Friday, July 28, 2017

28 july 2017, Tanzania ni shwari_Twaweza

Ripoti ya Taasisi ya Twaweza imeonesha kuwa zaidi ya 53% ya Wananchi wanasema kiwango cha usalama kimeimarika katika kipindi cha mwaka mmoja uliopita huku 10% wakisema hali imekuwa mbaya zaidi.

Utafiti huo wa Sauti za Wananchi, unaojulikana kama Hapa usalama tu: Usalama, Polisi na Haki Nchini Tanzania, umebaini kwamba, wananchi wana imani kubwa na Sungusungu katika masuala ya Ulinzi na Usalama kama wanavyoliamini Jeshi la Polisi.

Utafiti huo umeleeza kuwa, pamoja na viashiria chanya kuhusu usalama, viwango vya uhalifu vinaonekana kuwa juu, ambapo 41% ya wananchi wamewahi kushuhudia uhalifu ukifanyika hadharani ndani ya mwaka mmoja uliopita.

Akizungumza wakati wa utafiti huo Mkurugenzi Mtendaji wa Twaweza, Ndg Aidan Eyakuze, amesema, takwimu za muhtasari huo zinatoa taswira tofauti kabisa na ile inayotolewa na vichwa vingi vya habari; kwa mtazamo wa wananchi wengi, usalama unaonekana kuimarika lakini ameonya kwamba, imani ya wananchi kwa jeshi la polisi bado ni ndogo.

Vilevile takwimu za utafiti zimeonesha kwamba, ni 56% tu ya wananchi wanasema kuwa wanatoa taarifa ya wizi kwa mamlaka pindi wanaposhambuliwa wao wenyewe ama nyumba zao huku ikidaiwa kwamba mara nyingi wananchi hawaombi msaada kwa polisi, hasa pale wanapokuwa wahanga wa uhalifu, ambapo ni mwananchi mmoja tu kati ya wanne sawa 26% anayeomba msaada polisi.

Hata hivyo pamoja na kuwa ulinzi umeimarika nchini uwizi umetajwa kama tishio kubwa kwenye jamii ambapo 61% ya utafiti imesema wizi huku 5% ikidai wizi wa mifugo.

Pamoja na hayo kati ya asilimia zaidi ya 90 ya watu wanaomiliki simu hawana uelewa wa kutosha kuhusu namba za dharura za jeshi la Zimamoto pamoja na jeshi la Polisi.

Chanzo Eatv

No comments: