Wednesday, August 23, 2017

24 August 2017, Rais magufuli _amteua Kamishna wa kutokomeza dawa za kulevya

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania John Magufuli amemteua Luteni Kanali Fredrick Milanzi kuwa Kamishna wa Operesheni wa Mamlaka ya Kuzuia na Kupambana na Dawa za Kulevya.

Luteni Kanali Frederick Felix Milanzi anachukua nafasi ya Mihayo Msikela ambaye amerejeshwa Makao Makuu ya Polisi.

Rais Magufuli amezungumza na Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Kuzuia na Kupambana na Dawa za Kulevya Rogers William ambaye amemhakikishia kuwa kazi ya kukabiliana na tatizo la biashara na matumizi ya dawa za kulevya inaendelea vizuri.

Rogers amesema tatizo la dawa za kulevya lilikuwa kubwa na ametaja dawa za kulevya ambazo Mamlaka inapambana nazo kuwa ni bangi, heroine, cocaine, na kwamba kwa sasa imeanza kukamata na kuharibu mashamba ya bangi na bangi iliyovunwa.

Amebainisha mikakati mitatu inayotumika katika mapambano dhidi ya tatizo hilo kuwa ni kuzuia dawa za kulevya zisiingie nchini, kutoa elimu kuanzia shule za msingi, sekondari, vyuo na kwenye jamii ili watu waache kutumia dawa za kulevya na kutoa tiba kwa watu walioathirika na dawa za kulevya.

No comments: