Rais Dkt. John Magufuli amemuapisha Brigedia Jenerali John Mbungo kuwa Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa -TAKUKURU.
Pamoja na kula kiapo cha kuwa Naibu Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU, Brigedia Jenerali Mbungo amekula kiapo cha uadilifu kwa viongozi wa umma kilichoongozwa na Kamishna wa Maadili Jaji Mstaafu Harold Nsekela.
Akizungumza mara baada ya kiapo hicho Rais Magufuli amewataka viongozi wote nchini kushirikiana kupambana na rushwa ili kuepusha madhara ya tatizo hilo katika uchumi na ustawi wa jamii.
Rais Magufuli ameipongeza TAKUKURU kwa kazi iliyoanza kuifanya na kuitaka kuongeza juhudi ili watu wote wanaojihusisha na vitendo vya kutoa na kupokea rushwa washughulikiwe kwa mujibu wa sheria.
No comments:
Post a Comment