Wednesday, August 23, 2017

23 August 2017, Maasai wachomewa nyumba zao kwa ajili ya kulinda eneo la wanyama pori

Simat Rotiken na familia yake wanapigwa na baridi kali usiku wakiwa chini ya mti baada ya serikali kuichoma nyumba waliokuwa wakikaa kwa madai ya kutunza eneo kwa ajili ya wanyama pori.

Kwa mujibu wa habari,Maasai hao walifukuzwa katika eneo lao na maafisa usalama kwa madai kuwa serikali imeanzisha sera mpya ya kulilinda eneo la Loliondo karibu na hifadhi ya wanyama ya Serengeti.

Serikali inataka kuwatoa Maasai wote kutoka katika eneo hilo ili kuweza kutunza maji na chakula kwa ajili ya wanyama pori ambao mara nyingi huwindwa na watalii wenye uwezo mkubwa kifedha kutoka nchi za nje.

Ripoti zilizotolewa na shirika la biashara la Ortello kutoka Dubai ni kwamba makazi ya binadamu na mifugo vimechangia kwa kiasi kikubwa kupunguza idadi ya wanyama pori.Shirika hilo,mnamo mwaka 1992 lilipewa haki ya kuwinda ndani ya eneo la kilomita 1500.

Ripoti iliyotolewa na kampuni hiyo Novemba mwaka 2016 inaonyesha kuwa upungu wa wanyama pori umesababishwa pia na mabadiliko katika hali ya hewa.

Maasai wengi wametolewa katika maeneo waliokuwa wakiishi kwa karne na karne kwasababu tu ya ripoti zilizotolewa na kampuni ya Ortello.

Bwana Rotiken mwenye umri wa miaka 39 ni kati ya Maasai wengi waliokuwa wakiishi kaskazini mwa Ngorongoro na sasa wamebaki bila makazi baada ya nyumba zao kuchomwa moto.

No comments: