Saturday, July 29, 2017

29 july 2017, Uhuru Kenyatta ashutumiwa kupanga uwizi wa kura na upinzani nchini Kenya

Uhuru Kenyatta ashutumiwa kupanga uwizi wa kura na upinzani nchini Kenya

Mpinzani mkuu na mgombea urais nchini Kenya Raila Odinga amemshutumu rais Uhuru Kenyatta kwa kufanya mpango wa kuiba kura kwa kutumia jeshi katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika mwezi Agosti.

Raila Odinga alifahamisha haya katika mkutano na waandishi wa habari jijini Nairobi ambapo alitoa ushahidi usiobahatisha uliobainika kupitia nyaraka za maafisa wa ngazi za juu katika jeshi na rais Uhuru.

Odinga ambaye ni mgombea urais Kenya kwa tiketi ya chama pinzani cha NASA alisema kwamba wamepata ushahidi unaodhihirisha kwamba Jubilee ,chama tawala kinapanga kuiba kura .

Aliendelea kufahamisha kwamba wanajeshi 226 walio na urafiki wa karibu na serikali ya sasa  wamesajiliwa upya kwa lengo la kukata umeme , maji na njia zote za mawasiliano katika maeneo ambapo yanaunga mkono upinzani .

Hata hivyo rais Uhuru amekataa madai hayo na kusema kuwa ni mpango wa upinzani kutaka kuondolewa kwa jeeshi katika kutekeleza majukumu yao.

Wakenya wanatarajiwa kuchagua serikali mpya ifikapo Agosti 8.

Chanzo Trt

No comments: