Zaidi ya mataifa 200 yamekutana katika mkutano uliondaliwa na shirika la UNEP la Umoja wa Mataifa jijini Nairobi Kenya.
Kwa mujibu wa habari,mataifa hayo yamesaini mkataba na Umoja wa Mataifa katika azimio la kupambana na utupahi wa plastiki baharini.
Shirika la UNEP katika mkutano huo limesema kuwa endapo hali hiyo haitafanyiwa ukarabati basi kutakuwa na plastiki nyingi zaidi ya samaki baharini ifikapo mwaka 2050.
Ripoti zinaonyesha kuwa tani milioni nane za plastiki na uchafu mwingine hutupwa baharaini ndani ya mwaka mmoja.
Hali hiyo husababisha vifo vya vumbe wanaoishi majini.
No comments:
Post a Comment