KABLA HUJANYANYUA MKONO NA KUMPIGA MKE WAKO BASI SOMA MAKALA HII
Niliamka usiku baada ya kusikia kelele za mtoto wangu mkubwa wa miaka tisa. “Baba! Baba! Baba Zack hayupo katoroka! Kaondoka na nguo!” Nilistuka kutoka usingizini na kutoka sebuleni, niligonga kila chumba kumtafuta lakini hakuepo.
Watu wote waliokuepo mule ndani waliamka, ndiyo kwanza tulikua tumemaliza wiki tangu kumzika mke wangu na Zack mwenye umri wa miaka mitano alikua anampenda sana Mama yake hivyo nilijua kuna kitu.
Tulianza kazi ya kutafuta, tukiita huku na kule lakini wapi, mke wangu alikua amezikwa Kijijini hivyo hata mambo ya Polisi kulikua hakuna. Tulitafuta usiku mzima na mpaka asubuhi hatukua tumempata, kila mtu alichanganyikiwa tukihisi labda amejiua au kutoroka kutokana na kifo cha ghafla cha Mama yake.
Asubuhi tukiwaza nini cha kufanya, alikuja mtoto mmoja wa pale Kijijini na kutuambia kua maeona mtoto Kalala makaburini.
Tulikimbia ambapo hakukua mbali sana sema migombani tuliangalia kumkuta Zack katandika nguo chini kalala.
juu ya kaburi lake kalala.
Kila mtu alistuka, tulimsuta, alionekana kuchoka sana na njaa na aliponiona tu alianza kulia huku akishikilia msalaba wa kaburi la Mama yake akisema hawezi kuondoka na kumuacha Mama yake peke yake.
Tulijaribu kumbembeleza lakini wapi, hakutaka kuondoka na hatukutaka kumlazimishia.
Mtoto wangu mkubwa alienda na kukaa pembeni yake, akimuambia kuwa waondoke wamuache Mama apumzike.
Zack alimuuliza “Dada wewe humpendi tena Mama?” alimjibu nampenda na Zack alimuuliza tena, “Sasa kama unampenda mbona unamuacha huku porini peke yake..”
Watu wote walisikitika na mimi machozi yalianza kunitoka, kabla hajajibiwa alisema maneno ambayo yalinifanya nigande kwa mstuko na kushikwa na kigugumizi. “Mimi siwezi kuondoka Dada, tukimuacha Mama peke yake huku porini Baba atakuja usiku na kumpiga atamuumiza kama anavyofanyaga nyumbani.
Baba anatupenda sisi lakini hampendi Mama hivyo anampiga kila siku tukimuacha Mama mwenyewe, sasa tukimuacha huku porini si atakuja kumuua Mama na watu hawatajua, mimi sitaki Mama afe Dada nakaa nae hapahapa mpaka aamke huko chini walikomlaza ili Baba sijempiga..”
Niliumizwa na kifo cha Mke wangu lakini maneno ya mwanangu yalinifanya nijione kama shetani.
Nilianza kukumbuka namna ambavyo Zack kila siku alikua akimganda Mama yake, alikua akitaka kulala na sisi, alikua akitaka kuongozana hata kazini na Mama yake.
Sikujua sababu ya kufanya hivyo, kwani kweli nilikua namnyanyasa na kumtesa mke wangu lakini si mbele za watoto.
Mbele za watoto nilikua Baba bora na sikujua kama wanaona, nilijikuta napiga magoti kuombamsamaha lakini hakutaka kuondoka mpaka Babu mmoja alipokuja na kumuambia tutaleta Polisi wa kumlinda Mama yako.
Wewe bado mdogo, kuna hawa vijana ni Polisi watakaa na mapanga hapa watamlinda Mama yako na Baba yako hatampiga tena. Hapo ndipo alikubali kuondoka.
MOYO WANGU UNAFADHAIKA SANA KWANI MWANANGU HANIAMINI KABISA....Tafadhali SHARE hii ili wababa wajifunze kutowapiga wake zao.
Admit Uhondo planet
No comments:
Post a Comment