Thursday, August 24, 2017

24 August 2017, Pembe za kifaru zafanyiwa mnada nchini Afrika Kusini

Takriban pembe 264 za Kifaru zafanyiwa mnada ulioruhusiwa kufanyika kisheria nchini Afrika Kusini.

Uuzaji wa pembe hizo za mnyama aliye katika orodha ya wanyama walio hatarini kwa ajili ya uwindaji haramu zinamilikiwa na mfugaji na mmiliki wa shamba maalum la kukuza Vifaru nchini humo.

Kabla ya pembe hizo kuondolewa vifaru hivyo vilidungwa sindano ya ganzi ili kuhakikisha shughuli hiyo inafanywa kwa urahisi bila ya kuwaumiza .

Pelham Jones ,mmiliki wa binafsi wa shirika hilo la kufuga vifaru hao alifahamisha kwamba itachukua miaka 2 kwa vifaru hao kumea pembe tena .

Jones aliruhusiwa kufanyia biashara pembe hizo baada ya kushinda kesi mahakamani dhidi ya serikali .

Siku ya Jumapili mahakama moja Afrika Kusini ilimruhusu mmliki huyo kufanya mnada huo kupitia mtandaoni .

Hapo awali serikali ilikataa kumpa kibali cha kumruhusu kufanya biashara ya pembe hizo .

Afrika Kusini inachangia asilimia 80 ya jumla ya vifaru vyote vinavyopatikana ulimwenguni.

No comments: