Friday, July 28, 2017

28 july 2017, FIFA yatia maguu Tanzania

Meneja Miradi ya Maendeleo wa Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA) kwa Afrika, Mzimbabwe Solomon Mudege amewasili nchini kwa ajili ya kufuatilia mambo yanayoendelea katika shirikisho la soka Tanzania TFF.

Mudege tayari yupo nchini na pamoja na kukutana na Kamati ya Utendaji ya TFF, Dar es Salaam, pia atakuwa na kikao na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrisons Mwakyembe.

Bado haijafahamika Ofisa huyo amekuja kwa sababu zipi haswa na kama ameitwa na viongozi wa TFF au amekuja kwa maagizo ya FIFA tu.

Hata hivo hali si shwari katika uongozi wa soka Tanzania, kutokana na viongozi wakuu TFF yaani Rais Jamal Malinzi na Katibu wake Mwesigwa Selestine kuwekwa rumande tangu Juni 29 kwa tuhuma za ubadhirifu na matumizi mabaya ya madaraka na huenda Ofisa huyo akataka kujua kilichowasibu viongozi hao.

No comments: