Wednesday, February 28, 2018

28 February 2018,CHADEMA-Yadai kuwa baadhi Ya watendaji wa Serikali hawatendi haki

Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA kimedai kufanya tathmini kuhusu mwenendo na hali ya kisiasa nchini kwa kipindi cha wiki mbili zilizopita na kubaini kuwa baadhi ya watendaji wa Serikali hawatendi haki.

Akizungumza na waandishi wa habari Katika Makao Makuu ya CHADEMA jijini Dar es salaam, Mwenyekiti wa Chama hicho Taifa Freeman Mbowe amesema CHADEMA hakina ugomvi na Serikali wala mhimili wa mahakama bali baadhi ya watendaji wanaoshindwa kusimamia haki.

Aidha Mbowe amezungumzia mauaji yaliyotokea katika maeneo mbalimbali nchini hususani Mkoani Morogoro ambapo amesema vitendo hivyo ni ukiukaji wa haki za binadamu na hali inaweza kuhatarisha amani ya nchi.

Baada ya mkutano huo na waandishi wa habari Mbowe na baadhi ya viongozi wa CHADEMA walikwenda kuripoti katika kituo cha Polisi kanda Maalum ya Dar es salaam ikiwa ni kiitikia wito wa jeshi hilo.

No comments: