Shirika la chakula duniani WFP limetangaza kukata mgao wa chakula kwa wakimbizi kutoka Congo na Burundi nchini Tanzania.
Kwa mujibu wa habari,shirika hilo limepunguza ugawaji wa chakula kwa wakimbizi 320,000 katika maeneo ya Mtendeli,Nduta na Nyarugusu kaskazini magharibi mwa Tanzania.
Ripoti zinaonyesha kuwa mpaka kufiikia mwezi Desemba WFP inahitaji dola za kimarekani milioni 23.6 ili kuweza kukidhi mahitaji ya wakimbizi Tanzania.
Mwakilishi wa WFP Tanzania Michael Dunford amesema kuwa endapo wafadhili hawatojitokeza kulidhamini shirika hilo basi itawabidi wakate mgao wa chakula haraka iwezekanavyo.
Tanzania ni kati ya nchi yenye idadi kubwa ya wakimbizi kutoka nchi nyingi barani Afrika.
No comments:
Post a Comment