Friday, July 28, 2017

28 july 2017 ,Pikipiki zatumika kuiba nyara za Serikali

Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya limekamata nyara za serikali ambazo ni ngozi moja ya simba na vipande 15 vya meno ya tembo vilivyokuwa vimebebwa kwenye pikipiki.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Naibu Kamishina wa Polisi Mohamed Mpinga amesema tukio hilo limetokea majira ya 10:00 alasiri mnamo Julai 27, mwaka huu katika pori la hifadhi ya taifa la Ruaha lililopo Rujewa wilayani Mbarali mkoani humo katika msako uliofaywa kwa kushirikiana na TANAPA.

DCP Mpinga amesema jeshi hilo kwa kushirikiana na TANAPA liliendesha msako na kufanikiwa kukamata nyara hizo ambazo zilizogundulika baada ya kukamata pikipiki sita ambazo wahusika wake walikimbia na kuzitelekeza, mbili zikiwa hazina ‘plate namba’ na nyingine zikiwa na usajili.

Katika matukio mengine, jeshi hilo limefanikiwa kukamata wahamiaji haramu wenye uraia wa Ethiopia saba katika nyakati tofauti katika mkoa huo baada ya kufanya msako katika maeneo mbalimbali.

No comments: