Rai wapatao 20 mkoani Saada nchini Yemeni wamepoteza maisha baada ya kushambuliwa na ndege za kivita za Marekani na Saudi Arabia
Raia wengine kadhaa wamejeruhiwa katika mashambulizi hayo wakiwemo watoto watano waliolengwa kwa mabomu yaliyopigwa marufuku ya vishada.
Wakati huo huo ndege za kivita za Marekani na Saudi Arabia pia zimeshambulia mtandao wa mawasiliano wa mji wa Sheda katika mkoa huo huo wa Saada na kuuharibu kikamilifu. Ndege hizo pia zimeshambulia eneo la al Jarr katika mji wa Abas na kuua raia 4 wasio na hatia.
Ijumaa ya jana pia vibaraka wa Saudi Arabia kutoka jeshi al Sudan na wapiganaji wa Abdrabbuh Mansur Hadi walishambulia kwa mabomu miji miwili ya Midi na Haraz na kusababisha uharibifu mkubwa.
Mashambulizi hayo yanaendelea kufanywa na Saudi Arabia na washirika wake dhidi ya watu wa Yemen chini ya kimya cha jamii ya kimataifa.
Mwezi Machi mwaka 2015 Saudi Arabia ilianzisha mashambulizi ya pande zote dhidi ya nchi hiyo ya Kiislamu ikisaidiwa na Marekani, Israel na waitifaki wao na hadi sasa maelfu ya watu wakiwemo wanawake na watoto wadogo, wameuawa.
No comments:
Post a Comment