Monday, July 31, 2017

31 july 2017, Bolt kuuaga ulimwengu wa riadha

Anafahamika kwa kutimka kwa kasi ya radi! Usain Bolt ambaye anajiandaa kushiriki mashindano yake ya mwisho kabisa ya ubingwa wa Dunia yatakayoandaliwa jijini London kuanzia Agosti nne hadi 13.

Mahasimu wa Bolt watakuwa, kwa mara ya kwanza, na furaha kumwona akiondoka mtu ambaye ametawala mbio za masafa mafupi duniani kwa mwongo mmoja uliopita, lakini mchezo wa riadha hautakuwa na shauku kuhusu kumpa kwaheri ya mwisho Mjamaica huyo.

Bolt alitawala katika michezo mitatu ya mwisho ya Olimpiki na kama hangeondolewa kabla ya fainali ya mita 100 mjini Daegu mwaka wa 2011, mwanariadha huyo mwenye umri wa miaka 30 angeweza kutawala michezo minne ya mwisho ya Olimpiki.

Sasa swali ni je, nani ataweza kuchukua nafasi yake juu ya jukwaa la mbio za mita 100? Bingwa wa zamani wa Olimpiki na dunia Justion Gatlin, anatoa maoni yake "Yatakuwa mashindano ya kufurahisha zaidi kwa sababu ni wakati maalum sio kwangu tu na Usain Bolt lakini kuna wanariadha wengine wengi vijana ambao wanachipuka.

Nadhani hicho ndio kitakachokuwa maalum kuhusu sio tu nani atakayeweza kujaza pengo katika mchezo wetu lakini litajazwa na wanariadha vijana ambao wapo kwa sasa na wanataka kujitengenezea jina hivyo utakuwa wakati wa kusisimua na wa mabadiliko kwa wengi".
Na je, Gatlin anasemaje kuhusu kuwa na fursa ya mwisho kumpiku Usain Bolt katika mashindano ya London? "sitoshiriki na mawazo hayo. sitoshiriki kwa ajili ya kujifurahisha tu. Najaribu hasa kuweka pamoja Justin wawili ambapo nataka tu kushiriki kwa kufurahia kama tu iliyvokuwa chuoni na bado niweze kutawala lakini pia nataka kushiriki kwa kuangazia wakati maalum ambao ni wa mabadiliko ya kihistoria.

Hivyo utaona kiasi mambo hayo yote mawili. Ntakwenda tu kuwa na wakati mzuri.

Bolt atastaafu baada ya mashindano ya London na hivyo kuwapa nafasi wanariadha wengine chipukizi kujaribu kuvaa viatu vyake.

Lakini kama mwanariadha yeyote anaweza kukaribia kuifikia rekodi ya Bolt na haiba yake ni suala jingine tofauti.

31 july 2017, Misukosuko yazidi Venezuela baada ya uchaguzi wa jana

Watu 10 wameuwawa nchini Venezuela wakati wa kupiga kura ya kulichagua bunge maalum la kuibadilisha katiba ya nchi hiyo. Marekani na nchi zingine kadhaa zasema hazitayatambaua matokeo ya uchaguzi huo.

Tume ya uchaguzi nchini Venezuela imesema watu wapatao milioni nane ikiwa ni asilimia 41.53 wameshiriki katika zoezi la kupiga kura. Raia hao wamepiga kura yenye utata ya kulichagua bunge maalum litakalo ibadilisha katiba ya nchi hiyo.

Hata hivyo uchaguzi huo kwa kiwango kikubwa ulisusiwa na baadhi ya wananchi na uligubikwa na ghasia zilizosababisha mauaji.

Kwa mujibu wa habari watu wasiopungua kumi waliuwawa katika mji mkuu wa Caracas na sehemu nyingine za nchi hiyo.
Vyama vya upinzani vinalalamika na kusema kuwa uchaguzi huo ulijawa na visa vya kuiba kura na kwamba kura hiyo ina lenga kumuongezea mamlaka rais Nicholas Maduro.

Kiongozi wa wapinzani Henrique Capriles ambaye pia ni gavana wa jimbo la kati la Miranda amesema harakati za upinzani zitafanyika leo katika mji mkuu wa Venezuela, Caracas ili pia kuwakumbuka watu walio uwawa wakati waliposhiriki kwenye maandano ya kuipinga serikali ya rais Maduro.

Waandalizi wa maandamano ya wapinzani wamesema watu 15 waliuwawa wakati wananchi walipokuwa wanapiga kura hapo jana. Ofisi ya mwendesha mashtaka mkuu imethibitisha kwenye mtandao wa Twitter kwamba inachunguza vifo visivyopungua saba.

Wapinzani wanawalaumu viongozi wa serikali ya Venezuela kwa umwagikaji damu lakini
Waziri wa ulinzi wa Venezuela Jenerali Vladimir Padrino Lopez amesema jeshi la Venezuela halina lawama juu ya vifo vilivyotokea na ametowa mwito kwa ulimwengu uheshimu maamuzi ya raia wa nchi hiyo.

Rais wa Marekani Donald Trump amesema anatafakari kuiwekea Venezuela vikwazo katika sekta ya nishati. Vikwazo hivyo vitaiathiri kampuni ya mafuta ya Venezuela (PDVSA) ambayo tayari ni dhaifu.

Mpaka sasa watu zaidi ya 120 wameshauwawa katika kipindi cha miezi minne iliyopita kutokana na mvutano baina ya wapinzani na serikali ya rais Nicholas Maduro .

Rais Maduro amesema uchaguzi huo una lengo la kuutatua mgogoro wa kiuchumi na kisiasa nchini Venezuela, lakini wapinzani wa serikali wanasema kura hiyo itaua demokrasia katika taifa hilo la Kusini mwa Amerika. Marekani,Uingereza, Colombia, Mexico,Panama,Peru,Uhispania, Canada na mashirika kadhaa ya kimataifa yamesema hayatotambua matokeo ya kura hiyo.

Rais Maduro aliitisha kura hiyo baada ya serikali yake kukumbwa na upinzani mkubwa hatua ambyao imeitumbukiza Venezuela katika mzozo katika kipindi cha miaka minne ya uongozi wake.

Mshirika muhimu wa Rais Maduro Diosdado Kabello amesema wananchi wengi walishiriki katika kupiga kura hapo jana na kwamba wapinzani wanaodai kwamba ni watu wachache tu walioshiriki watashangaa.

31 july 2017, Mataifa ya Ghuba yasema yako tayari kuzungumza na Qatar

Mataifa manne ya Kiarabu yaliovunja uhusiano na Qatar yamesema yako tayari kwa mazungumzo ya kutatua mzozo huo ikiwa Doha itaonyesha nia ya kushughulikia madai yao.

Qatar imesema huo ni upotoshaji wa jamii ya kimataifa.

Kundi la mataifa hayo linaloongozwa na Saudi Arabia lilikata mahusiano na Qatar Juni 5, wakiituhumu kwa kuyaunga mkono makundi ya wanamgambo na kushirikiana na hasimu wao mkuu wa kikanda Iran, madai ambayo serikali mjini Doha inayakanusha vikali.

Juhudi za kidiplomasia za Kuwait na zinazoungwa mkono na mataifa ya magharibi zimeshindwa mpaka sasa kukomesha mzozo huo, ambao unahusisha kuwekewa vikwazo vya usafiri na mawasiliano Qatar na mataifa hayo manne.

Wasema Qatar haina ni ya kusuluhisha
Saudi Arabi na washirika wake awali walitoa orodha ya madai 13 kwa Qatar, ambayo yanahusisha kuitaka nchi hiyo kukomesha uungaji wake mkono kwa kundi la Udugu wa Kiislamu, kufunga kituo cha Televishen cha Al Jazeera chenye makao yake mjini Doha, kufunga kambi ya kijeshi ya Uturuki, na kushusha kiwango cha uhusiano na adui wa mataifa ya Ghuba Iran.
Waziri wa mambo ya nje wa Saudi Arabia Adel Al-Jubeir alisema Qatar haikuwa na nia ya kutekeleza matakwa hayo. "Tuko tayari kuzungumza na Qatar kuhusu utekelezaji wa matakwa, kuhusu utekelezaji wa kanuni, ikiwa Qatar ina nia, lakini imekuwa dhahiri kwamba haiko tayari," alisema waziri huyo katika mkutano na waandishi wa habari.

Mataifa hayo manne pia yameorodhesha kanuni sita wanzotaka Qatar itekeleze. Waziri wa mambo ya nje wa Qatar Sheikh Mohammed bin Abdurlrahman Al-Thani alipinga tamko la Jumapili kutoka kwa mataifa hayo na kusema vikwazo walivyoikwekea nchi yake vinakwenda kinyume na sheria za kimataifa.

Al-Thani alisema katika mahojiano na kituo cha Al Jazeera kwamba hakukuwa na dira ya wazi kutoka mkutano wa Manama, na kwamba kilichopo ni sera korofi kutoka mataifa yanayoizingira nchi yake na kukataa kwao kukiri kuwa hatua hizo ni haramu. Mapema Jumapili, gazeti la la al-Hayat lilisema likizinukuu duru zisizotajwa kutoka Ghuba, kwamba mataifa hayo manne yalitarajiwa kuweka vikwazo ambavyo taratibu vitaathiri uchumi wa Qatar.

Malumbano kuhusu Mahujjaji wa Qatar

Saudi Arabia imefunga mpaka wake wa nchi kavu na Qatar, huku mataifa yote manne yakikata mawasiliano ya angani na baharini na Doha, wakiitaka nchi hiyo inayosafirisha nishati ya gesi kwa wingi kuchukuwa hatua kadhaa kuonyesha inabadilisha sera zake.

Qatar imeituhumu Saudi Arabia kwa kuhatarisha safari ya hijja kwa raia wake kwa kukataa kuwahakikisha usalama wao.

Julai 20 Saudi Arabia ilisema Waqatari wanaotaka kufanya hijja mwaka huu wataruhusiwa kuingia nchini humo, lakini ikaweka masharti fulani. Wizara ya Hajji ya Saudia ilisema Mahujjaji wa Qatar wanaowasili kwa ndege laazima watumie zinazokubaliana na Riyadh.

Pia watapaswa kuomba viza waakti wa kuwasili Jedda au Madina, ambavyo ndiyo vituo pekee kwao kuingilia katika taifa hilo la Kifalme. Kwa mujibu wa taarifa ya wizara ya masuala ya Kiislamu ya Qatar, raia 20,000 wa nchi hiyo wamejiandikisha kushiriki katika ibada ya hijja mwaka huu.

31 july 2017, Tetesi za soka Ulaya michezoni leo Jumatatu

Jose Mourinho amesema Nemanja Matic, 28, "anataka sana" kuondoka Chelsea na kujiunga na Manchester United. Tayari United wamekubali kutoa pauni milioni 40 na wanatarajia kukamilisha usajili huo siku chache zijazo. (Sky)

Beki wa kulia wa Paris Saint-Germain Serge Aurier amekubali kujiunga na Manchester United, kwa mujibu wa taarifa kutoka Ufaransa. Mchezaji huyo wa kimataifa wa Ivory Coast ameruhusiwa kuondoka na meneja Unai Emery. (Sky Sports)

Alexis Sanchez anafikiria kuwasilisha ombi la kuondoka Emirates ili kulazimisha uhamisho wake kwenda Manchester City. Sanchez anataka sana kuondoka, na Pep Guardiola yuko tayari kufanikisha usajili wake. Sanchez anataka mshahara wa pauni 400,000 kwa wiki, na Arsenal wako tayari kutoa 300,000. (Daily Mirror)

Southampton wana matumaini kuwa Virgil van Dijk atabadili mawazo na kurejea mazoezini na kikosi cha kwanza wiki hii. Southampton hawataki kumuuza beki huyo anayenyatiwa na Liverpool. (Daily Echo)

Barcelona huenda wakaamua kumgeukia Mesut Ozil, 28, iwapo watashindwa kumpata kiungo wa Liverpool Philippe Coutinho. Huku hatma ya Neymar kwenda PSG ikiwa inazungumzwa, Barca wanatafuta mchezaji wa kuziba pengo lake. (Don Balon)

Cristiano Ronaldo hataki Real Madrid imnunue Kylian Mbappe kwa sababu huenda kinda huyo 'akamfunika' na kuathiri nafasi ya kushinda Ballon d'Or. (Diario Gol)

Matumaini ya Liverpool kumsajili Naby Keita yanazidi kupata wakati mgumu baada ya Inter Milan nayo kuingia katika harakati za kumtaka kiungo huyo. (CalcioMercato)

Arsenal na Tottenham wamepeleka maskauti wao kumtazama mshambuliaji kinda wa Caen, Yann Karamoh, ambaye ametajwa kuwa kama "Kylian Mbappe mwingine". Chipukizi huyo anafuatiliwa pia na Forentina na AC Milan na Inter Milan. (Sunday Mirror)

Chelsea wanapanga kutaka kumchukua kinda wa Celtic, Karamoko Dembele, 14. (The Sun)

Kiungo wa Everton Ross Barkley atalazimika kupunguza mshahara anaotaka iwapo anataka kujiunga na Tottenham ambao wapo tayari kumlipa pauni 120,000 kwa wiki, sawa na ambazo amezikataa Everton. (Mirror)

Everton watashikilia bei ya pauni milioni 35 kumuuza Ross Barkley licha ya kuwa mkataba wake utamalizika baada ya mwaka mmoja. (Mail)

Barcelona watawashitaki PSG kwa UEFA kwa kukiuka kifungu cha fedha hata kama hawatolipa pauni milioni 197 za kutengua kifungu cha uhamisho cha Neymar. (El Larguero)

PSG wana uhakika wa kumsajili Neymar, na tayari wanapanga jinsi ya kumtambulisha mchezaji huyo kwa mashabiki. (ESPN)

West Brom wanamtaka beki wa zamani wa Arsenal, Thomas Vermaelen, 31, ambaye alihamia Barcelona miaka mitatu iliyopita. (Sky Sports)

Meneja wa Bacelona Ernesto Valverde anataka kumpa namba Thomas Vermaelen msimu huu baada ya kufurahishwa na kiwango alichoonesha kwenye mechi za kujipima nguvu. (AS)

Wachezaji wa Manchester City wanazungumzia waziwazi kuwasili kwa Alexis Sanchez kutoka Arsenal kwa mkataba wa pauni milioni 50. (Manchester Evening News)

Meneja wa Arsenal, Arsene Wenger amesema wachezaji kama Alexis Sanchez na Mesut Ozil ambao wanaingia katika mwaka wa mwisho wa mikataba yao ndio "wazuri zaidi" kwa sababu watataka kuonesha kiwango cha juu. (Sun)

Meneja wa Manchester United Jose Mourinho hana mpango wa kumtoa kwa mkopo kiungo Andreas Pereira, 21, baada ya mchezaji huyo kuonesha kiwango katika mechi za kujipima nguvu. (Sun)

31 july 2017, Akatwa miguu usingizini bila damu kutoka

Mzee mmoja anayejulikana kwa jina la Yohana Mkwera mkazi wa wilaya ya Ludewa, alishangaza jamii inayomzunguka huku mwenyewe akipigwa na butwaa, baada ya kuamka asubuhi na kukuta miguu yake ikiwa imekatwa na kuwekwa pembeni, bila kumjua aliyemkata.

Akisimulia tukio hili ambalo lilitokea miaka kadhaa nyuma, Bw. Yohana amesema alishangazwa kuamka na kuikuta miguu yake pembeni , bila yeye kuwa na tone hata la damu mwilini wake wala maumivu, huku akihisi ni nguvu za giza na kumhisi jirani yake ambaye anamshuku alimuibia baiskeli yake.

Naye rafiki yake wa karibu bwana Clemence Lugongo amemsimulia bwana Mkwera amesema sehemu kubwa ya tukio lililomtokea bw. Mkwera ni la ajabu na mpaka sasa chanzo cha kukatika miguu kwa rafiki yake huku akihitaji wadau kujitokeza kumpatia msaada.

Hata hivyo Bw. Mkwera anaomba msada wa baiskeli ya kutembelea, baada ya miguu ya bandia aliyowahi kupewa kuchakaa.

31 july 2017, Serikali kumaliza adha ya maji Mbeya

Serikali imedhamiria kumaliza tatizo la upatikanaji majisafina salama katika maeneo mbalimbali nchiniikiwemo wilaya ya Rungwe mkoaniMbeya ambayo imetengewa sh.bilioni2.72kwa ajiliya ujenziwa miradiya maji.

Kaulihiyo imetolewa na WaziriMkuu Kassim Majaliwa wakatiakizungumza kwa nyakatitofauti na wananchiwa Halmashauriza Rungwe na Busokelo katika mikutano ya hadhara aliyoifanya Kandete na Tandale mkoaniMbeya.

WaziriMkuu amesema mkakatihuo unatekelezwa kupitia Kampeniya Rais Dkt.John Magufuliya kumtua mama ndoo kichwani,wananchikatika maeneo yote nchiniwatapata huduma ya maji safina salama katika umbaliusiozidimita 400 kutoka kwenye makaziyao.

WaziriMkuu alitaja mradimwingine unaotekelezwa wilayaniRungwe kuwa nipamoja na mradiwa majiwa Masoko wenye thamaniya sh.bilioni5.3,utakaohudumia jumla ya vijiji15. “Mradihuu nimiongonimwa miradiinayojengwa chiniya Programu ya Maendeleo ya Sekta ya Maji kwa fedha za ndani.” alisema WaziriMkuu.

Mradihuo utakapokamilika utawanufaisha wananchiwapatao 19,624katika vijijivya Bulongwe,Ngaseke,Igembe,Ntandabala, Lupando,Bujesi,Lufumbi,Nsyasa,Ikama,Itagata, Busisya,Mbaka,Isabula,Lwifa na Nsanga.

31 july 2017, Mafuriko yaua 3 na kuacha 140,000 bila makao Myanmar

Watu 3 wamefariki na wengine 140,000 kuachwa bila makao nchini Myanmaar baada ya mvuaa kubwa kunyesha nchini humo.

Mafuriko hayo yameripotiwa kuathiiri zaidi maeneo ya Sagaing, Magwe, Bago na Ayeyarwady .

Aidha shule 200 zimefungwa kwa muda na kuathiri takriban wanafunzi 25,000.

Taasisi ya masuala ya hali ya anga imeonya kwamba kwa bahati mbaya hali hiyo itaendelea katika siku za mbeleni kufuatia kuendelea kunyesha kwa mvua hiyo.

31 july 2017, Shambulio lawaua watu 6 Mogadishu

Watu sita wameuawa katika mlipuko wa bomu mjini Mogadishu Somalia na wengine 10 wamejeruhiwa.

Katika tukio jingine kusini magharibi mwa Mogadishu, wapiganaji wa Al Shabaab wanadai kuwaua maafisa wengi wa kikosi cha muungano wa Afrika - AMISOM.

Msemaji wa kikosi cha walinda amani wa Umoja wa Mataifa nchini Somalia (AMISOM) amethibitisha kuwepo mapigano lakini haukubaini ni wanajeshi wangapi wameuawa au kujeruhiwa.

Bomu la kutegwa ndani ya gari lililipuka dakika chache nje ya maduka dakika chache baada ya saa tano katika mtaa wenye shughuli nyingi katika mji huo mkuu.

Walioshuhudia wanasema ulikuwa mlipuko mkubwa sana na kwamba watu wengi walikufa ama kujeruhiwa.

Mashambulio haya yanakuja baada ya wiki kadhaa za utulivu katika mji mkuu Mogadishu kufuatia mashambulio ya hapa na pale ya kundi la Al-Shabaab.

Katika tukio jingine tofauti vikosi vya Muungano wa Afrika vilikabiliana na wanamgambo wa Alshaabab katika mkoa wa Lower Shabelle yapata kilomita 140 kusini magharibi mwa mji huo mkuu.

Kundi la Al-Shabaab limesema liliwauwa askari 39 katika shambulio la kuvizia, lakini idadi hiyo haijathibitishwa na vyanzo huhu vya habari.

31 july 2017, Naibu Waziri wa elimu atoa agizo

Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi Mhandisi Stella Manyanya amemuagiza msimamizi wa ukarabati wa shule ya Sekondari Kantalamba kuhakikisha kuwa walemavu wanajengewa vyoo vyao ndani ya mabweni wanamolalia nia ikiwa ni kujiepusha na kuwaamsha wenzao usiku pindi wanapotaka kwenda chooni.

Mhandisi Manyanya ametoa agizo hilo muda mfupi baada ya kufanya ukaguzi wa ukarabati wa shule hiyo iliyopo Wilayani Sumbawanga iliyopewa shilingi Bilioni 1.1 ikiwa ni mpango wa serikali wa kuzirudishia hadhi shule kongwe nchini huku shule hiyo ikiwa ni ya tangu 1964.

“Lazima muhakikishe kwamba mnakuwa na vyumba maalum kwa ajili ya wanafunzi wenye ulemavu na kuwawekea miundombinu hasa kwa wale walemavu ambao mazingira yao ni magumu zaidi, kwa mfano mwanafunzi ana ulemavu wa miguu na anatakiwa kwenda chooni hapaswi kutambaa kwenye mikojo ya wanafunzi wenziwe hii inawapelekea wao kuwa katika mazingira hatarishi zaidi,” amesema Manyanya.

Mbali na agizo hilo Mhandisi Manyanya ametoa wiki tatu ukarabati wa shule hiyo kumalizika baaada ya muda waliopangiwa kumalizika huku kipaumebele kikiwa ni kuhakikisha wanafunzi wanaendelea na masomo yao katika hali ya utulivu.

“Sijaridhishwa na kasi ya ukarabati huu hivyo tumewaongezea wiki tatu mhakikishe mnamaliza ili wanafunzi waendelee na masomo maana yake kama mngekuwa hamwezi kumaliza kwa wakati kwanini msingesema mapema", amesisitiza Manyanya.

Kwa upande mwingine, Mhandisi Manyanya amewasisitizia wanafunzi wa shule hiyo kuwa nia ya serikali ya awamu ya tano ni kuhakikisha kuwa hakuna tofauti kati ya shule za serikali na za binafsi kuanzia huduma za majengo, elimu mpaka vifaa vya kusomea.

31 july 2017, Aveva, Kaburu wapigwa kalenda

Kesi inayowakabili viongozi wa nafasi za juu klabu ya Simba Evans Aveva na Geofrey Nyange 'Kaburu' imehairishwa mpaka Agosti 7 mwaka huu ambapo watarudishwa tena mahakamani kusomewa mashtaka yao.

Uamuzi huo umetolewa na Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama ya Kisutu Jijini Dar es Salaam, Victoria Nongwa ambapo washtakiwa hao wanakabiliwa na mashtaka matano ambayo mawili kati ya hayo ni ya kutakatisha fedha.

Viongozi hao walikamatwa na TAKUKURU mwezi uliyopita wakikabiliwa na mashitaka ya kutakatisha fedha mpaka kupelekea kunyimwa dhamana.

Chanzo Eatv

31 july 2017, Matokeo ya kura yatarajiwa kutangazwa Senegal

Kura zimekwishapigwa nchini Senegal huku televisheni ya umma ikiripoti kuwa asilimia 54 ya raia wa nchi hiyo wamejitokeza kupiga kura.

Rais wa zamani wa nchi hiyo, Abdoulaye Wade, amemshutumu rais wa sasa anayewaniwa muhula mwingine, Rais Macky Sall, kwa wizi wa kura, akisema kuwa baadhi ya maeneo yalikuwa bado hayajapokea karatasi za kupigia kura.

Polisi imesema wajumbe watatu wa muungano wa Bwana Wade walikamatwa kwa kufanya vurugu kwenye vituo vya kupigia kura.
Rais Sall anatafuta wingi wa viti katika chama chake.

Abdoulaye Wade amethibitisha kuwa muunngano wa vyama vidogo vidogo unamuandaa mtoto wake wa kiume Karim kuwania urais mnamo mwaka 2019.

Mgombea mwingine ni meya wa mji mkuu wa Senegal , Dakar, ambaye yuko gerezani kwa mashtaka ya ubadhilifu wa mali ya umma.

Matokeo ya awali yanatarajiwa kutangazwa Jumatatu asubuhi.

31 july 2017, Watu kadhaa waokolewa baada ya magari ya angani kukwama Ujerumani

Watu kadhaa walibaki wamekwama hewani baada ya gari la angani la kutumia nyaya kugonga nguzo na kusimama juu wa mto Rhine nchini Ujerumani.

Wazima moto na makundi ya waokoaji mjini Cologne walitumia kreni kuwafikia abiria 75 waliokuwa wamekwama baadhi ambao waliripotiwa kuwa umbalia wa hadi mita 40 angani.

Picha zilionyesha watoto wakishushwa ardhini lakini hakuna majeruhi walioripotiwa.
Magari yote 32 yaliyokuwa yakihudumu waki huo yalisimama wakati ajali ilitokea.

Sunday, July 30, 2017

30 july 2017,Samatta afungua msimu kwa kucheka na nyavu

Nahodha wa timu ya taifa ya Tanzania (Taifa Stars) Mbwana Ally Samatta jana Jumamosi alikuwa na kibarua cha kuitumikia timu yake ya KRC Genk katika mechi yao ya kwanza wa Ligi Kuu Ubelgiji msimu wa 2017/18 dhidi ya Waasland Beveren.

Samatta aliifungia timu yake goli la pili katika dakika ya 80 na kutoa 'assist' ya goli la 3 ambapo lilifanya mchezo huo kumalizika kwa sare ya 3-3.

Magoli ya Genk yakifungwa na Jose Naranjo dakika ya 70, Mbwana Samatta dakika ya 80 na dakika ya 82 Shrivjers akafunga goli la mwisho.

Klabu ya KRC Genk ilicheza game yake ya kwanza katika uwanja wake wa nyumbani dhidi ya Waasland Beveren na kulazimishwa sare hiyo ya kufungana magoli 3-3.

30 july 2017, Trump aikosoa China kwa kutoichukulia hatua Korea Kaskazini

Rais wa Marekani Donald Trump amekosoa Uchina kwa kukosa kuchukua hatua madhubuti za kuhakikisha kuwa Korea Kaskazini inasitisha mipango yake ya silaha za nuklia.

Maoni yake yamechapishwa kwenye mtandao wa twitter siku moja baada ya Korea Kaskazini kufyatua kombora lake la pili linaloweza kusafiri kutoka bara moja hadi jingine mara ya pili chini ya muda wa mwezi mmoja.

Korea Kaskazini baadaye ilidai kuwa jaribio hilo linaonyesha kuwa silaha zake zinaweza kuishambulia Marekani.

Bwana Trump alisema amesikitishwa sana na Uchina na kuapa kuwa hataruhusu hali hii kuendelea.

Mnamo Jumamosi Uchina ilieleza masikitiko yake makubwa kuhusiana na kufyatuliwa kwa kombora hilo Korea Kaskazini

30 july 2017, NEC yatoa ufafanuzi kuhusu uteuzi wa wabunge CUF

Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imefafanua juu ya uteuzi wa wabunge wapya wa Viti Maalumu wa Chama cha Wananchi (CUF).

Imesema kuwa imesikitishwa na kushangazwa na taarifa za Baraza Kuu la Taifa la chama hicho kwamba tume hiyo imekiuka kanuni zake katika uteuzi wa wabunge wanane wa chama hicho ili kujaza nafasi za wazi zilizotokea hivi karibuni.

Aidha, imesema chama husika kilipewa fursa ya kupendekeza na kilifanya hivyo, kabla ya NEC kuanika majina ya wabunge wapya wa CUF katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Hayo yamo katika taarifa ya Mkurugenzi wa Uchaguzi wa NEC, Kailima Ramadhani aliyoitoa jana jioni, akizungumzia tuhuma dhidi ya tume hiyo, inayodaiwa kukiuka kanuni katika uteuzi wa wabunge wanane wa viti maalumu wa CUF.

Sehemu ya Taarifa ya CUF katika mitandao ya kijamii inayoituhumu NEC inasema; “Kanuni walizojiwekea wenyewe Tume katika uteuzi wa watu wa kujaza nafasi hizo zinasema uteuzi huo unafuata mpangilio wa majina, kama ulivyokuwa umewasilishwa na chama husika wakati wa uteuzi wa wagombea wa ubunge wa viti maalumu wakati wa uchaguzi mkuu uliopita.

“CUF ilipeleka orodha yake ambayo haihusishi majina yaliyotangazwa, hivyo ndiyo kusema hata kama hicho kinachoitwa kufukuzwa uanachama wabunge hao kingekuwa halali (jambo ambalo si halali kama ilivyokwishaelezwa hapo juu), basi kwa Kanuni za Tume yenyewe, watu wa kujaza nafasi hizo wasingekuwa hao waliotangazwa.”

Kailima, katika taarifa yake, alisema taarifa zinazotolewa katika mitandao zikihusisha NEC kukihujumu chama hicho ni za kushangaza na kwamba Baraza Kuu la Uongozi la CUF, linataka kuupotosha umma kuhusu utekelezaji wa kazi za Tume.

“Chama husika ndicho kinaweza kujua ni nani siyo mwanachama wa chama hicho kwa kipindi cha kujaza nafasi wazi inapotokea,” alieleza Kailima na kuongeza kuwa, kwa mujibu wa majina manane yaliyopendekezwa na CUF kujaza nafasi wazi za wabunge wa viti maalumu ni miongoni mwa majina 55 yaliyowasilishwa na chama hicho kwa barua yenye kumbukumbu Namba CUF/AK/DSM/ KM/003/1A/2015/14 ya Septemba 28, 2015 iliyosainiwa na Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Shariff Hamad.

30 july 2017, Waziri Mkuu Azindua Meli mbili zilizonunuliwa na Serikali Mkoani Mbeya

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amezindua Meli mbili za mizigo za Mv Njombe na Mv Ruvuma zitakazotumika katika kusafirishia mizigo kwenye Ziwa Nyasa na kuonya kwamba zisitumike kama eneo la kuvushia wahamiaji haramu na dawa za kulevya.

Amesema kuwa kukamilika kwa ujenzi wa Meli hizo zilizogharimu sh. bilioni 11.253 ni utekelezaji wa ahadi ya Rais Dkt. John Magufuli alizozitoa ikiwa na lengo la kutatua changamoto ya usafiri wa abiria na mizigo katika Ziwa Nyasa.

Amesema kuwa ni jambo la faraja na la kujivunia kwa Serikali na wananchi kwa pamoja kushuhudia meli zilizotengenezwa na Mtanzania, zikiwa zimekamilika tayari kwa kuanza kazi ya kuwahudumia wananchi, ambapo awali suala hilo lilikuwa likifanywa na raia wa kigeni.

Waziri Mkuu amezindua meli hizo zilizojengwa na kampuni ya Kitanzania ya M/S Songoro Marine Transport jana katika bandari ya Kiwira wilayani Kyela akiwa katika ziara yake ya kikazi mkoani Mbeya.

Aidha, alisema kuwa Meli hizo zitumike katika kukuza uchumi wa wananchi kwa kusafirisha mizigo na biashara halali kati ya nchi za Tanzania na Malawi na zisitumike kama eneo la kuingiza wahamiaji haramu pamoja na dawa za kulevya nchini.

“Changamoto ya usafiri wa mizigo katika ziwa Nyasa itakuwa historia kwani meli hizi zitarahisisha usafiri na kupanua wigo wa biashara kati ya Tanzania nan chi za Malawi na Msumbiji, hivyo tunamshukuru Mheshimiwa Rais Dkt. Magufuli kwa kutoa ahadi hii ambayo leo utekelezaji wake umekamilika.”

Kwa upande wake, Naibu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) anayeshughulikia Miundombinu, Mhandisi Karim Mataka alisema kuwa ujenzi wa meli hizo ulianza Juni 2015 na zina uwezo wa kubeba tani 1,000 za mizigo kwa kila moja.

30 july 2017, Mkutano wa dharura wa muungano wa kiislam kwa ajili yaAl Aqsa


Uturuki yaitisha mkutano wa dharura wa muungano wa kiislamu kwa ajili y'a Al Aqsa

Mkutano huo umetokea wito n'a Uturuki ili kujadili matukio katika mskiti wa al aqsa ambao umekumbwa n'a matukio tofauti Siku zilizopita.

Mkataba huo unatarajiwa kufanyika ifikapo Agosti mosi jijini Istanbul.

Taarifa zlizotolewa n'a ofisi ya wWaziri wa mambo ya nje wa UturukiA Mevlüt Çavuşoğlu zilifahamisha Kuwa Uturuki kama mwenyekiti wa mpito wa muungano huo imeomba mkutano huo wa dharura ili kuzungumzia halı inavyonukia Jerusalem

Saturday, July 29, 2017

29 july 2017, Mwanamume avamia duka na kuua mmoja Ujerumani

Mwanamume mmoja ameripotiwa kuvamia duka kubwa "supermarket" na kumchoma mwanamume mmoja kisu wakati watu wakihemea vitu mjini Hamburg nchini Ujerumani

Mwanamume mmoja ameripotiwa kuvamia duka kubwa "supermarket" na kumchoma mwanamume mmoja kisu wakati watu wakihemea vitu mjini Hamburg nchini Ujerumani.

Kwa mujibu wa habari,mtu huyo aliyechomwa kisu alifariki papo hapo huku wengine 6 wakiwa wamejeruhiwa vibaya.

Mwanamume huyo alikamatwa na polisi pale alipotaka kukimbia.Raia wa Uturuki mwenye umri wa miaka 35 ameripotiwa kusaidia katika kumkamata mshambuliaji huyo.

.Polisi wanaamini kuwa mshambuliaji huyo ni raia wa Emirates mwenye umri wa miaka 26.

Hata hivyo uchunguzi zaidi kuhusu shambulizi hilo unazidi kufanyika.
Tagi:

29 july 2017, Mitambo mitatu ya nyuklia kutumika mwaka 2030 Uturuki

Waziri wa nishati na mali ya asili wa Uturuki asema kuwa Uturuki inataraji kuzindua mitambo mitatu ya nyuklia ifikapo mwaka

Waziri wa nishati na mali ya asili wa Uturuki asema kuwa Uturuki inataraji kuzindua mitambo mitatu ya nyuklia ifikapo mwaka 2030

Waziri wa mali ya asili na nishati wa Uturuki Berat Albayrak amesema kuwa Uturuki inataraji kuzindua na kutumia mitambo yake yake mitatu ya uzalishaji wa nguvu za nyuklia  hadi ifikapo mwaka 2030.

Waziri Berat Albayrak katika miezi mitatu ya mwisho ya mwaka 2017 Uturuki itajipatia mashua yake binafsi itakayoshuhulika na uchimbaji mafuta na gesi asilia.

Hayo waziri wa nishati na mali ya asili wa Uturki aliyafahamisha akiwa katika mkutano Ijumaa uliaondaliwa mjini Istanbul kuhusu nishati na madini.

29 july 2017, TETESI ZA SOKA MICHEZONI LEO JUMAMOSI

Mshambuliaji wa Barcelona Neymar, 25, amekubali kusaini mkataba wa miaka mitano kujiunga na Paris Saint-Germain na huenda akakamilisha uhamisho wa pauni milioni 197 wiki ijayo. (RMC)

PSG watawapa Barcelona Angel Di Maria, 29, kama sehemu ya mkataba wa kumsajili Neymar, ili kupunguza kodi ya kutengua kifungu cha uhamisho cha mchezaji huyo wa Brazil. (AS)

Iwapo Neymar ataondoka, Barcelona wataamua kuwawinda wachezaji watatu kutoka EPL- Philippe Coutinho, 25, wa Liverpool, Eden Hazard, 26, wa Chelsea, na Delle Alli, 21 wa Tottenham kuziba pengo. (Mirror)

Barcelona wana wasiwasi kuwa bei kubwa ya kumsajili Philippe Coitinho kutoka Liverpool huenda ikawakatisha tamaa. (AS)

Kiungo wa Barcelona Andres Inisesta, 33, amesema ni Neymar pekee anayeweza kuzungumzia kuhusu hatma yake, akisema hadhani kama euro milioni 200-300 zina manufaa yoyote kwa klabu bila Neymar mwenyewe. (Marca)

Monaco wanasisitiza kuwa hawatamuuza Thomas Lemar, 21, licha ya Arsenal kupanda dau la tatu la takriban pauni milioni 45 kumtaka kiungo huyo. (Telegraph)
Manchester City watampa Alexis Sanchez, 28, mshahara wa pauni 320,000 kwa wiki akijiunga nao kutoka Arsenal. (Mail)

Kipa wa Manchester City Claudio Bravo amesema Alexis Sanchez atapokelewa kwa mikono miwili akiamua kwenda Etihad. Bravo na Sanchez wote wanachezea timu ya taifa ya Chile. (24 Horas)

Southampton wamedhamiria kutomuuza beki wao Virgil van Dijk, 26, na watamrejesha katika kikosi cha kwanza licha ya kuachwa katika kikosi kilichokwenda mazoezini Ufaransa wiki hii (Telegraph)

West Ham watakataa dau lolote la kumtaka kiungo mshambuliaji wake Manuel Lanzini, 24. (Evening Standard)

Swansea wanakabiliwa na ushindani kutoka Leeds United katika kumsajili Alvaro Negredo, 31, aliyecheza kwa mkopo Middlesbrough msimu uliopita. (Mirror)

Manchester United wamenza mazungumzo ya mkataba mpya na Ander Herera, 27, ili kuzuia Barcelona kumnyatia kiungo huyo. (Express)

Manchester United wamerejea tena katika kumfuatilia winga wa Inter Milan Ivan Perisic, 28, lakini wana wasiwasi huenda wakamkosa kwa kuwa wamepoteza muda mwingi kumfuatilia Gareth Bale, 28, wa Real Madrid. (Independent)

Meneja wa Inter Milan Luciano Spalletti anadhani mkataba wa Ivan Perisic kwenda Old Trafford haupo tena kutokana na kusuasua kwa mazungumzo kati ya Man Utd na Inter hivi karibuni. (Premium Sport)

Gareth Bale atakataa hatua ya Real Madrid kumuuza kwenda Manchester United kwa sababu hana mpango wa kuondoka Madrid. (Times)

Mchezaji kinda kutoka Brazil, Gabriel Martinelli, 16, anafanya majaribio na Manchester United akitarajia kukamilisha uhamisho wake kutoka Ituano. (Manchester Evening News)

Liverpool wameacha kumfuatilia kiungo wa RB Leipzig Naby Keita, 22, na huenda wakarejea tena msimu ujao ambapo inaaminika huenda wakaweza kumsajili kwa pauni milioni 48. (Liverpool Echo)

Liverpool, Arsenal na Tottenham, zote zinamnyatia kiungo wa Barcelona Rafinha msimu huu. (Mundo Deportivo)

Arsenal wanataka kumsajili kiungo Jakub Jankto, 21, kutoka Udinese. (SportItalia)

Chelsea watalazimika kutoa takriban pauni milioni 17.9 kama wanataka kumsajili kiungo wa Inter Milan Antonio Candreva. (Daily Star)

Everton watataka kumsajili kiungo wa Nice, Jean Seri, 26, ambaye pia ananyatiwa na Arsenal, ikiwa watashindwa kumpata Gylfi Sigurdsson, 27, kutoka Swansea. (L'Equipe)

29 july 2017, Wakili wa Lissu, Fatma Karume amburuza kortini askari Polisi Aliyemshika Mkono Mahakamani....Anadai Fidia ya Bilioni Moja

Wakili wa Mwanasheria Mkuu wa Chadema na Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika, Fatma Karume amefungua kesi ya madai Mahakama Kuu ya Tanzania dhdi ya Inspekta wa Polisi Eugene Mwampondela wa Kituo Kikuu cha Polisi Dar es salaam.

Fatma amesema kuwa Inspekta Mwampondela alimshika mkono na kumvuta kwa nguvu hali iliyomsababishia maumivu makali, hivyo anadai alipwe kiasi cha shilingi bilioni moja kwa kosa la kumwingilia mwilini mwake na kumbughudhi kwa kumzuia kufanya kazi yake.

“Aliniambia kuwa ameagizwa na wakubwa kutoka juu, hivyo namfikisha mahakamani ili amweleze jaji ni nani aliyemtuma, na mimi sitaki kushikwa shikwa mwili wangu kwa hiyo naomba anilipe shilingi bilioni moja ili liwe fundisho kwa wengine,”amesema Fatma.

Fatma ambaye ni mmoja wa mawakili wa Mbunge wa Singida Mashariki alikumbana na kadhia hiyo wakati akiwa katika harakati za kumtetea mteja wake ili aweze kupata dhamana.

29 july 2017, Maalim Seif aitaka jumuiya ya kimataifa kuiwekea vikwazo Tanzania

Baada ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kujaza nafasi nane za ubunge wa viti maalumu za CUF, kambi ya katibu mkuu wa chama hicho, Maalim Seif Sharif Hamad imesema bado inawatambua wabunge waliovuliwa uanachama na kambi pinzani na kutaka jumuiya ya kimataifa iiwekee vikwazo Tanzania.

Kambi inayoongozwa na Profesa Ibrahim Lipumba, ambayo inatambuliwa na vyombo vya Serikali, ilitangaza kuwavua uanachama wabunge wanane wa viti maalumu kwa tuhuma za utovu wa nidhamu.

Waliopoteza ubunge ni Halima Ali Mohamed, Khadija Salum Ally, Salma Mohamed Mwassa, Miza Bakari Haji, Rais Abdallah Mussa, Riziki Shahari Mngwali, Saumu Heri Sakala na Severina Mwijage.

Siku moja baada ya kambi ya Lipumba kupeleka majina hayo, Spika wa Bunge alikubaliana na uamuzi huo na kutangaza nafasi hizo kuwa wazi na siku iliyofuata Tume ya Uchaguzi ikatangaza wabunge wapya, uamuzi “wa mwendokasi” ambao umeishangaza kambi ya Maalim Seif ambayo imeupinga.

Akizungumza na waandishi wa habari baada ya kikao cha dharura cha Baraza Kuu kilichofanyika ofisi ndogo za CUF zilizopo Vuga mjini Zanzibar, Maalim Seif alisema kwa mujibu wa katiba na kanuni za CUF wanachama hao bado ni wabunge.

Alisema kikao hicho kilihudhuriwa na wajumbe 45 kati ya 52.

Katibu mkuu huyo alisema wabunge hao wataendelea na wadhifa huo kwa kuwa waliteuliwa na vikao halali vya Baraza Kuu lililo upande wake, ambalo ndilo halali kwa mujibu wa katiba na sheria za CUF.

Pia, alisema baraza hilo lina wajumbe 52, na kati yao 25 wanatoka Tanzania Bara na 27 wanatoka Zanzibar na litakuwa hai hadi mwaka 2019.

“Baraza Kuu la uongozi halijakutana mahali popote Jumapili Julai 23 na kufanya uamuzi wowote wa kuwafukuza uanachama wabunge wanane na madiwani wawili wa CUF kama inavyodaiwa na mtu anayeitwa Ibrahim Lipumba na kikundi chake,” alisema Maalim Seif.

Maalim Seif alisema kufukuzwa kwa wabunge na madiwani hao si mpango wa Lipumba pekee, bali ni mpango kabambe uliosukwa na dola kwa kushirikiana naye.

Alisema ushahidi wa hilo ni kufukuzwa kwao na Lipumba ambaye ni mwenyekiti anayetambuliwa na Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa na papo hapo Spika wa Bunge kuridhia na NEC kutangaza majina ya wateule wa kujaza nafasi hizo.

“Baraza Kuu limeshangazwa na hatua ya Spika wa Bunge, Job Ndugai kujifedhehesha na kujiaibisha kwa kusema uongo kwa Watanzania kwamba eti alijiridhisha kwamba wabunge hao wanane wamefukuzwa uanachama na chama chao na kudai kuwa tayari wamekosa sifa za kuendelea kuwa wabunge,” alisema Maalim Seif.

Maalim Seif alisema kutokana na hali hiyo ni vyema Spika akajiuzulu kutokana na kwenda kinyume cha utaratibu wa uendeshaji wa Bunge.

Alisema baraza hilo limemtaka kuandika barua kwa Rais wa Bunge la Afrika (PAP), katibu wa umoja wa mabunge ya jumuiya ya Madola (CPA), katibu wa umoja wa mabunge ya duniani (IPU) kuhusu suala hilo.

Kuhusu NEC, alisema ni dhahiri imezidi kupoteza sifa na kujionyesha wazi kuwa haipo huru.

“Hata kama hawa wabunge wangekuwa wamefukuzwa kweli na baraza linalotambulika, lazima tume ifuate utaratibu uliopo kwa kuchukua orodha ya majina ya watu iliyowasilishwa ofisini kwake mwaka 2015 kujaza nafasi za uteuzi, orodha yetu ipo halali mbona hawa walioteuliwa hawamo ndani ya orodha yetu,” alihoji Maalim Seif.

Waliopitishwa na NEC ni Rukia Ahmed Kassim, Shamsia Aziz Mtamba, Kiza Hussein Mayeye, Zainabu Mndolwa Amir, Hindu Hamis Mwenda, Sonia Jumaa Magogo, Alfredia Apolinary Kahigi na Nuru Awadh Bafadhili.

Alisema kutokana na kuvunjwa katiba na sheria za nchi zilizopo ni vyema sasa jumuiya ya kimataifa ikasitisha misaada kwa Serikali ya Tanzania hadi hapo itakapokuwa tayari kufuata Katiba na hasa katika masuala ya siasa.

Alisema vitendo vinavyofanyika ni dhahiri vinaonyesha kuwepo dhuluma na udhalilishaji wa demokrasia kwa vyama vya upinzani.

“Baraza la uongozi linaunga mkono wito uliotolewa na Rais wa Chama cha Mawakili wa Tanganyika (TLS) na mnadhimu mkuu wa kambi ya upinzani bungeni, Tundu Lissu kwa jumuiya ya kimataifa kuibana Tanzania kwa kuiwekea vikwazo vya kiuchumi na kuitenga kisiasa na kidiplomasia hadi hapo watawala watakapoamua kuheshimu katiba, sheria, misingi ya kidemokrasia na haki za binadamu na utawala bora,” alisema Maalim Seif.

Maalim Seif alisema anajiamini na yupo tayari kukamatwa kama utawala ukiona aliyosema hayafurahishi.

Alisema kukaa jela itakuwa si mara ya kwanza, akidai kuwa ameshawahi kukaa na wala haikuwa kitu, hivyo akipelekwa tena itakuwa ni kama jambo la kawaida tu kwa upande wake.

29 july 2017, Mkude awekwa kando

Kiungo wa Simba Jonas Mkude ambaye alikuwa Nohodha wa klabu hiyo leo amewekwa kando na kuwa mchezaji wa kawaida wa Simba huku nafasi yake ikichukuliwa na beki wa Kimataifa raia wa Zimbabwe Method Mwanjale.

Mabadiliko hayo ya Simba yametangazwa na Mkuu wa Idara ya Habari ya Simba, Haji Manara na kusema kuwa benchi la fundi la klabu ya Simba chini ya Kocha Mkuu Joseph Omog ndiyo wamefanya mabadiliko hayo wakiwa na lengo la kuboresha kikosi hicho.

"Benchi la ufundi la klabu ya Simba,chini ya kocha wake mkuu Joseph Omog limefanya marekebisho kwenye eneo la unahodha wa timu. Katika marekebisho hayo yaliyoridhiwa na uongozi wa klabu, beki wa kimataifa Mzimbabwe Method Mwanjale ameteuliwa kuwa nahodha mpya wa timu ya Simba, akichukua nafasi ya Jonas Mkude atakaendelea kuwa mchezaji mwandamizi kwenye kikosi" alisema Haji Manara

Aidha klabu hiyo ya Simba imefanya mabadiliko mengine kwa kuwateua wachezaji bora wa Ligi Kuu ya Tanzania kuwa manahodha wasaidizi wa timu hiyo.

"Kwenye mabadiliko hayo ya kawaida, benchi la ufundi pia limewateua Mchezaji bora wa ligi kuu ya Tanzania na klabu ya Simba kwa msimu huu, Mohammed Hussein(Tshabalala) na John Raphael Boko kuwa manahodha wasaidizi wa timu hiyo." aliongeza Haji Manara

Klabu ya Simba ipo nchini Afrika Kusini kwa ajili ya maandalizi ya msimu ujao wa Ligi Kuu bara 2017/2018 lakini kikosi hicho kinatarajiwa kurejea nchini siku za karibuni kwa ajili ya bonanza la Simba Day ambalo litafanyika tarehe 8 mwezi wa 8 mwaka huu.

29 july 2017, KAGOMA KUOGA KWA MUUDA WA MIAKA 43

Kailash Sing ambaye hivisasa ana umriwa miaka 71 hajawahikuoga wala kukata ndevu zake tangu alipooga kwa mara mwisho kabla ya sherehe ya harusiya kumuoa mkewe,mwaka 1974.

Sing anaelezea sababu ya msimamo wake huo kuwa nishartila utabirialiopewa na mmoja wa kiongoziwa diniya Hindu kuwa atakapopata mtoto wa kiume,basimtoto huyo atakuwa mwenye mafanikio makubwa sana kwenye maisha yake na atakuwa tajirisana.

Nimiaka 43 imepita lakini Sing anaendelea na msimamo wake wa kutooga mpaka pale atakapofanikiwa kupata mtoto wa kiume.

Sing ana jumla ya watoto saba wa kike lakini juhudi zake zote za kupata mtoto wa kiume bado hazijazaa matunda.

Mkewe ambaye sasa ana umri wa miaka 66, alishawahi kujaribu kuweka mgomo wa kutoa unyumba mpaka Sing atakapooga lakinimgomo huo uligonga mwamba kwani Sing hakujali chochote na matokeo yake mgomo huo uliisha.

Majirani na watoto wamekuwa wakimtania na kumtupia maneno ya kejeli mzee Sing ambaye amekuwa akipuuza kila anachoambiwa mpaka pale ndoto yake ya kuwa na mtoto wa kiume itakapotimia.

Familia yake nayo imewahi kujaribu kutumia maguvu kumuogesha kinguvu Sing kwenye mto lakini Sing alifanikiwa kuwazidi nguvu na kukimbia akisema kuwa niheri afariki kuliko kuvunja sharti litakalomwezesha kupata mtoto wa kiume.

Kinachomfanya Sing awe anatoa harufu kali ni kazi yake ya ufugaji ambayo huifanya akizunguka kuwalisha majani ng'ombe wake kwenye kijiji chake cha Chatav ambapo hali ya hewa yake niya joto kali wakatimwingine kufikia joto la nyuzi47C.

Mbaliya kutooga,Sing hajazikata ndevu zake na wala kuzinyoa nywele zake ambazo hivisasa zimefikia urefu wa mita 2

Ilikuusafisha mwiliwake,Sing huota moto kila siku jioni huku akisali kumuomba mungu wake wa Kihindu,Shiva.

'Wakati ninapoendesha baiskeli kwenda kwenye shughulizangu,watoto wamekuwa wakitania na kunipiga kelele kuwa siogi,hawaelewi kwanini nafanya hivi sitabadili uamuziwangu mpaka nitakapopata mtoto wa kiume",alisema Sing.

Huenda mwanaume huyu wa nchini India akawa ndiye mtu mwenye kunuka kuliko watu wote duniani kwani hajaoga wala kukata ndevu zake kwa miaka 43 sasa,sababu ya kufanya hivyo niiliaweze kupata mtoto wa kiume.

29 july 2017, Msuva awapovukia yanga

Kiungo wa Yanga Simon Msuva, ambaye jana amedondoka saini ya miaka mitatu kuitumikia klabu ya Difaa Al Jadida ya nchini Morocco ametoa neno la shukrani kwa klabu yake ya Yanga kwa mchango wao mpaka kufanikiwa kwenda kimataifa.

Msuva ambaye jana alitambulishwa rasmi na klabu hiyo kwa vyombo vya habari nchini humo amesema amefurahi na sasa ni rasmi mchezaji wa klabu hiyo iliyopo Morocco

"Ninafurahi kubwa sana kutangaza kwamba mimi sasa ni mchezaji rasmi wa Al Jadida baada ya kusaini mkataba na klabu hii, naomba nitumie nafasi hii kuwashukuru wote katika klabu yangu ya Yanga kwa kunisapoti, na kumbukumbu nzuri tulizokuwa nazo na kushirikiana pamoja kwa kipindi chote nipo hapo, siku zote mtabaki katika moyo wangu" alisema Simon Msuva

Simon Msuva alitua Yanga mwaka 2012 akitokea klabu ya Moro United na kuitumikia klabu ya Yanga kwa miaka mitano huku akiwa na mchango mkubwa katika klabu hiyo

29 july 2017, Tukutane Simba Day, niwape raha-Okwi

Mshambuliaji wa kimataifa wa Simba kutoka Uganda, Emmanuel Okwi, ametua kambini Afrika Kusini jana na kuwaambia mashabiki wa timu hiyo wajiandae kuona "vitu vyake" katika mechi ya kirafiki dhidi ya Rayon FC itakayofanyika Agosti 8 (Simba Day).

Okwi amewaambia mashabiki na wanachama wa Simba wawe watulivu, amejiandaa kuwapa kile wanachokitarajia kutoka kwake na anafahamu vizuri ndoto za klabu hiyo yenye makao makuu yake Mtaa wa Msimbazi, Kariakoo jijini.

"Nitakuwa Dar es Salaam siku ya Simba Day, najua watu wanahamu ya kuniona, mashabiki wawe watulivu," alisema mshambuliaji huyo.

Chanzo Eatv

29 july 2017, Uhuru Kenyatta ashutumiwa kupanga uwizi wa kura na upinzani nchini Kenya

Uhuru Kenyatta ashutumiwa kupanga uwizi wa kura na upinzani nchini Kenya

Mpinzani mkuu na mgombea urais nchini Kenya Raila Odinga amemshutumu rais Uhuru Kenyatta kwa kufanya mpango wa kuiba kura kwa kutumia jeshi katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika mwezi Agosti.

Raila Odinga alifahamisha haya katika mkutano na waandishi wa habari jijini Nairobi ambapo alitoa ushahidi usiobahatisha uliobainika kupitia nyaraka za maafisa wa ngazi za juu katika jeshi na rais Uhuru.

Odinga ambaye ni mgombea urais Kenya kwa tiketi ya chama pinzani cha NASA alisema kwamba wamepata ushahidi unaodhihirisha kwamba Jubilee ,chama tawala kinapanga kuiba kura .

Aliendelea kufahamisha kwamba wanajeshi 226 walio na urafiki wa karibu na serikali ya sasa  wamesajiliwa upya kwa lengo la kukata umeme , maji na njia zote za mawasiliano katika maeneo ambapo yanaunga mkono upinzani .

Hata hivyo rais Uhuru amekataa madai hayo na kusema kuwa ni mpango wa upinzani kutaka kuondolewa kwa jeeshi katika kutekeleza majukumu yao.

Wakenya wanatarajiwa kuchagua serikali mpya ifikapo Agosti 8.

Chanzo Trt

29 july 2017, Zaidi ya wafungwa 20 watoroka magereza DR Congo

Zaidi ya wafungwa 20 watoroka katika magareza Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo

Wafungwa zaidi ya 20 watoroka katika magareza Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo
Taarifa zinaripoti kuwa wafungwa zaidi ya 20 wametoroka katika magareza Ijumaa Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Wafungwa hao wameripotiwa kutoka katika gereza la Bukavu Mashariki mwa Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo.

Meya wa jiji la Bukavu Philemon Yogolelo aliliambia shirika la habari la Anadolu kuwa mfungwa mmoja alifariki katika tukio hilo.

Wafungwa wengine wane walijeruhiwa walipokuwa wakijaribu kutoroka.

Friday, July 28, 2017

28 july 2017, FIFA yatia maguu Tanzania

Meneja Miradi ya Maendeleo wa Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA) kwa Afrika, Mzimbabwe Solomon Mudege amewasili nchini kwa ajili ya kufuatilia mambo yanayoendelea katika shirikisho la soka Tanzania TFF.

Mudege tayari yupo nchini na pamoja na kukutana na Kamati ya Utendaji ya TFF, Dar es Salaam, pia atakuwa na kikao na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrisons Mwakyembe.

Bado haijafahamika Ofisa huyo amekuja kwa sababu zipi haswa na kama ameitwa na viongozi wa TFF au amekuja kwa maagizo ya FIFA tu.

Hata hivo hali si shwari katika uongozi wa soka Tanzania, kutokana na viongozi wakuu TFF yaani Rais Jamal Malinzi na Katibu wake Mwesigwa Selestine kuwekwa rumande tangu Juni 29 kwa tuhuma za ubadhirifu na matumizi mabaya ya madaraka na huenda Ofisa huyo akataka kujua kilichowasibu viongozi hao.

28 july 2017 ,Pikipiki zatumika kuiba nyara za Serikali

Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya limekamata nyara za serikali ambazo ni ngozi moja ya simba na vipande 15 vya meno ya tembo vilivyokuwa vimebebwa kwenye pikipiki.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Naibu Kamishina wa Polisi Mohamed Mpinga amesema tukio hilo limetokea majira ya 10:00 alasiri mnamo Julai 27, mwaka huu katika pori la hifadhi ya taifa la Ruaha lililopo Rujewa wilayani Mbarali mkoani humo katika msako uliofaywa kwa kushirikiana na TANAPA.

DCP Mpinga amesema jeshi hilo kwa kushirikiana na TANAPA liliendesha msako na kufanikiwa kukamata nyara hizo ambazo zilizogundulika baada ya kukamata pikipiki sita ambazo wahusika wake walikimbia na kuzitelekeza, mbili zikiwa hazina ‘plate namba’ na nyingine zikiwa na usajili.

Katika matukio mengine, jeshi hilo limefanikiwa kukamata wahamiaji haramu wenye uraia wa Ethiopia saba katika nyakati tofauti katika mkoa huo baada ya kufanya msako katika maeneo mbalimbali.

28 july 2017, Tiketi za kuuona mpambano kati ya Mayweather na McGregor $150000


Tiketi za kushuhudia mpambano wa masumbwi kati ya Floyd Mayweather dhidi ya Conor McGregor zinauzwa kwa dola 150,000.

Mpambano huo unatajwa kuwa wa gharama zaidi kuwahi kutokea na tiketi kwa sasa zinauzwa kama njugu.

Unatarajiwa kupigwa Agosti 26 katika uwanja wa T-Mobile mjini Las Vegas utakaoingiza watu elfu 20.

Mayweather mwenye miaka 40 awali alistaafu lakini amerejea kupambana na McGregor.

28 july 2017, Tetesi za soka michezoni leo Ijumaa

Arsenal wanakaribia kukamilisha usajili wa pauni milioni 45 kumchukua kiungo wa Monaco Thomas Lemar, 21. (Sun)

Monaco wamekataa dau la tatu la Arsenal la pauni milioni 44.7 la kumtaka Thomas Lemar. (L'Equipe)
Meneja wa Real Madrid Zinedine Zidane amesema hawezi kutoa hakikisho kuwa Gareth Bale atabakia Bernabeu msimu huu, huku Manchester United wakimfuatilia. (Mirror)

Monaco watakuwa tayari kumuuza Kylian Mbappe kwa timu itakayokuwa tayari kutoa euro milioni 180. (L'Equipe)

Meneja wa Chelsea Antonio Conte anapanga kutoa pauni milioni 50 kuwasajili Ross Barkley, 23, kutoka Everton na Alex Oxlade-Chamberlain, 23, kutoka Arsenal. (Sun)

Chelsea wamepanda dau kutaka kumsajili kwa mkopo Renato Sanches, 19, kutoka Bayern Munich. (Daily Telegraph)

Meneja wa Tottenham Mauricio Pochetitino anataka kumsajili Ross Barkley na kumfanya kuwa kiungo wa kati. (Times)

Roma wanajiandaa kupanda dau jipya la pauni milioni 32 kumtaka winga wa kimataifa wa Algeria, Riyad Mahrez, anayechezea Leicester. (Mirror)

Liverpool wapo tayari kutoa dau la mwisho la zaidi ya pauni milioni 70 kujaribu kumsajili kiungo wa RB Leipzig Naby Keita, 22. (Mirror)
Liverpool wanashikilia msimamo wao kuwa Philippe Coutinho, 25, hauzwi, huku Barcelona wakiendelea kumfuatilia. (ESPN)

Liverpool- kwa shingo upande- wameweka bei ya Philippe Coutinho kuwa ni pauni milioni 133, kama kweli Barcelona wanamtaka mchezaji huyo kutoka Brazil. (Sport)

Meneja wa Inter Milan Luciano Spalletti amesema anataka Ivan Perisic kubakia Italia, ingawa hana uhakika kama ataweza kufanya hivyo huku Manchester United wakiendelea kumfuatilia. (ESPN)

Inter Milan wameweka kipaumbele katika kumsajili kiungo wa Bayern Munich, Arturo Vidal, na wanajiandaa kutoa dau la euro milioni 50. (Gazzetta dello Sport)

Juventus wanaotafuta kiungo mkabaji sasa wamemgeukia Blaise Matuidi, 30, wa PSG, baada ya kuacha kumfuatilia Nemanja Matic, 28, anayenyatiwa na Manchester United. (Independent)

Mwenyekiti wa AC Milan Marco Fassone amesema klabu yake imezungumza na wakala wa mshambuliaji wa Chelsea Diego Costa, 28. (Sky Sports)

Mshambuliaji wa Real Madrid Karim Benzima, 29, anatarajiwa kusaini mkataba mpya hata kama klabu yake itamsajili Kylian Mbappe, 18, kutoka Monaco. (Marca)

Mshambuliaji wa kimataifa wa Argentina Paulo Dybala, 23, anayenyatiwa na Manchester United na Barcelona, hana mipango ya kuondoka Juventus msimu huu. (TalkSport)

Wakala wa mchezaji wa Arsenal Lucas Perez amekwenda London kuzungumzia kurejea kwa mshambuliaji huyo Deoportivo La Coruna. (AS)

28 july 2017, Kundi la Boko Haramu lateka wafanyakazi wa shirika la mafuta Nigeria

Shirika la mafuta linaliomilikiwa na serikali nchini Nigeria limetangaza kuwa baadhi ya wafanyakazi wake wametekwa na kundi la kigaidi la Boko Haram na hawajulikani walipo mpaka sasa.

Shirika la mafuta linaliomilikiwa na serikali nchini Nigeria limetangaza kuwa baadhi ya wafanyakazi wake wametekwa na kundi la kigaidi la Boko Haram na hawajulikani walipo mpaka sasa.

Ripoti hio imetolewa baada ya Boko Haramu kuvamia na kuua baadhi ya wafanyakazi katika eneo la Gubio siku mbili zilizopita.

Kwa mujibu wa habari,kati ya waliotekwa ni askari saba waliokuwa katika operesheni ya kukomboa watu.

Watu 48 wameripotiwa kuuawa wakiwemo askari,wafanyakazi wa shirika la mafuta ambao miili yao imefikishwa katika hospitali ya Maiduguri.

Mwenyekiti wa kampuni hiyo ya mafuta NNPC amesema kuwa uchunguzi utaendelea endapo kutakuwa na uhakika wa ulinzi bora na usalama.

Hata hivyo mkuu wa majeshi Tukur Buratai,wiki iliyopita aliagiza wanajeshi kumsaka mkuu wa Boko Haramu Abubakar Shekau ndani ya siku arobaini.

28 july 2017, Wapiga kura kutumia Pasipoti na leseni zao kupiga kura Senegal

Mahakama kuu ya Senegal imepitisha ombi la rais Macky Sall kuruhusu wapiga kura kutumia pasipoti na leseni za udereva katika zoezi la kupiga kura.

Mahakama kuu ya Senegal imepitisha ombi la rais Macky Sall kuruhusu wapiga kura kutumia pasipoti na leseni za udereva katika zoezi la kupiga kura.

.Kwa mujibu wa habari,Sall aliiomba mahakama siku ya Jumatatu kuwaruhusu wapiga kura wasiokuwa na vitambulisho kutumia pasipoti zao ama leseni kupiga kura.

Wapiga kura sasa wataweza kutumia pasipoti na leseni zao kupiga kura katika uchaguzi utakaofanyika tarehe 30 mwezi Julai endapo watakuwa hawana vitambulisho maalumu vya kupiga kura.

.Hata hivyo upinzani umepinga kabisa umauzi huo na kusema kuwa umauzi huo unahatarisha  demokrasia nchini Senegal.

Muweka sheria wa Democratic party of Senegal PDS, Mamadou Lamine Diallo amesema kuwa si sheria wala sahihi kwa mahakama kupitisha suala kama hilo ndani ya miezi sita ya uchaguzi nchini humo.Amesema kuwa uamuzi huo hauendani na sheria ya ECOWAS.

Polisi walipiga mabomu ya machozi siku ya Alhamisi kutawanya wale wote waliokuwa wakipingana na sheria hiyo.

Senegal inatarajia kufanya uchaguzi wake siku ya Jumapil..

28 july 2017, Waliovuliwa Ubunge na Lipumba CUF Wafungua Kesi Mahakamani

Siku chache baada ya Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi CUF, Prof. Lipumba kuwavua uanachama Wabunge wanane wa Viti Maalum kisha Spika Ndugai kuridhia uamuzi huo, jana July 27, 2017 Wabunge hao wamefungua kesi katika Mahakama Kuu ya Tanzania.

Wabunge hao wamefungua kesi hiyo iliyopewa namba 143/2017 kupitia Wakili wao Peter Kibatala lakini hata hivyo bado haijapangiwa Jaji huku Wabunge hao wakidai hawajapewa muda wa kujitetea.

Mbali na kufungua kesi katika Mahakama Kuu Tanzania, pia wamekata rufaa ndani ya Chama chao kupinga utekelezaji huo na kuiomba Mahakama isitishe utekelezaji wa uamuzi wa kufukuzwa Uanachama wao.

28 july 2017, Barrick (Acacia) Wakubali Yaishe.....Wiki Ijayo Wataanza Mazungumzo na Serikali

Kampuni ya Barrick Gold ya nchini Canada, imesema wiki ijayo timu ya wataalamu wake watakuja nchini kwa ajili ya kufanya mazungumzao na Serikali kuhusu uendeshaji wa migodi yake.

Tamko hilo limekuja siku chache baada ya Rais Dk. John Magufuli kutangaza kuwa iwapo Barrick inayoimiliki Kampuni ya Acacia itachelewa kuja kufanya mazungumzo ataifunga migodi yao.

Wakati kampuni hiyo ikijiandaa kuja nchini, Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) tayari imepeleka madaia ya Dola za Marekani bilioni 190 ambazo ni sawa na Sh trilioni 424), kwa Kampuni ya Acacia, ikiwa ni malimbikizo ya kodi kutoka mwaka 2000.

Taarifa iliyochapishwa kwenye mtandao wa Financial Post juzi ilisema. “Kampuni ya Barrick Gold kupitia ripoti yake ya robo mwaka imesema itaanza majadiliano na Serikali ya Tanzania wiki ijayo kuhusu marufuku ya kusafirisha nje madini na masuala mengine yaliyoikumba kampuni inayoimiliki ya Acacia.

“Taarifa hiyo ya mazungumzo inakuja baada ya Jumatatu wiki hii Tanzania kuwasilisha bili ya dola bilioni 190 kwa Accacia yenye makao makuu Uingereza.

“Serikali ya Tanzania inaituhumu Acacia, ambayo inamilikiwa na Barrick kwa asilimia 63.9 kudanganya mapato yake ili kukwepa kodi na hivyo kuitaka ilipe malimbikizo pamoja na faini. Acacia imekana tuhuma hizo.

“Tanzania pia iliweka marufuku ya kusafirisha mchanga wa dhahabu (makinikia) na fedha Machi mwaka huu, hatua ambayo inaweza kuathiri asilimia sita ya uzalishaji wa wakia milioni 5.3 hadi milioni 5.6 ya dhahabu kwa mwaka katika migodi ya Acacia.

“Barrick ilisema inasubiri hadi Acacia itakaporekebisha mwongozo wake wa uzalishaji kabla ya kubadili mwelekeo mzima wa uzalishaji wake kwa mwaka,” ilisema taarifa hiyo.

Taarifa hiyo ilisema, Barrick yenye makao yake makuu Toronto, Canada iliripoti kuongezeka kwa mapato kufikia Dola bilioni 1.08 robo iliyoishia Juni 30, kutoka dola milioni 138 kwa mwaka mwaka jana.

“Hilo lilichochewa na mafanikio makubwa ya mauzo ya hisa katika mgodi wa Veladero na mradi wa Cerro Casale. Mtiririko wa fedha kwa kipindi hicho ulikuwa dola milioni 43 ukiwa umeshuka kutoka dola milioni 274 kwa kipindi kama hicho mwaka jana kutokana na kiwango cha juu cha kodi, ongezeko la mtaji na ongezeko lililopangwa kwa ajili ya matumizi ya ukuaji wa badaye,” ilisema.

Juni 14 mwaka huu, Rais Magufuli alikutana na kufanya mazungumzo na Mwenyekiti wa Kampuni ya Barrick Gold Corporation Profesa John Thornton na Ikulu ikatoa taarifa kwa umma kwamba, katika mazungumzo hayo, kampuni hiyo imesema ipo tayari kufanya mazungumzo na Serikali ya Tanzania ili kulipa fedha ambazo Tanzania imezipoteza kutokana na kampuni hiyo kuendesha shughuli zake hapa nchini.

Julai 21, 2017 akizungumza kwenye mkutano wa hadhara mkoani Kigoma, Rais Magufuli alisema. “Nitasimamia haki siku zote katika maisha yangu, na niliwaambia nimeanzisha vita hii ya kiuchumi, vita ya kiuchumi ni mbaya sana, wakubwa wale huwa hawafurahi, kuna viongozi wengi tu mliona yaliyowapata ni kwasababu nchi zao zilikuwa na mali.

“Lakini wale wakubwa wakataka kuchezea hizo mali, kwa manufaa yao na siyo kwa manufaa ya wananchi wa pale, walitumia mbinu nyingi za kila aina, lakini Mungu wangu ni mwema na Watanzania ni wema watasimama kwa ajili ya taifa hili.

“Ninayoongea nayajua ni matrilioni ya fedha ambayo yameibiwa, na kwasasa hivi tumewaita waje wafanye mazungumzo, wamekubali lakini wakichelewachelewa nitafunga migodi yote.

“Ni mara 10 migodi hii tukaigawana Watanzania wachimbe wawe wanauza tuwe tunapata kodi, kuliko kuchimbwa na watu wanaojiita wawekezaji halafu hawalipo kodi.

“Walikuwa wanazungumza mle wanachimba dhahabu, madini machache tu, matatu. tumegundua mle kuna madini mengi.

“Tanzania hii ni nchi tajiri, lakini imekuwa ikiibiwa mno, tumechezewa sana, mimi nipo serikalini na mimi ndiye najua siri za serikali, tumechezewa sana kwa kuibiwa sana mali zetu, kwenye dhahabu huku tumeibiwa mno, ukiyajua yale yaliyokuwa yanafanyike mle unaweza ukalia.

“Unaweza ukatamani usiishi, mtu anachimba anapokea anapeleka na anashirikiana na baadhi ya watu tuliowaamini kwenda kulisimamia hili.

“Anasema hapa tunasafirisha mchanga na Watanzania wote tunaamini tunasafirisha mchanga, mbona hawajaja Kibondo kuchukua mchanga wa hapa mbona na penyewe tunao?

“Lakini tunaamini, wanaupeleka kwenye makontena wanapeleka Ulaya na wakisha enda kuusafisha kule ule mchanga unaobaki wala hawaurudishi, ulikuwa ni utapeli wa ajabu, na ni aibu kubwa kuona utapeli huu unafanywa na watu ambao ni wakubwa.

Julai 26 akiwa mkoani Singida, Rais Magufuli tena alisema “Haiingii akilini watu wanakuja wanachukua mali zetu na kuondoka nazo, ifike mahali tuamke, tumeibiwa vya kutosha, nendeni mkachimbe madini, hizo fedha tutagawana sisi, hata kama hatufanyi kazi hizo fedha tutagawana.

“Wapo wachina wanakuja kuchimba barabara hapa nchini, tunashindwaje kuwatumia hawa wakachimbe madini yetu kisha wakatuachia dhahabu yetu halafu wao wakaondoka?

“Mimi ndiye Rais, hakuna anayejua siri za serikali kama mimi na nawaambia mmepata mtu ambaye anazungumza ukweli, ningeweza kunyamaza kwa vingine ninavyoviona, lakini nataka kujenga Tanzania mpya.

“Yale makontena yote ningeweza kuwaambia tugawane mzee, hata kingereza ninajua, ningeweza kuwaambia give me ten percent (asilimia 10).

“Ningejenga mahoteli na kuwa na kampuni nyingi kwani wapo Watanzania wamejenga huko nje lakini nyumba za wazazi wao zimechakaa, mimi nimezaliwa hapa, ninaishi hapa na nitakufa hapa,” alisema Rais Magufuli.

28 july 2017, Tanzania ni shwari_Twaweza

Ripoti ya Taasisi ya Twaweza imeonesha kuwa zaidi ya 53% ya Wananchi wanasema kiwango cha usalama kimeimarika katika kipindi cha mwaka mmoja uliopita huku 10% wakisema hali imekuwa mbaya zaidi.

Utafiti huo wa Sauti za Wananchi, unaojulikana kama Hapa usalama tu: Usalama, Polisi na Haki Nchini Tanzania, umebaini kwamba, wananchi wana imani kubwa na Sungusungu katika masuala ya Ulinzi na Usalama kama wanavyoliamini Jeshi la Polisi.

Utafiti huo umeleeza kuwa, pamoja na viashiria chanya kuhusu usalama, viwango vya uhalifu vinaonekana kuwa juu, ambapo 41% ya wananchi wamewahi kushuhudia uhalifu ukifanyika hadharani ndani ya mwaka mmoja uliopita.

Akizungumza wakati wa utafiti huo Mkurugenzi Mtendaji wa Twaweza, Ndg Aidan Eyakuze, amesema, takwimu za muhtasari huo zinatoa taswira tofauti kabisa na ile inayotolewa na vichwa vingi vya habari; kwa mtazamo wa wananchi wengi, usalama unaonekana kuimarika lakini ameonya kwamba, imani ya wananchi kwa jeshi la polisi bado ni ndogo.

Vilevile takwimu za utafiti zimeonesha kwamba, ni 56% tu ya wananchi wanasema kuwa wanatoa taarifa ya wizi kwa mamlaka pindi wanaposhambuliwa wao wenyewe ama nyumba zao huku ikidaiwa kwamba mara nyingi wananchi hawaombi msaada kwa polisi, hasa pale wanapokuwa wahanga wa uhalifu, ambapo ni mwananchi mmoja tu kati ya wanne sawa 26% anayeomba msaada polisi.

Hata hivyo pamoja na kuwa ulinzi umeimarika nchini uwizi umetajwa kama tishio kubwa kwenye jamii ambapo 61% ya utafiti imesema wizi huku 5% ikidai wizi wa mifugo.

Pamoja na hayo kati ya asilimia zaidi ya 90 ya watu wanaomiliki simu hawana uelewa wa kutosha kuhusu namba za dharura za jeshi la Zimamoto pamoja na jeshi la Polisi.

Chanzo Eatv

28 july 2027, Panda apata mtoto China


Panda apata mtoto mwenye gramu 115

Panda mwenye miaka 11 Xiao Yatou amezaa mtoto katika kituo cha kufuga Panda mashariki mwa Sichuan nchini China.

Panda huyo amezaliwa akiwa na gram 115.

Miaka miwili iliyopiata Panda huyo alizaa mapacha wawili siku kama hiyo.

Thursday, July 27, 2017

27 july 2017, TETESI ZA SOKA MICHEZONI LEO ALHAMISI

Paris Saint_Germain wana uhakika wa kukamilisha uhamisho wa pauni milioni 198 wa Neymar, 25, kutoka Barcelona katika siku 15 zijazo. (L'Equipe)
Barcelona watajaribu kumsajili mshambuliaji wa Liverpool Philippe Coutinho, 25, iwapo watampoteza Neymar anayedhaniwa kuelekea PSG. (TalkSport)

Philippe Coutinho ameiomba Liverpool ruhusa ya kuondoka, na tayari amefikia makubaliano ya maslahi binafsi na Barca. (RAC1)

Barcelona watawapa Liverpool kiungo Ivan Rakitic kama sehemu ya mkataba wa kumchukua Philippe Coutinho. (Don Balon)

Hatua ya Real Madrid kutaka kumsajili mshambuliaji wa Monaco, Kylian Mbappe, 18, huenda ikasababisha winga Gareth Bale, 28, kwenda Old Trafford. (Indepenent)

Meneja wa Manchester City Pep Guardiola amesema klabu yake ina fedha za kutosha za kupambana na Real Madrid katika kumsajili Kylian Mbappe. (Mail)

Meneja wa Manchester United Jose Mourinho ameonesha dalili kubwa kuwa Zlatan Ibrahimovic, 35, atasaini mkataba kubakia Old Trafford. (Times)

Manchester United wanajiandaa kutoa dau la pauni milioni 44.6 kumtaka mchezaji wa RB Leipzig Emil Forsberg. (Daily Star)

Iwapo Kylian Mbappe atasaini kwenda Real Madrid, Manchester United watataka kumsajili Gareth Bale, huku taarifa kutoka Old Trafford zikisema kuna 'nafasi kubwa' ya Bale kwenda Old Trafford. (The Independent)
Manchester United bado wanataka kumsajili kiungo wa Chelsea, Nemanja Matic, 28, na wanaamini wataweza kuwashawishi Chelsea kuwauzia kwa zaidi ya pauni milioni 40. (Independent)

Licha ya kuhusishwa na kuhamia Manchester United, Ivan Perisic atapewa mkataba mpya kubakia Inter Milan, ambao hawaamini Man Utd watakubali kutoa fedha zaidi na kukubali mkataba ambao utamhusisha Anthony Martial kwenda Inter. (Football Italia)

Manchester United watamgeukia Emil Forsberg wa RB Leipzig iwapo watamkosa Ivan Perisic. (Calciomercato)

Gareth Bale amekataa nafasi ya kuhamia Arsenal, ambao wanamtaka ili kuziba nafasi ya Alexis Sanchez. (Don Balon)

Kiungo wa Arsenal Jack Wilshere, 25, anataka kubakia England iwapo ataondoka Emirates. (ESPN)
Arsenal wanakaribia kukamilisha usajili wa pauni milioni 45 wa kiungo wa Monaco Thomas Lemar. (Sun)

Thomas Lemar huenda akabakia Monaco, baada ya makamu wa rais wa klabu hiyo Vadim Vasilyev kusema kiungo huyo hauzwi. (Metro)

Arsenal watamkosa kiungo wa Barcelona Arda Turan, huku Galatasaray ya Uturuki ikikaribia kukamilisha usajili wake. (Mirror)

Kiungo wa Borussia Dortmund Mikel Merino, 21, anakaribia kujiunga na Newcastle. (Evening Chronicle)

Beki wa kati Mamadou Sakho, 27, hajajumuishwa kwenye kikosi cha Liverpool cha wachezaji 30 watakaocheza mechi tatu za kirafiki nchini Ujerumani. (Liverpool Echo)

Chelsea wanataka kukopa pauni milioni 500 ili kujenga uwanja wao mpya, badala ya kutegemea fedha za Roman Abramovic. (Times)

Chelsea wanazungumza na wadau mbalimbali kuhusu uuzaji wa haki za jina la uwanja mpya, ingawa klabu hiyo inasisitiza kuwa jina la Stamford Bridge litapewa heshima yake kwa njia moja ama nyingine. (Evening Standard)

Meneja wa Chelsea Antonio Conte amesema angepewa nafasi ya kununua mshambuliaji yoyote yule duniani angemnunua Harry Kane, 23, wa Tottenham. (Daily Mail)

AC Milan wamekuwa na mawasiliano na wakala wa Diego Costa kutaka kumsajili mshambuliaji huyo wa Chelsea. (Daily Express)

Wakurugenzi wakuu wa AC Milan Marco Fassone na Massimo Mirabelli wamekutana na wakala Jorge Mendes kumzungumzia Cristiano Ronaldo. Vigogo hao wa Milan wanataka wajulishwe mara tu Ronaldo atakapoweza kupatikana ingawa hakuna majadiliano yoyote kwa sasa. (Sky Sports)

Tottenham wanamnyatia kiungo wa Benfica Ljubomir Fejsa, 28. (Sun)
Meneja wa Everton Ronald Koeman anataka kusajili wachezaji wengine watatu- beki wa kati, mshambuliaji na kiungo mshambuliaji wa Swansea Gylfi Sigurdsson. (Mirror)

27 july 2017, Simba haina rekodi mbovu-Manara

Uongozi wa Klabu ya Simba wenye makao makuu yake Msimbazi Jijini Dar es Salaam umekanusha vikali taarifa iliyotembea katika mitandao ya kijamii inayodai timu hiyo imechapwa bao 7-0 katika mchezo wao wa kirafiki dhidi ya Royal Eagles ya nchini Afrika Kusini walipoweka kambi yao.

Hayo yameweka bayana na taarifa iliyotolewa na msemaji wa timu hiyo Haji Manara na kusema kama kweli wamechezea kichapo hicho kutoka kwa timu ya daraja la kwanza hakuna mtanzania asingeweza kuona matokeo hayo katika vyombo vya habari kutokana na sasa utandawazi umetawala.

"Kiukweli Simba haina rekodi za hovyo kama hizo kokote inapocheza duniani na haijawahi kufungwa na klabu yoyote idadi ya magoli kama hayo, kama zilivyo timu nyingine nchini hususan Klabu ambayo mashabiki wake ndiyo wanaozusha upuuzi huo", amesema Manara.

Kwa upande mwingine, Manara amewataka watanzania na mashabiki wa wekundu wa msimbazi watambue kuwa siku zote walizokuwa huko nchini Afrika Kusini, benchi lake la ufundi limejikita katika kutengeneza miili ya wachezaji kistamina ili iweze kufanya vizuri katika michezo yake ambayo ipo usoni kuanza.

27 july 2017 , NEC yateua wabunge nane CUF

Tume ya Uchaguzi (NEC) imefanya uteuzi wa wabunge nane wa viti Maalum kupitia (CUF) baada ya Tume hiyo kupokea barua kutoka kwa spika wa Bunge Ndugai ambaye alisema kuna nafasi za wazi nane katika bunge hilo kufuatia wabunge hao kuvuliwa uanachama

27 july 2017, Kibadeni atua Mbao FC

Zikiwa zimebakia takribani siku 10 kufungwa kwa dirisha la usajili wa msimu mpya wa ligi kuu Tanzania Bara, timu ya Mbao FC imeendelea kujiimarisha kwa kumsajili mchezaji chipukizi Suleiman Kibadeni kutoka Zanzibar kuwatumikia wakata mbao hao kwa
miaka miwili kuanzia hivi sasa.

Timu hiyo ilinusurika chupu chupu kushuka daraja katika msimu uliyopita ambapo hivi karibuni iliondokewa na nyota wake watano baada ya kuonekana wazuri katika vilabu vingine vya hapa nchini Tanzania.

Wachezaji hao ni makipa Benedict Haule na Emmanuel Mseja, kiungo Salmin Hoza waliokwenda Azam FC, beki Jamal Mwambeleko waliokwenda Simba na kiungo Pius Buswita aliyekwenda Yanga.

Chanzo Eatv

27 july 2017, TAASISI ZA DINI ZATAKIWA KUPIMA MAENEO YAO

Mkuu wa mkoa wa Arusha , Mrisho Gambo amewataka viongozi wa taasisi za dini kupima maeneo ya viwanja vya taasisi zao ili kuondokana na migogoro ya taasisi hizo kuporwa maeneo yao na baadhi ya viongozi wa vijiji wasio waaminifu.

Gambo amesema hayo alipokutana na viongozi wa dini, watendaji wa serikali na viongozi wa taasisi za umma kuzungumzia nafasi ya taasisi za dini katika maendeleo ya jamii ambaye pia amewaomba viongozi hao kutosita kukemea vitendo visivyo na maadili kwa viongozi wa umma na jamii.

Gambo amesema viongozi wa dini wana nafasi kubwa ya kuhamasisha jamii Kujenga umoja na kuepukana na vitendo vinavyoweza kuwagawa katika makundi ya dini ikiwemo masuala ya kisiasa.

Pia amewataka viongozi hao kuhakikisha wanapima maeneo ya taasisi zao ili kuepusha migogano inayosababishwa na baadhi ya maeneo hayo kumegwa kinyemela na baadhi ya viongozi wasiowaaminifu katika vijiji na mitaa.

Nao viongozi wa taasisi za dini wakapata nafasi ya kutoa michango yao katika sekta mbalimbali za kijamii.

Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya Arusha, Fabian daqqaro amewataka viongozi hao kuzingatia taratibu na sheria zinazowaongoza katika shughuli zao.

27 july 2017, Polisi wakamata wanachama wa dhehebu haramu la Yesu China

Polisi nchini China wamewakamata wanachama 18 wa dhehebu lililopigwa marufukua.

Baadhi ya wanachama wa kundi hilo ni maarufu kwa kumpiga mwanamke hadi kufa kwenye duka la McDonald mwaka 2014, baada ya mwanamke huyo kukataaa kuwapa namba yake ya simu.

Dhehebu hilo linalofahamika kama Church of Almighty God lilianzishwa miaka ya 1990 na linadai kuwa Yesu alirudi duniani kama mwanamke nchini China
Serikali ya China mara kwa mara huvamia madhehebu na kuwakamata wanachama wengi kwa miaka kadhaa.

Wakati wa kuwakamata polisi pia walichukua kompiuta na vitabu vinavyotumiwa na dhehebu hilo.

Imani ya dhehebu hilo ni kuwa Yesu alirudi duniani kama mwanamke.

Mtu pekee anayedai kuwasiliana na mwanamke huyo ni mwalimu wa zamani Zhao Weishan, ambaye alilianzisha miaka 25 iliyopita na sasa ametorokea Marekani.

27 july 2017,Mwanafunzi mdogo afaulu mtihani wa wanafunzi wakubwa Benin

Peace Delaly Nicoue, ndiye mwanafuniz mwenye umri mdogo zaid aliyefanya mtihani wa mwisho unaofahamika kama Baccalaureate nchini Benin mwaka huu na kupata alama za juu.

Mwanafunzi huyo mwenye umri wa miaka 11 anasema alifurahishwa baada ya kupata alama 17 kwa 20 katika somo la hesabu.

Huku wanafunzi wengi wakifanya mtihani huo wa mwisho wakiwa na umri wa miaka 18, Peace aliruhusiwa na serikali kuufanya mtihani huo miaka saba kabla ya kuhitimu.

Mwalimu wake anasema kuwa Peace alionyesha mapema dalili za kufanikiwa.

"Akiwa na umiri wa miaka 4 alikuwa akiandika kifaransa na kiingereza bila ya kufanya makosa" alisema mwalimu wake.
Peace anasema kuwa ndoto yake na kusomea nchi inayozungumza lugha ya Kiingereza.

27 july 2017, Manji afungua maombi Mahakama Kuu akiiomba mahakama hiyo imuondolee zuio la dhamana

Mahakama Kuu ya Tanzania imesema inatarajia kuanza kusikiliza maombi ya dhamana yaliyotolewa na Mfanyabiashara maarufu Tanzania Yusuf Manji, August 4, 2017.

Jaji Isaya Arufani amesema hayo jana baada ya Mawakili wa Serikali Paul Kadushi na Simon Wankyo kuyapokea maombi hayo na kusema wana nia ya kuyapinga huku Jaji akisema anakubaliana na hoja zao na August 4, 2017 maombi hayo ya dhamana yataanza kusikilizwa.

Katika maombi hayo Yusuf Manji anaiomba Mahakama Kuu itengue hati ya kunyimwa dhamana iliyowasilishwa na Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) kwa kuwa ana matatizo ya kiafya akisumbuliwa na matatizo ya moyo.

27 july 2017, Wabunge wapiga kura kupinga kuondolewa kwa Obamacare Marekani

Wabunge nchini Marekani wamepiga kura na kupinga kuondolewa kwa mpango wa Obamacare

Baraza la seneti limepiga kura na kupinga wazo la Donald Trump kuondoa mpango wa Obamacare ulioanzishwa na rais wa zamani Barack Obama .

Wanachama wa Republican bungeni walipata pigo lingine baada ya wafuasi 7 wa chama chao kuungana na Democrats na kupiga kura kupinga kuondolewa kwa Obamacaare.

Matokeo ya kuraa ya maoni yalikuwa 45 kwa 55 .

27 july 2017, Mama Amuua Mwanae kisa kuwa na Masikio Marefu

Mama amemuua mwanae baada ya kutaka kumuondolea aibu ya kuwa na masikio makubwa.

Inadaiwa mama huyo amesababisha kifo hicho akidhani kwamba mwanae akibaki na masikio makubwa yatamfanya akose raha maishani mwake kulingana na sheria za Uturuki atakabiliwa na kesi ya mauaji.

Nuray Sacan mwenye umri wa miaka 37 alitoa kiasi cha fedha ili mwanae aweze kufanyiwa upasuaji kwenye hospital ya Gazi jijini Ankara lakini oparesheni hiyo haikuweza kufanikiwa baada ya masikio hayo kubaki katika hali ile ile.

Mama amedai kuwa alimpeleka mwanae chooni muda wa asubuhi lakini alishangaa kumuona mwanae akiwa amejinyomga kwa kutumia nguo yake.

Nuray baada ya kuona mwanae amepoteza maisha alitaka kukimbia kwenye gari lake lakini alijikuta akikimbilia gari tofauti na la kwake. Mama huyo alikiri kufanya mauaji hayo pale aliporudishwa hospitalini kwa gari la wagonjwa

Sacan aliwambia polisi kuwa”masikio yake yalibakia kuwa makubwa hata baada ya kufanyiwa upasuaji”