HOSPITALI ya Taifa Muhimbili (MNH) imeweka mfumo mpya wa kurahisisha utoaji wa majibu kwa magonjwa ili kuongeza ufanisi na kupunguza malalamiko ya kusubiri majibu ya vipimo maabara.
Mkurugenzi Mtendaji wa MNH, Profesa Lawrence Museru alisema jana hospitalini hapo alipokuwa akitambulisha mfumo huo kwa waandishi wa habari.
Alisema hospitali imeboresha utoaji wa huduma katika Idara ya Rediolojia kwa kutumia mfumo huo ambao wagonjwa 200 na zaidi wamekuwa wakipimwa kila siku vipimo mbalimbali.
Aliongeza mfumo huo mpya utawezesha daktari kuongea huku mashine ikiandika moja kwa moja kile anachokiongea, pale atakapomaliza kuongea, majibu nayo yatakuwa yametoka muda huo huo tofauti na ilivyokuwa zamani.
“Lakini utaalamu huu mpya ukiongea kompyuta inaandika. Hatua hii inawezesha majibu kutoka haraka,” alisema.
Profesa Frank Minja kutoka Idara ya Rediolojia nchini Marekani, ambaye ameongozana na Wamarekani watatu, alisema wapo nchini kwa ajili ya kuweka mfumo huo katika Hospitali hiyo ya Muhimbili, ambapo kompyuta inachukua sauti na kutafsiri moja kwa moja.
No comments:
Post a Comment