Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge Kazi Vijana Ajira na Wenye Ulemavu Anthony Mavunde ameagiza kufikishwa mahakamani kwa waajiri 11,900 nchini ambao wamekaidi agizo la serikali la kujiunga na mfuko wa fidia kwa wafanyakazi.
Naibu Waziri Mavunde ametoa agizo hilo Mkoani Mwanza wakati wa ziara yake kukagua utekelezaji wa agizo hilo ambapo amebaini kuwepo kwa waajiri ambao hawajajiunga na mfuko huo unaolenga kuwezesha wafanyakazi kupata fidia pindi wanapopatwa na matatizo kutokana na kazi wanazozifanya.
Mfuko wa fidia umeanzishwa na serikali ili kuwezesha wafanyakazi kupata fidia pindi wanapougua, kupata ajali au kufariki kutokana na kazi wanazozifanya ambapo mpaka sasa ni waajiri 12,689 ndio wamefanikiwa kujisajili kwenye mfuko huo.
No comments:
Post a Comment