Kiungo wa Yanga Simon Msuva, ambaye jana amedondoka saini ya miaka mitatu kuitumikia klabu ya Difaa Al Jadida ya nchini Morocco ametoa neno la shukrani kwa klabu yake ya Yanga kwa mchango wao mpaka kufanikiwa kwenda kimataifa.
Msuva ambaye jana alitambulishwa rasmi na klabu hiyo kwa vyombo vya habari nchini humo amesema amefurahi na sasa ni rasmi mchezaji wa klabu hiyo iliyopo Morocco
"Ninafurahi kubwa sana kutangaza kwamba mimi sasa ni mchezaji rasmi wa Al Jadida baada ya kusaini mkataba na klabu hii, naomba nitumie nafasi hii kuwashukuru wote katika klabu yangu ya Yanga kwa kunisapoti, na kumbukumbu nzuri tulizokuwa nazo na kushirikiana pamoja kwa kipindi chote nipo hapo, siku zote mtabaki katika moyo wangu" alisema Simon Msuva
Simon Msuva alitua Yanga mwaka 2012 akitokea klabu ya Moro United na kuitumikia klabu ya Yanga kwa miaka mitano huku akiwa na mchango mkubwa katika klabu hiyo
No comments:
Post a Comment