Wednesday, February 28, 2018

28 February 2018,CHADEMA-Yadai kuwa baadhi Ya watendaji wa Serikali hawatendi haki

Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA kimedai kufanya tathmini kuhusu mwenendo na hali ya kisiasa nchini kwa kipindi cha wiki mbili zilizopita na kubaini kuwa baadhi ya watendaji wa Serikali hawatendi haki.

Akizungumza na waandishi wa habari Katika Makao Makuu ya CHADEMA jijini Dar es salaam, Mwenyekiti wa Chama hicho Taifa Freeman Mbowe amesema CHADEMA hakina ugomvi na Serikali wala mhimili wa mahakama bali baadhi ya watendaji wanaoshindwa kusimamia haki.

Aidha Mbowe amezungumzia mauaji yaliyotokea katika maeneo mbalimbali nchini hususani Mkoani Morogoro ambapo amesema vitendo hivyo ni ukiukaji wa haki za binadamu na hali inaweza kuhatarisha amani ya nchi.

Baada ya mkutano huo na waandishi wa habari Mbowe na baadhi ya viongozi wa CHADEMA walikwenda kuripoti katika kituo cha Polisi kanda Maalum ya Dar es salaam ikiwa ni kiitikia wito wa jeshi hilo.

28 February 2018,Brendan Rodgers , Mikel Arteta na Thierry Henry kuwania mikoba ya Wenger

Kocha wa Monaco, Leonardo Jardim, kocha wa Ujerumani, Joachim Low, kocha Mkuu wa Celtic, Brendan Rodgers na kocha wa Manchester City, Mikel Arteta ni miongoni mwa watu awali walioorodheshwa kuwania mikoba ya Arsene Wenger

Hata hivyo kama tathmini itakayofanywa mwishoni mwa msimu huu itaridhisha, Wenger ambaye nafasi yake iko hatarini baada ya kipigo cha Jumapili katika fainali ya Carabao Cup kutoka kwa Manchester City, atalazimika kupambana ili kumalizia miezi yake 12 ya mkataba wake.

Lakini inavyoonekana sasa ndani ya Arsenal nguvu ya kumng’oa Wenger klabu hiyo ya Kaskazini mwa London mwishoni mwa msimu ni kubwa.

Tathmini ya mwishoni mwa msimu ndio itabeba mustakabali wa Wenger kama apewe nafasi nyingine ya kubaki kwa msimu mwingine au aondolewe.

28 February 2018,Watu zaidi Kumi mbaroni kwa tuhuma za mauaji ya aliyekuwa Diwani wa CHADEMA Kata ya Namwawala Mkoni Morogoro

Jeshi la Polisi Mkoani Morogoro linawashikiliwa watuhumiwa zaidi ya 10 wa mauaji ya aliyekuwa Diwani wa Chadema, Kata ya Namwawala Wilaya ya Kilombero, Godfrey Lwena

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Ulrich Matei, amesema, watuhumiwa hao wanashikiliwa kwa uchunguzi na upelelezi ukikamilika watafikishwa Mahakamani.

Lwena aliuawa na watu wasiojulikana kwa kukatwa na mapanga sehemu mbalimbali za mwili wake akiwa nyumbani kwake Februari 22,.

Kamanda Matei amesema, kwa sasa majina ya watuhumiwa hayo yanahifadhiwa ili kutoharibu uchunguzi, na kwamba yatawekwa wazi baada ya upepelezi kukamilika.

Awali, katika taarifa yake kwa vyombo vya habari Kamanda Matei, amesema, mauaji hayo yanatokana na kisasi kufuatia kifo cha mkazi wa Kata hiyo, Kennan Haule aliyeuawa na watu wasiojulikana mwanzoni mwa mwaka 2016.

Amesema mtu huyo ameuawa kufuatia mgogoro wa shamba uliopo kati ya wananchi na Bodi ya Sukari ambapo Lwena alinukuliwa akiwaambia wananchi kuwa Haule asipokufa hawatapata haki yao na baada ya siku kadhaa aliuawa.

28 February 2018,Halmashauri zote nchini zapewa Siku Saba kukamilisha miradi ya maendeleo

WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Selemani Jafo ametoa siku saba kwa halmashauri zote nchini, kukamilisha mipango ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo iliyo michache, itakayotekelezwa kwa asilimia 100.

Ametoa agizo hilo wakati anafungua kikao kazi cha kujadili Mpango wa Utekelezaji wa Miradi ya Fedha za Maendeleo za Serikali za Mitaa (LGDG) iliyoboreshwa kwa mwaka wa fedha 2017/2018 na kushirikisha wakurugenzi, wenyeviti wa halmashauri, maofisa mipango, makatibu tawala wasaidizi wa afya.

Amesema serikali inatarajia kutoa Sh bilioni 251 za maendeleo kwa ajili ya serikali za mitaa, kipaumbele cha kwanza kikiwa ni afya iliyotengewa Sh bilioni 69.

Jafo amesema, baada ya kupitia mipango ya halmashauri, imebainika kuwa halmashauri nyingi zimeelekeza fedha hizo kwenye utekelezaji wa miradi midogo isiyo na tija na kwa sasa imekubaliana na Wizara ya Fedha na Mipango kutoa fedha kwa miradi michache yenye tija.

Katibu Ofisi ya Rais, TAMISEMI, Mussa Iyombe aliwataka maofisa mipango, kufanya kazi yao kwa kuzingatia taaluma na kuacha kuwa na nidhamu ya woga katika kuweka mipango katika halmashauri zao.

"Mkatekeleze wajibu wenu ipasavyo, kwani mkifanya makosa mtasababisha halmashauri zenu kukosa fedha, hapa tuna halmashauri 10 ambazo hazitapelekewa fedha kwa sababu yenu, sasa msiwakoshe haki watu wengine," amesema.

Mkurugenzi wa Mbulu, Hudson Kamoga aliipongeza serikali kwa kuja na utaratibu huo na kusema utasaidia kuondokana na halmashauri kuwa na miradi viporo.

Mbunge wa Busokelo, Atupele Mwakibete (CCM) aliwataka wabunge, madiwani na wenyeviti wa halmashauri, kuunga mkono pendekezo la serikali la kuwa na miradi michache inayotekelezwa kwa asilimia 100 na kusisitiza kuwa mpango huo utaondoa tatizo la kuwapo kwa miradi viporo iliyokuwa ikitokana na kila diwani kutaka apate mradi.

28 February 2018,Kila mwaka Tanzania kuna ongezeko la watu milioni moja

Ripoti ya makadirio ya watu nchini inaonyesha Tanzania kuna idadi ya watu 54.2 milioni hadi kufikia mwaka 2018 huku ikieleza kuwa kila mwaka kuna ongezeko la watu milioni 1.6.

Ripoti hiyo inaonyesha Tanzania Bara ina watu 52.6 na Zanzibar milioni 1.6 inaifanya Tanzania kuwa nchi ya sita barani Afrika kwa ongezeko kubwa la watu ikitanguliwa na Nigeria, Ethiopia, DRC na Misri.

Akizindua ripoti hiyo leo Jumatano Februari 28, 2018 Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Phillip Mpango amesema idadi hiyo ya watu inakadiriwa kufikia 77.5 milioni ifikapo mwaka 2030 wakati nchi zote duniani zitakuwa zinatathmini mafanikio na changamoto za Malengo ya Mpango wa Dunia wa Maendeleo Endelevu (SDGs).

Amesema kwa kuzingatia matokeo ya sensa ya watu ya mwaka 2012, inakadiriwa kuwa kila mwaka kuna ongezeko la wastani wa watu wapatao 1.6 milioni hapa nchini.

"Ongezeko hili linatokana na idadi kubwa ya vizazi vipatavyo milioni 2 ikilinganishwa na idadi ndogo ya vifo ambavyo nintakribani 400,000 kwa mwaka," amesema.

Kutokana na takwimu hizo, Dk Mpango amesema hairuhusiwi shirika lolote kufanya makadirio ya idadi ya watu na kuchapisha makadirio hayo bila kuishirikisha Ofisi ya Taifa ya Takimu (NBS).

"Kwa kufanya hivyo ni kosa, makadirio hayo hayaendani na hali halisi ya watu na inahatarisha maendeleo ya nchi.
Takwimu za nchi ambazo vigezo vyake haviendani na hali halisi vinapotosha hali ya ustawi wa nchi na wananchi waje," amesema.

Awali Mkurugenzi Mkuu wa NBS, Dk Albina Chuwa amesema kasi hiyo kubwa ya ongezeko la watu inasababishwa na kiwango cha juu cha uzazi ambapo tafiti zinaonyesha wastani wa mwanamke kuzaa ni watoto watano kwa kipindi chake cha uzazi.

Amesema pia kasi hiyo inasababishwa na matumizi madogo ya njia za uzazi, umaskini na kiwango duni cha elimu miongoni mwa wanawake hasa katika maeneo ya vijijini.

Tuesday, February 27, 2018

27 February 2018,Waajiri 11,900 kufikishwa mahakamani

Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge Kazi Vijana Ajira na Wenye Ulemavu Anthony Mavunde ameagiza kufikishwa mahakamani kwa waajiri 11,900 nchini ambao wamekaidi agizo la serikali la kujiunga na mfuko wa fidia kwa wafanyakazi.

Naibu Waziri Mavunde ametoa agizo hilo Mkoani Mwanza wakati wa ziara yake kukagua utekelezaji wa agizo hilo ambapo amebaini kuwepo kwa waajiri ambao hawajajiunga na mfuko huo unaolenga kuwezesha wafanyakazi kupata fidia pindi wanapopatwa na matatizo kutokana na kazi wanazozifanya.

Mfuko wa fidia umeanzishwa na serikali ili kuwezesha wafanyakazi kupata fidia pindi wanapougua, kupata ajali au kufariki kutokana na kazi wanazozifanya ambapo mpaka sasa ni waajiri 12,689 ndio wamefanikiwa kujisajili kwenye mfuko huo.

27 February 2018,Njia yakuondokea Arsene Wenger yaonekana

Uongozi wa klabu ya Arsenal, huenda ukafanya mabadiliko katika benchi la ufundi mwishoni mwa msimu huu, endapo hautoridhishwa na kazi ya mzee Arsene Wenger ambaye mwishoni mwa msimu uliopita alisaini mkataba mpya wa miaka miwili.

Uongozi wa klabu hiyo ya kaskazini mwa jijini London, umepanga kufanya tathimini ya kina kuhusu mwenenndo wa mzee huyo kutoka nchini Ufaransa, baada ya kuona hali sio nzuri katika kikosi chao msimu huu.

Taarifa iliyochapishwa na kwenye gazeti la Daily Mail ya nchini England, imeeleza kuwa, uongozi wa The Gunners haukutarajia matokeo yanayopatikana hivi sasa, kufuatia imani kubwa waliyoiweka kwa babu huyo aliyedumu kwa kipindi cha miaka 20 tangu alipoajiriwa klabuni hapo.

Taaifa hiyo imeongeza kuwa, The Gunners tayari wameshaanza kuandaa orodha ya makocha wa kuwatathmini katika kumpata mbadala wa Wenger kama itaamua kuachana naye mwishoni mwa msimu.

Kocha wa Monaco, Leonardo Jardim, kocha wa Ujerumani, Joachim Low, kocha Mkuu wa Celtic, Brendan Rodgers na kocha wa Manchester City, Mikel Arteta ni miongoni mwa watu awali walioorodheshwa.

Hata hivyo kama tathmini itakayofanywa mwishoni mwa msimu huu itaridhisha, Wenger ambaye nafasi yake iko hatarini baada ya kipigo cha Jumapili katika fainali ya Carabao Cup kutoka kwa Manchester City, atalazimika kupambana ili kumalizia miezi yake 12 ya mkataba wake.

Lakini inavyoonekana sasa ndani ya Arsenal nguvu ya kumng’oa Wenger klabu hiyo ya Kaskazini mwa London mwishoni mwa msimu ni kubwa.

Tathmini ya mwishoni mwa msimu ndio itabeba mustakabali wa Wenger kama apewe nafasi nyingine ya kubaki kwa msimu mwingine au aondolewe.

Hii inamuacha apambane maswali magumu juu ya nini amevuna katika msimu hadi sasa.
Neym

27 February 2018,Viongozi wa CHADEMA waripoti kituo kikuu cha polisi

Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na viongozi wengine wa chama hicho wanakwenda kuripoti Kituo Kikuu cha Polisi.

Akizungumza na waandishi wa habari leo mchana Jumatatu Februari 27, 2018 Mbowe amesema wanakwenda kuripoti kuitikia wito wa Polisi.

Amesema katibu mkuu wa Chadema, Dk Vincent Mashinji hatakwenda kwa kuwa yupo nje ya nchi na atakaporejea atakwenda kwa kuwa hawana sababu ya kugoma.

Februari 20,2018 Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam iliagiza kukamatwa viongozi saba waandamizi wa Chadema akiwamo Mbowe.

Wito huo ulikuja siku chache baada ya tukio la kuuawa kwa mwanafunzi wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT), Akwilina Akwilini.

Akwilina aliuawa kwa kupigwa risasi akiwa ndani ya daladala eneo la Mkwajuni, Kinondoni jijini Dar es Salaam wakati polisi wakiwatawanya wafuasi wa Chadema waliokuwa wakienda ofisi za mkurugenzi wa Halmashauri ya Kinondoni kudai viapo vya mawakala wao.

Viongozi wengine mbali ya Mbowe na Dk Mashinji ni naibu makatibu wakuu, John Mnyika (Bara) na Salum Mwalimu (Zanzibar).

Pia, wamo mwenyekiti wa Baraza la Wanawake Chadema (Bawacha), Halima Mdee; mwenyekiti wa Kanda ya Serengeti, John Heche na Esther Matiko ambaye ni mweka hazina wa Bawacha.

Mdee, Matiko, Heche na Mnyika walisharipoti awali na walitakiwa kurejea kituoni leo. Viongozi wengine waliwakilishwa na wanasheria.
Mbowe akizungumza na waandishi wa habari amesema wana taarifa kuwa watakamatwa na kwamba kuna mpango wa kubambikiziwa kesi.

Monday, February 26, 2018

26 February 2018,Thierry Henry kurithi mikoba ya Arsene Wenger

Mshambulizi wa zamani wa Arsenal Thierry Henry anasema angependa kuchukua nafasi yake Arsene Wenger kama meneja wa Arsenal (Sky Sports)

Chelsea ndio wako kifua mbele katika kumsaini mshambuliaji wa Bayern Munich Robert Lewandowski. Mchezaji huyo raia wa Poland anataka kujiunga na Premier League. (Sun)

AC Milan wana mpango wa kumsaini kiungo wa kati wa Swansea raia wa Korea Kusini Ki Sung-yueng, 29. (Calciomercato - in Italian)

Arsenal wanamtaka kiungo wa kati wa Paris St-Germain, Yacine Adli 27. Manchester City, Barcelona na Juventus pia wanamwinda raia huyo wa Ufaransa. (L'Equipe, via Sun)

26 February 2018,Halmashauri ya Jiji la Mbeya yapata Diwani wa viti maalumu kutoka CHADEMA

Kufuatia kifo cha aliyekuwa Diwani wa Viti Maalumu katika Halmashauri ya jiji la Mbeya kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Ester L.

Mpwiza, Tume ya Uchaguzi katika kikao chake cha tarehe 23 Februari, 2018 imemteua Jane Japhaly Jojo kushika nafasi hiyo.

Maamuzi hayo ni kulingana na matakwa ya kifungu cha 86A cha Sheria ya Uchaguzi ya Serikali za Mitaa, Sura ya 292.

Uteuzi huu umefanyika baada ya kupokea taarifa kutoka kwa Waziri mwenye dhamana ya Serikali za Mitaa ambaye kwa mujibu wa kifungu cha 13 (1) cha Sheria ya Uchaguzi ya Serikali za Mitaa, Sura ya 292, aliitaarifu Tume ya Taifa ya Uchaguzi uwepo wa nafasi hiyo wazi baada ya kifo cha aliyekuwa Diwani wa Viti Maalum kupitia CHADEMA Ndugu Ester L. Mpwiza.

Tume baada ya kupokea Taarifa hiyo, ilikifahamisha Chama cha Demokrasia na Maendeleo Demokrasia ambacho kiliwasilisha jina la mpendekezwa wa kushika nafasi hiyo ambapo jina hilo limetoka katika orodha ya majina yaliyowasilishwa Tume ya Taifa ya Uchaguzi mwaka 2015.

26 February 2018,Jeshi la polisi lamtia mbaroni anayewafanyia vitendo vya ukatili wanawake

Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Saalaam limemkamata mkazi wa Kinondoni, Rajabu Mohamed (25) maarufu Rajeshi kwa tuhuma za kuwakamata wanawake, kuwaingiza kwa nguvu kwenye gari lake, kuwapora na kuwafanyia vitendo vya ukatili.

Akizungumza leo Februari 26, 2018, Kamanda wa Polisi wa kanda hiyo, Lazaro Mambosasa amesema mtuhumiwa huyo amekamatwa eneo la Kinondoni akituhumiwa kuwapata wanawake kwa kuwalaghai kuwa ni mfanyabiashara.

Amesema mtuhumiwa huyo baada ya kuwapora wanawake huzunguka nao katika gari na kuwatishia kuwa ni freemason na anaweza kuwaua kwa kuwanyonya damu au kuwakata maeneo mbalimbali ya miili yao.

“Kupitia vitisho hivyo wanawake walilazimika kutoa neno la siri la simu zao ambapo alichukua kadi zao za benki na kuwaibia fedha zao kupitia mashine za kutolea fedha (ATM),” amesema Mambosasa.

Amesema mbali na kuwabaka na kuwalawiti huwashusha na kuwatelekeza vichochoroni.

“Hadi sasa tumepokea kesi tatu na nilipomhoji aliniambia kuwa ni kweli alikuwa akifanya vitendo hivyo, lakini kwa sasa ameacha. Hatuwezi kuvumilia vitendo vyake. Upelelezi unaendelea ili kuwabaini wale wote anaoshirikiana nao,” amesema.

26 February 2018,Scott Westgarth afariki na ushindi mkononi

Bondia wa Uingereza, Scott Westgarth amefariki dunia kutokana na maumivu aliyoyapata katika pambano lake la Jumamosi ambalo alishinda kwa alama.

Bondia huyo mwenye umri wa miaka 31 alimshinda Dec Spelman lakini alipoenda kwenye mahojiano baada ya pambano hilo alionekana mwenye maumivu na baadaye kukimbizwa hospitalini.

Westgarth alikuwa anapambana kubeba mkanda wa ubingwa wa Uingereza. Rekodi yake ya mapambano inaonesha aliwahi kushinda mapambano sita, akapoteza mawili na kutoa sare moja.

Taarifa ya kifo chake iliyotolewa na promota wake ilieleza kuwa bondia huyo alikuwa kijana mdogo aliyekuwa akifanya kazi anayoipenda.

Shyrose akanusha kumponda JPM
Mpinzani wake katika pambano la usiku huo, Spelman alitoa heshima yake na kuonesha kusikitishwa na kifo chake.

“Nimevunjika moyo na nimeishiwa maneno ya kusema. Nitaendelea kuiombea familia ya Scott na watu wake wa karibu. Pumzika salama rafiki yangu,” aliandika.

26 February 2018,Sugu,Masonga wahukumiwa miezi mitano kwenda jela

Mahakama ya Hakimu Mkazi Mbeya imewatia hatiani mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi maarufu Sugu na Katibu wa Chadema Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, Emmanuel Masonga na kuwahukumu kifungo cha miezi mitano jela.

Hukumu hiyo imetolewa leo Februari 26,2018 na Hakimu Mkazi Mfawidhi wa mahakama hiyo, Michael Mteite.
Sugu na Masonga wamehukumiwa kwa kosa la kutumia lugha ya fedheha dhidi ya Rais John Magufuli.

Wawili hao wanadaiwa kutenda kosa hilo kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika Desemba 30,2017 eneo la Uwanja wa Shule ya Msingi Mwenge jijini Mbeya.

Sunday, February 25, 2018

25 February 2018,WOLPER-Bongo Movie inarudi kwenye chati ya zamani

Msanii wa filam nchini Wolper amefunguka na kusema sio kweli Bongo movie imekufa bali ni ilikuwa imelega tu ila hivi sasa wamepata madirector wapya hivyo wanategemea kurudi Kwenye chati kama zamani

Ameandika haya hii leo kupitia ukurasa wake wa Instagram "Oya msituchukulie poa Bongo movie hii ndio class yetu na tunapeta kazi zinafanya zituweke mjini msidharau jamani…kwanza nasikia Bongo movie tumepata director mpya tutarudi tu chatini” .amesema

25 February 2018, Magaidi wa ISIS waua watu 14 kusini mwa Yemen

Maagaidi wakufurishaji wa kundi la ISIS au Daesh wamehujumu kituo cha polisi katika mji wa bandarini wa Aden kusini mwa Yemen na kuuawa watu 14.

Kwa mujibu wa maafisa wa tiba katika hujuma hiyo ya Jumamosi iliyojiri katika mtaa wa Tawahi kusini magharibi mwa Aden, watu wengine 40, wakiwemo wanawake na watoto walijeruhiwa.

Kundi la kigaidi la ISIS lilitangaza kuhusika na jinai hiyo ambayo ilijumuisha magari mawili yaliyokuwa yamesheheni mabomu.

Hujuma hiyo ni ya kwanza ya aina yake tokea mwezi Januari wakati yalipojiri mapigano makali baina ya wanamgambo wanaotaka kujitenga eneo la kusini mwa Yemen na wafuasi wa rais wa zamani wa nchi hiyo Abdu Rabbu Mansour Hadi wanaoudhibiti mji huo.

Machafuko hayo yalijiri baada ya wanaotaka kujitenga kufanikiwa kudhibiti kambi kadhaa za kijeshi zilizokuwa zikisimamiwa na mrengo wa Hadi. Duru zinadokeza kuwa wanaotaka kujitenga kusini mwa Yemen wanaungwa mkono na Umoja wa Falme za Kiarabu huku Saudi Arabia ikiripotiwa kuunga mkono mrengo wa Hadi.

Mji wa bandarini wa Aden una umuhimu wa kistratijia na kwa msingi huo inatazamiwa malumbano ya kuwania mji huo yataendelea huku Yemen ikiendelea kushuhudia hujuma ya kila siku ya ndege za kivita za Saudia.

Saudia kwa kusaidiwa na Marekani, Israel na baadhi ya nchi za Kiarabu ilianzisha mashambulizi ya kila upande dhidi ya Yemen tangu mwezi Machi mwaka 2015 kwa lengo la kumrejesha madarakani kibaraka wake, Abdrabbuh Mansur Hadi rais wa zamani wa nchi hiyo aliyejiuzulu na kisha kukimbilia Saudia.

Hata hivyo licha ya njama hizo hadi sasa Saudia na washirika wake wameshindwa kufikia malengo yao ndani ya Yemen.

25 February 2018,Jokate atoboa siri ya mafanikio.......

Mwanamitindo Jokate Mwegelo amefunguka na kuitaka jamii ya kitanzania na wengineo kuacha tabia ya kukata tamaa katika mambo wanayopanga kuyafanya kwani kitendo hicho kinaweza kupelekea kuumiza walioko nyuma yao bila ya wao kutegemea.

Jokate ametoa ushauri huo baada ya kuonekana dibwi kubwa la vijana wa leo kushindwa kufanya biashara au jambo lolote kwa kuhofia kuchekwa na marafiki wanaomzunguka na kupelekea kukata tamaa katika uthubutu wa kufanya maamuzi ambayo yangepelekea kuinua maisha yake kwa namna moja ama nyingine.

"Kabla hujakata tamaa hebu jiulize ni watu wangapi wanaokutegemea?, ni wangapi walioko nyuma yako ambao wanatiwa moyo na mafanikio yako, ni wangapi ambao wanaku-support?. Ndio ujue kuwa kukata kwako tamaa kutaumiza wengi hata kama unahisi kuchoka hebu jitie moyo kwa ajili ya hao", amesema Jokate.

Kwa upande mwingine, Jokate amesema mtu hapaswi kukata tamaa kwa jambo lolote madamu anapumua kwa madai bado anauwezo wa kufanikiwa katika kitu chake.


25 February 2018,Mourinho awaandalia sherehe mashabiki wa United

Kocha wa Manchester United Jose Mourinho, amewataka mashabiki wa timu hiyo kujiandaa na burudani kwenye uwanja wa nyumbani wa Old Trafford, ambapo timu hiyo inatarajia kukwaana Chelsea.

Akizungumzia mchezo wa leo dhidi ya Chelsea, Mourinho amesema ana imani huo ni mchezo wa kwanza kati ya michezo mingine ambayo watacheza nyumbani ndani ya mwezi huu na Machi hivyo hana shaka kuwa watatumia vizuri uwanja wao.

“Nadhani wiki chache zijazo Old Trafford itashangaza, tuna mechi mbili kubwa za ligi, tutafanya vizuri dhidi ya Chelsea na Liverpool pamoja na mechi yetu ya ligi ya Mabingwa,”amesema Mourinho

Aidha, Baada ya mchezo wa leo dhidi ya Chelsea vijana wa Mourinho wataanza mwezi Machi na safari ya kwenda kucheza na Crystal Palace kabla ya kuwakaribisha Liverpool.

Hata hivyo, United itakuwa mwenyeji wa Sevilla kwenye mechi ya Ligi ya Mabingwa hatua 16 kabla ya kucheza robo fainali ya Kombe la FA dhidi ya Brighton. Man United kwasasa inashika nafasi ya pili ikiwa na alama 56.


25 February 2018,Mahakama kesho kutoa hatima ya Sugu

Hatima ya mbunge wa Mbeya Mjini (Chadema), Joseph Mbilinyi maarufu Sugu anayeshtakiwa kwa kosa la kutumia lugha ya fedheha dhidi ya Rais John Magufuli itajulikana kesho.

Sugu na Katibu wa Chadema Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, Emmanuel Masonga wanakabiliwa na kesi hiyo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Mbeya ambayo kesho Februari 26,2018 itatoa hukumu.

Washtakiwa wanadaiwa kutenda kosa hilo kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika Desemba 30,2017 eneo la Uwanja wa Shule ya Msingi Mwenge jijini Mbeya.

Hakimu Mkazi Mfawidhi, Michael Mteite anatarajiwa kutoa hukumu baada ya upande wa mashtaka na ule wa utetezi kukamilisha ushahidi Februari 9,2018.
Jamhuri iliwasilisha mashahidi watano na kielelezo kimoja cha sauti iliyodaiwa kurekodiwa na shahidi wa tano, Inspekta Joram Magova.

Upande wa utetezi uliwasilisha mashahidi sita wakiwamo Sugu na Masonga waliokana kutamka maneno wanayoshtakiwa kuyatoa.

Washtakiwa walitetewa na mawakili Sabina Yongo, Boniface Mwabukusi na Hekima Mwasipu kabla ya kujitoa na sasa wanawakilishwa na Peter Kibatala.
Kwa mara ya kwanza, Sugu na Masonga walifikishwa mahakamani Januari 16 na kusomewa mashtaka na Wakili wa Serikali Mkuu, Joseph Pande aliyeeleza upelelezi ulikuwa umekamilika na walikuwa tayari kuendelea na usikilizaji.

Saturday, February 24, 2018

24 February 2018,Wenger ashangazwa na kiwango cha Guardiola

Mkufunzi wa Arsenal Arsene Wenger haamini kwamba Pep Guardiola ameleta kiwango cha juu cha soka alipokuwa Barcelona na Manchester City.. (Guardian)

Mshambuliaji wa Real Madrid Gareth Bale, 28, amehusishwa na uhamisho wa klabu nyengine lakini mkufunzi wa klkabu hiyo Zinedine Zidane anasema mchezaji huyo wa Wales atakuwa muhimu sana katika kikosi hicho.(Sun)

Maafisa wa Manchester United wanakasirishwa na tabia ya ajenti wa kiungo wa kati Paul Pogba Mino Raiola, ambaye alimwambai mkufunzi wa klabu hiyo Jose Mourinho, kumchezesha mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24 raia wa Ufaransa. (Times - subscription required)

24 February 2018,Anusulika kuuawa kwa tuhuma za kumuua mwanae

MSICHANA mwenye umri wa miaka 25, Anastazia Elias, mkazi wa Kata ya Kipindu wilayani Nkasi mkoani Rukwa, amenusurika kifo baada ya kuokolewa na polisi akituhumiwa kumuua mtoto wake baada ya kujifungua.

Majirani wa msichana huyo aliyetambuliwa kama Mama Bara, walilieleza gazeti hili kuwa mama huyo ana mtoto wa mwaka mmoja, na alimuachisha kunyonya, na kwamba alikuwa akiishi na bibi yake.

Wananchi wakiwa na silaha za jadi yakiwemo mawe walianza kumshambulia mwanamke huyo wakimtuhumu kumuua mwanawe wa kiume baada ya kujifungua ambapo alimviringisha na vipande vya khanga na kuweka kwenye kikapu alichokifi cha chini ya uvungu wa kitanda chake. Kamanda wa Polisi wa Mkoa, George Kyando amethibitisha kutokea kwa tukio hilo lililotokea juzi saa nane mchana katika Kijiji cha Kipundu kilichopo mjini Namanyere wilayani Nkasi.

Kamanda Kyando alisema mtuhumiwa huyo anashikiliwa na Polisi wilayani Nkasi kwamba atafi kishwa mahakamani baada ya upelelezi wa awali wa tukio hilo kukamilika.

Wakizungumza na gazeti hili, baadhi ya wanawake kwa masharti ya kutoandikwa majina yao, walidai mtoto huyo alizikwa juzi usiku katika kaburi lililochimbwa ndani ya nyumba ambayo mama yake mzazi anaishi na bibi yake.

Akisimulia mkasa huo, Diwani wa Kata ya Kipundu, John Kapandila alisema mchana wa siku ya tukio, watoto wadogo walimuona mwanamke huyo akiwa amebeba kitu kwenye mfuko wa plastiki na kwenda chooni alipotoka hakurudi nao.

“Watoto hao walikimbia na kuwataarifu wazazi wao kuwa Mama Baraka amejifungua mtoto, lakini amemtupa chooni....

Wazazi hao walienda mbio nyumbani kwa mzazi huyo kwa mshangao wao walimkuta akipepeta mahindi nje ya nyumba alimokuwa akiishi.

“Walimpa hongera huku wakitaka kumuona mtoto, lakini aliwakatalia akidai kuwa hajajifungua na kwamba hakuwa na mimba,” alidai diwani huyo.

Kwa mujibu wa diwani, wananchi hao walimhoji huku wakitishia kumpiga ndipo alipokubali kuwa amejifungua muda mchache uliopita.

“Wananchi hao walienda chooni na wakafanikiwa kutoa mfuko wa plastiki na kubaini kuwa kilichokuwemo humo ilikuwa ni kondo ‘placenta ‘ na sio mtoto kama walivyoelezwa.

Ndipo alipowapeleka chumbani kwake na kuwaonesha mtoto alipo ambapo alikuwa amefungwa na vipande vya khanga na kuwekwa kwenye kikapu, bila shaka alikuwa akisubiri muda ufi ke akamtupe,” alieleza diwani.

Inadaiwa wananchi hao walipandwa na hasira wakiwa na silaha za jadi wakitaka kumshambulia ndipo askari polisi walipofi ka eneo hilo la tukio na kumwokoa.

24 February 2018 ,Kauli ya CHADEMA Juu ya wanachama wake waliokamatwa

Wakati Chadema wakilalamikia wanachama wake watatu kushikiliwa na polisi katika kituo cha Oysterbay wakiwa na majeraha ya risasi bila kupatiwa matibabu, Polisi Mkoa wa Kinondoni imesema hakuna mahabusu mgonjwa anayeshikiliwa bila kutibiwa.

Kwa mujibu  wa MCL Digital leo Februari 24, 2018 Mkurugenzi wa Itifaki, Mawasiliano, Uenezi na Mambo ya Nje wa Chadema, John Mrema ameeleza  kuwa wanachama hao walishambuliwa kwa risasi Februari 16, 2018.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Jumanne Murilo amesema polisi wanafanya kazi kwa mujibu wa sheria, ikiwa ni pamoja na kuhakikisha mahabusu wagonjwa wanatibiwa katika hospitali za Serikali bila malipo yoyote.

Katika ufafanuzi wake, Mrema amebainisha kuwa wanachama hao walishambuliwa kwa risasi wakati Polisi wakiwatawanya wanachama wa chama hicho waliokuwa wakielekea ofisi ya msimamizi wa uchaguzi wa ubunge Jimbo la Kinondoni kudai barua za viapo vya mawakala wao.

Amewataja kuwa ni Isaack Ngaga, Erick John na Aida Oromi.

“John na Ngaga wao walikamatwa wakiwa majumbani mwao baada ya kuruhusiwa kutoka Hospitali. Hawa hawakukamatiwa kwenye vurugu,” amesema Mrema.

“Mmoja kati yao (John) alikamatwa na watu waliojifanya watumishi wa haki za binadamu na kudai kuwa wanataka kwenda kumhoji, alipokataa ndipo walitoa vitambulisho vyao vinavyoonyesha wao ni Polisi.”

Amesema hatua iliyochukuliwa hadi sasa ni kuwaelekeza wanasheria wa Chadema kufungua kesi Mahakama Kuu kumshtaki Mwanasheria Mkuu wa Serikali na polisi, kuwataka wawafikishe mahakamani wanachama hao.

“Tumemwelekeza mwanasheria wetu kufungua kesi ili wanachama wetu hao watatu wapelekwe mahakamani na kupatiwa matibabu,” amesema Mrema.

Amesema kuendelea kushikiliwa bila kupelekwa hospitali wakati wana majeraha ni hatari kwa maisha yao, kwa kuwa vidonda hivyo vinaoza.

“Wanakaa nao kinyume na sheria, mpaka sasa walipaswa wawe wameshawapeleka mahakamani,” amesema.

Kwa upande wake, Murilo amesema sheria ipo wazi inawaelekeza mahabusu wote wanapougua kutibiwa.

“Siyo hao mahabusu wa Chadema pekee, mahabusu yeyote anapougua hupelekwa hospitali za Serikali ambako hutibiwa bure kwa mujibu wa sheria,” amesema.

“Kama wanaolalamika wangekuwa
mahabusu ningekuwa na cha kuzungumza, lakini kama wapo nje waache waendelee kusema, ninachojua hakuna mahabusu ambaye hajatibiwa.”
Mmoja wa ndugu wa Aida, Hilda Sigala amesema, “Jana nilikwenda kumtemebela ndugu yangu kituoni.

Amenieleza kuwa mpaka sasa hajapelekwa hospitali na wanampaka dawa tu ya kukausha kidonda wakati ana jeraha la risasi. Yupo kituoni tangu Februari 16.”

24 February 2018,Tundu Lissu-jaji Mtungi anastahili kujibiwa hadharani

Mbunge wa Singida Mashariki Mhe. Tundu Lissu amefunguka na kumtaka Msajili wa vyama vya siasa nchini Jaji Mtungi kujitafakari, kwani amedai kuwa Jaji huyo amekuwa ni mpofu kwa mambo mabaya wanayofanyiwa watu wa upinzani nchini. 

Lissu amesema hayo kufuatia Msajili wa Vyama vya Siasa, Jaji Francis Mutungi kuwaandikia barua CHADEMA ambayo anadai inatuhuma mbalimbali pamoja na vitisho mbalimbali 

"Nimesoma barua ya Msajili wa Vyama vya Siasa, Jaji Francis Mutungi, yenye tuhuma na vitisho vingi dhidi ya CHADEMA, bila kutoa ushahidi wowote na kwa kutegemea taarifa za upande mmoja tu, Msajili Mutungi ameituhumu CHADEMA kwa kufanya siasa za kibabe na vurugu na kukiuka Sheria ya Vyama vya Siasa na Kanuni za Maadili ya Vyama vya Siasa. Msajili Mutungi anastahili kujibiwa hadharani na kukumbushwa mambo kadhaa. Inaelekea amejisahau sana au anafikiria Watanzania ni wajinga wasioelewa mambo yake."

"Msajili wa Vyama vya Siasa amekosa sifa na uadilifu (moral authority) ya kunyooshea kidole CHADEMA au chama kingine chochote cha upinzani kuhusiana na jambo lolote linahusu Sheria ya Vyama vya Siasa na kanuni zake. Tangu 2015 nchi yetu imeshuhudia ukiukwaji mkubwa wa Sheria ya Vyama vya Siasa ukifanywa. Mikutano ya hadhara na maandamano ya amani, ambavyo ni haki ya vyama vya siasa kwa mujibu wa Sheria hiyo, imepigwa marufuku bila uhalali wowote. Msajili Mutungi hajawahi kukemea ukiukwaji huo wa sheria wala kutetea haki ya vyama vya siasa"

Tundu Lissu aliendelea kusema kuwa 

"Viongozi wa vyama vya upinzani, hasa CHADEMA, wameuawa, wametekwa nyara na kupotezwa, wamepigwa risasi katika majaribio ya kuuawa, wameteswa, wamekamatwa na kushtakiwa kwa kesi za uongo. Msajili Mutungi amekuwa bubu na kiziwi asiyesikia wala kukemea uonevu na ukandamizaji huu dhidi ya vyama anavyovisimamia. CCM na serikali yake zimetoa hongo kurubuni madiwani, wabunge na viongozi wengine wa vyama vya upinzani kujiuzulu nafasi zao. Yote ni makosa ya maadili kwa mujibu wa sheria. Msajili Mutungi hajawahi kuliona hilo. 
 

Friday, February 23, 2018

23 February 2018,Rais Magufuli ,Kenyatta kumaliza tofauti za kibiashara baina ya Tanzania na Kenya

Rais Dkt. John Pombe Magufuli na Rais wa Kenya Uhuru Muigai Kenyatta wamewaagiza Mawaziri wa Tanzania na Kenya kutatua tofauti ndogondogo zinazojitokeza katika biashara kati ya nchi hizo mbili.

Marais hao wametoa maagizo hayo leo asubuhi tarehe 23 Februari, 2018 walipokutana na kufanya mazungumzo katika hoteli ya Munyonyo mjini Kampala muda mfupi kabla ya kuanza kwa vikao vya mkutano wa wakuu wa nchi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Dkt. Magufuli na Rais Kenyatta wamesema wanataka kuona biashara kati ya Tanzania na Kenya inazidi kukua na bidhaa zinauzwa na kununuliwa baina ya nchi hizo bila vikwazo vyovyote na hivyo kuagiza tofauti zilizojitokeza katika baadhi ya bidhaa zimalizwe.

Kuna mambo madogo madogo yanakuwa yanajitokeza katika biashara kati ya Kenya na Tanzania, tunataka kwa haya yote Mawaziri wa Kenya na Mawaziri wa Tanzania wakae kuyatatue, sisi hatuna tatizo, mambo mengine madogo madogo mno, mambo ya viatu, nguo, ngano, gesi ni madogo sana, mnatakiwa myatatue nyinyi yasifike kwetu, sisi huku tuko sawa sawa” amesema Rais Magufuli na kuungwa mkono na Rais Kenyatta.

Wametoa maagizo hayo kwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wa Tanzania Dkt. Augustine Mahiga, Waziri wa Katiba na Sheria wa Tanzania Prof. Palamagamba Kabudi, Waziri wa Mambo ya Nje wa Kenya Balozi Monica Juma na Waziri wa Afrika Mashariki na Maendeleo ya Ushoroba wa Kaskazini wa Kenya Mhe. Peter Munya.

23 February 2018,Real Madrid yamvaa Sterling

Real Madrid inamchunguza winga wa Manchester City Raheem Sterling, 23, ambaye hajaanza mazungumzo rasmi ya kuongeza kandarasi mpya na klabu yake .Mkataba wa raia huyo wa Uingereza unakamilika 2020. (Mirror)

Kipa wa Spain David de Gea, 27, anatarajiwa kuandikisha kandarasi mpya na klabu ya Manchester United akiipuzilia mbali uhamisho wake kuelekea Real Madrid. (Times - subscription)

23 February 2018,T.I Apiga vita umiliki wa silaha za moto zinazotumika katika mauaji ya halaiki

Mwanamuziki wa muziki wa Rap nchini Marekani  Clifford Joseph Harris Jr. maarufu Kama T.I amezungumzia mpango wa Serikali ya nchi yake kuweka sheria kali inayobana umiliki wa silaha za moto kutokana na mauaji ya kutumia silaha dhidi ya halaiki ya watu nchini humo, ambapo hivi karibuni shule ya Douglas imekuwa mfano.

T.I ameiambia TMZ kuwa anaamini inapaswa kuwa na vikwazo vya hali ya juu kwa umiliki wa silaha kwa watu ambao wana matatizo ya akili.

Lakini alieleza kuwa ana hofu kama raia watanyang’anywa silaha, Serikali inaweza kuwageuza watumwa.

“Ninahisi kama mtu atapoteza haki ya kumiliki silaha kama mwananchi, unairahisishia Serikali kuwageuza wananchi watumwa, wanapokuwa hawana haki ya kuwa na silaha za moto,” alisema T.I.

Rapa huyo ni mmoja kati ya watu waliowahi kushtakiwa kwa makosa ya kumiliki silaha kinyume cha sheria.

Mkali huyo wa ‘Live Your Life’ alisema kuwa anachokiona sasa kama tatizo zaidi ni mpasuko au ubovu wa mfumo wa uongozi.

23 February 2018,Dhamana yamtoa Zitto Mahabusu

Kiongozi wa Chama cha ACT Wazalendo, Zitto Kabwe ameachiwa kwa dhamana ya maneno ya Sh50 milioni na kudhaminiwa na wakili wake, Lazarus Mvula.

Kiongozi huyo alishikiliwa tangu jana alipokamatwa kwa kufanya mkusanyiko bila kibali. Zitto alikamatwa katika Kata ya Kikeo iliyopo wilayani Mvomero na alitarajiwa kuhojiwa katika Kituo Kikuu cha Polisi Dakawa lakini akahamishiwa Morogoro Mjini.

Tangu jana saa 4:42 mpaka saa 5:40 usiku, alikuwa akitoa na kuandika maelezo ya kosa analotuhumiwa kutenda akiwa na wakili Mvula.

Taarifa iliyotolewa leo Ijumaa Februari 23, 2018 na Mvula inaeleza kuwa baada ya Zitto kulala mahabusu kwa sababu za ziara ya kutembelea madiwani wa ACT katika mikoa nane nchi nzima, ameachiwa kwa dhamana.

“Muda huu ameachiwa kwa dhamana ya maneno yenye thamani ya Sh50milioni. Anatakiwa kuripoti Polisi Kituo Kikuu cha Polisi cha Mkoa wa Morogoro Jumatatu, Machi 12, 2018,” inaeleza taarifa hiyo.


Thursday, February 22, 2018

22 February 2018,Hii ndo sababu iliyomfanya Manara aungane na Wanayanga

Afisa habari wa timu ya Simba SC, Haji Manara amekuwa miongoni mwa watu walioweza kuguswa na msiba uliomfika Nahodha wa Yanga SC, Nadir Haroub 'Cannavaro' leo wa kufiwa na mwanae na kumtaka awe mwenye moyo wa subra.

Manara amefunguka hayo kupitia ukurasa wake maalumu wa kijamii baada ya kupokea taarifa hizo za msiba wa Anwar aliyefariki katika hospitali ya Taifa Muhimbili leo asubuhi wakati akipatiwa matibabu ya maradhi yaliyokuwa yakimsumbua

"Pole sana Cannavaro kwa kufiwa na mtoto wako wa miezi miwili Anwar. Mimi binafsi, viongozi, wachezaji, benchi la ufundi, wanachama pamoja na mashabiki wa Simba tunaungana na Cannavaro katika kipindi hiki kigumu alichonacho yeye pamoja na familia yake kiujumla. Poleni wanayanga wote",amesema Manara.

Kwa upande mwingine, muandishi wa habari hii alipomtafuta Cannavaro kwa njia ya simu amesema japo kuwa yeye yupo njiani kurudi nchini akiwa anatokea Visiwa vya Shelisheli ameruhusu mwili wa marehemu mwanae kuzikwa leo (kuhifadhiwa).

22 February 2018,Watu 28 Wanaodaiwa kuwa wafuasi wa CHADEMA kizimbani kwa kosa la kufanya mkusanyiko usio halali

Watu 28 wanaodaiwa kuwa wafuasi wa
CHADEMA wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakikabiliwa na kosa la kufanya mkusanyiko usiokuwa halali katika Barabara ya Kawawa maeneo ya Kinondoni Mkwajuni jijini Dar es Salaam.

Washtakiwa hao wamesomewa kosa hilo na Wakili wa serikali, Faraji Nguka mbele ya Hakimu Mkazi, Godfrey Mwambapa .

Wakili Faraji Nguka, amedai kosa hilo wamelitenda February 16, 2018 barabara ya Kawawa maeneo ya Kinondoni Mkwajuni ambapo walifanya mkusanyiko usio halali wakiwa na nia ya kusababisha uvunjifu wa amani.

Baada ya kusomewa kosa hilo washtakiwa walikana ambapo Wakili Nguka ameeleza kuwa upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika.

Hata hivyo, Hakimu Mwambapa alitoa masharti ya dhamana kwa washtakiwa ambapo wametakiwa kuwa na mdhamini mmoja atakayesaini Bondi ya Sh.Milioni moja na nusu, ambapo ameahirisha kesi hiyo hadi March 8, 2018 kwa ajili ya kusomewa maelezo ya awali (PH) .

Admit Millard ayo

22 February 2018,Hii ndo njia mpya wanaoitumia wahamiaji kwenda Ulaya

Wahamiaji haramu wagundua njia mpya ya kuingia katika mataifa ya Ulaya Magharibi kwa kupitia nchini Bosnia Herzegovina.

Hapo awali wahamiaji walikuwa wakipitia nchini Ugiriki, Makedonia, Serbia, Hungary au Kroasia kuingia katika mataifa ya Ulaya Magharibi.

Njia hiyo ambayo ilikuwa ikitumiwa na wakimbizi ilifungwa Machi mwaka 2016.
Kwa sasa wahamiaji haramu na wakimbizi wanajaribu kutumia Kroasia kupitia Bosnia Herzegovina kuingia katika mataifa ya Ulaya Magharibi kutafuta hifadhi.

Katika kipindi hiki cha baridi, maimamu katika hutoa hifadhi za muda kwa wahamiaji wanaoathirika na baridi katika safari zao.

Wahamiaji 35 wamepewa hifadhi na maimamu mjini Sarayevo wajikinge na baridi.

Wengi miongoni mwa wahamiaji hao ni raia kutoka Pakistan, Afghanistan, Syria, Libya na Morocco.

Jeshi la Polisi Bosnia limefahamisha kuwa watu zaidi ya 750 wameingia nchini humo kinyume cha sheria Januari mwaka 2018 wakştaraji kuendelea na safari yao Ulaya Magharibi.

22 February 2018,Viongozi wa Dini na siasa kumuona Rais Magufuli juu ya katiba mpya

Viongozi wa dini na wanasiasa wamejadili na kukubaliana kwenda kumuona Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, John Pombe Magufuli wakiwa na pendekezo la kukamilishwa kwa mchakato wa kupatikana katiba mpya itakayoongoza nchi bila uminywaji wa demokrasia.

Ambapo viongozi hao wamejadili mada hiyo pindi walipofanya kongamano la viongozi wa siasa na dini lililoandaliwa na Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD), na kufanyika jijini Dar es salaam.

Mwenyekiti wa (TCD), James Mbatia amesema lengo la kongamano hilo ilikuwa kujadili hali ya nchi kutokana na hofu iliyomo miongoni mwa wananchi, huku kukiwa na malalamiko ya ukandamizwaji wa demokrasia kutoka kwa vyama vya siasa, na kupendekeza kuwa ipo haja ya kujenga taasisi imara za usawa na haki.

Viongozi hao wamelalama juu ya uminywaji wa demokrasia hasa kwa vyama vya upinzani hali ambayo imetandaza hofu kwa wananchi.

Aidha baadhi ya viongozi wamepinga vikali tabia ya jeshi la polisi kutumia nguvu na mabavu kwa wananchi wake na kuwatia uoga.

Vile vile wameomba na kupendekeza uhuru wa katoa maoni uimarishe na kuwataka wadau wa siasa kujiepusha na chuki.

Hata hivyo, mwakilishi wa CCM, Wilson Mukama amesema katiba mpya si kipaumbele cha Serikali kwa sasa.



Admit dar24


Wednesday, February 21, 2018

21 February 2018,Chelsea yajitosa Kwa Christian Pulisic.

Chelsea inakabiliwa na ushindani mkali kutoka kwa Bayern Munich katika kumsajili kiungo wa kati wa Borussia Dortmund Christian Pulisic. (Mail)

West Ham iko tayari kumpatia David Moyes mkataba wa miaka miwili mwisho wa msimu huu iwapo atawasaidia The Hammers katika ligi ya Uingereza na raia huyo wa Uskochi tayari anatafuta wachezaji wa kuwasajili msimu ujao(Express)

Beki wa Lazio na Uholanzi Stefan de Vrij , 26 yuko tayari kuondoka katika klabu yake na kuelekea Manchester United lakini Everton na Arsenal pia wana hamu ya kumsajili(Mirror).

21 February 2018,Serikali yapiga marufuku uagizaji wa mabomba nje

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amepiga marufuku tabia ya wakandarasi wa miradi ya maji kuagiza mabomba nje ya nchi wakati kuna mabomba yanayozalishwa hapa nchini tena kwa ubora.

Hivyo amewataka wakandarasi hao kutumia mabomba yanayotengenezwa ndani ya nchi.

“Niwatake wakandarasi tuendelee kutumia mabomba ya ndani ili kuendelea kutoa sapoti kwa wawekezaji hawa,”amesema

“Kuna mradi wa kusambaza maji katikati ya mji wa Sh14 bilion ambao upo hatua za manunuzi, mkurugenzi wa Mwauwasa simamia hilo wakandarasi wanunue mabomba kiwanda hiki,” amesema Waziri
Ameyasema hayo Februari 20 wakati akiweka jiwe la msingi katika kiwanda cha kuzalisha mabomba cha Mwanza Plastics eneo la Nyamhongolo wilayani Ilemela Mwanza.

Aidha Mkurugenzi Mtendaji wa kiwanda hicho, John Charles amesema kiwanda hicho chenye wafanyakazi 15 ambao ni wazawa wenye ajira za kudumu na watatu kutoka nje ya nchi, kilianza mwaka 2008 kwa kutengeneza plastiki na vikombe.

Amesema wanakabiliwa na uhaba wa umeme wa kutosha kwani wakati mwingine unakosa nguvu na miundombinu ya barabara hivyo kuongeza gharama za uzalishaji.

Kutokana na hayo Waziri alimwagiza mkurugenzi wa manispaa ya Ilemela John Wanga kuhakikisha maeneo yote ya uwekezaji miundombinu yote muhimmu inafika.


21 February 2018,Serikali yabaini udanganyifu wa kiwango cha dhahabu mgodi wa Nyakavangala

SERIKALI imebaini udanganyifu wa wastani wa kiwango cha dhahabu kinachozalishwa katika mgodi wa dhahabu wa Nyakavangala wilayani Iringa.

Imeagiza wataalamu wake wakokotoe kiasi cha fedha ambacho serikali imekuwa ikiibiwa kupitia mrabaha wake ili wamiliki wa mgodi huo walazimishwe kulipa.

Mgodi huo uliopo katika kijiji cha Nyakavangala, Kata ya Malengamakali tarafa ya Isimani ulikabidhiwa na kijiji hicho kwa Thomas Masuka kama Msimamizi Mkuu wa mgodi na wenzake wengine 19 Mei mwaka jana ili kuondokana na uchimbaji holela, wakati taratibu zingine za kupata leseni zikiendelea.

Taarifa hiyo ilitolewa juzi na Naibu Waziri wa Madini, Dotto Biteko alipokuwa akizungumza na wachimbaji na viongozi wa mgodi huo uliofungwa hivi karibuni baada ya kutokea maafa yaliyohusisha baadhi ya wachimbaji hao kufukiwa wakati wakiwa katika shughuli ya uchimbaji na wengine kufariki dunia.

Akiagiza mgodi huo ufunguliwe katika kipindi cha wiki mbili zijazo baada ya changamoto zake zote kushughulikiwa, Biteko alisema taarifa ya wachimbaji hao ilikuwa ikionesha kila kiroba cha mchanga wa dhahabu kilikuwa kikitoa wastani wa gramu 0.28 ya dhahabu, lakini wataalamu wa wizara walipokwenda kupima ilibainika kila kiroba kimekuwa kikitoa wastani gramu 2.5 ya dhahabu.

“Acheni kuidanganya serikali, mnapofanya kazi zenu hakikisheni serikali inapata kinachoihusu ili iweze kuwahudumia ninyi na wengine kwa kupitia huduma mbalimbali inazotoa kama barabara, maji, afya, elimu na nyinginezo,” alisema.

Alisema baada ya kubaini udanganyifu huo, serikali itaunda timu kungalia kiasi cha mrabaha uliopotea na namna wamiliki wa mgodi huo watakavyotakiwa kulipa.

“Yako mambo yanayosameheka, lakini sio hela ya serikali, naomba msiniponze mimi na waziri wangu, katika hili hakuna msamaha na mnajua mwenye wajibu wa kutoa msamaha yupo kwa mujibu wa sheria kwa hiyo maagizo yangu mtalazimika kulipa kiasi chote kitakachobainika mlikwepa kuilipa serikali,” alisema.

Awali Meneja wa Mgodi huo, John Denis alisema tangu mgodi huo uanze kuzalisha dhahabu Mei, mwaka jana, jumla ya viroba 21,150 vya mchanga wa dhahabu vimezalishwa hadi ilipofika Desemba mwaka jana.

Denis alisema asilimia 20 ya viroba hivyo vilitolewa kwa wafanyakazi wanaosimamia mgodi, serikali ya kijiji na halmashauri ya wilaya ya Iringa huku vingine 932 vikitolewa kwa ajili ya kusaidia ujenzi wa kituo cha afya Mkulula.

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Iringa, Robert Masunya alisema kwa kupitia mgawo huo, halmashauri yake ilipata Sh milioni 17.1, kijiji cha Nyakavangala Sh milioni 36.8 na Kituo cha Afya Mkulula kilichangiwa Sh milioni 64.9.

21 February 2018,CCM Yapata nguvu Ngarenaro

Wanachama 400 na aliyekuwa Diwani wa Kata ya Bagara na Mwenyekiti wa Kitongoji cha Ngarenaro Mjini Babati mkoani Manyara, Nicodemus Tlaghasi (Chadema) aliyejiuzulu hivi karibuni wamekabidhiwa kadi za CCM.

Katibu wa Uenezi, Siasa, Uhusiano wa Kimataifa Kanali Mstaafu Ngemela Lubinga alikabidhi kadi ya CCM kwa wanachama hao wapya na diwani huyo aliyejiuzulu jana mjini Babati.

Akizungumza wakati wa kuwakabidhi kadi hizo mpya, Lubinga amewataka wanachama hao 400 na Tlaghasi, kuwa waaminifu kwenye chama hicho.

Amesema CCM ya hivi sasa inaendana na kasi kulingana na dunia ilivyo, hivyo wajiandae kwenda mwendo kasi ili kufikia maendeleo chanya.

Amesema inapotajwa CCM mpya na Tanzania mpya maana yake ni kuwa Watanzania wa sasa mahitaji yao si ya juzi na jana hivyo viongozi waliopatiwa dhamana ya kuongoza inawabidi watimize wajibu wao ipasavyo.

Akizungumza baada ya kukabidhiwa kadi ya CCM, Tlaghasi amesema amechoka kuishi maisha ya wasiwasi yasiyo na amani, ambayo alikuwa anayaishi wakati akiwa kiongozi wa jamii kupitia Chadema.

Amesema alikuwa anaishi maisha ya kuvizia ili asionekane na viongozi wa Chadema pindi akitaka kutimiziwa mahitaji ya jamii kwenye Serikali kwani alikuwa anaonekana kama msaliti.

"Ili kuonana na kiongozi wa serikali ilinipasa kuvizia, lengo likiwa nitimize mahitaji ya wapiga kura wangu, nikajiuliza nateseka hivi kwa ajili ya nini?" Alihoji Tlaghasi.

Amesema dhamira yake ikamtuma kuachana na Chadema na kujiunga na CCM ili aungane na Rais John Magufuli na mkuu wa mkoa huo Alexander Mnyeti katika kuwatumikia wananchi.

Tuesday, February 20, 2018

20 February 2018,Magaidi 1,715 Wauawa na Jeshi la Uturuki

Makao makuu ya jeshi la Uturuki yafahamisha kuwa tangu kuanza kwa operesheni yake dhidi ya ugaidi Januari 20, magaidi wapatao 1715 wamekwishauawa.

Jeshi la Uturuki lilianza operesheni yake rasmi Afrin kwa lengo la kuwaondoa magaidi wa kundi la PKK/PYD katika mpaka bain aya Uturuki na Syria.

Jeshi la Uturuki kwa ushirikiana na jeshi huru linazidi kusonga mbele Afrin katika operesheni yake dhidi ya ugaid

20 February 2018,Tetesi Za soka Ulaya michezoni Leo Jumanne

Kiungo wa kati wa Real Madrid na mjerumani Toni Kroos, 28, ni lengo kuu la Manchester United, ikitaka achukue mahala pake Michael Carrick ambaye anastaafu msimu ujao. (Independent)

Alan Pardew anajaribu kuokoa kazi yake huko West Brom na kipigo walichokipata kutoka Huddersfield siku ya Jumapili kinaweza kumaliza kuwepo kwake katika klabu hiyo baada ya wiki 12 tu.

Tottenham ina mpango wa kufanya jitihada mpya kumpata wing'a wa Crystal Palace Wilfried Zaha, 25. Klabu hiyo ya Mauricio Pochettino ilishindwa baada ya kujaribu mara mbili kumpata mchezaji huyo raia wa Ivory Coast. (Mirror)

Paris St-Germain hawana nia ya kumsaini mlinzi wa Manchester United Marcos Rojo, 27, licha ya kuhushwa na mpango wa pauni milioni 30 na mchezaji huyo wa Argentina. (ESPN)

Kiungo wa kati wa Real Madrid Marco Asensio, 22, anasema amepata ofa kutoka vilabu vitano vikiwemo Liverpool, Chelsea, Arsenal, Bayern Munich na Juventus, lakini rais wa klabu ya Florentino Perez hataki kumuuza raia huyo wa Uhispania. (Diario Gol - in Spanish)

Ajenti wa Nabil Fekir amekataa kuthibitisha ikiwa kiunga huyo wa kati wa Ufaransa ambaye amelengwa na Arsenal atajiunga na Lyon msimu ujao. (Telefoot via Mirror)

Mshambuliaji wa Argentina Leonardo Ulloa, 31, anasema anataka kufanya kuhama kwake kwa mkopo kutoka Leicester kwenda Brighton kuwa wa kudumu mwisho wa msimu. (Argus)
Klabua ya Sunderland imetangazwa kuzwa kwa pauni milioni 50. Klabu hiyo imekuwa ikizushwa ngazi mara kwa mara. (Mirror)

Kylian Mbappe atakamilisha kuhama kwake kwa pauni milioni 166 kutoka Monaco ikimaanisha kuwa PSG watamnunua mchezaji huyo wa miaka 19 raia wa Ufaransa baada ya kuepuka kuzushwa. (Mail)

Everton itabaki bila ya mlinzi wa kukopwaa wa Manchester City Eliaquim Mangala kwa msimu wote baada ya mlinzi huyo mfaransa kupata jeraha wakati wa ushindi dhidi ya Crystal Palace. (ESPN)

Meneja wa West Bromwich Albion Alan Pardew ana mechi mbili za kuokoa kazi. (Sun)

Paris St-Germain wanafikiria kutumia pauna millioni 30 kumsaini mlinzi wa Manchester United Marcos Rojo, 27. Mkataba wa raia huyo wa Argentina huko Old Trafford unafikia mwisho msimu ujao. (Sun)

20 February 2018,MUHIMBILI Yaweka mfumo mpya wakurahisisha utoaji Wa majibu kwa wagonjwa

HOSPITALI ya Taifa Muhimbili (MNH) imeweka mfumo mpya wa kurahisisha utoaji wa majibu kwa magonjwa ili kuongeza ufanisi na kupunguza malalamiko ya kusubiri majibu ya vipimo maabara.

Mkurugenzi Mtendaji wa MNH, Profesa Lawrence Museru alisema jana hospitalini hapo alipokuwa akitambulisha mfumo huo kwa waandishi wa habari.

Alisema hospitali imeboresha utoaji wa huduma katika Idara ya Rediolojia kwa kutumia mfumo huo ambao wagonjwa 200 na zaidi wamekuwa wakipimwa kila siku vipimo mbalimbali.

Aliongeza mfumo huo mpya utawezesha daktari kuongea huku mashine ikiandika moja kwa moja kile anachokiongea, pale atakapomaliza kuongea, majibu nayo yatakuwa yametoka muda huo huo tofauti na ilivyokuwa zamani.

“Lakini utaalamu huu mpya ukiongea kompyuta inaandika. Hatua hii inawezesha majibu kutoka haraka,” alisema.

Profesa Frank Minja kutoka Idara ya Rediolojia nchini Marekani, ambaye ameongozana na Wamarekani watatu, alisema wapo nchini kwa ajili ya kuweka mfumo huo katika Hospitali hiyo ya Muhimbili, ambapo kompyuta inachukua sauti na kutafsiri moja kwa moja.

20 February 2018,Vijiji vyote vya Wilaya ya Misungwi jijini Mwanza kupata huduma ya maji safi na salama

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amewahakikishia wananchi wa wilaya ya Misungwi Mkoa wa Mwanza kuwa vijiji vyote vitapatiwa huduma ya maji safi kupitia miradi inayotekelezwa katika wilaya hiyo ukiwemo wa Mbarika-Misasi utakaogharimu Sh12.4bilioni.

Alitoa kauli hiyo jana Februari 19, 2018 wakati akizungumza na wananchi mara baada ya kuweka jiwe la ujenzi wa mradi huo akiwa katika siku ya tano ya ziara yake ya kikazi mkoani Mwanza. Mradi huo unatarajiwa kuhudumia vijiji 12.

Vijiji hivyo ni Igenge, Lutalutale, Bugisha, Ngaya, Ikula, Sumbugu, Matale, Kasololo, Isuka, Nduha, Manawa na Misasi ambapo jumla ya wakazi 47,011 wanatarajiwa kunufaika na mradi huo.

Amesema Serikali ya Awamu ya Tano ina mikakati mizuri inayolenga kumaliza tatizo la upatikanaji wa maji safi na salama katika maeneo mbalimbali nchini vikiwemo vijiji vya wilaya ya Misungwi ili kuwawezesha wananchi hasa wanawake kushiriki katika shughuli za maendeleo kuliko kutafuta maji.

Waziri Mkuu amesema Serikali kupitia kampeni ya Rais John Magufuli ya kumtua mama ndoo, itahakikisha wananchi katika maeneo yote nchini wanapata huduma ya maji safi na salama katika umbali usiozidi mita 400 kutoka kwenye makazi yao.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya ya Misungwi, Eliud Mwaiteleke amesema mradi huo umegawanyika katika miradi midogo minne ambayo ni Igenge, Mbarika-Ngaya, Ngaya-Matale na Matale-Manawa-Misasi.

Amesema shughulli zilizokamilika ni pamoja na ujenzi wa vituo 48 vya kuchotea maji, matanki mapya manne na moja limekarabatiwa pamoja na mtandao wa mabomba wenye urefu wa kilomita 73,087.

Awali, Waziri Mkuu aliweka jiwe la msingi la ujenzi wa shule ya Sekondari ya Kata ya Gulumungu katika kijiji cha Nyamayinza, ambapo aliwapongeza wakazi wa kata hiyo kwa uamuzi wa kujenga shule, ambayo itawawezesha watoto wao kupata elimu.

Monday, February 19, 2018

19 February 2018,Mwili wa aliyekuwa katibu wa CHADEMA jimbo la Kinondoni kuhifadhiwa kesho

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kimesema kinatarajia kuongoza shughuli za utoaji wa heshima za mwisho kwa mwili wa aliyekuwa Katibu wa chama hicho Kata ya Hananasif Jimbo la Kinondoni, Daniely John siku ya kesho (Jumanne).

Hayo yamebainishwa na taarifa zilizotolewa na Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano, Tumaini Makene jioni ya leo (Jumatatu) na kudai mwili wa marehemu Daniel unatarajiwa kufika nyumbani kwake Hananasif ukiwa unatokea hospitali ya Taifa Muhimbili majira ya saa 4 asubuhi na kisa kupelekwa katika Kanisa la Katoliki kwa ajili ya misa ya kumuombea marehemu itakayoanza saa 5 asubuhi kanisani hapo.

Baada ya ibada hiyo, waombolezaji watatoa heshima zao za mwisho kwa Daniel kabla ya mwili wake kusafirishwa kwenda mkoani Iringa ambako atazikwa siku ya Jumatano, katika kijiji cha Chikelewatu wilayani Mafinga.

19 February 2018,Hii ndo sababu iliyoifanya Mahakama iamuru Nabii Tito akapimwe akili

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Mfawidhi Wilaya ya Dodoma imwamuru Mkuu wa Gereza la Isanga, ampeleke mshitakiwa Tito Onesmo Machibya 'Nabii Tito' akapimwe afya ya akili kama korti ilivyoagiza.

Ametoa agizo hilo leo.
Hakimu Mkazi Mfawidhi wa mahakama hiyo, James Kareyemaha amemuagiza mkuu huyo wa gereza ampeleke Tito katika Taasisi ya Magonjwa ya Akili Isanga ili mahakama iendelee na shauri hilo.

Awali, wakili wa Serikali, Beatrice Nsana aliiambia mahakama hiyo kuwa kesi hiyo imekuja kusikilizwa ndipo Hakimu Kayeremaha alipohoji vielelezo vilivyotakiwa kuwasilishwa mahakamani hapo.

Mshitakiwa Tito ameieleza mahakama hiyo kuwa bado hajapelekwa kufanyiwa vipimo kama ilivyoagizwa, hivyo mahakama imeamuru jambo hilo kutekelezwa.

Kesi hiyo imeahirishwa hadi Machi 5, mwaka huu, kwa ajili ya kusikilizwa tena.

19 February 2018,Eden Hazard afurahia kuwa Stamford Bridge

Mchezaji wa Chelsea mbelgiji Eden Hazard, 27, anasema yuko na furaha huko Stamford Bridge lakini hajasema kuwa hatakihama klabua hiyo siku za usoni. (Telefoot - in French)

Meneja wa zamani wa Chelsea Carlo Ancelotti hana fikra za kurudi Paris St-Germain kwa sababu anataka kurudi kwa Premier League. (Mirror)

Leicester wametuma maajenti kumtazama beki wa Benfica Andre Almeida, 27, na wing'a Rafa Silva, 24. Wachezaji wote hao walihusishwa na Leicester mwezi Januari. (O Jogo via Leicester Mercury)

AC Milan na Inter Milan wana nia ya kumsaini mshambuliaji Mario Balotelli, 27, kutoka Nice. Raia huyo wa Italia amekasirishwa kwa kupewa kadi ya njano wakati akimlalamikia refa kuhusu kisa ya ubaguzi wa rangi. (Sun)

Kiunga wa kati ya Manchester United Paul Pogba, 23, amerejea kwenye mazoezi baada ya kuwa mgonjwa kabla ya mechi ya Jumamosi ya kombe la FA ambapo Man United walipata ushindi dhidi ya Huddersfield. (Mail)

Real Madrid wanataka kumuuza kwa zaidi ya pauni milioni 100 kwa wing'a Gareth Bale ili kumununua mashambulizi wa Chelesea Eden Hazard, 27. (Sunday)

Chelsea watamuuliza mshambulizi raia wa Argentina Sergio Aguero, 29, ikiwa Manchester City iliongea na Hazard. (Star

Meneja wa Manchester United Jose Mourinho alijibizana na kiungo wa kati mfaransa Paul Pogba na mlinzi raia wa England Phil Jones baada ya kikosi chake kulimwa na Newcastle wiki iliyopita. (Sun on Sunday)

Mourinho alifanya mkutano wa saa moja kukana tofauti zake na Pogba.

19 February 2018,Vijiji vitatu vilivyokuwa vimetekwa na magaidi mpakani mwa Uturuki na Syria vyakombolewa na Jeshi la Uturuki

Jeshi laUturuki lakomboa vijiji vitatu kutoka mikononi mwa magaidi katika operesheni yake ya Tawi la Mzaituni ilioanzishwa kwa lengo la kuwaondoa magaidi mipakani mwa Uturuki na Syria.

Hacika, ni kijiji cha tatu kilichokombolewa na jeshi la Uturuki.

Katika operesheni nyingine ilionendeshwa Darmık, ngome za magaidi wa PKK/PYD zilishambuliwa.

Sunday, February 18, 2018

18 February 2018,Wapalestina kadha wauawa baada ya Israel kushambulia Gaza

Wapalestina wawili wameripotiwa kupoteza maisha baada ya Israel kufanya mashambulizi Gaza.

Kwa mujibu wa habari,jeshi la Israel limeshambulia ngome za Hamas katika ukanda wa Gaza na kusababisha vifo vya wapalestina wawili huku wengine wakiwa wamejeruhiwa.

Msemaji wa wizara ya afya nchini Palestina amesema kuwa majeruhi hawapo katika hali mbaya.

Jeshi la Israel nalo limeripoti kuwa askari wake wanne walijeruhiwa baada ya mlipuko kutokea karibu na kusini mwa mpaka wa Gaza na Israel.

Israel inaamini kuwa Hamas ndio wanahusika na kutokea kwa mlipuko huo.

18 February 2018,Maulid Mtulia atangazwa kuwa Mbunge wa Jimbo la Kinondoni

Mgombea wa CCM Jimbo la Kinondoni, Maulid Mtulia ameibuka mshindi katika uchaguzi mdogo wa ubunge uliofanyika jana Februari 17,2018.

Msimamizi wa uchaguzi ambaye pia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni, Aron Kagurumjuli ametangaza matokeo hayo leo Februari 18,2018.

Amesema Mtulia ameshinda kwa kupata kura 30,247 akifuatiwa na Salum Mwalimu wa Chadema aliyepata kura 12,353 na Rajab Salum wa CUF aliyepata kura 1,943.

“Kwa matokeo hayo na kwa mujibu wa mamlaka niliyopewa na sheria ya uchaguzi, namtangaza Maulid Mtulia kuwa Mbunge wa Kinondoni,” amesema msimamizi huyo wa uchaguzi.

Jana jioni Februari 17,2018 Kagurumjuli alisema kazi ya kutangaza matokeo ingekamilika saa sita usiku lakini hilo lilishindikana.

Ulinzi uliimarishwa katika eneo la kujumlisha matokeo la Biafra, ambako Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa; Mkuu wa Mkoa, Paul Makonda na Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Ally Hapi wamekesha katika eneo la kuhesabu kura.

Mgombea wa CCM, Maulid Mtulia naye alikesha eneo hilo akisema hataki kuuchukulia kirahisi uchaguzi huo.

Wawakilishi wa vyama vya upinzani hawakuwepo eneo hilo.

Saturday, February 17, 2018

17 February 2018,Arsenal iko karibuni kuinasa saini ya Timo Werner

Arsenal ndio klabu ya hivi karibu ambayo inamnyatia mshambuliaji wa klabu ya RB Leipzig Timo Werner, 21. Raia huyo wa Ujerumani ambaye pia anasakwa na Chelsea, Liverpool na Manchester United ana thamani ya £50m na amekataa kandarasi mpya katika klabu hiyo ya Bundesliga. (Sun)

Mkufunzi wa Arsenal Arsene Wenger amemuorodhesha kiungo wa kati wa Lyon Nabil Fekir kuwa mchezaji anayemtaka sana .Wenger yuko tayari kutoa dau la £45m ili kumsajili mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24- (Mail)

17 February 2018,Kifo cha katibu wa CHADEMA kuchunguzwa kwa kina

WAZIRI wa Mambo ya Ndani, Dk Mwigulu Nchemba amemuagiza Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Simon Sirro na timu yake kufanya uchunguzi wa kina kuhusu mauaji ya Katibu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Kata ya Hananasifu, Daniel John yaliyotokea Kinondoni, Dar es Salaam.

Alitoa maagizo hayo jana katika Kata ya Kasindaga Wilaya ya Muleba mkoani Kagera katika uzinduzi wa uandikishaji wa vitambulisho vya taifa mkoani humo.

Alisema ni vyema jeshi la polisi lichunguze kwa kina tukio hilo na kujua undani wake na kuwaeleza wananchi chanzo cha mauaji hayo na hatua zinazochukuliwa.

“Mataifa mengine mtu akiuawa shughuli zote zinasimama, tusiweke haya mazoea ya watu kupoteapotea kama mtu kapuliza dawa ya mbu na kuona ni jambo la kawaida tu, lazima mfanye uchunguzi kwa kina kujua nani amehusika na tukio hili,” alisema Dk Mwigulu.

17 February 2018,Mkurugenzi wa Manispaa ya kinondoni amaliza tofauti za viongozi wa vyama Jimbo la kinondoni

Mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni, Aron Kagurumjuli amejitokeza na kuzimaliza tofauti ambazo zilikuwa zimejitokeza katika jimbo hilo huku akiwalaumu viongozi wa vyama kushindwa kutekeleza wajibu wao.

Kagurumjuli ambaye ndiye Msimamizi wa Uchaguzi Kinondoni amesema kuwa baadhi ya vyama wameshindwa kuwapa barua za utambulisho mawakala wao na kutaka kutumia barua za kiapo kama utambulisho.

Amesema kuwa wao kama wasimamizi jukumu lao lilikuwa kutoa barua hizo na pia ni jukumu la viongozi wa vyama kuhakikisha kuwa wanatekeleza wajibu wao kwani huwa ni rahisi kwa wao kukutana na mawakala wao kwani mpaka mawasiliano yao wanakuwa wanayo

Aidha Mkurugenzi huyo ameweka wazi sababu za wao kutoa barua za utambulisho saa tano usiku ni kuhofia barua hizo kugushiwa

Hata hivyo amethibitisha kuwa dosari hizo zimeshamalizika na hali ya vituo ni shwari hivyo wananchi wasisite kwenda kupiga kura.

17 February 2018,Sanduku la kuhifadhia kura lilivyoleta hali ya sintofahamu kata ya Magomeni

Hali ya sintofahamu imeibuka muda huu katika kituo cha Idrisa kata ya Magomeni baada ya wananchi kudai kuwa kuna mtu ametoroka na sanduku lenye kura.

Kwa mujibu wa MCL Digital   kituo hicho leo Februari 17, 2018 na kukuta wananchi wakiwa wamekaa katika makundi huku polisi wakiimarisha ulinzi.

Wakazi hao ambao hawakutaka kutaja majina yao kwa kuhofia kukamatwa wameieleza kuwa wana uhakika sanduku hilo limechukuliwa na kurejeshwa.

"Kuna gari ilikuja ikaegeshwa pale jirani kabisa na walipo askari halafu ghafla jamaa mmoja akashuka kuzuga zuga hatimaye akanyakua sanduku na kutokomea nalo,"
amesema mmoja wa wananchi hao.
Amesema baada ya watu kushikwa na butwaa Polisi waliondoka eneo hilo na baada ya muda mfupi walirejea na mtu huyo akiwa na sanduku.

“Yaani wameenda kuweka kura zao halafu wanajifanya sanduku limerudi huo ni mchezo," amesema mwananchi mweingine.

Hata hivyo msimamizi wa uchaguzi wa kituo hicho, Zuhura Mohamed amekanusha kutokea kwa tukio hilo.
"Hakuna kitu kama hicho , mambo yamekwenda vizuri, vituo vilifunguliwa kwa wakati na watu wameonyesha kujitokeza ingawa kasi yao si kubwa sana. Tunaamini wataongezeka,” amesema.

Naye msimamizi wa uchaguzi kituo cha Kwamkunduge kata ya Tandale, Alex Cassian amesema idadi ya wapigakura iliyopo kwenye vitabu vya kupiga kura haiendani na mwitikio wa wapiga kura waliojiandikisha kwenye eneo hilo.

Cassian amesema hadi saa 5:15 asubuhi wapiga kura waliojitokeza walikuwa 60 wakati waliojiandikisha ni 445.

"Hadi muda huu waliopiga kura ni 60 kati ya 445 waliojiandikisha na siku imeisha maana tupo hapa tangu saa 1 asubuhi na nusu siku imeisha kwa kuwa ikifika saa 10 jioni ndiyo mwisho wa kupiga kura," alisema Cassian.

Friday, February 16, 2018

16 February 2018,Real Madrid kujenga rekodi mpya na Pogba

Real Madrid inamuwania mchezaji wa kiungo cha kati wa Manchester United Paul Pogba msimu huu wa joto, lakini watahitaji kutoa zaidi ya £ milioni 120 kwa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24 ambaye ndiye mchezaji aliyevunja rekodi ya usajili alipohamia Old Trafford. (Sun)

Lakini Pogba ana uwajibikaji kuondosha tofuati zozote za kimaono na meneja wa United Jose Mourinho. (Telegraph)

Jitihada za Pogba akiwa ndani ya Manchester United zimepungua baada ya kuwasili kwa mchezaji wa kiungo cha mbele wa Chile Alexis Sanchez, mwenye mri wa miaka 29, kutoka Arsenal, kwa mujibu wa aliyekuwa kapteni wa timu hiyo ya mashetani wekundu Paul Ince. (Mirror)