Wednesday, August 23, 2017

23 August 2017, Talaka za papo hapo zatangazwa kuwa kinyume na katiba India

Sheria ya kiislamu ya talaka za papo kwa hapo imetangazwa kuwa kinyume na katiba na mahakama kuu nchini India.

Mahakama hiyo imepiga kura 3-2 dhidi ya utamaduni wa kuwa mwanamume anaweza kumpa mke wake talaka kwa kutamka neno "talaka" mara tatu.
Mahamakama inaamini kuwa kitendo hicho ni kinyume na sheria ya kiislamu pia.

Kwa mujibu wa habari,India ni kati ya nchi chache zilizobaki na utamaduni wa kutoa talaka kwa kutamka neno talaka mara tatu.

Matumizi ya talaka hiyo yameongezeka zaidi baada ya ukuaji wa teknolojia kwani wanawake wamekuwa wakipewa talaka kupitia simu za mkononi,barua, meseji na hata kupitia mtandao wa Facebook.

Waziri wa wanawake nchini humo Maneka Gandhi ameunga mkono uamuzi wa mahakama hiyo na kusema kuwa ni wakati wa haki sawa kwa wote.

No comments: