Watu zaidi ya 17 wapoteza maisha na wengine 30 kujeruhiwa kwenye shambulizi la anga lililoendeshwa mashariki mwa Libya eneo la Derne.
Mpaka sasa hakuna aliedai kuendesha shambulizi hilo.
Kulingana na habari zilizotolewa na Hospitali ya Jimbo la El-Hureysh katika mji huo, watu 17 walipoteza maisha yao katika shambulio hilo na watu zaidi ya 30 walijeruhiwa.
Tangaza la dharura lilitolewa na Hospitali hiyo ili kuita watu wajitolee kuchangia damu.
Mji wa Derne unashikiliwa na baraza la chama cha Mujahideen tangu 2015 ulipokombolewa kutoka mikononi mwa kundi la DAESH.
Derne ndiyo mjii pekee mashariki mwa nchi ambayo hauko chini ya udhibiti wa jeshi la Khalifa Hafter.
No comments:
Post a Comment