Makao Makuu ya chama cha upinzani cha Alliance Democratic Party (ADP ) yamechomwa moto mjini Freetown nchini Sierra Leone.
Kwa mujibu wa habari,wazima moto walifika kujaribu kusaidia kuuzima moto ulioanzia ghorofa ya juu kabisa ya jengo hilo.
Kiongozi wa upinzani Mohamed Kamaremba Mansaray amekiambia kituo cha habari cha Anadolu kuwa anashuku huo moto umeanzishwa na chama tawala APC.
Bwana Kamaremba amesema kuwa bomu lenye petroli lilirushwa ndani ya ofisi yake majira ya asubuhi na kusababisha vitu vya thamani ikiwemo makaratasi muhimu kuungua.
Bwana Kamaremba amesema anaamini ni chama tawala ndio kinahusika kwani waliwahi kumchomea ofisi yake miaka ya nyuma na hakuna hatua yoyote ya kisheria iliyochukuliwa.
Kiongozi huyo wa upinzani amesema kuwa chama tawala kimefanya hivyo kutokana na yeye kupinga na kukosoa siasa zao kila mara.
Hata hivyo chama tawala kimeyakanusha mashtaka hayo na kuitaka polisi kufanya uchunguzi zaidi.
No comments:
Post a Comment