Monday, August 28, 2017

28 August 2017, Lisu awataka Mawakili kutohudhuria mahakamani jumanne na jumatano

Baraza la Uongozi wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) limewataka mawakili nchi nzima kutohudhuria  mahakamani  Jumanne na Jumatano kama njia ya kupinga Kampuni ya Immma Advocate kuvamiwa.

Alizungumza  jana Jumapili, Rais wa TLS, Tundu Lissu alisema uamuzi huo umefikiwa juzi na kikao cha baraza la uongozi la chama hicho.

Alisemaa mawakili wote wanaotetea wananchi kwenye mahakama na kwenye mabaraza wasifanye kazi siku hiyo.

Aidha baraza hilo linafahamu kwamba wateja wao wataathirika siku hizo lakini usalama wa mawakili ni muhimu zaidi.

Lissu alisema baraza la uongozi linavitaka vyombo vya ulinzi na usalama kuwahakikishia ulinzi mawakili wa Immma Advocate dhidi ya vitisho vinavyoweza kuhatarisha usalama wao.

Pia baraza hilo linafanya jitihada za haraka za kukutana na Mkuu wa Jeshi la Polisi na Idara la usalama ili kujadiliana kuhusu shambulio hilo.

Lissu amewataka wananchi kuhakikisha wanalinda usalama,uhuru na heshima ya wanasheria na mawakili ili waweze kutekeleza wajibu wao wa kuwatetea wananchi.

No comments: