NYWELE humfanya mtu kuwa na muonekano mzuri kutokana na kuzijali, lakini muda mwingine husababisha kupoteza muonekano mzuri na kuwa kama kichaa sababu ya kutozijali
JAMBO la kuzingatia kabla ya kuendelea kusoma na makala haya ni kufahamu kuwa ukuzaji wa nywele unakwenda pamoja na dhamira nzima ya utunzaji wake.
Ifahamike kuwa kama mtu anafuata kwa makini mbinu za utunzaji wa nywele, basi itakuwa rahisi kuzikuza nywele zake.
MAMBO SABA YAKUZINGATIA ILI KUREFUSHA NYWELE ZAKO ZIKIWA NA MUONEKANO MZURI
kuna mambo muhimu ambayo mtu anatakiwa kuyazingatia ili kuhakikisha nywele zake zinarefuka huku zikiwa na muonekano mzuri .
1. Jambo la kwanza ambalo ni muhimu kwa muhusika kuwa makini nalo, ni uchaguzi wa shampoo. Kama mhusika si mtaalamu katika kuchagua shampoo, anatakiwa kuonana na wataalamu wa urembo ili wampe ushauri juu ya aina ya nywele zake na shampoo anayotakiwa kutumia.
2. Jenga tabia ya kupunguza nywele zake kila baada ya wiki mbili, hapa namaanisha kukata ncha. Kufanya hivyo kutasabaisha nywele zikue huku zikiwa na ubora unaotakiwa.
3. Jambo jingine la muhimu ni kupaka mafuta ambayo yanakwenda sambamba na nywele zako, kama ilivyo katika shampoo.
4.Mhusika pia anatakiwa kupata ushauri kutoka kwa wataalamu wa nywele ili kufahamu aina sahihi ya mafuta yake.
5. Vile vile stiming ni kitu muhimu kwa mhusika katika kuhakikisha kwamba nywele zake zinakuwa katika ubora unaotakiwa.
6. Jambo jingine ambalo mhusika anatakiwa kufahamu ni kuhakikisha anazichana nywele zake kwa kutumia kitana kikubwa kabla ya kumalizia kwa kitana kidogo, hii ni kila baada ya kuosha nywele zake. Kitana kikubwa kitasaidia kufungua nywele ambazo zimefungamana na kile kidogo husaidia kulainisha nywele.
7.Pia ni muhimu kuosha nywele kila baada ya siku tatu na kama mhusika akiona hana muda wa kutosha, basi afanye hivyo kila baada ya wiki moja.
No comments:
Post a Comment