa asilimia hamsini mwezi Januari, baada ya kusaini tena kubakia Old Trafford. (The Sun)

Barcelona wamekubaliana mkataba wa pauni milioni 138 na Borussia Dortmund wa kumsajili mshambuliaji Ousmane Dembele, 20. (L'Equipe)

Barcelona wamesema kiungo Arda Turan, 30, anaruhusiwa kuondoka kwa uhamisho usio na malipo yoyote.. (Sport)

Wakala wa Julian Draxler wa PSG wamekwenda Ujerumani kuzungumza na Bayern Munich kuhusiana na uhamisho wake. (L'Equipe)

Swansea wamepuguza kasi ya kutaka kumsajili kiungo wa West Brom Nacer Chadli, 28, baada ya kuambiwa walipe zaidi ya pauni milioni 25. (Daily Mail)

Crystal Palace wanataka kumsajili kipa wa Tottenham Michel Vorm, 33. (Evening Standard)

Crystal Palace pia wanataka kumsajili mshambuliaji wa Barcelona Munir El Haddadi, 21. (Sport)

Winga wa RB Leipzig Oliver Burke, 20, anakaribia kufanya vipimo vya afya kujiunga na West Brom. (Sky Sports)

PSG huenda wakamsajili kipa wa Napoli Pepe Reina. (Talksport)

25 August 2017, Rais Magufuli amuapisha mkurugenzi mkuu wa Takukuru

Rais Dkt. John Magufuli amemuapisha Brigedia Jenerali John Mbungo kuwa Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa -TAKUKURU.

Pamoja na kula kiapo cha kuwa Naibu Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU, Brigedia Jenerali Mbungo amekula kiapo cha uadilifu kwa viongozi wa umma kilichoongozwa na Kamishna wa Maadili Jaji Mstaafu Harold Nsekela.

Akizungumza mara baada ya kiapo hicho Rais Magufuli amewataka viongozi wote nchini kushirikiana kupambana na rushwa ili kuepusha madhara ya tatizo hilo katika uchumi na ustawi wa jamii.

Rais Magufuli ameipongeza TAKUKURU kwa kazi iliyoanza kuifanya na kuitaka kuongeza juhudi ili watu wote wanaojihusisha na vitendo vya kutoa na kupokea rushwa washughulikiwe kwa mujibu wa sheria.

25 August 2017, Kwa mara ya kwanza mfungwa mwenye ngozi nyeupe kunyongwa Florida

Florida kwa mara ya kwanza katika historia imetoa adhabu ya kifo kwa mfungwa mzungu kwa kosa la kumuua mwanamume mweusi.

Mfungwa huyo aliuawa Alhamisi iliyopita katika moja ya gereza la serikali.

Mark James Asay mwenye umri wa miaka 53 amehukumiwa kifo na kuuawa baada ya kumuua Rober Lee Booker mwenye umri wa miaka 34 na Robert McDowell mwenye umri wa miaka 26 mnamo mwaka 1987.Bwana James alipangiwa kuuawa kwa kutumia sindano.

Kwa mujibu wa habari,toka adhabu ya kifo irejeshwe mwaka 1976 Florida ni takriban watu weusi 18 wameuawa kwa makosa ya kuwaua watu weupe.

Adhabu ya kifo kwa kutumia sindano aliyopewa Asay na ni mara ya kwanza kutumika katika historia ya Marekani ni adhabu ya kwanza kutolewa Florida ndani ya miezi 18 iliyopita.

Hata hivyo wale wanaopinga adhabu ya kifo wamekuwa wakipingwa watengeneza sindano hiyo kutoisambaza serikalini.

Ripoti zinaonyesha kuwa bwana Asay na rafiki zake walikuwa wamelewa usiku wakati alipompiga risasi Booker aliyekuwa akitembea mtaani.

25 August 2017, Tundu Lissu aachiwa huru

Mbunge wa Singida mashariki na mwanasheria mkuu wa chama cha Demokrasia na maendeleo, (CHADEMA) TUNDU LISSU ameachiwa kuwa huru kwa dhamana

Kwa mujibu wa Mwananchi  wakili wake PETER KIBATALA amesema ameachiliwa kwa dhamana na atatakiwa kurejea tena  ijumatatu

Baada yakutoka ndani ya kituo cha  polisi Lissu hakutakiwa kuzungumza  kutokana na masharti ya dhamana, nakumlazimu kuelekea kwenye gari la wakili wake

"Lissu anatuhumiwa kwa  uchochezi na kumkashfu Rais", alisema Kibatala

Thursday, August 24, 2017

24 August 2017, Tetesi za soka Ulaya michezoni leo Alhamis

Barcelona wanajiandaa kupanda dau kumtaka winga wa Chelsea Willian, 29. (Times)

Chelsea wamepanda dau jipya la pauni milioni 35 kumtaka winga wa Arsenal Alex Oxlade-Chamberlain, 24. (Telegraph)

Chelsea wanajiandaa kutoa pauni milioni 32 kumsajili kiungo wa Leicester Danny Drinkwater, 27. (Sun)

Nyota wa Chelsea Eden Hazard atafanya kila awezalo kulazimisha uhamisho wake kwenda Real Madrid msimu huu. (Don Balon)
Beki wa kati wa Southampton Virgil van Dijk amekutana na Chelsea bila ruhusa ya klabu yake. (Star)

Mshambuliaji wa Real Madrid Cristiano Ronaldo, 32, huenda akaondoka Hispania kabla ya mwisho wa wiki hii. (El Pais)

Kiungo wa Liverpool Philippe Coutinho, 25, anafikiria kutoa taarifa rasmi kwa umma kuzungumzia kutoridhishwa kwake na klabu hiyo, ili kulazimisha uhamisho wake. (Yahoo Sports)

Juventus wanapanga kupambana na Liverpool katika kumsajili beki wa Schalke Benedikt Howedes. (Bild)

Inter Milan wamepanda dau la kumtaka beki wa Arsenal Shkodran Mustafi, 25, kwa mkopo, katika mkataba wa kumsajili kikamilifu baadaye kwa pauni milioni 20. (Mirror)

Baba yake Lionel Messi amezungumza na Manchester City kuhusiana na mwanae huyo kuhamia Etihad. (Sun)

Kylian Mbappe, 18, anakaribia kukamilisha uhamisho wake kwenda PSG kwa euro milioni 150. Monaco na PSG tayari zimefikia makubaliano ingawa wanasubiri kuona nani kati ya Julian Draxler, Lucas Moura au Javier Pastore atakuwa tayari kwenda Monaco kama sehemu ya mkataba huo. (L'Equipe)

Beki wa West Brom Jonny Evans, 29, anatarajia kukamilisha uhamisho wa pauni milioni 30 kwenda Manchester City wiki ijayo. (Mirror)

Manchester City hawajakata tamaa ya kumsajili Alexis Sanchez, 28, na wanafikiria kupanda dau la pauni milioni 50, kumsajili mchezaji huyo kabla dirisha la usajili halijafungwa wiki ijayo. (Times)

Manchester City wanataka kupanda dau la euro milioni 40 kutaka kumsajili beki wa Espanyol Aaron Martin, 20. (Sport)

Meneja wa Manchester United Jose Mourinho amezuia uhamisho wa mkopo wa kiungo Andreas Pereira kwenda Valencia. (Marca)

Barcelona wamekuwa na mazungumzo na PSV Eindhoven kuhusiana na uhamisho wa winga kinda Steven Bergwijn, 19. (gianlucadimarzio.com)

Schalke wamewaambia Barcelona wanaweza kumsajili Leon Goretzka, ili kuzuia mahasimu wao Bayern Munich wasimchukue. (Mundo Deportivo)

Vincent Janssen na Kevin Wimmer wa Tottenham wanakaribia kuhamia West Brom. (Sun)

Beki wa Manchester City Eliaquim Mangala anakaribia kuhamia Inter Milan. (Sky Sports)

Paris Saint-Germain wanafikiria kumsajili kipa wa Napoli Pepe Reina, 34. (AS)

Barcelona wanakaribia kukamilisha usajili wa Angel Di Maria, 29, kutoka PSG. (Sport)

Tottenham wanajiandaa kupanda dau jipya kumtaka mshambuliaji wa Lazio Balde Diao, 22, ambaye pia amehusishwa na kwenda Juventus. (Corriere dello Sport)

Tottenham wapo kwenye mazungumzo ya kina na PSG kuhusu uhamisho wa beki Serge Aurier kwa pauni milioni 24. (Telegraph)

Mshambuliaji wa Arsenal Joel Campbell, 25, ameiambia klabu yake kuwa hataki kwenda popote kwa mkopo msimu huu. (Guardian)

Arsenal watakubali pauni milioni 14 kutoka kwa Deportivo La Coruna ili kumsajili Lucas Perez kabla ya dirisha la usajili kufungwa wiki ijayo. (Evening Standard)

24 August 2017, Dawa za usingizi za zua utata kwa Manji

MKEMIA kutoka Ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali, Domician Dominic, ameiambia Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwa dawa aina ya Benzodiazepines iliyokutwa katika sampuli ya mkojo wa aliyekuwa Mwenyekiti wa Yanga, Yusufali Manji, hutumika hospitalini kutuliza maumivu makali ama kumpatia mtu usingizi.

Shahidi huyo wa tatu wa upande wa mashtaka aliyaeleza hayo jana akiongozwa na Wakili wa Serikali Mkuu,Timon Vitalis kutoa ushahidi katika kesi ya kutumia dawa za kulevya aina ya Heroin inayomkabili mfanyabiashara huyo. .

Akitoa ushahidi, Dominic alidai katika uchunguzi wa awali alioufanya katika sampuli ya mkojo wa Manji alikuta una dawa aina ya Benzodiazepines.

Alidai yeye kama Mkemia, kuwepo kwa dawa hiyo kwenye sampuli hiyo ya mkojo kulimpa picha kuwa mtu huyo alikuwa anaitumia kwa kutuliza maumivu makali au kukosa usingizi na kwamba ina matumizi mengi.

Pia alisema kwa uzoefu wake mara nyingi mtu anayetumia dawa hiyo huwa anatumia Heroine ama cocaine.

Manji aliyekana mashtaka anawakilishwa na Mawakili Alex Mgongolwa, Hudson Ndusyepo na Mosses Kimaro.

24 August 2017 , Rais Madulo _atuhumiwa kuhusika na rushwa

Muendesha mamshitaka wa zamani wa Venezuela Luisa Ortega Diaz amesema kuwa ana ushahidi kwamba Rais Nicolous Maduro na kundi la maofisa wengine walipokea hongo kutoka kampuni moja ya ujenzi.

Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari mjini Brasilia, Ortega amewataja wanaotuhumiwa kuchukua hongo pamoja na Rais Maduro kuwa ni Makamu Rais chama tawala Diosdado Cabello na kiongozi mwingine wa chama Jorge Rodriguez.

Akizungumza kutoka mjini Caracas, muendesha mashitaka mpya Tarek Saab ambaye anatuhumiwa pia na Ortega anasema kuwa madai hayo yanakosa ushahidi.

Amemkosoa Bi Ortega kwamba alifukuzwa utumishi serikalini kutokana na kufanya vitendo kinyume na maadili na kwamba ndani ya miaka kumi akiwa kazini ameshindwa kuchunguza tuhuma za rushwa.

Hata hivyo haya yanajiri, huku makamu wa Rais wa Marekani Mike Pence akisema kuwa utawala wa Rais Trump unatarajia kuongeza nguvu dhidi ya Venenzuela ili kurejesha utawala wa kidemokrasia.

Pence anasema kuanguka kwa nchi ya Venenzuela kuna madhara kwa ukanda mzima na kusababisha ongezeko la usafirishaji wa dawa za kulevya na ongezeko la wahamiaji kinyume cha sheria.

24 August 2017, Pembe za kifaru zafanyiwa mnada nchini Afrika Kusini

Takriban pembe 264 za Kifaru zafanyiwa mnada ulioruhusiwa kufanyika kisheria nchini Afrika Kusini.

Uuzaji wa pembe hizo za mnyama aliye katika orodha ya wanyama walio hatarini kwa ajili ya uwindaji haramu zinamilikiwa na mfugaji na mmiliki wa shamba maalum la kukuza Vifaru nchini humo.

Kabla ya pembe hizo kuondolewa vifaru hivyo vilidungwa sindano ya ganzi ili kuhakikisha shughuli hiyo inafanywa kwa urahisi bila ya kuwaumiza .

Pelham Jones ,mmiliki wa binafsi wa shirika hilo la kufuga vifaru hao alifahamisha kwamba itachukua miaka 2 kwa vifaru hao kumea pembe tena .

Jones aliruhusiwa kufanyia biashara pembe hizo baada ya kushinda kesi mahakamani dhidi ya serikali .

Siku ya Jumapili mahakama moja Afrika Kusini ilimruhusu mmliki huyo kufanya mnada huo kupitia mtandaoni .

Hapo awali serikali ilikataa kumpa kibali cha kumruhusu kufanya biashara ya pembe hizo .

Afrika Kusini inachangia asilimia 80 ya jumla ya vifaru vyote vinavyopatikana ulimwenguni.

Wednesday, August 23, 2017

24 August 2017, Rais magufuli _amteua Kamishna wa kutokomeza dawa za kulevya

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania John Magufuli amemteua Luteni Kanali Fredrick Milanzi kuwa Kamishna wa Operesheni wa Mamlaka ya Kuzuia na Kupambana na Dawa za Kulevya.

Luteni Kanali Frederick Felix Milanzi anachukua nafasi ya Mihayo Msikela ambaye amerejeshwa Makao Makuu ya Polisi.

Rais Magufuli amezungumza na Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Kuzuia na Kupambana na Dawa za Kulevya Rogers William ambaye amemhakikishia kuwa kazi ya kukabiliana na tatizo la biashara na matumizi ya dawa za kulevya inaendelea vizuri.

Rogers amesema tatizo la dawa za kulevya lilikuwa kubwa na ametaja dawa za kulevya ambazo Mamlaka inapambana nazo kuwa ni bangi, heroine, cocaine, na kwamba kwa sasa imeanza kukamata na kuharibu mashamba ya bangi na bangi iliyovunwa.

Amebainisha mikakati mitatu inayotumika katika mapambano dhidi ya tatizo hilo kuwa ni kuzuia dawa za kulevya zisiingie nchini, kutoa elimu kuanzia shule za msingi, sekondari, vyuo na kwenye jamii ili watu waache kutumia dawa za kulevya na kutoa tiba kwa watu walioathirika na dawa za kulevya.

23 August 2017, Tetesi za soka Ulaya michezoni leo jumatano

Barcelona watapanda dau la mwisho la pauni milioni 136 kumtaka kiungo wa Liverpool Philippe Coutinho, 25, baada ya dau la kwanza, la pili na la tatu kukataliwa. (Sun)

Barcelona wamepanda dau la pili la pauni milioni 119 kumtaka mshambuliali wa Borussia Dortmund Ousmane Dembele, 20, lakini Dortmund wanataka pauni milioni 138. (Sky Deutschland)

Barcelona wamebadili mawazo ya kumsajili kiungo wa Nice, Jean Michael Seri. (Mundo Deportivo)

Chelsea watamchukua meneja wa zamani wa Borussia Dortmund Thomas Tuchel kuziba nafasi ya Antonio Conte, huku taarifa za mvutano kati ya Conte na utawala wa Chelsea zikizidi kurindima. (Bild)

Chelsea wanakaribia kukamilisha usajili wa Danny Drinkwater, 27, kutoka Leicester kwa pauni milioni 30. Chelsea pia wanamtaka kiungo wa Inter Milan Antonio Candreva, 30, ambaye ameambiwa atauzwa kwa pauni milioni 25. (Mirror)

Chelsea wanafikiria kumchukua mshambuliaji wa Leicester City Jamie Vardy, 30. (Mirror)

Chelsea bado wanamfuatilia mshambuliaji wa Torino Andrea Belotti, 23. (Star)

Licha ya kukataliwa mara kadhaa, Chelsea watapanda dau jingine la euro milioni 70 kumtaka beki wa Juventus Alex Sandro. (Calciomercato.com)

Chelsea wapo tayari kupanda dau la pauni milioni 35 kumtaka kiungo mshambuliaji wa Arsenal Alex Oxlade-Chamberlain, ambaye ameiambia klabu yake kuwa anataka kuondoka. (The Sun)

Alex Oxlade-Chamberlain, 24, hana uhakika wa kusaini mkataba mpya Emirates, huku Chelsea na Liverpool wakiendelea kumnyatia. (Telegraph)

Paris Saint-Germain watamlipa mshambuliaji wa Monaco, Kylian Mbappe, 18, mshahara wa pauni milioni 13.8 kwa mwaka, mara mbili ya mshahara alioahidiwa kupewa na Real Madrid. (Marca)

Beki wa kushoto wa Tottenham Danny Rose, 27, atakuwa na mazungumzo ya mkataba mpya na klabu yake huku Chelsea na Manchester United wakiendelea kumnyatia. (Independent)

Tottenham wana matumaini ya kumsajili beki wa kulia wa PSG Serge Aurier, 24, pamoja na beki wa Estudiantes Juan Foyth. (Sky Sports)

Manchester City wanajiandaa kupanda dau la pili kumtaka beki wa kati wa West Brom Jonny Evans, 29, baada ya dau la pauni milioni 18 kukataliwa wiki iliyopita. (ESPN)

Manchester United wamekuwa namazungumzo na Inter Milan kuhusu uhamisho wa Ivan Perisic, 28, tangu mwisho wa msimu uliopita, lakini mchezaji huyo wa kimataifa wa Croatia anatarajiwa kusaini mkataba mpya Inter. (Star)

Manchester United ni miongoni mwa timu zinazomfuatilia beki wa kati wa Valencia Ezequiel Garay. (The Sun)

Manchester United, West Ham, Everton, Monaco na Anerlecht zinamnyatia mshambuliaji Raul Jiminez wa Benfica. (ESPN Mexico)

Everton wamepanda dau la pauni milioni 27.5 kumtaka mshambuliaji wa Benfica Raul Jiminez. (The Sun)

Arsenal huenda wakashawishiwa kumuuza Alexis Sanchez kwa pauni milioni 70, lakini Arsene Wenger amedhamiria kutomuuza. (Daily Mirror)

Marseille wamethibitisha kuwa wanataka kumsajili mshambuliaji wa Chelsea Diego Costa, 28, iwapo atashindwa kwenda Atletico Madrid. (Telegraph)

Meneja wa Liverpool Jurgen Klopp anataka kumsajili beki wa Schalke Benedikt Howedes, 29, kwa pauni milioni 18. (DW Sports)

23 August 2017, Angola wamchagua rais mpya baada ya miaka 38

Rais Jose Eduardo dos Santos amekuwa madarakani tangu mwaka 1979 na kuwa rais wa pili barani Afrika kuwa madarakani kwa kipindi kirefu zaidi.

Rais Santos hawanii tena uchaguzi huu, ambao waziri wa ulinzi Joao Lourenco anawania kama mgombea kupitia chama tawala cha MPLA.

Mpinzani wake mkuu anatarajiwa kuwa Isias Samakuva, kutoka chama cha hasimu wa MPLA, Unita.

Wachangazi wanasema kuwa chama cha MPLA ambacho kimekuwa madarakani tangua uhuru wa nchi hiyo mwaka 1975, kinaokana kuwa kitaibuka mshindi.

Chama cha tatu kwa ukubwa cha Casa-CE, kinaongozwa na Abel Chivukuvuku, ambaye alikuwa afisa wa cheo cha juu wa Unita wakati kilikuwa ni kundi la waasi

Baada ya vita, Angola ilikuwa moja ya nchi zilizokuwa aa uchumi uliikua kwa haraka zaidi duniani kutona na utajiri wake mkubwa wa mafuta.

Lakini wakati bei ya mafuta ilishuka miaka miwili iliyopita iliadhiri uchumi wote.

Ikiwa asimia kubwa ya watu wako chini ya umri wa maiak 35, watu hao ndio na watakuwa na uamuzi mkubwa.

23 August 2017, Mataifa ya kiislam yatakiwa kushirikiana_Rais Erdgan

Rais wa Uturuki Recep Tayyıp Erdoğan ametoa wito kwa mataifa ya kiislamu kuongeza ushirikiano baina yao .

Erdoğan alisema haya akiwa ziarani Jordan katika mji mkuu wa Amman kuadhimisha miaka 70 ya uhusiano wa kidiplomasia baina ya Uturuki na Jordan .

Rais Erdoğan alifahamisha haya akiwa katika mkutano na wajumbe kutoka nchi hizo mbili katika ikulu ya Hussainiah Palace na kusema kuwa kipindi hiki ulimwengu wa kiislamu unapitia wakati mgumu .

Aliendelea usisitiza kwamba ni nyakati hizi ambazo waislamu wanatakiwa kuongeza ushirikiano baina yao .

Awali siku ya Jumatatu rais Erdoğan alikutana na mfalme Abdullah wa Jordan na kuzumgumza kuhusu matukio na mzozo baina ya Israel na Palestina .

Mfalme Abdullah alitoa shukrani za dhati kwa Erdoğan kwa kuendelea kuunga mkono Jordan na pia msimamo wake kuhusu suala la Al Aqsa .

Erdoğan aliahidi kuendelea kushirikiana na Jordan katika juhudi za kulinda hadhi ya mskiti wa Al Aqsa .

23 August 2017, Talaka za papo hapo zatangazwa kuwa kinyume na katiba India

Sheria ya kiislamu ya talaka za papo kwa hapo imetangazwa kuwa kinyume na katiba na mahakama kuu nchini India.

Mahakama hiyo imepiga kura 3-2 dhidi ya utamaduni wa kuwa mwanamume anaweza kumpa mke wake talaka kwa kutamka neno "talaka" mara tatu.
Mahamakama inaamini kuwa kitendo hicho ni kinyume na sheria ya kiislamu pia.

Kwa mujibu wa habari,India ni kati ya nchi chache zilizobaki na utamaduni wa kutoa talaka kwa kutamka neno talaka mara tatu.

Matumizi ya talaka hiyo yameongezeka zaidi baada ya ukuaji wa teknolojia kwani wanawake wamekuwa wakipewa talaka kupitia simu za mkononi,barua, meseji na hata kupitia mtandao wa Facebook.

Waziri wa wanawake nchini humo Maneka Gandhi ameunga mkono uamuzi wa mahakama hiyo na kusema kuwa ni wakati wa haki sawa kwa wote.

23 August 2017, Maasai wachomewa nyumba zao kwa ajili ya kulinda eneo la wanyama pori

Simat Rotiken na familia yake wanapigwa na baridi kali usiku wakiwa chini ya mti baada ya serikali kuichoma nyumba waliokuwa wakikaa kwa madai ya kutunza eneo kwa ajili ya wanyama pori.

Kwa mujibu wa habari,Maasai hao walifukuzwa katika eneo lao na maafisa usalama kwa madai kuwa serikali imeanzisha sera mpya ya kulilinda eneo la Loliondo karibu na hifadhi ya wanyama ya Serengeti.

Serikali inataka kuwatoa Maasai wote kutoka katika eneo hilo ili kuweza kutunza maji na chakula kwa ajili ya wanyama pori ambao mara nyingi huwindwa na watalii wenye uwezo mkubwa kifedha kutoka nchi za nje.

Ripoti zilizotolewa na shirika la biashara la Ortello kutoka Dubai ni kwamba makazi ya binadamu na mifugo vimechangia kwa kiasi kikubwa kupunguza idadi ya wanyama pori.Shirika hilo,mnamo mwaka 1992 lilipewa haki ya kuwinda ndani ya eneo la kilomita 1500.

Ripoti iliyotolewa na kampuni hiyo Novemba mwaka 2016 inaonyesha kuwa upungu wa wanyama pori umesababishwa pia na mabadiliko katika hali ya hewa.

Maasai wengi wametolewa katika maeneo waliokuwa wakiishi kwa karne na karne kwasababu tu ya ripoti zilizotolewa na kampuni ya Ortello.

Bwana Rotiken mwenye umri wa miaka 39 ni kati ya Maasai wengi waliokuwa wakiishi kaskazini mwa Ngorongoro na sasa wamebaki bila makazi baada ya nyumba zao kuchomwa moto.

23 August 2017, Lisu kupandishwa mahakamani

Mwanasheria wa Chadema na Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu amenyimwa dhamana baada ya kukamatwa leo kwa tuhuma za kumkashifu Rais John Magufuli na uchochezi.

Kwa mujibu wa  Mwananchi  mwanasheria wake Faraji Mangula amesema kwamba kesho Lissu atapandishwa mahakamani.

Amesema Polisi wamedai kwamba amemkashifu Rais a wakati wa mkutano wake na waandishi wa habari kwenye hoteli ya Protea.

‘’Polisi wamemnyima dhamana wamesema wanafanya utaratibu wakumfikisha mahakamani’’amesema.

Tuesday, August 22, 2017

22 August 2017, Tetesi za soka Ulaya michezoni leo jumanne

Paris Saint- Germain wanakaribia kukamilisha usajili wa mshambuliaji wa Monaco Kylian Mbappe, 18, na Fabinho kwa pauni milioni 200. Mbappe pekee atagharimu pauni milioni 128.PSG pia watamtoa na Lucas Moura katika mkataba huo. (Sky Sport)

Barcelona wamekubali kuwa Liverpool hawatowauzia Philippe Coutinho, 25, mwezi huu. (Mirror)

Kiungo wa Real Madrid Mateo Kovacic, 23, amekubali kwa kauli kujiunga na Liverpool kuziba nafasi ya Philippe Coutinho iwapo ataondoka kwenda Barcelona. (Daily Mirror)

Liverpool bado wanataka kumsajili Virgil van Dijk na watakuwa tayari ikiwa Southampton watabadili msimamo wao kuhusu beki huyo. (Liverpool Echo)

Diego Costa, 28, ameambiwa na Atletico Madrid atafute suluhu na Chelsea kwanza kabla ya kununuliwa kwa pauni milioni 25. (Sun)

Kiungo wa Juventus Claudio Marchisio anataka kuondoka Italia na kujiunga na Chelsea. (Corriere della Sera)

Manchester City wanakaribia kukata tamaa ya kumsajili beki wa West Brom Jonny Evans, 29, na badala yake watapanda dau la pauni milioni 20 kumtaka beki wa Middlesbrough Ben Gibson, 24. (Independent)

Tottenham wanajiandaa kupanda dau la pauni milioni 20 kumtaka kiungo wa Everton Ross Barkley, 23, ingawa wanakabiliwa na ushindani kutoka kwa Chelsea pia. (Telegraph)

West Ham tayari wanatafuta kocha wa kuziba nafasi ya Slaven Bilic ambaye amekuwa na mwanzo mbovu wa msimu. (Mirror)

Manchester United wanamtaka kinda wa Fulham Ryan Ssesegnon, 17, ambaye pia anasakwa na Tottenham. (Sky Sports)

Valencia wanakaribia kukamilisha usajili wa mkopo wa kiungo wa Manchester United Andreas Pereira. (Cadena Ser Valencia)

Bayern Munich wanafikiria kumsajili mshambuliaji wa Paris Saint-Germain Julian Draxler ambaye hatma yake iko mashakani baada ya kuwasili kwa Neymar.

Draxler pia ananyatiwa na Arsenal, Liverpool na Manchester United. (Westdeutsche Allgemeine Zeitung)

Meneja wa Leicester Craig Shakespeare amesema hatma ya Riyad Mahrez, 26, na Danny Drinkwater, 27, pengine haitafahamika mpaka siku za mwisho za dirisha la usajili. (Leicester Mercury)

Beki wa kati wa Southampton ameonekana akifanya mazoezi na kikosi cha chini ya miaka 23 baada ya kuwasilisha maombi ya kuondoka. (Express)

Chelsea hawatopanda dau la kumtaka Virgil van Dijk hadi pale Southampton watakapokuwa tayari ingawa klabu hiyo imesema beki huyo hauzwi. (Telegraph)

Chelsea huenda wakaweza kumsajili Antonio Candreva, 30, kwa sababu Inter Milan inatafuta fedha za kutaka kumsajili Suso, 23, kutoka AC Milan. (Gazzetta dello Sport)

Galatasaray wanataka kumsajili beki wa Arsenal Kieran Gibbs. (The Times)

Crystal Palace wamepanda dau la pauni milioni 15 kumtaka beki wa Tottenham Kevin Wimmer, ambaye pia anasakwa na West Brom na Stoke. Spurs wanataka pauni milioni 20. (Daily Mail)

22 August 2017, Tatizo sio mashamba _Sumaye

Waziri Mkuu Mstaafu wa Serikali ya Awamu ya Tatu, Frederick Sumaye amesema kunyang'anywa mashamba yake si sababu ya yeye kufikiria kurudi CCM.

“Kunyang’anywa mashamba yangu najua ni uamuzi wa juu haunidhoofishi nifikirie kurudi CCM’’

Sumaye amesema mashamba yaliyofutwa na Serikali yalikuwa yanalipiwa kodi na yalikuwa yanamilikiwa kisheria.

"Wanataka nirudi CCM, mimi sitaki kurudi CCM, kwanini wananilazimisha? Nilisema sababu za kuondoka huko, waseme wazi sababu za kuyafuta ni za kisiasa tu," amesema Sumaye leo katika mkutano wa waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.

22 August 2017, Rais wa kwanza wa Kosovo afariki dunia

Rais wa kwanza wa Kosovo Bayram Recepi amefariki dunia baada ya kukutwa kapungukiwa damu katika ubongo.

Kiongozi huyo amefariki katika moja ya hospitali nchini Uturuki alipokwenda kutibiwa.

Kwa mujibu habari,bwana Recepi alikuwa rais wa kwanza wa Kosova mnamo mwaka 2002 mwezi Machi.

Recep alisomea udaktari na kuishia kuwa rais wa kwan.za wa nchi hiyo kupitia chama cha KDP.