Wednesday, August 23, 2017

23 August 2017, Mataifa ya kiislam yatakiwa kushirikiana_Rais Erdgan

Rais wa Uturuki Recep Tayyıp Erdoğan ametoa wito kwa mataifa ya kiislamu kuongeza ushirikiano baina yao .

Erdoğan alisema haya akiwa ziarani Jordan katika mji mkuu wa Amman kuadhimisha miaka 70 ya uhusiano wa kidiplomasia baina ya Uturuki na Jordan .

Rais Erdoğan alifahamisha haya akiwa katika mkutano na wajumbe kutoka nchi hizo mbili katika ikulu ya Hussainiah Palace na kusema kuwa kipindi hiki ulimwengu wa kiislamu unapitia wakati mgumu .

Aliendelea usisitiza kwamba ni nyakati hizi ambazo waislamu wanatakiwa kuongeza ushirikiano baina yao .

Awali siku ya Jumatatu rais Erdoğan alikutana na mfalme Abdullah wa Jordan na kuzumgumza kuhusu matukio na mzozo baina ya Israel na Palestina .

Mfalme Abdullah alitoa shukrani za dhati kwa Erdoğan kwa kuendelea kuunga mkono Jordan na pia msimamo wake kuhusu suala la Al Aqsa .

Erdoğan aliahidi kuendelea kushirikiana na Jordan katika juhudi za kulinda hadhi ya mskiti wa Al Aqsa .

No comments: