MKEMIA kutoka Ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali, Domician Dominic, ameiambia Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwa dawa aina ya Benzodiazepines iliyokutwa katika sampuli ya mkojo wa aliyekuwa Mwenyekiti wa Yanga, Yusufali Manji, hutumika hospitalini kutuliza maumivu makali ama kumpatia mtu usingizi.
Shahidi huyo wa tatu wa upande wa mashtaka aliyaeleza hayo jana akiongozwa na Wakili wa Serikali Mkuu,Timon Vitalis kutoa ushahidi katika kesi ya kutumia dawa za kulevya aina ya Heroin inayomkabili mfanyabiashara huyo. .
Akitoa ushahidi, Dominic alidai katika uchunguzi wa awali alioufanya katika sampuli ya mkojo wa Manji alikuta una dawa aina ya Benzodiazepines.
Alidai yeye kama Mkemia, kuwepo kwa dawa hiyo kwenye sampuli hiyo ya mkojo kulimpa picha kuwa mtu huyo alikuwa anaitumia kwa kutuliza maumivu makali au kukosa usingizi na kwamba ina matumizi mengi.
Pia alisema kwa uzoefu wake mara nyingi mtu anayetumia dawa hiyo huwa anatumia Heroine ama cocaine.
Manji aliyekana mashtaka anawakilishwa na Mawakili Alex Mgongolwa, Hudson Ndusyepo na Mosses Kimaro.
No comments:
Post a Comment