Thursday, July 27, 2017

27 july 2017, TAASISI ZA DINI ZATAKIWA KUPIMA MAENEO YAO

Mkuu wa mkoa wa Arusha , Mrisho Gambo amewataka viongozi wa taasisi za dini kupima maeneo ya viwanja vya taasisi zao ili kuondokana na migogoro ya taasisi hizo kuporwa maeneo yao na baadhi ya viongozi wa vijiji wasio waaminifu.

Gambo amesema hayo alipokutana na viongozi wa dini, watendaji wa serikali na viongozi wa taasisi za umma kuzungumzia nafasi ya taasisi za dini katika maendeleo ya jamii ambaye pia amewaomba viongozi hao kutosita kukemea vitendo visivyo na maadili kwa viongozi wa umma na jamii.

Gambo amesema viongozi wa dini wana nafasi kubwa ya kuhamasisha jamii Kujenga umoja na kuepukana na vitendo vinavyoweza kuwagawa katika makundi ya dini ikiwemo masuala ya kisiasa.

Pia amewataka viongozi hao kuhakikisha wanapima maeneo ya taasisi zao ili kuepusha migogano inayosababishwa na baadhi ya maeneo hayo kumegwa kinyemela na baadhi ya viongozi wasiowaaminifu katika vijiji na mitaa.

Nao viongozi wa taasisi za dini wakapata nafasi ya kutoa michango yao katika sekta mbalimbali za kijamii.

Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya Arusha, Fabian daqqaro amewataka viongozi hao kuzingatia taratibu na sheria zinazowaongoza katika shughuli zao.

No comments: