Tuesday, October 31, 2017

31 October 2017, Shambulio la anga laua 17 na kujeruhi 30 nchini Libya

Watu zaidi ya 17 wapoteza maisha na wengine 30 kujeruhiwa kwenye shambulizi la anga lililoendeshwa mashariki mwa Libya eneo la Derne.

Mpaka sasa hakuna aliedai kuendesha shambulizi hilo.

Kulingana na habari zilizotolewa na  Hospitali ya Jimbo la El-Hureysh katika mji huo, watu 17 walipoteza maisha yao katika shambulio hilo na watu zaidi ya 30 walijeruhiwa.

Tangaza la dharura lilitolewa na Hospitali hiyo ili kuita watu wajitolee kuchangia damu.

Mji wa Derne unashikiliwa na baraza la chama cha Mujahideen tangu 2015 ulipokombolewa kutoka mikononi mwa kundi la DAESH.

Derne ndiyo  mjii pekee mashariki mwa nchi ambayo hauko chini ya udhibiti wa jeshi la Khalifa Hafter.

31 October 2017,Zitto Kabwe akamatwa na kupelekwa kituo cha polisi

Kiongozi wa Chama cha ACT Wazalendo na Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe amekamatwa na Jeshi la Polisi nyumbani kwake jijini Dar es salaam  na kupelekwa kituo cha Polisi Chang’ombe.

Taarifa fupi iliyotolewa na Afisa habari wa Chama hicho Abdallah Khamis, amethibitisha kukamatwa kwa kiongozi huyo huku akibainisha kwamba sababu za kukamatwa kwake zinawezekana kuwa ni kutokana na hotuba yake aliyoitoa juzi katika kata ya Kijichi, Jijini Dar es salam.

Amesema kuwa katika hotuba yake aliyoitoa Kijichi jijini Dar es salaam, Zitto alizungumzia mambo mbalimbali kuhusu masuala ya mwenendo wa uchumi wa Taifa unavyoyumba, hivyo inawezekana ikawa ni miongoni mwa sababu za kukamatwa kwake.

Admit Dar 24

31 October 2017,MBOWE,LOWASSA:Wamfungulia milango Nyalandu kujiunga na CHADEMA

Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe amesema milango iko wazi kwa aliyekuwa mbunge wa Singida Kaskazini (CCM), Lazaro Nyalandu kujiunga na chama hicho na kuwakaribisha wengine wanaochukizwa na yanayoendelea CCM.

Akizungumza jana muda mfupi baada ya Nyalandu kutangaza kujiondoa CCM, Jijini Dar es salaam Mbowe amesema, “Chadema si ya Mbowe ni ya Watanzania, tunamkaribisha sana aje tuendeleze mapambano kwani Chadema si ya mtu.”

Mbowe ambaye pia ni Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani bungeni amesema hoja alizozitoa Nyalandu ndiyo kilio chao cha muda mrefu na kitendo chake cha kusimama hadharani na kueleza yote ni ujasiri na wengine wanapaswa kuiga mfano wake.

“Tunawakaribisha na wengine wanaochukizwa na yanayoendelea, wapo mawaziri, wabunge, Ma-RC (wakuu wa mikoa), Ma-DC (wakuu wa wilaya) na viongozi wengine wanachukizwa na ukandamizaji unaofanywa, tunawakaribisha sana, wasiogope kusema ukweli na kusimamia yale wanayoamini,” alisema

Mbowe alisema, “tunamkaribisha hata kama kuna makosa aliyoyafanya huko nyuma kama tulivyo na makosa sisi wengine, tunamkaribisha aje tufanye mambo mema kwani tunaambiwa hakuna urafiki wa kudumu au uadui wa kudumu.”

Lowassa: Tumelamba dume
Kwa upande wake Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema, Edward Lowassa amemkaribisha Nyalandu.
Akionyesha kuwa na furaha alipozungumza na Mwananchi jana Lowassa hakuwa na maneno mengi, akiyafupisha kwa kusema “tumelamba dume”.

Nyalandu (47), ambaye pia alikuwa mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM, alitumia nafasi hiyo kuomba kujiunga na Chadema, akisema anaiomba imfungulie mlango.

“Mbona amechelewa?Alitakiwa awe amejiunga muda mrefu, tena hasa wakati wa Uchaguzi Mkuu. Ninamkaribisha sana kwa sababu ni mwanasiasa mzuri na anayejua majukumu yake,” alisema Lowassa ambaye alikuwa waziri mkuu wa kwanza katika Serikali ya Awamu ya Nne.

“Nyalandu ni hazina, ni mbunge imara na ni mwanasiasa wa mfano,” alisema Lowassa, ambaye alijiunga na Chadema mwaka 2015 na kuwania urais kupitia muungano wa Umoja wa Katiba ya Watanzania (Ukawa).

Lowassa alimsifu Nyalandu kwa kuisaidia jamii na akatoa mfano jinsi alivyosaidia watoto watatu wa Shule ya Lucky Vincent waliokwenda kutibiwa Marekani baada ya kupata ajali ya basi iliyoua wanafunzi 32, walimu wawili na dereva mmoja.

“Nyalandu ana contacts (anafahamu watu wengi) nyingi na jumuiya ya kimataifa ni bidhaa nzuri kuwa nayo,” alisema Lowassa, ambaye katika uchaguzi wa urais alishika nafasi ya pili kwa kupata kura 6,072,848 (asilimia 39.97) ikiwa ni rekodi ya kura nyingi kwa upinzani tangu mfumo wa vyama vingi urejeshwe mwaka 1992.

Zitto amwambia ni uamuzi sahihi
Mbunge wa Kigoma Mjini(ACT Wazalendo), Zitto Kabwe amempongeza Nyalandu kupitia ujumbe wake aliouandika Facebook akisema ameonyesha uongozi.

“Lazaro Nyalandu, uomeonyesha uongozi. Kwa namna haki za watu zinavyovunjwa na uchumi wa nchi unavyoporomoka, unahitaji roho ngumu sana kuwa CCM. Umefanya uamuzi sahihi, wakati sahihi kwa sababu sahihi. Kila la heri,” alisema Zitto.

Mbunge wa Bukoba Vijijini ambaye pia ni Mwenyekiti wa Wabunge wa CCM, Jason Rweikiza alipoulizwa kwa njia ya simu alicheka kisha akasema hawezi kuzungumza kwa wakati huo.

Viongozi wengine wa CCM akiwemo Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Humphrey Polepole hawakupokea simu wala kujibu ujumbe kila walipotafutwa.

Monday, October 30, 2017

30 October 2017,Nyalandu aeleza sababu zilizomfanya kujiuzulu

NIMEAMUA kujiuzulu NAFASI yangu ya Ujumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi CCM, pamoja na nafasi zote za Uongozi ndani ya Chama kuanzia leo, Oktoba 30, 2017.

HALIKADHALIKA, asubuhi ya leo nimemwandikia Spika wa Bunge, Mh. Job Ndugai, Mb., barua ya kujiuzulu nafasi yangu ya UBUNGE wa Jimbo la Singida Kaskazini kupitia tiketi ya CCM, nafasi ambayo nimeitumikia kwa vipindi vinne mfululizo tangu nilipochaguliwa kwa mara ya kwanza mnamo mwaka 2000 hadi Sasa.

AIDHA, Nimechukua UAMZI huo kutokana na kutoridhishwa kwangu na mwenendo wa hali ya Kisiasa nchini, ikiwa ni pamoja na ukiukwaji wa HAKI za Kibinadamu, ongezeko la vitendo vya dhuluma wanavyofanyiwa baadhi ya watanzania wenzetu, na kutokuwepo kwa mipaka ya wazi kati ya MIHIMILI ya dola (Serikali, Bunge, na Mahakama) kunakofanya utendaji kazi wa Kibunge wa Kutunga Sheria na wa Kuisimamia Serikali kutokuwa na uhuru uliainishwa na kuwekwa bayana KIKATIBA.

VILEVILE, Naamini kwamba bila Tanzania kupata Katiba Mpya Sasa, hakuna namna yeyote ya kuifanya mihimili ya dola isiingiliane na kuwepo kwa ukomo wa wazi na kujitegemea kwa dhahiri kwa mihimili ya Serikali, Bunge na mahakama ambayo ndio chimbuko la Uongozi Bora wa nchi, na kuonesha kwa uwazi kuwa madaraka yote yatokana na wananchi wenyewe, na kwamba Serikali ni ya Watu kwajili ya Watu.

MIMI Naondoka na kukiacha Chama Cha Mapinduzi CCM, nikiwa nimekitumikia kuanzia ngazi ya Uenyekiti wa UVCCM Mkoa, Ujumbe wa Kamati za Siasa Wilaya na Mkoa, Ujumbe wa Kamati ya Wabunge Wote wa CCM na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM TAIFA, kwani nimejiridhisha kuwa kwa mwenendo wa hali ya kisiasa, kiuongozi na kiuchumi uliyopo Tanzania Sasa, CCM imepoteza mwelekeo wake wa kuisimamia Serikali kama ilivyokuwa hapo awali.

AIDHA, Naamini kuwa, kama ilivyotokea kwa mihimili ya Bunge na Mahakama kutokuwa na uhuru kamili, bila kuingiliwa kiutendaji kwa namna Moja au nyigine, CCM nayo imekuwa Chini ya miguu ya dola badala ya chama kushika hatamu na kuikosoa Serikali inapobidi kama yalivyokuwa maono ya Baba wa TAIFA MWALIMU Julius Kambarage Nyerere.

HIVYOBASI, kwa dhamira yangu, na kwa uamuzi wangu mwenyewe, nikiwa na haki ya KIKATIBA, natangaza KUKIHAMA Chama Cha Mapinduzi CCM leo hii, na nitaomba IKIWAPENDEZA wanachama wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA, basi waniruhusu kuingia MALANGONI mwao, niwe mwanachama, ili kuungana na CHADEMA na watanzania wote wanaopenda kuleta mabadiliko ya kisiasa na kiuchumi nchini kwa kupitia mfumo wa ki demokrasia na uhuru wa mawazo.

VILEVILE, nimemua kujiuzulu KITI Cha Ubunge, Jimbo la Singida Kaskazini kuruhusu kufanyika kwa UCHAGUZI mwingine ili wananchi wapate fursa ya kuchagua ITIKADI wanayoona inawafaa kwa majira na nyakati hizi zenye changamoto lukuki nchini Tanzania. Ni imani yangu, kamwe hayatakuwa ya bure maneno haya, wala uamuzi huu niufanyao mbele ya Watanzania leo ili kwamba, SOTE kama TAIFA tuingie kwenye mjadala wa kuijenga upya misingi ya nchi yetu.

30 October 2017,Waziri Mkuu kushughulikia migogoro ya wafugaji Mkoani Arusha

Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega amewataka wafugaji wa Ololosokwan wilayani Ngorongoro mkoani Arusha kuwa watulivu wakati suala la mgogoro kati yao na hifadhi likiwa linashughulikiwa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa.

Naibu Waziri Ulega ameeleza hayo jana katika mkutano na wafugaji hao uliofanyika kwenye Kata ya Ololosokwan wilayani humo.

Amesema Serikali ya awamu ya Tano inayoongozwa na Rais John Magufuli ni inawajali watu wanyonge hivyo wafugaji hao wavulimie na kwamba timu iliyoundwa na waziri mkuu siku za nyuma iliwashirikisha baadhi ya viongozi wao wakiwamo madiwani.

30 October 2017,Rais Magufuli awapongeza waliovunja nyumba ya CCM Jijini Mwanza

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli amewapongeza viongozi waliohusika kuvunja nyumba ya CCM iliyokuwa imejengwa katika hifadhi ya barabara jijini Mwanza.

Rais Magufuli ametoa pongezi hizo leo alipokuwa akizindua daraja la kisasa la waenda kwa miguu la Furahisha jijini humo.

“Ile nyumba moja ya CCM nayo ilikuwa kwenye road reserve (hifadhi ya barabara).

Nawashukuru viongzi wa mkoa kwa kulibomoa. Maendeleo yana madhara yake. Kwahiyo, nawashukuru Mkuu wa Mkoa, mmefanya vizuri sana,” alisema Rais Magufuli.

30 October 2017,Kuuawa kwa watu sita na saba kujeruhiwa kwa dhihirisha hofu kwa wakazi wa Ghuta nchini Syria

Hofu kubwa yatanda kwa wakazi wa Ghuta baada ya Watu 6 kuuawa na wengine 7 kujeruhiwa katika shambulizi lililotekelezwa Ghuta Mashariki nchini Syria

Ghuta Mashariki ni miongozi mwa meaneo yalikuwa yameokolewa na mashambulizi na jeshi la Uturuki kwa ushirikiano na Urusi na Iran.

Eneo hilo liliokolewa baada ya mazungumzo ya amani yaliofanyika mjini Astana nchini Kazakhstan.

Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa ni kwamba jeshi la serikali lilishambulia kijiji hicho na kusababisha vya watu 6.

Adham Mahmud amesema kuwa shambulizi hilo limewaua watu watano na mtoto mmoja katika kijiji cha Hamuriya.

Majeruhi wa shambulizi hilo walipelekwa katika hospitali zilizoko karibu na eneo la tukio kupewa matibabu.

Uongozi wa Ghuta umesema kuwa jeshi la Assad lilijenga Jumapili eneo la Sakba , Hamuriya na Karf Batna.

Sunday, October 29, 2017

29 October 2017,Wakuu wa vyombo vya usalama Somalia wafutwa kazi

Wakuu wa vyombo vya usalama nchini Somalia wamepigwa kalamu nyekundu kufuatia mashambulizi ya kigaidi ya jana Jumamosi yaliyosababisha makumi ya watu kuuawa na kujeruhiwa.

Shirika la habari la Reuters limenukuu ripoti iliyochapishwa na tovuti ya radio ya serikali ya Somalia inayosema kuwa: Baada ya kikao cha dharura cha baraza la mawaziri na wakuu wa usalama, Kamanda Mkuu wa Polisi, Jenerali Abdihakim Dahir Saiid na Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Taifa ya Intelijensia na Usalama NISA, Abdullahi Mohamed Ali wamefutwa kazi.

Miongoni mwa shakhsia waliouawa katika mashambulizi hayo ya jana Jumamosi ni Waziri wa Mambo ya Ndani wa jimbo la Kusini Magharibi, Madoobe Njunow Mohammed, Mbunge wa zamani Andinasir Garane na Kanali Yusuf Nur, afisa mwandamizi wa polisi ya federali ya Somalia.

Huku hayo yakirifiwa, idadi ya watu waliopoteza maisha katika mashambulio hayo imeongezeka na kufikia 29. Kadhalika watu 30 walijeruhiwa katika hujuma hizo, zilizolenga hoteli mashuhuri ya Nasa-Hablod katika mji mkuu wa Somalia, Mogadishu siku ya Jumamosi.

Kundi la kigaidi la al-Shabaab limedai kuhusika na hujuma hiyo. Taarifa zinasema magaidi waliwashikilia mateka watu kadhaa tokea jana usiku hadi leo asubuhi wakati maafisa wa polisi walipoingilia kati na kuwanushuru mateka hao.

Maafisa wa usalama wanasema wamefanikiwa kuwakamata wakiwa hai magaidi watatu huku wengine wawili wakijilipua baada ya kufyatuliwa risasi.

Mashambulio ya jana Jumamosi yamejiri wiki mbili bada ya watu 350 kuuawa katika hujuma nyingine ya kigaidi mjini Mogadishu ambayo ilitajwa kuwa hujuma mbaya zaidi ya kigaidi kuwahi kushuhudiwa Somalia.

29 October 2017,Rais Magufuli kuzindua daraja la Furahisha na miundombinu mingine kesho Mkoani Mwanza

Rais John Pombe Magufuli anatarajiwa kufanya ziara ya siku mbili ya kikazi mkoani Mwanza na kufungua miradi minne inayolenga kuboresha uchumi wa nchi.

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella alisema rais ambaye atafanya ziara kesho na kesho kutwa, ataongozana na viongozi wengine hadi katika Daraja la Furahisha na kulizindua.

Daraja hilo limejengwa ili kurahisisha mawasiliano kati ya waenda kwa miguu na vyombo vya moto.

Mkuu huyo wa mkoa alisema baadaye rais ataelekea Nyakato wilayani Nyamagana kufungua Kiwanda cha Sayona Drinks Limited na kuhitimisha ziara kwa siku hiyo.

Jumanne, rais atafungua Kiwanda cha Victoria Moulders and Polybags, kilichopo Igogo jijini Mwanza.

Alisema siku hiyo hiyo, ataelekea Buhongwa kwa ajili ya kufungua Kiwanda cha Dawa cha Prince Pharmaceutical Industry.

Mkuu huyo wa Mwanza aliomba ushirikiano kutoka kwa wananchi na wadau wengine ili kufanikisha ziara ya Rais Magufuli.

“Naamini mkoa wetu umejaaliwa amani na ulinzi wa kutosha, hivyo basi, sitarajii kusikia ripoti yeyote ya utovu wa nidhamu,” alisema Mongella.

29 October 2017,Wabunge washerehesha mada kuhusu,DC ma RC

Hoja ni kiongozi gani kati ya wabunge, wakuu wa wilaya na mikoa ni mkubwa kwa cheo imeibuka kwenye semina ya wabunge mjini Dodoma.

Hoja hiyo imeibuka leo Jumapili Oktoba 29,2017 katika semina ya wabunge wa kamati mbili za Bunge kuhusu masuala ya kidiplomasia na itifaki.

Semina hiyo imeandaliwa na Bunge kupitia mradi wa kujengea uwezo wabunge na wawakilishi unaofadhiliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Maendeleo (UNDP).

Washiriki wa semina ni wajumbe wa Kamati ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama; Kamati ya Hesabu za Serikali (PAC) na wawakilishi kutoka vyama vya kibunge.

Akizungumza katika majadiliano, Mbunge wa Sumbawanga Mjini (CCM), Aeshi Hillal ametoa mfano wa ziara za kikazi akisema mbunge huwekwa wa mwisho, akitanguliwa na mkuu wa mkoa na mkuu wa wilaya.

“Unakuta mkoa katika ziara gari la mbele yupo RC ameweka bendera, linalofuatia ni la DC naye ameweka bendera na la mbunge linakuwa nyuma. Tunaomba utufafanulie katika hilo,” amesema.

Katika hilo, Mbunge wa Morogoro Kusini-Mashariki (CCM), Omary Mgumba amesema mkuu wa wilaya anamwakilisha Rais na katika wilaya nyingine huwa zina
majimbo mawili ya uchaguzi, hivyo kumfanya mbunge kuwa na eneo dogo la kiutawala ikilinganishwa na mkuu wa wilaya.

“Siku zote ukweli ni mchungu na hasa ukiwa hutaki kuusikia.

Utakuta wilaya moja ina majimbo mawili, mbunge wa jimbo moja utawala wake ni kwenye jimbo lake tu lakini mkuu wa wilaya ni mtawala katika majimbo yote mawili yaliyo katika wilaya yake,” amesema.

Akizungumzia hilo, Mbunge wa Mtambile (CUF), Mosoud Abdallah, amehoji itifaki inazungumzaje kuhusu mbunge wa jimbo na wa viti maalumu wanapokuwa jimboni.

“Tunapokuwa jimboni ni mbunge gani anakuwa mkubwa kwa cheo kati ya mbunge wa viti maalumu na wa jimbo,” amehoji.

Akijibu hoja hizo, ofisa kutoka Wizara ya Mambo ya Nje, Kitengo cha Uhusiano wa Kimataifa, Ally Masabo amesema kiitifaki mkuu wa mkoa ndiye mwenye mamlaka katika mkoa, hivyo ndiye anayetakiwa kuwa mbele katika msafara mkoani.

"Suala hili wabunge wana wajibu wa kuangalia, na utatuzi upo kwenu wabunge," amesema Masabo ambaye ametoa mada katika semina hiyo

29 October 2017,MAKONDA-Serikali inaendelea kurekebisha miundombinu iliyoharibiwa na mvua

MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amesema serikali inaendelea na jitihada za kurekebisha miundombinu iliyoharibiwa na mvua, zilizonyesha hivi karibuni ili wananchi waendelee na shughuli za kiuchumi.

Aidha, Makonda amesema Benki ya Dunia imetoa Sh bilioni moja kwa ajili ya kusafisha eneo la Jangwani, bonde la Mto Msimbazi na kazi ya usafishaji inatarajiwa kuanza wiki ijayo baada ya kukamilisha hatua za kumpata mkandarasi.

Makonda alisema hayo jana wakati wa ziara ya kukagua athari, zilizosababishwa na mvua hizo katika maeneo mbalimbali ya jiji na kuliagiza Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) kujenga daraja la muda katika eneo la Mbezi Beach Daraja la Malecela, lililoharibika kutokana na mvua hizo.

“Wakati Tanroads wanaendelea kurejesha miundombinu katika hali ya kawaida, Jeshi letu la (JWTZ) litatusaidia kujenga daraja la muda ili kuhakikisha watu wanapita na kuendelea na shughuli zao, niwaombe tu muwape ushirikiano wakati wakifanya kazi hiyo na mimi naamini watafanya haraka na itapitika muda mchache,” alisema wakati akiongea na wananchi wa maeneo hayo.

Aidha, Makonda alisema mbali na barabara na madaraja, pia wahusika wa umeme na maji, wanaendelea na jitihada ili kuhakikisha miundombinu hiyo inarejea na wananchi kuendelea kupata huduma hizo muhimu.

Hata hivyo, Makonda aliwataka watu wanaoishi katika maeneo hatarishi, kuondoka katika maeneo hayo ili kujiepusha na hatari wanazoweza kuzipata, kwa kuwa mvua hizo bado zinaendelea kwa mujibu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa (TMA).

Pia Makonda aliwataka wananchi wenye tabia za kuchimba michanga kwenye mito, kuacha kwa kuwa kitendo hicho kwani kinachangia uharibifu mazingira, ambayo yanawaadhibu sasa.

“Serikali inapotoa rai, siyo kwamba inawachukia inawatakia mema, niwaombe tena leo kwa unyenyekevu tuchukue tahadhari, ni kwa faida yako na familia yako, kuna baadhi tumeziba mito wengine wamefanya dampo na wengine kuchimba mchanga, jambo ambalo linaongeza madhara kuwa makubwa, ningeomba tu muwe mnatii tahadhari zinazotolewa na serikali,” alisema Makonda.

Alisema kwa Manispaa ya Kinondoni pekee, kuna nyumba 200 ambazo zipo kwenye maeneo hatarishi huku nyumba 190 zikiwa zimebomoka, hivyo ni vyema wananchi hao wakaendelea kuchukua tahadhari ili kuepusha madhara zaidi.

Saturday, October 28, 2017

28 October 2017,Sare yaibakisha Simba kileleni

Tambo za wiki nzima, utani wa hapa na pale, Yanga na Simba zimetoshana nguvu baada kutoka sare ya bao 1-1 katika mchezo mkali uliofanyika leo kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.

Simba ilikuwa ya kwanza kupata bao dakika ya 57 kupitia kwa Shiza Kichuya aliyemalizia pasi ya Erasto Nyoni ambaye naye aliuwahi mpira uliopanguliwa na kipa wa Yanga, Youth Rostand wakati akiokoa krosi ya Emmanuel Okwi.

Dakika tatu baadae, Yanga ilisawazisha bao hilo kupitia kwa Obrey Chirwa aliyemalizia kwa shuti la kawaida pasi ya Geofrey Mwashiuya.

Timu zote zilianza mpira kwa kasi kipindi cha kwanza huku Simba ikionekana kumiliki mpira zaidi, lakini ilikuwa haiko vizuri katika umaliziaji wakati Yanga ilikuwa ikifanya mashambulizi ya kustukiza kupitia kwa Chirwa na  Ajib.

Wachezaji  wanaotajwa sana kwa sasa na mashabiki wa soka hapa nchini kutokana na aksi yaop ya ufungaji, Ajib wa Yanga na Emmanuel Okwi wa Simba walidhibitiwa vilivyo na mabeki wa timu zote mbili hivyo kushindwa kupachika bao katika mchezo huo.

Kipindi cha pili Yanga walionekana kuja na mbinu mpya na kufanya mashambulizi kadhaa golini kwa Simba, lakini safu ya ulinzi iliyoongozwa na Method Mwanjali ilikuwa makini.

Hata hivyo kipindi cha pili kulikuwa na rafu za mara kwa mara kwa timu hizo na kupelekea Ajib na Juma Abdul kupewa kadi ya njano huku kwa upande wa Simba aliyeonyesha kadi ya njano ni Kichuya baada ya kuvuka hadi kwa mashabiki kushangilia bao lake alilofunga.

Katika mchezo huo Simba ilifanya mabadiliko kwa kuwatoa Laudit Mavugo,James Kotei na Mzamiru Yassin na kuwaingiza John Bocco, Jonas Mkude na Said Ndemla wakati Yanga iliwatoa Geofrey Mwashiuya na Raphael Daud na kuwaingiza Emmanuel Martin na Pato Ngonyani.

Kutokana na matokeo hayo, Simba imerejea kileleni kwa kufikisha pointi 16  sawa na Yanga na Azam, lakini ikiongoza kwa mabao ya kufunga na kufungwa.

28 October 2017,Askari wa jeshi la kutuliza ghasia (FFU) mbaroni baada ya kumuua mzazi mwenzake

Polisi wilayani Babati mkoani Manyara inamshikilia askari wa jeshi hilo  Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU), Cosmas James akituhumiwa kumuua mzazi mwenzake, Regina Daniel (23) kwa kumpiga risasi nne.

Chanzo cha mauaji hayo inadaiwa ni mzozo ulitokea Daniel alipomfuata James lindoni kudai fedha za matumizi ya mtoto.

Akithibitisha tukio hilo, Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Manyara, Longinus Tibishubwamu amesema lilitokea mjini Babati Ijumaa Oktoba 27,2017 saa 12:30 jioni.

Amesema askari huyo alikuwa lindoni katika Benki ya NMB tawi la Babati, mtaa wa Usalama, Kata ya Bagara.

Kaimu Kamanda Tibishubwamu amesema Daniel ni mkazi wa Mtaa wa Ngarenaro mjini Babati.

Amesema uchunguzi wa awali unaonyesha kabla ya kifo cha mwanamke huyo kulitokea mzozo kati ya wawili hao kuhusu fedha za matumizi ya mtoto.

"Wakati wakiendelea na mzozo, ndipo askari huyo kwa kutumia silaha aliyokuwa nayo alimpiga Rehema risasi nne kwenye paji la uso, kifuani na shingoni," amesema.

Amesema askari huyo alitumia silaha aliyokuwa nayo lindoni aina ya SMG mali ya Jeshi la Polisi.
Baada ya tukio, amesema askari huyo aliitelekeza silaha lindoni na kwenda kujisalimisha polisi.

Amesema askari waliokwenda eneo la tukio waliokota maganda matatu ya risasi na waliichukua silaha hiyo.

Kaimu Kamanda Tibishubwamu amesema mtuhumiwa yupo mahabusu kwa mahojiano kabla ya hatua nyingine kuchukuliwa na mwili wa marehemu umehifadhiwa katika Hospitali ya Mji wa Babati ya Mrara.

Askari wa FFU mjini Babati, aliyezungumza kwa sharti la kutotajwa jina amesema anashangazwa na tukio hilo kutokana na upole alionao James.

Amesema James ni askari mwenye nidhamu, hivyo hafahamu jambo gani limempata hadi akamuua mzazi mwenzake.

28 October 2017,Ahukumiwa miaka 24 jela kwa kusambaza ukimwi kwa kukusudia

Mhasibu mmoja nchini Italia anayeitwa Valentino Talluto amefungwa jela miaka 24 kwa kuwaambukiza virusi vya Ukimwi kwa makusudi wanawake 30.

Valentino Talluto anadaiwa kushiriki mapenzi bila kinga na wanawake wanaofikia 53 baada kugundulika kuwa na virusi vya ukimwi mwaka 2006, mwanamke mdogo katika hao akiwa na miaka 14.

Mhasibu huyo ambaye alikuwa anatumia mitandao ya kijamii na tovuti za kuchumbiana kuwawinda wanawake na mara zote wanawake walipomgundua alikanusha madai kwamba alikuwa na virusi hivyo ambavyo husababisha Ukimwi.

Pamoja na mawakili wa Talluto kumtetea mteja wao wakisema vitendo vyake havikuwa vya busara, lakini havikuwa makusudi Ijumaa jaji alimhukumu Talluto mwenye umri wa miaka 33 kifungo cha miaka 24 jela.

Talluto alijitetea kwamba wanawake wote aliokuwa nao alikuwa na mahusiano nao ya kimapenzi na kwamba lengo lake halikuwa kuwaambukiza virusi.
“Wanasema kwamba nilitaka kuwaambukiza Ukimwi watu wengi zaidi.

Kama lingekuwa ndio lengo langu ningeenda basi kwenye baa na kushiriki ngono kiholela nisingewaingiza katika maisha yangu” alisema Tallulo
Mama yake Talluto alikuwa anatumia madawa ya kulevya na aliuambukizwa pia virusi vya Ukimwi nakufariki Talluto akiwa na miaka minne.

Kwa mujibu wa vyombo vya habari Italia, mhukumiwa alilia hukumu ilipokuwa inasomwa hata hivyo, adhabu hiyo haikufikia hukumu ya kufungwa jela maisha ambayo viongozi wa mashtaka walikuwa wameomba mahakama ahukumiwe.

28 October 2017,Polisi nchini Kenya wazidi kutawanya magenge wa waandamanaji

Jana jioni jeshi la polisi nchini Kenya lilikabiliana na magenge ya wafanya fujo katika eneo la Kawangware jijini Nairobi ambapo magenge hayo yalikuwa yanapora maduka na nyumba za raia na kuchoma moto maeneo ya biashara.

Kwa mujibu wa gazeti la kila siku la Daily Nation la nchini Kenya, magenge hayo ambayo yanadaiwa kufanya fujo kulalamikia marudio ya uchaguzi wa rais uliofanyika juzi Alkhamisi, wamewashambulia na kuwajeruhi vibaya raia.

Gazeti hilo limeongeza kuwa, wafanya fujo hao wamekuwa wakifukuzana na polisi tangu siku ya Alkhamisi.

Wakazi wa eneo hilo wamesema kuwa, watu watatu wameuawa na wengine wengi kujeruhiwa katika fujo hizo wakiwemo wanafunzi watatu wa Shule ya Msingi ya Ndurarua ambao wanauguza majeraha waliyoyapata kutokana na fujo hizo.

Gazeti hilo limewanukuu watu walioshuhudia wakisema kuwa wameona kundi la takriban vijana 100 wakiingia katika eneo la Kawangware kutokea majimbo ya uchaguzi ya Waithaka na Dagoretti Kusini.

Limeandika: Nyumba na maduka yamevunjwa na mali zilizokuwemo kuporwa huku sauti za risasi zikisikika kila mahali.

Maduka yote ya barabara za 56 na 46 yakiwemo mabucha, hoteli na saluni yamevunjwa.

Hayo yamejiri huko viongozi wa muungano wa NASA wakiwataka wafuasi wao kutofanya fujo na kujiweka mbali na risasi.

Kwa upande wake, tume ya uchaguzi ya Kenya IEBC imesema inafanya jitihada kubwa za kuhakikisha inamaliza haraka zoezi la kuhesabu kura na kutangaza matokeo ambapo ni wazi kwamba mshindi wa uchaguzi huo wa marudio atakuwa ni Rais Uhuru Kenyatta baada ya mpinzani wake mkuu Raila Odinga kuususia.

Friday, October 27, 2017

27 October 2017,Burundi yawa nchi ya kwanza kujiondoa katika Mahakama ya (ICC)

Burundi imekuwa nchi ya kwanza kujiondoa katika Mahakama ya Kimataifa ya Jinai (ICC) inayotuhumiwa na viongozi wa Kiafrika kwamba, imekuwa ikiwaandama viongozi wa bara la Afrika tu.

Msemaji wa Mahakama ya Kimataifa ya Jinai ICC yenye makao yake mjini The Hague Uholanzi amethibitisha kujitoa Burundi katika mahakama hiyo na kueleza kwamba, kujitoa huko kumeanza kutekelezwa rasmi leo Ijumaa ikiwa ni mwaka mmoja tangu nchi hiyo ya Afrika Mashariki ilipomuandikia barua Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ikimjulisha kuhusu uamuzi wake huo.

Kwa muktadha huo, Burundi inakuwa nchi ya kwanza kujiondoa rasmi katika mkataba wa Rome uliounda mahakama hiyo ya kimataifa ya jinai ICC.

Nchi nyingine ambazo ziko katika mchakato wa kujitoa katika mahakama hiyo ni Afrika Kusini ambayo iliwasilisha barua yake ya kujitoa katika mahakama hiyo Machi mwaka huu na Gambia ambayo iliandika barua Februari mwaka huu pia.

Burundi kama zilivyo Afrika Kusini na Gambia inaituhumu Mahakama ya Kimataifa ya Jinai ICC kwamba, imekuwa ikiwaandama viongozi wa Afrika tu katika utendaji wake.

Burundi inajitoa rasmi katika mahakama hiyo ya ICC katika hali ambayo, serikali ya Bujumbura imekuwa ikituhumiwa na asasi mbalimbali za kutetea haki za binadamu kwamba, imekuwa ikikiuka haki za bindamu na kuwakandamiza wapinzani.

Zaidi ya watu 700 wameuawa na wengine wanaokadiriwa kufikia laki nne wamekimbilia katika nchi jirani tangu Rais Pierre Nkurunziza alipogombea urais kwa mara ya tatu mfululizo licha ya upinzani mkubwa wa vyama vya upinzani ambavyo vilisema ni kinyume cha katiba na makubaliano ya Arusha Tanzania.

27 October 2017, Mvua yasababisha uharibifu mkubwa katika mikoa ya Pwani

Mvua kubwa ya vuli ambayo imekuwa ikinyesha katika maeneo mengi pwani ya Tanzania imesababisha mafuriko na uharibifu mkubwa.

Ripoti kutoka Dar es Salaam zinasema kuwa, mvua hizo zimesababisha hasara na madhara makubwa katika mikoa mbalimbali ikiwemo ya Pwani na Dar es Salaam kiasi cha barabara kufungwa, mabasi yaendayo kwa kasi kusimamisha huduma kwa muda, watu wawili kufa na saba kunusurika kusombwa na maji.

Aidha  kwa mara ya kwanza kituo cha kupimia mvua cha Kibaha mkoani Pwani kimetumia saa 24 kupima milimita 177.9 za mvua tangu kilipoanzishwa mwaka 1964, upimaji huo umeanzia juzi saa tatu asubuhi mpaka jana muda huo, hivyo kuweka rekodi.

Jijini Dar es Salaam, kutokana na mvua zilizonyesha katika maeneo mbalimbali kwa siku mbili mfululizo, Jeshi la Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani kimefunga kwa muda baadhi ya barabara ili kuzuia maafa zaidi yasitokee.

Kutokana na mvua hizo, vijana wawili wanasemekana kupoteza maisha katika maeneo ya Tabata Kimanga na Mbezi Luis kutokana na kusombwa na mafuriko.

Kamanda wa Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani, Fortunatus Musilimu alitaja maeneo yaliyofungwa kwa muda kuwa ni Barabara ya Morogoro eneo la Jangwani, Kibaha Mizani na Barabara ya Mwai Kibaki karibu na Daraja la Malecela.

Aidha, kutokana na hilo, wananchi wanaotokea Morogoro kwenda Chalinze hadi Dar es Salaam, jana walishauriwa kutumia Barabara ya Bagamoyo na wanaotumia Barabara ya Mwai Kibaki watumie Barabara ya Coca-Cola kwenda Mwenge.

27 October 2017,Mashahidi wakili mbele ya mahakama walihaidiwa milion 17 kumua Msuya

Mahakama Kuu Kanda ya Moshi imeelezwa kuwa washtakiwa katika kesi ya mauaji ya bilionea Erasto Msuya waliahidiwa kiasi cha shilingi milioni 17 kila mmoja ili kuweza kutimiza adhma hiyo.

Hayo yamesemwa katika maelezo ya mshtakiwa wa saba katika kesi hiyo, Ally Mussa Majeshi yaliyosomwa mahakamani hapo na shahidi wa 10 wa upande wa mashtaka, Sajini Atway Omary baada ya kupokelewa kama kielelezo.

Aidha, Jopo la utetezi linaloundwa na mawakili, Hudson Ndusyepo, Majura Magafu, Emmanuel Safari na John Lundu wamepinga maelezo hayo huku wakisema mshtakiwa alitoa maelezo hayo baada ya kuteswa na polisi.

Hata hivyo, bilionea Msuya aliyekuwa akimiliki vitega uchumi mbalimbali ndani na nje ya Arusha aliuawa kwa kupigwa risasi Agosti 7, 2013 maeneo ya Mijohoroni wilayani Hai mkoani Kilimanjaro.

27 October 2017,Sugu afunguka juu ya kufungiwa kwa vyombo vya Habari

Waziri kivuli wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, na Mbunge wa Mbeya mjini, Joseph Mbilinyi maarufu kwa jina la (Sugu) ameitaka Serikali kuacha mara moja mwenendo wa kutisha, kushambulia na kudhibiti uhuru wa vyombo vya habari.

Sugu ambaye ni Mbunge wa Mbeya Mjini kupitia tiketi ya Chadema, amesema kuwa kufungiwa kwa magazeti na baadhi ya vyombo vya habari ni vitisho ambavyo vinadidimiza uhuru wa habari.

Amesema kuwa uamuzi wa serikali wa kuvifungia baadhi ya vyombo habari ni kwenda kinyume na misingi ya utoaji haki ya utoaji wa habari, ambapo kunaiathiri kwa kiasi kikubwa jamii ambayo ndiyo mlaji mkuu wa habari.

Aidha, ameongeza kuwa kifungu cha 51(1) cha sheria hiyo inayotumiwa na serikali kufungia baadhi ya vyombo vya habari, hakitoi mamlaka yeyote kwa serikali kuchukua hatua dhidi ya chombo cha habari.

“Kutokana na msingi huu, serikali inatakiwa ifikirie upya uamuzi iliochukua wa kuvifungia baadhi ya vyombo vya habari, iubatilishe maana kufungia chombo cha habari unaathiri moja kwa moja waandishi wa habari na familia zao,”amesema Sugu

Thursday, October 26, 2017

26 October 2017,CHADEMA wajipanga kumtoa Mkurugenzi wao mahabusu

Baada ya Polisi kuendelea kumshikilia  Mkurugenzi wa Chadema wa Operesheni na Mafunzo, Kigaila Benson  Jijini Dar es salaam chama hicho kimesema kimekwenda Mahakama Kuu kuiomba itoe amri kwa jeshi hilo kumfikisha kortini.

Wakati Chadema ikisema hayo, Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa akizungumza na Mwananchi leo Alhamisi Oktoba 26,2017 amesema, “Upelelezi unaendelea na huenda kesho akafikishwa mahakamani.”

Kigaila anashikiliwa na polisi tangu Jumatatu Oktoba 23,2017 aliporipoti Kituo Kikuu cha Polisi cha kanda hiyo kuitikia wito wa jeshi hilo.

Taarifa ya Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano ya Chadema, Tumaini Makene iliyotolewa leo Oktoba 26,2017 imesema baada ya kumaliza mahojiano, askari kutoka Ofisi ya Mkuu wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai Kanda Maalumu ya Dar es Salaam (ZCO), waliokuwa wakimhoji Kigaila walisema hawana mamlaka ya kumwachia kwa dhamana.

Makene amesema sababu waliyoitoa ni kwamba wakubwa na wenye mamlaka ya kuruhusu dhamana au kutoa dhamana hawakuwepo ofisini.

“Juhudi za mawakili waliokuwepo polisi kumpatia Kigaila msaada wa kisheria, kueleza kuwa dhamana ni haki yake kwa mujibu wa sheria, huku wakihoji ni kwa nini kusifanyike mawasiliano ili hao wakubwa watoe ruhusa hiyo hata kama wako nje ya ofisi, hazikufua dafu!” amesema Makene.

Amesema tuhuma alizohojiwa Kigaila zilihusu kauli za uchochezi anazodaiwa kuzitoa Septemba 12,2017 siku chama hicho kilipotoa tamko la maazimio ya kikao cha dharura cha Kamati Kuu iliyoketi kujadili tukio la kushambuliwa na kujeruhiwa  mwanasheria wa Chadema, Tundu Lissu.

Makene amesema kwa kuitikia wito wa Jeshi la Polisi na kwenda mwenyewe kituoni, ni sababu inayojitosheleza kuonyesha kuwa Kigaila ni mwaminifu na anatoa ushirikiano kwa sheria za nchi.

“Bila kumfikisha mahakamani au kumwachia huru, tafsiri yake ni kwamba Kigaila anashikiliwa na jeshi hilo kinyume cha sheria za nchi,” amesema.

Amesema Chadema imeagiza Kurugenzi ya Katiba na Sheria kuratibu na kusimamia hatua za kisheria ili kuhakikisha Kigaila anapata haki zake za msingi kwa mujibu wa sheria za nchi.

26 October 2017,NIGERIA:Mke wa kiongozi wa Boko Haramu auawa

Jeshi la Nigeria linachunguza ripoti zinazoashiria kuwa mmoja wa wake wa kiongozi wa kundi la kigaidi na kitakfiri la Boko Haram, Abubakar Shekau ameuawa katika shambulizi la anga la hivi karibuni.

Olatokunbo Adesanya, Kamanda wa Kikosi cha Anga cha jeshi hilo amesema yumkini mke huyo wa Shekau aliyetambulika kama Fitdasi aliuawa pamoja na wanachama kadhaa wa Boko Haram katika shambulizi la anga la Oktoba 19, katika kijiji cha Durwawa, mjini Konduga, katika jimbo la Borno.

Shambulizi hilo la anga lilionekana kuwa la ulipizaji kisasi kwa kuzingatia kuwa, siku moja kabla ya hujuma hiyo ya jeshi la Nigeria, wanajeshi watatu wa nchi hiyo ya magharibi mwa Afrika waliuawa baada ya kushambuliwa na genge hilo la kigaidi na la ukufurishaji, katika eneo lililoko baina ya Damboa na Maiduguri, makao makuu ya jimbo la Borno.

Fitdasi anaaminika kuwa mmoja wa wake wanne za Abubakar Shekau, huku mke mwingine akisemekana kuwa mjane wa muasisi wa genge hilo la ukufurishaji, Muhammad Yusuf ambaye alifia korokoroni nchini humo mwaka 2009.

Tangu kundi hilo lilipoanzisha mashambulizi yake mwaka 2009, limekwishaua zaidi ya watu elfu 20, na kupelekea zaidi ya watu milioni mbili na laki sita kuwa wakimbizi ndani na nje ya nchi.

26 October 2017,Askari wawili wa FFU mbaroni baada ya kupiga raia

Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam linawashikilia Askari wawili wa kikosi cha kutuliza ghasia (FFU) kwa tuhuma za kuwashambulia wananchi wa Ukonga jijini humo.

Askari hao wanashikiliwa na jeshi mara baada ya mkuu wa wilaya ya Ilala, Sophia Mjema kutoa agizo kwa jeshi hilo kuwasaka askari wote waliohusika katika tukio hilo la kuwapiga wananchi hao.

Aidha, akitoa agizo hilo, pia mkuu huyo wa wilaya alitoa wito kwa wananchi waliopigwa na askari hao kujiorodhesha majina yao kwenye Ofisi ya Ofisa Mtendaji Kata ili kuweza kuona namna ya kuwasaidia.

Wananchi hao wa Ukonga Mombasa waliandamana na kufunga barabara kwa madai ya kuchoshwa ma mateso ambayo wamekuwa wakiyapata ikiwemo kupigwa kutoka katika kikosi hicho kilichopo Mombasa.

Kwa upande wake Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam, Lazaro Mambosasa amesema kuwa mpaka sasa wanawashikilia askari wawili na bado linaendelea na uchunguzi

Wednesday, October 25, 2017

25 October 2017,BULAYA :Mbunge mmoja wa CHADEMA ni sawa na 100 wa CCM

Mbunge wa Bunda Mjini kupitia tiketi ya (CHADEMA), Ester Bulaya amesema kuwa uwezo wa wabunge wa CHADEMA kwa wanawake ni mkubwa mno ukilinganisha na uwezo wa wabunge wanawake wa CCM na kusema kuwa Mbunge mmoja wa CHADEMA ni sawa na wabunge 100 wa CCM.

Ameyasema hayo alipokuwa akihojiwa na kituo kimoja cha Televisheni nchini Kenya alipokwenda kumtembelea na kumjulia hali Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu ambaye anapatiwa matibabu kufuatia kupigwa risasi na watu wasiojulikana Septemba 7, 2017.

“Tanzania wanawake wa upinzani tuna uwezo zaidi kuliko wanawake wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kabisa, sisi tuna msemo wetu kwamba Mbunge mmoja wa CHADEMA ni sawa na wabunge 100 wa Chama Cha Mapinduzi na hiyo ni kauli ya Mwenyekiti wetu, Freeman Mbowe, sasa ukiona wabunge wengine wageni bungeni hawana uzoefu, wamekuja na wanataka kupata umaarufu anafanya vioja sisi wazoefu ambao tumepambana na kushindana na wakongwe wa kwenye chama hicho tunampuuza,”amesema Bulaya

Admit Dar24

25 October 2017,NEC yatoa vibali kwa vyama vya siasa kufanya mikutano ya hadhara

Mkurugenzi wa wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Ramadhan Kailima amesema Tume imetoa kibali cha mikutano ya hadhara ya kampeni ndani ya kata zitakazofanya uchaguzi mdogo wa madiwani na si nje ya kata hizo.

Kailima ametoa ufafanuzi huo leo Jumatano Oktoba 25,2017 alipozungumzia maandalizi ya uchaguzi mdogo wa madiwani katika kata 43 utakaofanyika Novemba 26,2017.

Akihojiwa katika kipindi cha East Africa Breakfast kinachotangazwa na Redio East Africa amesema, “Ni kweli mikutano ya hadhara imezuiwa na sipendi kuzungumzia sana huko, lakini Tume inatoa kibali cha mikutano ya kampeni ya hadhara kwenye kata husika na si nje ya hizo.”

Kuhusu watakaoruhusiwa kufanya kampeni amesema, “Watakaoruhusiwa kwa mujibu wa sheria ni mgombea mwenyewe, wanachama, chama chake au mtu yeyote ambaye mgombea ataridhia kumnadi.”

Mkurugenzi huyo amesema mazungumzo yatakayoruhusiwa ni kuwashawishi wananchi kumpiga kura. “Kwa mazungumzo mengine kuna hatua zitakazofuata ambazo Tume itashughulikia,” amesema.

Oktoba 4,2017 Tume ilitangaza uchaguzi mdogo wa madiwani katika kata 43 kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo baadhi ya madiwani kufariki dunia, kujiuzulu, kutohudhuria vikao na wengine ushindi wao kutenguliwa na Mahakama.

Alisema ratiba ya mchakato wa uchaguzi huo inaanza Oktoba 26 kwa kufanya uteuzi wa wagombea wa udiwani na kampeni zitaanza Oktoba 27 na kumalizika Novemba 25.

Admit Mwananchi

25 October 2017, Rais wa Msumbiji awatumbua wakuu wa upelelezi na majeshi

Rais wa Msumbiji amewafuta kazi Mkuu wa Shirika la Upelelezi na Mkuu wa Majeshi ya nchi hiyo wiki mbili baada ya mauaji ya watu 16 katika shambulizi lililofanyika kaskazini mwa nchi hiyo.

Taarifa iliyotolewa jana na Rais Filipe Jacinto Nyusi imesema kuwa, Mkurugenzi Mkuu wa Upelelezi na Huduma za Usalama, Lagos Lidimo amefutwa kazi na nafasi yake itachukuliwa na Julio Jane aliyekuwa kamanda wa polisi ya nchi hiyo.

Imeongeza kuwa Mkuu wa Majeshi ya nchi hiyo, Graça Chongo pia ameachishwa kazi.

Hata hivyo ripoti hiyo haikuainisha nani atachukua nafasi hiyo.

Taarifa ya Rais wa Msumbiji haikutaja sababu ya kufutwa kazi maafisa hao wa juu wa masuala ya upelelezi na jeshi.

Mapema mwezi huu polisi ya Msumbiji ilikabiliana na watu waliokuwa na silaha katika bandari ya Mocimboa da Praia katika Bahari ya Hindi ambapo watu 16 waliuawa wakiwemo maafisa wawili wa jeshi la polisi.

Haikujulikana mara moja sababu ya mapigano hayo wala utambulisho wa watu waliokuwa wakipigana na polisi.

25 October 2017,Kampuni 15 kuwekeza Dar

Kampuni 15 za kibiashara na uwekezaji kutoka nchini Ujerumani zimeonyesha nia ya kuwekeza jijini Dar es Salaam.

Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Isaya Mwita akizungumza na waandishi wa habari jana Jumanne 24,2017 alisema kampuni hizo zitawekeza katika sekta za mawasiliano, mafuta, viwanda vya chakula na vifaa vya umeme, elimu na Tehama.

"Tunaamini kampuni hizi zitasaidia kupatikana ajira mpya kwa vijana na kuboresha sekta ya uwekezaji," amesema.

Amesema baada ya mazungumzo kampuni hizo zimeonyesha nia ya kushirikiana na jiji na wafanyabiashara katika uwekezaji.

"Kabla ya kuondoka watakutana na wafanyabiashara kwa ajili ya mazungumzo na kubadilishana uzoefu," amesema.

Balozi wa Ujerumani nchini Tanzania, Detlef Wachter amesema wanaona fahari kuunganisha wawekezaji kutoka nchi hiyo na Tanzania.

Amesema wafanyabiashara wanapokuwa na mawazo mazuri kibiashara ni fursa kwa uwekezaji.

Dk Wachter amesema licha ya wizara na taasisi kuhamia Dodoma bado Dar es Salaam itaendelea kuvutia uwekezaji na hasa kutokana na uwepo wa bandari.

Kiongozi wa msafara wa kampuni hizo, Christoph KannengieBer amesema kampuni hizo za uwekezaji zitasaidia kuimarisha uchumi na urafiki wa kibiashara kati ya mataifa hayo mawili.

Amesema kilichowavutia wawekezaji hao kuwekeza ni jitihada za Serikali katika kupambana na rushwa na ufisadi.

KannengieBer amesema wanatarajia Tanzania itajitangaza vizuri kwa sekta binafsi ili kuvutia uwekezaji na kupunguza tatizo la ajira.

Tuesday, October 24, 2017

24 October 2017,Tegete amfagilia Dante

Jijini Mwanza. Kocha John Tegete amesifu kiwango cha juu alichoonyesha beki wa Yanga, Andrew Vicent “Dante” katika michezo ya Ligi Kuu Bara.

Tegete alisema amekuwa akimfuatilia beki huyo tangu alipokuwa Mtibwa Sugar kubaini kuwa ni mchezaji mwenye kipaji cha kipekee hapa.

Alisema bado mashabiki wa Yanga hawajamuelewa Dante kwa kuwa ni mchezaji mkimya awapo uwanjani, lakini amekuwa msaada mkubwa kwa timu yao.

Kocha huyo alisema sifa kubwa ya mchezaji huyo ni nidhamu yake hawapo uwanjani ambayo imekuwa ikimsaidia sana kucheza mechi kwa kiwango kikubwa na kuisaidie timu yake.

“Mchezaji mzuri ni nidhamu hivi ushawahi kumwona Dante ametaka kupigana uwanja hata ukimkera vipi hawezi kukasirika hivi ndivyo mabeki wanavyotakiwa kuwa,” alisema Tegete.

Mzee Tegete alisema pia uchapaji kazi wake akiwa uwanjani ndio jambo ambalo linamvutia yeye kwani anapenda mchezaji anayejituma kila wakati.

24 October 2017,Polisi Kanda Maalumu ya Dar es salaam yalaani kupigwa kwa wananchi

Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam imelaani vitendo vilivyofanywa na askari ambavyo havina maadili ya kazi.

Taarifa ya polisi ya leo Jumanne Oktoba 24,2017 imesema jalada limeshafunguliwa na uchunguzi unaendelea ili kuwabaini waliohusika kuwapiga wananchi.

Imeelezwa askari hao walijichukulia sheria mikononi baada ya mwenzao Charles Yanga kukutwa ameuawa na mwili wake kuachwa pembezoni mwa uzio wa kambi ya Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU) iliyoko Ukonga.

Kamanda wa kanda hiyo, Lazaro Mambosasa amesema Jumapili Oktoba 22,2017 walipokea malalamiko ya watu wanaosadikiwa kuwa askari kufanya msako na kuwapiga wananchi wanaoishi jirani na kambi ya FFU ambao hawana hatia.

“Jeshi la Polisi linalaani vitendo hivyo ambavyo havina maadili ya kazi za polisi. Jalada limefunguliwa na uchunguzi unaendelea ili kuwabaini watuhumiwa wa tukio hilo. Tunaomba wananchi watoe ushirikiano kutoa taarifa za wahusika waweze kuwachukulia hatua watu au askari waliohusika na matukio hayo,” amesema.

Kamanda Mambosasa amesema Oktoba 21,2017 saa sita usiku maeneo ya kambi hiyo askari wakiwa kazini walikuta mwili wa askari huyo, huku pikipiki aliyokuwa akiendesha ikiwaka taa za tahadhari.

Amesema mwili wa askari huyo ulikuwa na majeraha kwenye paji la uso na sikio moja likiwa limekatwa.

Kamanda Mambosasa amesema walipofuatilia wamebaini askari huyo aliuawa na watu wasiojulikana na kutelekezwa katika maeneo ya kambi ya polisi.

Amesema kupitia kikosi kazi cha polisi wanaendelea na msako kuhusu tukio hilo la kikatili li kuwabaini watuhumiwa waliohusika.

24 October 2017,Serikali yabainisha hatua zitakazochukuliwa kwa wala Rushwa

Serikali imesema mtumishi anayefanya kazi katika Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge Tanzania (Mkurabita) akibainika kushiriki vitendo vya rushwa atachukuliwa hatua mara moja.

Mkurabita ilianzishwa kwa lengo la kumsaidia anayemiliki ardhi kimila atambulike kisheria na apewe hati itakayomwezesha kupata mkopo ili aendeleze biashara.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Utumishi na Utawala Bora), Kapteni mstaafu George Mkuchika alitoa onyo hilo alipotembelea taasisi hiyo. Alisema asingependa kusikia kuna mwananchi anatafuta hati au wanataka eneo lake lipimwe lakini mtumishi wa Mkurabita anamweleza kuwa ili kazi yako iende haraka lazima ‘waonane’ jambo ambalo si sawa.

“Naomba muelewe, anayepambana na rushwa ni Rais mwenyewe kwa sababu Takukuru (Taasisi ya Kuzuia na Kupambana Rushwa) ipo chini yake. Pia, Mkurabita ipo chini ya Ofisi ya Rais Ikulu.

“Maana yake Waziri wa Mkurabita ni Rais John Magufuli, mimi namsaidia kwa hiyo mnapofanya kazi hapa mjue mkuu wa nchi ndiyo mwenye wizara,” alisema Kapteni Mkuchika ambaye pia ni Mbunge wa Newala Mjini (CCM).

Mratibu wa Mkurabita, Seraphia Mgembe alisema licha ya mafanikio walionayo kuna changamoto ya kutopata fedha za kutosha ili kujiendesha. Alisema mwaka 2009 Mkurabita iliomba Sh43 bilioni kwa ajili kufanya shughuli zake kulingana na mpango kazi wao, lakini fedha walizopata hadi sasa ni asilimia 55 sawa na Sh23 bilioni.

24 October 2017,Watoto nchini Yemen wakabiliwa na ugonjwa wa kipindupindu na njaa

Ofisi ya Uratibu wa Misaada ya Kibinadamu ya Umoja wa Mataifa jana ilitoa taarifa na kueleza kuwa uvamizi wa kijeshi wa Saudi Arabia huko Yemen na uharibifu na kusisitiza kuwa jinai zinazofanywa na utawala wa Aal Saudia zimewasababishia watoto wa Yemen kukumbwa na mgogoro mkubwa zaidi wa chakula dunia na mlipuko wa ugonjwa wa kipindupindu.

Ofisi hiyo ya Umoja wa Mataifa imeeleza kuwa watoto milioni 11 wa Yemen wanahitaji misaada ya haraka ya kibinadamu. Taarifa ya Ofisi ya Uratibu wa Misaada ya Kibinadamu ya Umoja wa Mataifa imeongeza kuwa hakuna uwezekano wowote wa kupatikana huduma za tiba za msingi na chakula huko Yemen na kwamba watoto nchini humo hawana uwezo wa kujidhaminia mahitaji yao.

Taarifa ya Ofisi ya Uratibu wa Misaada ya kibinadamu ya Umoja wa Mataifa imeashiria pia mustakbali usiojulikana wa mamilioni yha wanafgunzi wa malefu ya walimu huko Yemen na kusisitiza mfumo wa elimu chini humo unakaribia kusambaratika.

Wanafunzi zaidi ya milioni tano wanakabiliwa na hatari ya kushindwa kuendelea na masomo.

Saudi Arabia huku ikiungwa mkona na Marekani mwezi Machi mwaka 2015 ilianzisha uvamizi wa kijeshi huko Yemen na kuweka mzingiro wa nchi kavu, baharini na anga dhidi ya nchi hiyo kwa kisingizio cha kutaka kumrejesha madarakani kibaraka wake Rais mstaafu wa Yemen Abdu Rabuh Mansour Hadi.

Monday, October 23, 2017

23 October 2017,Mwigamba ataja sababu zilizomfanya kukataa mahojiano na ACT WAZALENDO

Aliyewahi kuwa Katibu Mkuu wa ACT -Wazalendo, Samson Mwigamba ametaja sababu mbili zilizomfanya kukataa wito wa kikao cha Kamati ya Uongozi ya chama hicho Jijini Dar es salaam kwa ajili ya mahojiano.

Jumamosi Oktoba 21,2017 Kiongozi wa ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe aliwaeleza waandishi wa habari kwamba Kamati ya Uongozi ya chama hicho, ilimwita Mwigamba ili atoe maelezo baada ya kukituhumu chama hicho kukiuka misingi yake lakini hakufika.

Zitto alisema kamati hiyo baada ya kukutana na kujadiliana ilibaini hakuna misingi iliyokiukwa.
Mwigamba aliyekihama chama hicho na kujiunga na CCM, leo Jumatatu Oktoba 23,2017 amesema hakuona jambo jipya litakalojadiliwa dhidi yake katika kikao cha Kamati ya Uongozi kwa kuwa mengi aliyoyalalamikia alishayatolea ufafanuzi kwenye barua yake ya kujiuzulu.

Amesema jambo lingine lililomfanya kutohudhuria kikao hicho ni Kamati ya Uongozi kuwa na wajumbe 12 badala ya watano waliopo kwa mujibu wa Katiba ya ACT-Wazalendo.

Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mawasiliano kwa Umma wa chama hicho, Ado Shaibu amesema hawana muda wa kulumbana na Mwigamba na wanaheshimu uamuzi wake wa kujiuzulu, hivyo wanamtakia kila la kheri kwenye safari yake ya kisiasa.

23 October 2017,Mkurugenzi wa chadema atupwa rumande Dar

Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam 'limemtupa' rumande Mkurugenzi wa Operesheni na Mafunzo wa Chadema, Kigaila Benson.

Kigaila anayetuhumiwa kutoa lugha za kichochezi Oktoba 12 katika mkutano wake na waandishi wa habari, alikutana na kadhia hiyo jana aliporipoti kituoni kituo kikuu cha kanda hiyo.

Mwanasheria wa Kigaila, Frederick Kihwelo akizungumza na waandishi wa habari nje ya kituo hicho leo Jumatatu amesema hatima ya dhamana ya mkurugenzi huyo itaamuliwa kesho Jumanne.

''Amehojiwa kwa masaa 3 kuanzia saa 7 hadi saa 10  na amehojiwa kwa makosa aliyoyafanya katika mkutano wake wa Oktoba 12 na wamekataa kutoa dhamana labda hadi kesho,'' amesema Kihwelo.

''Lakini makosa yake yana dhamana ila wametueleza wanaoweza kuamua ama kupata dhamana au kukosa hawapo ofisini,"

Mwanasheria huyo amesema katika mkutano huo alizungumza mambo mengi ikiwamo kupigwa risasi kwa Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu na kutekwa kwa Ben Saanane ambaye ni msaidizi wa mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe.

Mwananchi imezungumza na kaimu kamanda wa kanda hiyo, Benedict Kitalika ambaye amesema upepelezi kwa sehemu kubwa umekamilika.

23 October 2017, Wizara ya Ardhi ,Nyumba na Maendeleo ya Makazi yatoa ufafanuzi juu ya nyumba zilizowekewa X

Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi imetoa ufafanuzi kuhusu uwekaji wa alama za X na kuvunja majengo yanayojengwa katika miji bila kibali na katika viwanja vya watu wengine walio na hati miliki za ardhi kwa dhuluma.

Taarifa ya wizara iliyotolewa leo Jumatatu Oktoba 23,2017 imesema kwa wale waliojenga kwenye viwanja vyenye hati za watu wengine kwa nguvu na kuwadhulumu wenye hati miliki haki yao ya kisheria, hatua zitachukuliwa ili kuwarudishia haki wanaostahili.

“Hatutabomoa nyumba ya mtu bali tutaendelea na urasimishaji wa makazi kwa maeneo yaliyojengwa holela ili yawe makazi rasmi na wananchi wapelekewe huduma muhimu kama vile barabara, umeme na maji,” imesema taarifa hiyo.

Wizara imesema, “Muhimu wapewe hati miliki ili ziwasaidie kiuchumi na waweze kulipa kodi ya ardhi... lakini tutazuia ujenzi mpya holela katika miji yetu kwa mujibu wa sheria.”

Taarifa imesema viongozi wote wa wilaya na mitaa wahamasishe wananchi kushiriki kikamilifu katika urasimishaji wa makazi yao kwa faida yao na Taifa kwa jumla.

23 October 2017, Mpinzani wa Serikali ya Urusi Alexei Navalny aachiwa huru kutoka kifungoni

Mpinzani wa serikali nchini Urusi Alexei Navalny atangaza Jumapili kuwa ameachwa huru kutoka kifungoni .

Mpinzani huyo alikamatwa na kuwekwa kifungoni kwa muda wa siku 20.

Alexei Navalny alikamatwa akituhumiwa kuandaa maandamano yaliopigwa marufuku na serikali.

Mpinzani huyo katika ukurasa wake katika mtandao wa kijamii aliandika kuwa yupo huru kuhu akipeperusha picha inayoashiria kuwa yupo huro katika mitaa mjini Moscow.

Navalny alitangaza kuwa atashiriki katika uchagzui mkuu unaotarajiwa kufanyika ifikapo Machi mwaka 2018.

Sunday, October 22, 2017

22 October 2017, NAPE NNAUYE:Watanzania watimize wajibu wao

Mbunge wa Mtama, kwa tiketi ya (CCM) Nape Moses Nnauye amefunguka na kuwataka watu kuacha ushamba kwani kusifu au kukosoa juu ya jambo fulani ni kazi ambazo Mungu amewapa watu kuzifanya hivyo mtu baki hupaswi kukerwa na kuhangaika na hayo.

Nape Nnauye amesema hayo kupitia ukurasa wake wa Twitter na kusema mtu ambaye anachukizwa na watu ambao wana sifu juu ya jambo fulani au kukosoa basi huyo mtu ni mshamba.

"Mungu kagawanya kazi, wengine kusifu, wengine kukosoa, wengine yote pamoja! Kwanini unakerwa na kuhangaika na mgawanyo wa kazi? !Acha ushamba" alisistiza Nape Nnauye

Aidha kiongozi huyo amezidi kusisitiza kuwa watu wanapaswa kutimiza wajibu wao na kuacha kuhangaika na watu ambao wanasifia juu ya mambo au kukosoa.

22 October 2017,Makonda akabidhiwa magari 15 ya Polisi

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam  PAUL MAKONDA amekabidhiwa magari 15 ya polisi yaliyokuwa yakitengenezwa Mkoani Kilimanjaro.

MAKONDA amesema amefikia hatua hiyo baada ya kuona changamoto zilizokuwa zikiwakabili polisi katika mkoa wake kutokana na aina ya magari waliyokuwa wanatumia.

Kamanda wa Kanda Maalumu ya DSM, LAZARO MAMBO SASA amesema kuwa uvumbuzi wa tatizo hilo la magari utasaidia katika doria na ukaguzi wa polisi kwani yametengenezwa maalumu kwa kazi hiyo.

Naye Mkurugenzi wa RSA, MANMOHAM BHAMRAH amesema anamshukuru Mkuu wa Mkoa wa DSM PAUL MAKONDA kwa kumpa nafasi hiyo ya kutengeneza magari kupitia kampuni yake.

Magari ishirini na sita yalipelekwa mkoani Kilimanjaoro kwa jaili ya matengenezo ambapo magari 15 yamepona kabisa na tayari yamekabidhiwa kwa Mkuu wa Mkoa huku magari 11 yakishindikana.

22 October 2017, 20 wapoteza maisha Yemen baada ya kushambuliwa na ndege za kivita za Marekani na Saudi Arabia

Rai wapatao 20  mkoani  Saada nchini  Yemeni wamepoteza maisha baada ya kushambuliwa na ndege za kivita za Marekani na  Saudi Arabia

Raia wengine kadhaa wamejeruhiwa katika mashambulizi hayo wakiwemo watoto watano waliolengwa kwa mabomu yaliyopigwa marufuku ya vishada.

Wakati huo huo ndege za kivita za Marekani na Saudi Arabia pia zimeshambulia mtandao wa mawasiliano wa mji wa Sheda katika mkoa huo huo wa Saada na kuuharibu kikamilifu. Ndege hizo pia zimeshambulia eneo la al Jarr katika mji wa Abas na kuua raia 4 wasio na hatia.

Ijumaa ya jana pia vibaraka wa Saudi Arabia kutoka jeshi al Sudan na wapiganaji wa Abdrabbuh Mansur Hadi walishambulia kwa mabomu miji miwili ya Midi na Haraz na kusababisha uharibifu mkubwa.

Mashambulizi hayo yanaendelea kufanywa na Saudi Arabia na washirika wake dhidi ya watu wa Yemen chini ya kimya cha jamii ya kimataifa.

Mwezi Machi mwaka 2015 Saudi Arabia ilianzisha mashambulizi ya pande zote dhidi ya nchi hiyo ya Kiislamu ikisaidiwa na Marekani, Israel na waitifaki wao na hadi sasa maelfu ya watu wakiwemo wanawake na watoto wadogo, wameuawa.

Saturday, October 21, 2017

21 October 2017, Watu watano wafariki kwa ajari Kagera

Watu watano wamekufa baada ya gari dogo la abiria aina ya Toyota Hiace kugongana na lori la mizigo katika eneo la Kasharunga barabara kuu ya Muleba –Biharamulo mkoani Kagera na kusababisha kulipuka kwa moto ulioteketeza magari hayo.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kagera, Augustino Ollomi amewataka madereva wanaoendesha vyombo vya moto kuongeza umakini wanapokuwa barabarani.

Chanzo cha ajali hii iliyokatisha uhai wa watu watano kinaelezwa kuwa ni mwendo kasi wa gari dogo la abiria aina ya Toyota Hiace lenye namba za usajili T 470 Dey lililokuwa likitoka Muleba mkoani Kagera kugongana na Lori lililokuwa limebeba shehena ya mahindi kuelekea nchini Uganda .

Inasemekana dereva wa gari dogo Magesa Masolele ambaye kwa sasa ni marehemu, alitaka kulipita trekta lililokuwa mbele yake akiwa katika mwendo mkali na kisha kukutana uso kwa uso na lori lenye nambari za usajili T 214 AJD na kusababisha kulipuka kwa moto ambao umekatisha maisha ya abiria watatu ,kondakta na dereva wa Hiace hiyo huku dereva wa lori pamoja na

21 October 2017, Waliouawa katika shambulio la Mogadishu, Somalia yafikia 358

Idadi ya watu waliouawa katika shambulio la kigaidi la siku ya Jumamosi iliyopita katika mji mkuu wa Somalia, Mogadishu imeongezeka na kufikia 358.

Waziri wa Habari wa Somalia Abdurahman Othman ametangaza kuwa kwa mujibu wa taarifa za karibuni kabisa kuhusu waathirika wa shambulio la kigaidi la mjini Mogadishu, watu wasiopungua 358 wameuawa, 228 wamejeruhiwa na wengine 56 hawajulikani waliko hadi sasa.

Abdurahman Othman ameongeza kuwa majeruhi 122 wa shambulio hilo la kigaidi wamesafirishwa kupelekwa Uturuki, Sudan na Kenya kwa ajili ya kupatiwa matibabu.

Shambulio hilo la tarehe 14 Oktoba lililofanywa kwa kutumia lori lililotegwa bomu lilitokea katika eneo la kibiashara la Hodan lenye msongamano mkubwa wa watu katika mji mkuu wa Somalia, Mogadishu.

Majengo na magari yaliyokuweko umbali wa mita mia kadhaa yaliharibiwa vibaya na mripuko mkubwa uliosababishwa na bomu hilo na watu wengi waliteketea kwa moto wakiwa hai au miili yao kukatika vipande vipande.

Kabla ya shambulio la siku ya Jumamosi iliyopita, shambulio kubwa zaidi la kigaidi kutokea nchini Somalia lilikuwa la mwezi Oktoba mwaka 2011 ambapo watu 82 waliuawa na wengine 120 walijeruhiwa.

Ijapokuwa hadi sasa hakuna mtu au kundi lolote lililotangaza kuhusika na shambulio hilo lakini viongozi wa serikali ya Somalia hawana shaka kuwa kundi la kigaidi na kitakfiri la Al Shabab ndilo lililofanya shambulio hilo

21 October 2017, Watu sita wamefariki kwa ajali tofauti moto na radi Mwanza na Tabora

Watu sita wamefariki dunia katika matukio tofauti likiwamo la mtoto Charles Samson (14), mkazi wa Kijiji cha Iseni wilayani Sengerema kupigwa radi.

Tukio hilo la mtoto Samson kupigwa na radi lilitokea juzi saa tano asubuhi wakati akiwa na wenzake 12 walipokuwa wakijisomea kujiandaa na masomo ya kidato cha kwanza mwakani.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Ahmed Msangi alisema mtoto Claud Mussa alijeruhiwa katika tukio hilo huku wenzao wakitoka salama licha ya kupata mshtuko wa kawaida.

Katika tukio lingine lililotokea wilayani Kwimba, moto ambao chanzo chake hakijajulikana uliteketeza nyumba ya Kaleb Swema iliyoko Mtaa wa Ngumo na kusababisha vifo vya watu wawili na kumjeruhi mmoja.

Waliofariki dunia ni Jackline Machumu (38) na mwanaye Juliana David (4), huku mwingine aliyejulikana kwa jina moja la Jesca akijeruhiwa na kukimbizwa hospitalini kwa matibabu.

Wakati huohuo, mtu mmoja ambaye jina lake halijajulikana amefariki dunia na wengine watatu kunusurika baada ya mtumbwi waliokuwa wakitumia kuvua samaki ndani ya Ziwa Victoria kupinduka kutokana na kupigwa na upepo mkali.

Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Tarime/Rorya, Henry Mwaibambe aliwaambia waandishi wa habari ofisini kwake juzi kuwa tukio hilo lilitokea katika Kijiji cha Nyamagaro.

Huko Igunga mkoani Tabora, wanafunzi wawili wa Shule ya Awali ya Ncheli wamefariki dunia baada ya kutumbukia kwenye kisima cha maji walipokuwa wakirejea nyumbani kutoka shule.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora, Wilbroad Mutafungwa alisema kuwa tukio hilo lilitokea katika Kijiji cha Ncheli saa tano asubuhi ya Oktoba 17 na kuwataja marehemu kuwa ni Mwashi Yohana (6) na Wande Shija (6).

“Mwenzao, Kwimba Sanongo (6), waliyekuwa wameongozana alipoona wenzake wamezama kisimani alikimbia kurejea shuleni kutoa taarifa kwa walimu ambao hata hivyo walipofika na kuwaopoa walikuta tayari wamefariki dunia,” alisema Kamanda Mutafungwa.

Friday, October 20, 2017

20 October 2017, (NECTA) yatangaza matokeo ya darasa la saba 2017

Baraza la Taifa la Mitihani (NECTA) Limetangaza Matokeo ya Mtihani wa Taifa wa Darasa la 7 mwaka 2017 Uliofanyika Septemba mwaka huu. Bonye...

http://www.necta.go.tz/matokeo/2017/psle/psle.htm

20 October 2017,Mbunge wa (CCM) apigania Katiba mpya

Wakati mbunge wa Singida Kaskazini (CCM), Lazaro Nyalandu akieleza kuwa anakusudia kuwasilisha hoja ya muswada binafsi kwa Spika utakaoweka sharti la kurejea upya mjadala wa Katiba mpya, utafiti umeonyesha kuwa wananchi wawili kati ya watatu wanasema Tanzania inahitaji Katiba mpya.

Pia, nusu ya wananchi wanasema mchakato wa Katiba uanze upya na tume mpya.

Jana kupitia katika akaunti zake za mitandao ya kijamii ya Instagram, Twitter na Facebook Nyalandu aliandika, “Nakusudia kuwasilisha kwa Spika wa Bunge, mheshimiwa Job Ndugai azma yangu ya kuleta muswada binafsi wa sheria katika kikao kijacho cha Bunge itakayoweka sharti la kurejea upya mjadala wa Katiba mpya ya Tanzania, kwa kuzingatia rasimu ya Katiba ilivyowasilishwa na Tume ya Jaji Warioba.”

Nyalandu alisema muswada huo anatarajia kuuwasilisha kwenye kikao kijacho cha Bunge.
Akizungumza na gazeti hili kwa simu baada ya kuandika maneno hayo, Nyalandu alisema amekusudia kupeleka muswada huo kwa sababu mchakato wa Katiba mpya haukufikia mwisho.

“Nitafurahi sana kama jambo hili litafanikiwa kwa kuwa lina umuhimu wake kwa kila mtu. Suala hili pia halina itikadi za vyama vya siasa na lina masilahi, kwa sababu Katiba ina uwezo wa kukaa zaidi ya miaka 100,” alieleza Nyalandu.

Mbali na Nyalandu kueleza hayo, mwezi uliopita asasi za kiraia zaidi ya 80 zilijitokeza hadharani na kutoa tamko zijusema kwamba huu ni wakati mwafaka wa mchakato wa Katiba kuanza upya ili ifikapo 2020 iwe imepatikana.
Kabla ya asasi hizo kutoa tamko, Jukwaa la Katiba lilijitokeza na kusema litaandaa maandamano ya amani kumueleza Rais John Magufuli umuhimu wa kuandika Katiba mpya.

Mbali na hayo, jana matokeo yaliyotolewa na Twaweza katika utafiti uitwao ‘Zege imelala?’ yameeleza kuwa wananchi wawili kati ya watatu wanasema Tanzania inahitaji Katiba mpya, huku nusu yao wakisema mchakato wa Katiba uanze upya na tume mpya.

Utafiti huo umesema muhtasari unatokana na takwimu kutoka sauti za wananchi ukiwa ni utafiti wa kwanza barani Afrika wenye uwakilishi wa kitaifa unaotumia simu za mikononi.

Mkurugenzi mtendaji wa Twaweza, Aidan Eyakuze alisema, “Wananchi wanataka Katiba mpya. Wengi wao wanataka mchakato uanze upya na tume mpya katika ukurasa mpya.

Hata hivyo, wapo wananchi ambao wapo tayari kusonga mbele kwa kutumia rasimu iliyoandaliwa na tume iliyotangulia.”

Pia, alisema kuwa wananchi wanaunga mkono kipengele kilichoongeza madaraka ya Bunge katika suala la kuwapitisha mawaziri walioteuliwa na kinachowapa wananchi haki ya kuwaondoa wabunge wanaozembea kazini.

Eyakuze alisema utafiti umedhihirisha uwajibikaji wa siasa kwenye uhalali wa mchakato wa Katiba.

“Matokeo yameonyesha dhahiri kwamba wananchi wengi wanatatizwa katika kutofautisha kitendo cha Ukawa kugomea Bunge la Katiba na migomo mingineyo. Ushabiki wa kisiasa huwafanya watu wengi kutozingatia uhalali wa jambo husika,” alisema.

Eyakuze alisema, “Hivyo basi; vyovyote tutakavyofufua mchakato wa Katiba ni muhimu kwa wahusika wakuu kuheshimu na kutambua kwamba sheria mama ya nchi ni ya thamani zaidi kuliko tofauti za kisiasa.

Tanzania inahitaji mchakato wa Katiba utakaozingatia uhalali na ujumuishi wa Watanzania wote.”

Taarifa ya Twaweza kwa vyombo vya habari ilisema asilimia 67 ya Watanzania wanasema ni muhimu kwa Tanzania kupata Katiba mpya na asilimia 56 wanasema toleo la mwisho la rasimu ya Katiba lipigiwe kura na wananchi.

Hata hivyo, asilimia 48 ya wananchi wanasema kwa maoni yao, Katiba mpya haitapatikana ndani ya miaka mitatu ijayo.
Taarifa hiyo ilisema wananchi wanaendelea kuunga mkono kwa nguvu kubwa uundwaji wa Katiba mpya inayotilia mkazo suala la uwajibikaji.

Ilisema asilimia 79 wanataka mawaziri wanaoteuliwa wapitishwe na Bunge na asilimia 64 wanataka wawe na uwezo wa kuwaondoa wabunge katikati ya mihula yao iwapo hawatatekeleza majukumu yao ipasavyo.

Hata hivyo, wananchi wamegawanyika kwenye baadhi ya hatua za uwajibikaji zilizopendekezwa ikiwamo kuzuia viongozi na watumishi wa umma kuwa na akaunti nje ya nchi (asilimia 52 wanaunga mkono), kuwapo kwa ukomo wa ubunge (asilimia 52 wanaunga mkono) na kuweka kanuni za uwazi na uwajibikaji kuwa sehemu ya tunu za Taifa (asilimia 48 wanaunga mkono).

Hivyo vyote ni vipengele vya rasimu ya Katiba ambavyo viliondolewa na Bunge Maalumu la Katiba.

Twaweza ilisema wananchi pia wanaunga mkono kuondolewa kwa kipengele kinachotaka kuchunguza na kudhibiti ofisi ya Rais (asilimia 55) na mawaziri kuchaguliwa kutoka nje ya Bunge (asilimia 62).

Matokeo hayo taasisi hiyo imesema yanatokana na takwimu zilizokusanywa kutoka kwa wahojiwa 1,745 kutoka maeneo mbalimbali ya Tanzania Bara (Zanzibar haihusiki kwenye utafiti huu) Juni hadi Julai 2017.

Kuhusu muundo wa Serikali ni moja kati ya vipengele vilivyoibua mjadala mzito wakati wa mchakato wa kuunda Katiba mpya na hatimaye kuwagawa wananchi.

Asilimia 42 ya wananchi wa Tanzania Bara waliunga mkono muundo wa Serikali mbili.

Twaweza imesema muundo wa Serikali moja ulikubalika kwa asilimia 25 na ule wa Serikali tatu uliopendekezwa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba ulipendwa na asilimia 16.

Mchakato wa Katiba mpya ulisimama Oktoba 2014 baada ya Tume ya Uchaguzi kudai kuwa ungeiliana na Uchaguzi Mkuu wa 2015.

20 October 2017,Kesi ya Mdee na Bulaya Mahakama Kuu kutoa uamuzi Octoba 30-2017

Mahakama Kuu Oktoba 30,2017 itatoa uamuzi wa pingamizi zilizowasilishwa na upande wa Serikali katika maombi ya wabunge wa Chadema waliosimamishwa kuhudhuria mikutano mitatu ya Bunge Jijini Dodoma kwa
kosa ya kudharau kiti cha Spika.

Wabunge hao waliosimamishwa katika Bunge la bajeti Juni, 2017 ni Halima Mdee wa Kawe na Ester Bulaya wa Bunda Mjini.

Mdee na Bulaya wamefungua mashtaka
katika Mahakama Kuu wakidai uamuzi huo umekiuka Kanuni za Bunge na Katiba.

Katika kesi hiyo jana Alhamisi Oktoba 19,2017 mawakili wa wabunge hao, Jeremia Mtobesya na Fred Kalonga wameiomba Mahakama iwaelekeze Spika wa Bunge au Katibu Bunge wawapatie taarifa walizoomba na kutoa ruhusa ya kuzitumia.

Wakili Mkuu wa Serikali, Angaza Mwipopo aliyewasilisha pingamizi kwa hati ya kiapo amedai wabunge hao hawakutumia fursa zingine walizonazo kabla ya kufungua shtaka hilo mahakamani.

Jaji Awadhi Mohamed aliyesikiliza pingamizi hizo ameahirisha maombi hayo akisema uamuzi atautoa Oktoba 30,2017.

20 October 2017, Tembo aliyekaa majini takribani siku mbili aokolewa Thailand

Wakazi wa Thailand wameshirikiana kumuokoa tembo aliyenasa katika maji yaliyosababishwa na mafuriko Kaskazini mwa nchi hiyo.

Tembo huyo alishindwa kutoka katika maji hayo kwa muda wa siku mbili.

Daktari wa wanyama alimpatia tembo huyo chanjo ya kunusuru maisha yake baada ya kuokolewa.

Thursday, October 19, 2017

19 October 2017,Mdogo wa Kanumba afunguka kilichotokea siku ya Kifo cha kaka yake

Shahidi wa kwanza wa upande wa mashtaka Seth Bosco, ambaye ni mdogo wa aliyekuwa msanii wa fani ya uigizaji, Steven Kanumba ameieleza Mahakama Jijini Dar es salaam  kwamba ndugu yake alikuwa na ugomvi na msanii mwenzake Elizabeth Michael, maarufu Lulu.

Lulu ambaye yupo nje kwa dhamana anakabiliwa na kesi katika Mahakama Kuu akishtakiwa kwa kumuua Kanumba bila kukusudia.

Anadaiwa kutenda kosa hilo Aprili 7, 2012, nyumbani kwa marehemu Kanumba, Sinza Vatican jijini Dar es Salaam.

Seth akitoa ushahidi mahakamani leo Alhamisi Oktoba 19,2017 amedai Aprili 7, 2012 Lulu alifika nyumbani kwa Kanumba saa sita kasoro dakika kadhaa usiku.

Amesema alimsikia Kanumba akimlaumu kwa kuzungumza na wanaume wengine kwenye simu mbele yake.

Shahidi huyo amedai wakati ndugu yake akimlalamikia Lulu, wawili hao walikuwa wakielekea chumbani kwa Kanumba.

Amedai baadaye wakaanza kuvutana, huku Lulu akiwa anataka kutoka na Kanumba akiwa anamvuta kuingia ndani.

Seth amesema Kanumba na Lulu waliingia chumbani na kufunga mlango lakini baadaye akiwa chumbani kwake alisikia kelele za ugomvi kati ya wawili hao.

Amesema baadaye Lulu alitoka chumbani na alimweleza kuwa Kanumba ameanguka.

Shahidi huyo amesema alikwenda chumbani kwa Kanumba ambako alikuta amekaa chini ameegemea ukuta, akiwa katika hali ya kukosa pumzi.

Seth amedai alimpigia simu daktari wao, Dk Paplas Kageiya ambaye alimtaka amfuate, hivyo wakati akielekea kwa daktari alimwambia Lulu abaki na Kanumba.

Amesema akiwa njiani, Lulu alimpigia simu akamweleza amemmwagia maji Kanumba lakini haamki, hivyo yeye anaondoka.

Shahidi huyo amesema walipofika na daktari hawakumkuta Lulu na kwamba, Dk Kageiya alishauri wampeleke Kanumba katika Hospitali ya Taifa Muhimbili ambako baada ya daktari kumchunguza aliwaeleza alikuwa ameshafariki dunia.

Baada ya ushahidi huo, Jaji Sam Rumanyika anayesikiliza kesi hiyo aliiahirisha hadi kesho itakapoendelea kwa kusikiliza shahidi mwingine wa upande wa mashtaka.

Hilo linatokana na Wakili wa Serikali, Faraja George kuieleza Mahakama hakuwa na shahidi mwingine.

Awali, Wakili George aliieleza Mahakama kuwa walikuwa na mashahidi wawili akiwemo Dk Kageiya lakini wakati wakifanya mazungumzo na shahidi huyo, aliwaeleza asingeweza kutoa ushahidi kwa kuwa hajisikii vizuri na ameomba autoe kesho.

Wakili George ameileza Mahakama awali walikuwa na mashahidi wanne lakini kulingana na maelezo ya kesi, wataomba kuongeza shahidi mwingine mmoja.

19 October 2017,Mwigamba aingia CCM na wanachama 10 wa ACT Wazalendo

Siku tatu baada ya Samson Mwigamba kujiuzulu uenyekiti wa Kamati ya Kampeni na Uchaguzi Taifa na ujumbe wa Kamati Kuu ya ACT Wazalendo Jijini Dar es salaam, amejivua uanachama na kujiunga na CCM.

Baada ya Mwigamba Jumatatu, Oktoba 16,2017 kuandika barua ya kujizulu uongozi na kueleza atabaki kuwa mwanachama wa kawaida wa ACT Wazalendo, chama hicho kilipanga kukutana Ijumaa Oktoba 20, 2017 kujadili masuala kadhaa, likiwe ..mo la kujizulu kwake.

Hata hivyo, leo Oktoba 19,2017 Mwigamba katika mkutano na waandishi wa habari jiji^^...ni Dar es Salaam, ametangaza kujivua uanachama wa ACT Wazalendo na kujiunga na CCM.

Mwigamba amesema baada ya kutafakari kwa kina ameamua pamoja na wanachama wengine 10 kukihama chama hicho.

Amezitaja sababu za kuhamia CCM kuwa ndicho chama kinachoakisi kwa karibu itikadi, falsafa na sera za ACT Wazalendo.

Amesema wanasukumwa na kufuata misingi ya azimio la Tabora ambayo kwa kiasi kikubwa CCM inalitekeleza. Pia, wamefanya hivyo ili kujiunga katika mapambano dhidi ya rushwa na ufisadi.

Mwigamba ametaja sababu nyingine ni kujitenga na upinzani unaokerwa na mafanikio ya Serikali ya Awamu ya Tano.

"Baada ya kutangaza kujivua uongozi baadhi ya viongozi wa ndani ya chama waligeuka vichaa wakinitukana kila aina ya matusi. Cha ajabu hata wale wanaofahamu na kuitetea misingi ya chama walitukanwa na viongozi wakiwepo na wamekaa kimya, hii inaonyesha wamewatuma," amesema Mwigamba.

19 October 2017, Korea Kaskazini: Vita vya nyuklia vinaweza kutokea wakati wowote

Mwakilishi wa kamisheni kuu ya Korea Kaskazini katika Umoja wa Mataifa amesema kuwa, ni suala linalowezekana sana kutokea kwa vita vya nyuklia katika Rasi ya Korea, kutokana na kuendelea maneva ya kijeshi ya Marekani na Korea Kusini katika eneo hilo.

Kim In-ryong ameyasema hayo katika hali ambayo Marekani na Korea Kusini zinaendelea na maneva ya kijeshi ya siku tano katika eneo hilo.

Inaelezwa kuwa, maneva hayo ni kati ya maneva makubwa zaidi kufanywa na Washington na Seoul.

In-ryong ambaye pia ni naibu balozi wa Korea Kaskazini katika Umoja wa Mataifa amesema kuwa, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Watu wa Korea ni nchi pekee duniani ambayo tangu mwaka 1970 imekuwa ikilengwa moja kwa moja na Marekani kwa kila aina ya vitisho.

Akiendelea amesema kuwa, maadamu siasa za uhasama za Marekani zitaendelea dhidi ya nchi yake, Pyongyang kamwe haitositisha kwa aina yoyote miradi ya silaha zake za nyuklia na makombora ya balestiki.

Katika hatua nyingine Waziri wa Mambo ya Nje wa Korea Kusini amesisitizia udharura wa ushirikiano wa karibu sana wa nchi yake, Marekani na Japan kwa ajili ya kile alichokisema kuwa ni kukabiliana na Korea Kaskazini.

Kang Kyung-hwa alisema hayo jana (Jumatano) alipokutana na Shinsuke Sugiyama, naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Japan mjini Seoul na kuongeza kuwa, ushirikiano huo wa nchi tatu utasaidia kujadiliwa hatua zinazopaswa kuchukuliwa dhidi ya Pyongyang ikiwemo vikwazo.

Naye John Sullivan Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani amefanya safari nchini Korea Kusini ambako amekutana na kufanya mazungumzo marefu na viongozi wa nchi hiyo kuhusiana na Korea Kaskazini.

Wednesday, October 18, 2017

18 October 2017,Tetesi za soka Ulaya michezoni leo Jumatano

Mshambuliaji wa Real Madrid Christiano Ronaldo, 32, anamtaka mshambuliaji wa Manchester United Marcus Rashford kujiunga na Madrid.(Don Balon in Spanish)

Mchezaji wa safu ya kati wa Manchester United Juan Mata, 29, amekataa mshahara wa pauni 375,000 kwa wiki kujiunga na ligi kuu ya China. (Daily Mail)

Meneja wa zamani wa Leicester Nigel Pearson haonekani kama mtu ambaye anaweza kuchukua usukani wa klabu hiyo kufuatia kufutwa kwa Craig Shakespeare (Leicester Mercury)

Meneja wa Wales Chris Coleman, 52, ambaye anamaliza mkataba wake mwezi ujao, anatakuwa huru kwa mazungumo kuhusu nasafi iliyo huko Leicester. (The Sun)

Meneja wa Manchester United Jose Mourinho amekataa kutangaza msimamo kuwa atasalia na klabu hiyo siku za usoni (Guardian)

Meneja wa Chelsea Antonio Conte, amekiri kuwa alijaribu kumsaini mchezaji wa kiungo cha kati Radja Nainggolan, 29, kutoka Roma wakati wa majira ya joto.(Daily Express)

Aliyekuwa meneja wa England Sam Allardyce, anasema anataka kuenda kufanya kazi nchini Marekani. (ESPN)

Newcastle United hawajapinga kuwepo mazungumzo na mfanyabiashara Amanda Staveley kuhusu kununuliwa kwa klabu hiyo. (Evening Chronicle)

Southampton wako kwenye mazungumzo na Barcelona kuhusu kuhama mshambuliaji Paco Alcacer, lakini wanakabiliwa na ushindani kutoka Lille ya Ufaransa.(Mirror)

Aston Villa wanaripotiwa kumwinda kipa Joe Lewis,30, kutoka Aberdeen. (Birmingham Mail)

Mchezaji wa kiungo cha kati wa Liverpool Roberto Firmino,26, alizuiwa kwa muda kuingia uwanja wa Mariborbaada ya kusahau kitambulisho chake. (Express)

Meneja wa Liverpool Jurgen Klop amemuambia Alex Oxlade-Chamberlain, 24 kuwa hatacheza katika safu ya kati kati hivi karibuni. (Daily Mail)

Mejeja wa England Gareth Southgate anatathinia kumuita Jay Rodriguez,28, kutoka West Bron kujiunga na kikosi chake. (Telegraph)

Barcelona wana nia ya kumsaini mshambuliaji raia wa Brazil wa umri wa miaka 16 Lincoln kutoka Flamengo. (AS - in Spanish)