Wednesday, January 31, 2018

31 January 2018,Hii ndo rekodi ya ufungaji wa Emerick Aubameyang kabla ya kusaini mkataba wa kuitumikia Arsenal

Aubameyang ametia saini mkataba wa "muda mrefu kwa uhamisho ambao umevunja rekodi ya klabu" kutoka Borrussia Dortmund.

"Mchezaji wetu wa pili wetu kumnunua wakati wa kipindi cha kuhama wachezaji Januari.

Auba ni miongoni mwa washambuliaji stadi zaidi duniani.

Amefunga mabao 98 katika mechi 144 akichezea klabu ya Dortmund ligi ya Bundesliga na amesaidia ufungaji wa mabao 172 katika mechi 213 ambazo ameshiriki akichezea klabu hiyo yake ya zamani michuano yote," Arsena wameandika kwenye mtandao wao.

The Gunners waliwasilisha maombi mawili ya kutaka kumsajili mchezaji huyo ambayo yalikataliwa na Dortmund kabla ya kukubali dau la juu ya £46.5m walilomsajilia Alexandre Lacazette.

31 January 2018,Fahamu siri hii juu ya wanafunzi waliofanya vizuri matokeo ya kidato cha nne 2017

MWANAFUNZI bora wa Kidato cha Nne 2017, Filson Mde wa Shule ya Sekondari ya Marian Boys ya Bagamoyo, mkoa wa Pwani, amesema ameshika nafasi hiyo kutokana na usikivu, nidhamu na kuwasumbua walimu wake mara kwa mara ili wamwelekeze masomo asipoelewa.

Akizungumza kwa njia ya simu na HabariLeo kutoka nyumbani kwao Kasulu, Kigoma, Filson alisema, tangu alipoanza kidato cha kwanza amekuwa akiwasumbua walimu wamwelekeze pale anapokuwa hajaelewa kitu darasani mwake.

Alisema kutokana na hali hiyo, amejikuta akiwa anaelewa vitu vingi na mwisho wake amekuwa hana wasiwasi muda wa kufanya mitihani yake ikiwemo mtihani wa mwisho alioibuka kidedea.

Alisema, hajawahi kusoma masomo ya ziada na badala yake amekuwa makini katika kufuatilia masomo muda wa kawaida wa darasani.

Aliwashauri wanafunzi wenzake kutambua kuwa ili wafanikiwe kwenye masomo, wanatakiwa kujipanga kusoma tangu mwanzo wa mwaka.

Akizungumzia mikakati ya baadaye alisema anataka kuwa daktari bingwa wa magonjwa ya binadamu na ndio maana alichagua masomo ya mchepuo wa sayansi amabayo ni Fizikia, Baiolojia na Kemia (PCB).

Mama yake mzazi, Elizabeth Ndabatinye alisema mwanaye alianza kufanya vema katika masomo na mitihani tangu akisoma Shule ya Msingi Amani, Kagera akishika nafasi za juu .

Alisema alifahamu fika mwanaye angeshinda mtihani lakini hakuwahi kufikiria kuwa angekuja kuwa mwanafunzi bora ilivyotokea.
“Kweli ninamshukuru Mungu kwa kuwa huyu kijana tangu mdogo kweli amekuwa akifanya vyema na tena vyema sana na leo amewakilisha vema Mkoa wa Kigoma yaani Waha leo tuna raha kutoa Tanzania One ni furah,”alisema.

Alisema kijana huyo ni wa pili kuzaliwa katika familia ya watoto wanne. Wa kwanza ni Stamili kisha Filson, Marick na wa mwisho ni Enri.

Mkuu wa Shule ya Marian Boys, Ihonde Joseph alisema Filson amekuwa akifanya vema tangu alipoanza kidato cha kwanza na kuwa walimu walikuwa wakitarajia kuwa angefanya vema. “Kweli tulijua angekuja kuwa mmoja kati ya wanafunzi ambao wangefaulu kwa daraja la juu na tuliposikia amekuwa bora Tanzania nzima imetufurahisha, “alisema Mwalimu Joseph.

Naye mshindi wa pili kitaifa, Elizabeth Mangu alisema siri kubwa ya matokeo aliyoyapata ni kumwomba Mungu muda wake mwingi na jitihada alizokuwa amezielekeza katika masomo wakati wote alipokuwa shuleni hapo.

Alisema aliamini bila Mungu hakuna kitu kinachoweza kufanyika ikiwemo kufanya vizuri katika mitihani yake hatua iliyompelekea kujiamini muda mwingi hadi jana alipopokea matokeo yake ya mtihani huo akiwa amefaulu.

“Nawausia wanafunzi wenzangu walio shuleni kuongeza bidii muda wote huku wakimtumaini Mungu kwa kuwa ndiyo kila kitu katika maisha ya kila siku ya mwanadamu,” alisema Elizabeth. Alisema matarajio yake ni kuwa Mhandisi Mungu akimsaidia kufanya vyema masomoni.

Mama mzazi wa Elizabeth aliyejitambulisha kwa jina moja la Mwalimu akifundisha katika Shule ya Sekondari ya Kilolezi Jijini Mwanza, alimshukuru Mungu akisema ameyapokea matokeo hayo kwa moyo mkunjufu na zaidi anamwombea mtoto wake azidi kufanya vyema.

Alisema Elizabeth ni mtoto wake wa pili kuzaliwa akitanguliwa na kaka yake anayesoma utabibu Chuo cha Uuguzi Sengerema, Mwanza.

Mwanafunzi aliyeshika nafasi ya tatu ,Anna Mshana naye alisema siri ya kufanya vyema katika mtihani huo ni kujituma na kujiwekea malengo akitumia muda mwingi kumwomba Mungu awapo shuleni hapo na hata nyumbani.

Alisema malengo yake ni kuwa Msanifu Majengo Mungu akimsaidia huku mzazi wake ambaye ni Mwalimu Shule ya Sekondari ya Jitegemee, Dar es Salaam, Benjamin Mshana akieleza kupokea matokeo hayo kwa furaha. “Namshukuru Mungu, mimi ni Mwalimu wa Sayansi, muda wote nilikuwa naomba mwanangu aige kupenda masomo ya Sayansi, kaenda mbali na kunistaajabisha kwa kufanya vizuri zaidi kitaifa, ni jambo la kumshukuru Mungu,” alisema Mwalimu Mshana jana.

31 January 2018,Rais Magufuli aitaka idara ya uhamiaji kuhakikisha inapambana na wahamiaji haramu bila kumwogopa mtu

Rais John Magufuli ameitaka Idara ya Uhamiaji kuhakikisha inapambana na wahamiaji haramu pasipo kumwogopa mtu.

Amemwagiza Kamishna wa Uhamiaji, Dk Anna Makakala kuwachukulia hatua kali watumishi wake watakaoshindwa kutekeleza wajibu wao ipasavyo.

Dk Magufuli akizungumza leo Jumatano Januari 31,2018 akizindua hati ya kusafiria ya kielektroniki jijini Dar es Salaam, amesema utambuzi wa wananchi wanaoishi bila vibali na wenye vibali vilivyoisha ni muhimu.

Amesema uhamiaji ina jukumu kubwa katika kutekeleza hayo.

"Haiwezekani wahamiaji haramu wanakamatwa Mbeya halafu wamepita Kilimanjaro, Manyara. Kamishna (Dk Makakala) ifike mahali unapoona hili washushe vyeo, mwondoe nyota moja ili wajue wajibu wao," ameagiza Rais Magufuli.

Amesema awali Uhamiaji iligubikwa na matatizo yakiwamo ya utoaji hovyo wa vibali vya uraia, hata kwa watu ambao walikuwa hawana sifa.
"Kuna raia wengi walipata uraia bila sifa na wapo waliopata uraia na vyeo vya juu kabisa serikalini wakati si raia," amesema.

Dk Magufuli amesema hiyo ndiyo sababu iliyofanya akamteua Dk Makakala kuwa Kamishna.

"Wanawake ni waaminifu sana na ameanza kutatua matatizo haya."
Baadhi ya viongozi waliohudhuria uzinduzi huo ni Rais wa Zanzibar, Ali Mohamed Shein; Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan; na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa.

Wengine ni marais wastaafu Amani Abeid Karume na Ali Hassan Mwinyi; Jaji Mkuu, Profesa Ibrahim Juma; na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Ali Iddi.

Pia, viongozi wa Serikali, Bunge, Baraza la Wawakilishi, wa dini, wanasiasa, na mabalozi wanaoziwakilisha nchi zao Tanzania.


Tuesday, January 30, 2018

30 January 2018,Hii ndo sababu inayoweza kukwamisha Matarajio ya wapenzi wa Arsenal kwa Aubameyang

Kufanikiwa kwa Arsenal kumnunua mshambuliaji wa Borussia Dortmund Pierre-Emerick Aubameyang kwa £60m kutategemea makubaliano kuhusu wachezaji wengine wawili.

Na mshambuliaji wa Gunners Olivier Giroud ndiye huenda akawa na usemi zaidi kuhusu iwapo mkataba wa kuhama kwa Aubameyang utakamilishwa kabla ya muda wa mwisho wa kuhama wachezaji kipindi hiki, Jumatano saa 23:00 GMT.

Arsenal wamekubali kulipia gharama na mikataba ya kibinafsi ya mchezaji huyo kutoka Gabon mwenye umri wa miaka 28.

Lakini Dortmund itaidhinisha hatua hiyo kama watapata mchezaji wa kuchukua nafasi yake.

30 January 2018,Yanga yawa king'ang'anizi

Klabu ya soka ya Yanga imefanikiwa kuingia hatua ya 16 bora ya michuano ya kombe la shirikisho nchini baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 6-5 kupitia mikwaju ya Penalti dhidi ya Ihefu FC.

Yanga iliwabidi kusubiri hadi dakika za majeruhi kusawazisha bao la mapema la Ihefu FC inayoshiriki ligi daraja la pili, kupitia mkwaju wa penalti uliopatikana baada ya Chirwa kuangushwa kwenye eneo la hatari ambapo alipiga mwenyewe na kufunga.

Baada ya timu hizo kutoka sare ya 1-1 ndani ya dakika 90 mwamuzi akaamuru mikwaju ya penalti ambapo Yanga wameibuka na ushindi wa jumla ya 6-5.

Nyota wa Yanga raia wa Zambia Obrey Chirwa alikosa mkwaju wake kabla ya golikipa Youthe Rostand kusawzisha makosa yake.

Yanga sasa inaungana na timu zingine zilizoshinda katika hatua ya 16 bora ikiwemo Azam FC ambayo mapema imesonga mbele baada ya kushinda 5-0 dhidi ya Shupavu FC ya Morogoro.

Matokeo katika mechi zingine.
Mwadui FC 1-2 Dodoma FC
Kagera Sugar 0-2 Buseresere
Kariakoo Lindi 0-1 Mbao FC

30 January 2018,Neymar kurudishwa Hispania

Rais wa La Liga, Javier Tebas amesema kuwa anatamani kumuona tena nyota wa Klabu ya Paris Saint Germain ya Ufaransa, Neymar jr akicheza ligi kuu ya Hispania.

Ameyasema hayo wakati wa sherehe za utoaji tuzo za waandishi wa habari za michezo nchini humo, ambapo amesema kuwa Neymar ni mchezaji mwenye kiwango cha juu na anastahili kurudi nchini Hispania.

”Neymar ni mchezaji mkubwa, natamani nimuone tena akicheza La Liga ila kuhusu timu atakayocheza sitaki kujua,”amesema Tebas

Aidha, Neymar ambaye alisajiliwa na PSG kutoka Barcelona Juni 2017 hadi sasa amefanikiwa kufunga mabao 26 kwenye mechi 24 alizoichezea timu hiyo.

Hata hivyo, bosi huyo wa La Liga amewahakikishia wanahabari kuwa msimu ujao wa ligi 2018/19 hakutakuwa na matatizo ya uamzi kwenye baadhi ya matukio kwasababu teknolojia ya VAR itaanza kutumika nchini humo.

30 January 2018,Wafahamu kwa Majina wanafunzi waliofanya vizuri na kuongoza kitaifa matokeo ya kidato cha nne 2017

Yafuatayo ni majina ya wanafunzi waliofanya vizuri na kuongoza kitaifa katika matokeo ya kidato cha nne kwa mwaka 2017.

Kumi bora wanafunzi waliongoza ni
1. Felison Mdee, Marian Boys
2. Elizabeth Mangu, Marian Girls
3. Anna Benjamini Mshana, Marian Girls
4. Emmanuel Lameck Makoye, Iliboro
5. Lukelo Thadeo Luoga, Iliboro
6. Fuad Thabit, Feza Boys
7. Godfrey Mwakatage, Uwata
8. Baraka Mohamed, Angels
9. Lilian Moses Katabalo, Marian Boys.
10. Everline Edward Mlowe, St. Francis

wasichana 5 bora, waliofanya vizuri mtihani kidato cha nne, 2017.

1. Elizabeth Mangu
2. Anna Benjamin Mshana
3. Lilian Moses Katabalo
4. Everline Edward Mlowe
5. Rose Godfrey

Wavulana 5 bora, waliofanya vizuri mtihani kidato cha nne 2017.

1. Filson mdee
2. Emmanual lameck makwe
3. Lukelo Thadeo
4. Fuad Thabit
5. Godfrey baraka



Admit Dar 24

30 January 2018,Serikali yawafuta chozi wabunge baada ya kukubali ombi lao juu ya umri wakustaafu mtumishi wa umma

Serikali imekubali maoni ya Kamati ya Bunge ya Katiba na Sheria ya kukifuta kifungu kilichokuwa kikimpa mamlaka Waziri wa Utumishi na Rais kubadili umri wa kustaafu kwa mtumishi wa umma.

Muswada wa Sheria Mbalimbali Namba 5 wa Mwaka 2017 unapendekeza kufanya marekebisho katika sheria ya utumishi kwa lengo la kubadili umri wa kustaafu kwa baadhi ya kada za utumishi wa umma.

Kada zinazopendekezwa kuongozewa umri wa kustaafu kutoka miaka 55 hadi 60 kwa hiari na 60 hadi 65 kwa lazima ni maprofesa, madaktari bingwa na wahadhiri waandamizi wa vyuo vikuu vya umma.

Mwanasheria Mkuu wa Serikali, George Masaju amesema bungeni leo Jumanne Januari 30,2018 kuwa kifungu kipya cha 25B ambacho kilikuwa kinapendekeza umri wa kustaafu kimefutwa.

Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Katiba na Sheria, Mohamed Mchengerwa amesema kamati haikuona haja ya kuwa na kifungu hicho kipya kwa sababu kinaweza kutumika vibaya kwa sababu mfanyakazi husika hapewi nafasi ya kushirikishwa katika uamuzi.

Monday, January 29, 2018

29 January 2018,Yaliyozungumzwa baina ya Rais Magufuli na Slaa

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli leo emekutana na Dkt. Wilbroad Slaa, Ikulu jijini Dar es Salaam ikiwa ni mara ya kwanza tangu alipomteua kuwa Balozi.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Ikulu, Dkt. Slaa amempongeza Rais Magufuli kwa kazi nzuri anayoifanya na kwamba ametekeleza mambo mengi ambayo yalipigiwa kelele kwa takribani miaka 20 iliyopita.

“Kwakweli nimepata faraja kwa sababu Serikali ya Awamu ya Tano inatekeleza hatua kwa hatua karibu yote tuliyokuwa tunayapigania kwa miaka takribani 20 huko nyuma. Mimi nilikuwa napiga kelele kwa sababu nilikuwa naona kuna upungufu,” taarifa hiyo inamnukuu Dkt. Slaa.

Naye Rais Magufuli amemsifia Dkt. Slaa kuwa ni Mtanzania mzalendo mwenye moyo safi ambaye anaamini atatekeleza majukumu yake vizuri kama Balozi katika nchi atakayopangiwa.

“Dkt. Slaa alinijulisha kuwa anakuja na akaomba akija aweze kuniona, nikampangia leo.

Tumezungumza mambo mengi na ameniahidi kuwa atakwenda kufanya kazi yake vizuri kwenye nchi atakayokwenda kuwa Balozi,” alisema Rais Magufuli kwa mujibu wa taarifa hiyo.

Dkt. Slaa ambaye aliwahi kuwa Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo na kugombea nafasi ya Urais, mwaka 2015 alitangaza kuachana na masuala ya siasa baada ya chama hicho kumkaribisha waziri mkuu wa zamani, Edward Lowassa na kumpa nafasi ya kugombea urais kupitia umoja wa vyama vitano vya upinzani ulioitwa Ukawa.

Rais Magufuli alimteua kuwa Balozi na anasubiri kumpangia nchi atakayokwenda kuiwakilisha Tanzania.

29 January 2018,Meya wa Jiji la Dar es salaam afafanua juu ya kukamatwa kwa gari lake

Meya wa Jiji la Dar es salaam, Isaya Mwita ametolea ufafanuzi taarifa zilizozagaa kwenye mitandao ya kijamii kuhusu kukamatwa kwa gari lake katika ofisi za chama cha mapinduzi wilaya ya Kinondoni.

Amesema kuwa maeneo kama hayo huwa yanalaza magari hivyo hapakuwa na nia yeyote ya kufanya uhalifu katika ofisi hizo.

Ameyasema hayo hii leo jijini Dar es salaam wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu taarifa hizo, ambapo amesema kuwa yeye ni mstaarabu wala hawezi kufanya chochote kibaya.

“Niwaondoe wasiwasi kuhusu dereva wangu, hakuwa na nia yeyote ya kufanya uhalifu, dereva wangu ni mtumishi wa umma na pale wanalaza magari ya binafsi na ya umma, hivyo pale aliona kuwa ni sehemu salama ndio maana akapaki pale,”amesema Mwita.

Aidha, ameongeza kuwa yeye hana nia mbaya na mgombea wa ubunge wa chama cha mapinduzi CCM, Maulid Mtulia kwani yeye kazi yake ni kuleta maendeleo ya jiji la Dar es salaam.

29 January 2018,UVCCM Wilaya ya Kinondoni Yaliomba Jeshi la polisi kuchunguza juu ya kukamatwa kwa gari la Meya wa Jiji la Dar es salaam

UMOJA wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM), wilaya ya Kinondoni umeliomba Jeshi la Polisi kuchunguza na kutoa majibu ya haraka baada ya kulikamata gari la Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Issaya Mwita (Chadema) likiwa na dereva wake ofi si za CCM wilaya hiyo.

Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa UVCCM wilaya hiyo, Lilian Rwebangira alisema matukio kama hayo hayapaswi kufumbiwa macho na kuchukuliwa kwa wepesi kipindi hiki cha kampeni za uchaguzi mdogo wa ubunge jimbo la Kinondoni.

“Nataka kuwafahamisha wana Kinondoni matukio yanayofanywa na wenzetu upande wa pili ambao ni wapinzani wetu hasa Chadema katika kipindi hiki cha kampeni, Chadema wameshajiona wanaenda kushindwa katika uchaguzi utakaofanyika Februari 17,” alisema.

Alisema baada ya kuona wanashindwa wameamua kutumia mbinu mbadala za kuhujumu kampeni ili kutia hofu wananchi waanze kuogopa ili wasijitokeze kupiga kura kama ilivyofanyika katika Kata ya Bweni kwenye uchaguzi mdogo wa madiwani.

Alisema juzi walimkamata mwanamke mmoja wa Chadema akiwa amevaa nguo za kiraia ofisi hizo za CCM akijifanya mwendawazimu lakini baada ya kumhoji vizuri na kumfuatilia hadi katika familia yake walibaini ni wa Chadema.

Pia alisema juzi limetokea tukio katika ofisi hizo za CCM ambapo saa 2:30 usiku walikamata gari la Meya wa jiji wa Dar es Salaam likiwa na vijana wawili waliovalia kofia za CCM na wametokea wilaya ya Kigamboni.

“Baada ya tukio hilo tulibahatika kumbana dereva na kutoa taarifa Polisi na walifika wakamkamata dereva na gari na kulipeleka kituo cha polisi Magomeni... natoa rai kwa vyombo vya dola hili jambo wasilichukulie kimasihara ni jambo nyeti, wasifumbie macho jambo hili na wachukue hatua haraka,” alisema.

“Tumeshapata taarifa nyingi kutoka Chadema wanapanga kufanya fujo na kutishia wananchi wasipige kura lakini sisi kama UVCCM tukiwa walinzi wa chama tunatoa angalizo kwa vijana wa Chadema wanaojipanga kufanya vurugu, hatutavumilia vitendo hivyo,” alisema Lilian.

Alisema walipombana dereva aliwaambia alikuja kupaki gari katika eneo hilo kwa kuwa ni eneo salama lakini baadaye akadai alikuja na Meya akampeleka kikao mtaa wa Hananasif.

“Dereva huyu baadaye alisema alikuja na vijana wawili ambao aliwataja kwa jina moja, Alex na God ambao walimwambia awapeleke ofisi za CCM na kwa maelezo yake alipowashusha hakujua wameelekea wapi,” alisema Lilian.

“Wale vijana baada ya kushuka kwenye gari waliomba kuingia maliwatoni na kwa kuwa walitambuliwa walielekezwa vyoo vya ndani na wakashtuka wakajua wametambuliwa wakatoka nje wakakimbia na dereva naye alitoka lakini alirudi,” Lilian aliwaambia waandishi wa habari.

Pia alisema walitahadharishwa kuhusu vijana hao kwamba ni watu wa fujo ambao wamekuwa wakifanya vurugu wilaya ya Temeke hasa kwenye misiba ya wanachama wa CCM, mikutano ya chama na sherehe za chama.

Kamanda wa Polisi, Mkoa wa kipolisi Kinondoni, Jumanne Muliro alithibitisha kushikiliwa kwa gari hilo la Meya kwa madai linachunguzwa lakini hakutoa ufafanuzi zaidi. Meya wa Dar es Salaam, Mwita alipotafutwa kuzungumzia tukio hilo simu yake iliita bila majibu.



Admit Habarileo

Sunday, January 28, 2018

28 January 2018,Afikishwa rumande kwa tuhuma za kumbaka mfanyakazi wake

Mwanamke mmoja jijini New York nchini Marekani amedai kubakwa na bosi wake katika ofisi yake ndani ya jengo la klabu ya usiku ya Kijapani inayojulikana kama Usagi.

Kwa mujibu wa taarifa za mashtaka yaliyowasilishwa Katika Mahakama ya Juu ya Manhattan, mwanaume huyo aliyetajwa kwa jina la Hazumu Suzuki ambaye ni meneja wa klabu hiyo alimueleza msichana huyo kuwa anamuomba abaki ofisini ili wajadili masuala ya kazi, lakini baada ya kubaki alimvamia na kumuangusha sakafuni kabla hajamvua nguo kwa nguvu na kumbaka.

Mwanamke huyo alidai kuwa alifanya jitihada za kupiga kelele na kujihami lakini hakufanikiwa kupata msaada wowote.

Nguo zilizochanwa katika tukio hilo zilikabidhiwa kwa polisi ambao wameeleza kuwa wanaendelea na upelelezi.

Katika maelezo yake, mwanamke huyo alidai kuwa awali aliripoti kwa mmiliki wa klabu hiyo, Atsuko Kinoshita ambaye alikiri kuwa meneja huyo alikuwa na tabia ya kufanya fujo anapolewa na kwamba alikuwa akipata majeraha ambayo asubuhi alieleza kuwa hafahamu kilichomtokea.

Kwa mujibu wa New York Post, mmiliki wa klabu ya Usagi alieleza kuwa alimuongezea mkataba wa kazi Suzuki ili aweze kupata sifa za kuongeza muda wa Visa yake nchini Marekani.

Mmiliki wa klabu hiyo pia ni mmoja ya washtakiwa katika kesi hiyo akidaiwa kuendelea kumuajiri Suzuki licha ya kujua kuwa alikuwa na tabia ya kuwadhuru wanawake anapolewa.

Mwanamke aliyefungua mashtaka hayo anadai pia fidia ya dola milioni 10 ($10 million) kutokana na tukio hilo.

28 January 2018,Vijana nchini kufundishwa uendeshaji Treni za mwendo kasi ili kuhudumia reli ya kisasa (SGR)

WAZIRI wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa amemuagiza Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni Hodhi ya Rasilimali za Reli Tanzania (RAHCO), Masanja Kadogosa, kutayarisha timu ya vijana kuwafundisha kwa ajili ya kuhudumia reli ya kisasa ya Standard Gauge (SGR) itakapokamilika.

Profesa Mabarawa alitoa agizo hilo jana wakati alipotembelea mradi huo kutoka Soga Kibaha mkoani Pwani hadi Pugu jijini Dar es Salaam, ili kujionea maendeleo ya mradi huo unaotarajiwa kukamilika Juni 2020 na kwa awamu ya kwanza ikiwa imeanzwa kutekelezwa kutoka Dar es Salaam mpaka Morogoro kwa urefu wa kilometa 300.

Alisema suala la kuwafundisha vijana kwa ajili ya kuhudumia reli hiyo lipo kwenye mkataba kati ya Rahco na Kampuni ya Yapi Merkezi ya Uturuki inayojenga reli hiyo hivyo ni vyema wakaandaa vijana sasa kwa ajili ya kuwapeleka kwenye mafunzo ili reli hiyo itakapoanza kazi iendeshwe na Watanzania.

“Hii treni inajengwa leo baada ya miaka miwili itakuwa imekamilika, treni hii ni ya umeme kila kitu hapa kitakuwa cha kisasa kama vijana hatukuwapeleka leo kwenda kujifunza tutakuwa tumejenga treni ya kisasa, lakini haina watu wa kuendesha na sisi hatutaki iwe hivyo, tunataka tuone Watanzania waendeshaji wa treni, mafundi wa sehemu mbalimbali ili kuhakikisha mradi huu wa Watanzania unaendeshwa na Watanzania,” alisema Mbarawa.

Alisema mradi huo kwa sasa umekamilika kwa asilimia 5.86 badala ya asilimia 6.8 kama ilivyotakiwa, na hiyo imetokana na mvua zilizonyesha na kusababisha ujenzi huo kushindwa kukamilika kama ilivyotakiwa.

“Kuna tofauti ya asilimia moja na imetokana na hali ya mvua, lakini sasa wamejipanga upya kuhakikisha kwamba wanaongeza watu na vifaa ili kuhakikisha kama tulivyopanga ifikapo Juni 2020, reli hii Watanzania iwe imemalizika na kuanza kutumika,” aliongeza.

Alieleza kuwa kazi inayoendelea sasa ni kukata maeneo, kujaza na kuweka sawa kwa ajili ya kutandika reli na wataanza kujenga madaraja katika eneo la Pugu.

Admit Habarileo

28 January 2018,Serikali yazitaka Kaya 83 zilizovamia Hifadhi ya Ngorongoro kuondoka

Waziri wa Maliasili na Utalii, Hamis Kigwangallah amezitaka kaya 83 zinazodaiwa kuvamia eneo la serikali la Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro kujiandaa kuondoka.

Akizungumza na waandishi leo Januari 28 baada ya kutembelea eneo hilo la Njiro, Kigwangallah amesema ana taarifa viwanja hivyo waliuziana maafisa wa Serikali bodi la Utalii na Mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro kinyume cha sheria.

"Katika eneo tumepewa taarifa waliopewa viwanja wapo mawaziri wakuu wastaafu wawili ,viongozi wa serikali wastaafu na tayari tumewasiliana na Waziri wa ardhi kupata nyaraka zao" amesema

Katika eneo hilo, kuna nyumba za wakuu kadhaa wa mikoa wastaafu, viongozi wa taasisi za serikali wastaafu na wafanyabiashara kadhaa.

Awali Meneja wa huduma za sheria wa Ngorongoro, Egudius Mweyunge amesema NCAA ilinunua eneo hilo mwaka 2006 kutoka tume ya ubinafsishaji mashirika ya umma(PSRC) mwaka 2006 ekari 40 kwa Sh1.8bilioni.

Hata hivyo amesema baada ya kutaka kuendeleza eneo walikuta tayari halmashauri ya jiji la Arusha wamegawa viwanja 83 tangu mwaka 1996.

"Tulipowafuata jiji wakakiri wamefanya makosa na watatufidia eneo jingine lakini tumeshindwa kufikia muafaka" amesema Meneja huyo

Awali Mhifadhi mkuu wa Mamlaka ya hifadhi Ngorongoro Dk Fredy Manongi amesema eneo walilovamiwa ni mali ya NCAA na wana mikakati ya kuwekeza.

Admit Mwananchi

Saturday, January 27, 2018

27 January 2018,Watu wasiopungua 40 wafariki,zaidi ya 100 kujeruhiwa kwa mlipuko nchini Afghanistan

Watu zaidi ya 40 waripotiwa kufariki na wengine zaidi ya 100 kujeruhiwa katika mlipuko wa bomu uliotokea mjini Kabul nchini Afghanistan.

Bomu lililokuwa limetengwa katika gari la wagonjwa lililipuka  na kusababisha maafa hayo Jumamosi mjini Kabul nchini Afghanistan.

Wanamgambo wa kundi la Taliban wamefahamisha kuhusika na shambulizi hilo.

Taarifa kutoka katika wizara ya afya zinafahamisha kuwa idadi ya watu waliofariki katika mlipuko huo itaongezeka kutokana na hali ya majeruhi.

27 January 2018,Serikali yatoa mwaka mmoja kwa taasisi zake kuhama kwenye matumizi ya mkaa kuhamia gesi

SERIKALI imetoa muda wa mwaka mmoja kwa taasisi zake kujiandaa kuhama kwenye matumizi ya mkaa na kuhamia kwenye nishati ya gesi na mkaa mbadala ili kuondokana na uharibifu wa mazingira.

Kauli hiyo ilitolewa jana na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais anayeshughulikia Muungano na Mazingira January Makamba wakati wa upandaji miti kuendeleza programu ya kuifanya Dodoma kuwa ya kijani lililofanyika katika Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM).

Alisema miongoni mwa taasisi hizo ni magereza, shule, vyuo na hospitali nchini ambazo zinatumia mkaa kupikia. January alisema ofisi yake inatarajia kutoa waraka na kwamba asilimia 90 ya Watanzania wanatumia mkaa kupikia na kumuagiza Katibu Mkuu wa wizara hiyo kuandaa mkakati wa kupunguza matumizi ya mkaa nchini.

“Tunazitaka taasisi za umma ziache kutumia mkaa tutatoa tamko hilo rasmi kwa waraka hata wazabuni hawatapata zabuni kama hawatatumia gesi. Kifungu cha 13 cha sheria ya mazingira, waziri mwenye dhamana ya mazingira ana uwezo wa kutoa maelekezo kufanya jambo litakalookoa mazingira,” alisema January.

“Mkaa ni nishati yenye gharama kushinda sehemu yoyote, maisha ya watu wa vijijini yanazidi kuharibiwa kutokana na uharibifu wa mazingira,” alisema.

Kwa upande wake, Naibu Waziri wake, Kangi Lugola alisema serikali haitawavumilia wawekezaji katika nyanja mbalimbali ikiwemo viwanda vinavyotiririsha kemikali za sumu kwa kisingizio cha sera ya Tanzania ya viwanda.

“Serikali haitawafumbia macho watu wote wanaoharibu mazingira kwa kisingizio cha sera ya Tanzania ya Viwanda. Watu wamejisahau sana wanajua wanaweza kuishi bila kutunza mazingira,” alisema Lugola.

Alisema wapo watu binafsi na kampuni wanawekeza katika sekta mbalimbali, lakini wamekuwa hawazingatii utunzaji wa mazingira.

Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, Joseph Malongo alisema awamu ya pili ya zoezi la upandaji miti litafanyika kwenye barabara zote zinazoingia mkoani Dodoma.

Naye Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Anthony Mavunde ambaye pia ni Mbunge wa Dodoma Mjini, alisema jimbo lake linatekeleza programu ya upandaji miti kwa kila kata na kwamba utunzaji mazingira wao kama viongozi wa kisiasa wameifanya kama ajenda ya kudumu kwenye mikutano yao ili kuifanya Dodoma kuwa ya kijani.

Makamu Mkuu wa chuo hicho, Profesa Idris Kikula alisema miti 30,000 itapandwa katika maeneo ya chuo hicho huku akihimiza wanachuo kutunza mazingira na kwamba wameunda kikosi kazi cha kudhibiti uharibifu wa mazingira unaofanywa na jamii inayozunguka chuo.

Kadhalika, Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara na Mazingira, Sadiq Murad alisema sera ya viwanda iende sambamba na utunzaji mazingira kwa kuwa viwanda vimekuwa havitunzi mazingira huku akitoa angalizo kwa chuo hicho kuhakikisha miti iliyopandwa inastawi.

Upandaji huo wa miti ni utekelezaji wa kampeni ya Kijanisha Dodoma iliyozinduliwa na Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan inayofadhiliwa na Kampuni ya The Network inayoendesha bahati nasibu ya Tatu Mzuka.

27 January 2018,Azam yapatiwa adhabu hii kutoka kamati ya Usimamizi na Uendeshaji wa Ligi

Klabu ya Azam FC inayoshiriki ligi kuu Tanzania bara imekumbana na adhabu kutoka kwa Kamati ya Usimamizi na Uendeshaji wa ligi.

Adhabu hiyo imetangazwa hii leo jijini Dar es salaam na Afisa Mtendaji Mkuu wa Bodi ya ligi, Boniface Wambura ambapo amesema Klabu hiyo imepigwa faini ya shilingi laki 5.

Amesema kuwa baada ya kamati kupokea ripoti ya mechi namba 103 kati ya wenyeji Majimaji FC dhidi ya Azam FC timu ya Azam FC iligoma kuingia kwenye vyumba vya kubadilishia nguo kitendo ambacho ni kosa kwa mujibu wa kanuni za ligi kuu.

Aidha, mbali na faini hiyo klabu hiyo pia imetakiwa kuwasilisha ushahidi kuhusu malalamiko yake kwenye mchezo huo ambapo ilidai kutoingia kwenye vyumba hivyo kwasababu vilikuwa vimepuliziwa dawa ambayo ilikuwa inatoa harufu kali.

Hata hivyo, Azam FC leo itakuwa mwenyeji wa Yanga kwenye mchezo wa ligi kuu raundi ya 15.

ingawa Jumatano iliyopita waliwasilisha barua TFF wakiomba kubadilishwa mwamuzi ili achezeshe mwingine badala ya Israel Nkongo lakini ombi lao limetupiliwa mbali

Friday, January 26, 2018

26 January 2018,Lowassa ,Mbowe kesho kufungua kampeni za Ubunge Jimbo la Kinondoni

Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Edward Lowassa pamoja na Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Freeman Mbowe kesho Januari 27, 2018 watakuwepo katika uzinduzi wa kampeni za Ubunge jimbo la Kinondoni

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na CHADEMA leo inasema kuwa viongozi hao watakuwepo katika uzinduzi wa kampeni za uchaguzi wa marudio katika jimbo la Kinondoni kumtambulisha Mgombea Ubunge kwa tiketi ya CHADEMA, Salum Mwalimu.

Uzinduzi wa kampeni hizo utafanyika katika viwanja vya Mapilau kuanzia saa nane mchana mpaka saaa kumi na mbili jioni ambapo wageni rasmi watakuwepo Lowassa pamoja na Mbowe na viongozi wengine wa CHADEMA.

Tarehe 17 Februari mwaka huu unatarajiwa kufanyika uchaguzi wa marudio katika majimbo ya Siha na Kinondoni kutokana na wabunge wa majimbo hayo kujiuzulu nafasi zao za Ubunge wakiwa katika vyama vya upinzani na kuingia Chama Cha Mapinduzi (CCM) na sasa wanagombea nafasi hizo wakiwa chini ya CCM.

26 January 2018,Rais Magufuli na mkewe wamfuta chozi wastara kwa kumchangia milioni 15 kwaajiri ya matibabu

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na mkewe Mama Janet Magufuli wamemchangia muigizaji wa filamu Tanzania, Wastara Juma shilingi milioni 15, kumsaidia katika matibabu yake.

Mchango huo umekabidhiwa kwa Wastara na Katibu wa Rais, Ngusa Samike , sambamba na kiasi kingine cha milioni moja na laki tisa ambayo ni michango kutoka kwa wasaidizi wa Rais.

Aidha, Msanii huyo amekuwa akisumbuliwa na mguu kwa muda mrefu na alikuwa akiomba msaada kwa Watanzania mitandaoni ili aweze kwenda nchini India kupatiwa matibabu.

Hata hivyo, Rais Magufuli anakuwa mtu wa kwanza kutoa fedha nyingi kwa msanii huyo, tangu aanze kutoa rai ya kuomba michango, ambapo wiki iliyopita Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na michezo Dkt. Harison Mwakyembe alimkabidhi shilingi milioni moja


Admit Dar 24

26 January 2018,Tido Mhando apa dhamana baada ya kukidhi masharti ya Mahakama

Mkurugenzi Mkuu wa zamani wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC), Tido Mhando amepata dhamana baada ya kukidhi masharti na kutakiwa kurejea Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Februari 23, mwaka huu.

Tido alifikishwa mahakamani hapo saa 5:22 asubuhi na aliingizwa katika ukumbi wa mahakama ya wazi kabla ya kusomewa mashtaka matano.

Leo Januari 26, mwaka 2018 wakili wa Takukuru, Leonard Swai amedai mbele ya hakimu mkazi mkuu wa makahama hiyo, Victoria Nongwa kuwa Mhando anatuhumiwa kwa mashtaka matano.

Swai amesema Juni 16, 2008 katika maeneo ya Dubai, United Arab Emirates (UAE), Tido akiwa mwajiriwa wa TBC kama Mkurugenzi Mkuu kwa makusudi alitumia madaraka yake vibaya kwa kusaini mkataba wa makubaliano kwa ajili ya kuendesha na utangazaji wa vipindi vya televisheni kati ya TBC na Channel 2 group Corporation ( BV1) bila ya kupitisha zabuni kinyume na sheria ya manunuzi na kuisababishia BVl kupata manufaa.

Shtaka la pili, Tido anadaiwa Juni 20, 2008 katika maeneo ya utekelezaji wa kazi yake alitumia madaraka vibaya kwa kusaini makubaliano (wakuu wa makubaliano) kwa utangazaji wa digital duniani kati ya TBC na BVl.

Shtaka la tatu, Agosti 11, 2008 na Septemba 2008 katika maeneo hayo, Tido anadaiwa kutumia vibaya madaraka yake kwa kusaini mkataba wa makubaliano (kuongeza wakuu wa mkataba ) kwa ununuzi, usambazaji kufunga vifaa vya usambazaji na mnara wa utangazaji kati ya TBC na BVI na kuisababishia BVI kupata faida.

Shtaka la nne, Tido anadaiwa Novemba 16,2008 akiwa Dubai, United Arab Emirates alitumia vibaya madaraka yake kwa kusini mkataba wa makubaliano (kuongeza wakuu wa mkataba ) kwa kuendesha miundombinu ya utangazaji (DTT broadcast infrastructure) kati ya TBC na BVI na kusababisha BVI kupata manufaa.

Katika shtaka la tano, Tido anadaiwa kati ya Juni 16 na Novemba 16, 2008 katika maeneo hayo ya United Arab Emirates aliisababishia hasara TBC ya Sh 887, 122,219.19.

Baada ya kusomewa mashtaka hayo, Tido ambaye anatetewa na wakili Ramadhani Maleta alikana mashtaka yote.

Swai alidai mahakamani hapo kuwa upelelezi wa kesi hiyo umekamilika.
Hakimu Nongwa alimtaka mshtakiwa kutoa fedha taslimu mahakamani hapo Sh444 milioni ama hati ya mali isiyohamishika yenye thamani ya kiasi hicho cha fedha.

Mbali na sharti hilo, pia awe na wadhamini wawili ambapo watasaini hati ya dhamana ya maneno yenye thamani ya Sh500 milioni na asitoke nje ya nchi bila ya kuwa na kibali cha mahakama.

Mshtakiwa alikamilisha masharti hayo kwa kuwasilisha hati za mali na wadhamini wawili nyakati za saa sita mchana na kuondoka.
Kesi imeahirishwa hadi Februari 23, 2018 kwa ajili ya kusomewa maelezo ya awali (PH).

Kuhusu dhamana hiyo, DPP alipeleka hati ambayo inaipa mamlaka Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuisikiliza kesi hiyo.

Mhando ni miongoni mwa waandishi wa habari na watangazaji mahiri na wakongwe ndani na nje ya nchi ambaye amewahi kufanya kazi Shirika la Utangazaji Uingereza (BBC).

Pia amewahi kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Mwananchi Communications Limited (MCL) inayochapisha magazeti ya Mwananchi, Mwanspoti na The Citizen na sasa ni Mkurugenzi Mtendaji wa Azam Media.

Thursday, January 25, 2018

25 January 2018,Aguero huenda akajiunga na Atletico Madrid

Manchester City huenda ikaingia katika makubaliano na Atletico Madrid kubadilishana mshambuliaji raia wa Argentina Sergio Aguero, mwenye umri wa 29, ili kwa upande wake imchukue Antoine Griezmann, raia wa Ufaransa mwenye umri wa miaka 26 katika msimu ujao wa joto. (Sun)

Lokomotiv Moscow imeifuata Liverpool kumtaka kumsajili winga mwenye umri wa miaka 23 Lazar Markovic. Msimu uliopita Mserbia huyo alichukuliwa kwa mkopo huko Sporting Lisbon na Hull City. (Mirror)

Chelsea imekubaliwa ombi lenye thamani ya pauni milioni 44, na marupurupu kwa msahmbuliajo wa Roma Edin Dzeko, na full beki raia wa Brazil Emerson Palmieri. (Guardian)

Kipa raia wa Uhispani wa Getafe Vicente Guaita, mwenye umri wa miaka 31, amefuzu ukaguzi wa kiafya huko Crystal Palace - lakini mazungumzo yangali yanaendelea kuhusu iwapo atajiunga na timu hiyo sasa au katika msimu wa joto. (Mail)

Brighton imewasilisha ombi la pauni milioni 6 kwa mlinzi wa Bristol City Aden Flint, aliyedhihirisha umahiri wake katika mashndano ya taji la Carabao. (Argus)

Klabu ya Ufaransa Monaco imekubali kumuuza mshambuliaji raia wa Argentina Guido Carrillo, kwa Southampton kwa pauni milioni 19.2. (Telegraph)

Sevilla imekubali makubaliano ya kumsajili mchezaji kiungo cha kati wa Swansea City Roque Mesa, mwenye umri wa miaka 28, kwa mkopo kwa muda uliosalia. (Marca - in Spanish)

25 January 2018,Wabunge kumtafuta Faru Ndugai huku Tanzania ikiwa na faru 110 kati ya faru 5000 duniani

FARU Ndugai, mnyama aliyepewa jina la Spika wa Bunge la Jamhuri ya Tanzania, Job Ndugai, ndiye hasa alikuwa kivutio kwa wabunge katika Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Ardhi, Maliasili na Mazingira waliotembelea Hifadhi mseto ya Ngorongoro, ingawa hawakufanikiwa kumuona faru huyo.

Kutomuona kwao, wabunge hao waliambulia kumuona faru mwingine maarufu kwa kuwa na umri mkubwa kuliko wote, yaaniBibi Fausta (55) ambaye kwa sasa amejengewa banda maalum ili kumhifadhi kutokana na faru Fausta kuwa hana tena nguvu za kujilinda katika kutafuta malisho ndani ya bonde kuu la Ngorongoro ambalo limesheheni maelfu ya wanyama wakali wakiwemo simba, chui, mbwa mwitu na fisi (wapatao 500) ambao ni rahisi kumshambulia mnyama yeyote mnyonge.

Faru Ndugai ambaye hivi sasa kashika nafasi ya ‘Faru John,’ kwa kuwa ndiye mnyama mkali zaidi Ngorongoro na mwenye kupenda kuzua rabsha ndani ya kreta, aliripotiwa kuwa alikuwa amekwenda ‘kutalii,’ sehemu nyingine ya hifadhi hiyo, kama ilivyo kawaida yake.

“Huwa kiusalama hatutakiwi kutaja idadi ya wanyama adimu kama Faru ambao huwindwa sana kwa pembe zao, lakini inatosha kusema kuwa kwa sasa Bonde la Ngorongoro ndilo sehemu pekee yenye faru wengi nchini Tanzania,” alisema Mhifadhi wa Ngorongoro, Dakta Fred Manongi.

Tanzania ina zaidi ya Faru 110 huku idadi ya wanyama hao waliobaki duniani kwa sasa ikiwa ni takriban Faru 5,000 tu.

Nchi za Kenya, Namibia, Zimbabwe, Afrika Kusini na Tanzania zinamiliki asilimia 98 ya faru wote weusi waliopo duniani Kuhusu Faru Ndugai, Dk Manongi alieleza kuwa mnyama huyo anayebeba jina la Spika wa Bunge, hawezi kuonekana kwa urahisi bondeni humo, maana mara nyingi ni mzururaji anayependa kuzurura huku na kule na ni mkorofi.

“Hivi karibuni Faru Ndugai aliua ng’ombe wawili alipotoka nje ya kreta,” alifafanua Dk Manongi na kuongeza kuwa, kutokana na mazingira hatarishi wanapoishi faru, wanyama hao wamejenga tabia ya kujihami na kitu chochote ambacho watakiona kuwa ni kigeni na kutishia usalama wao.

Mbunge wa Geita, Joseph Kasheku ‘Musukuma’ (CCM) na Mbunge wa Arumeru Mashariki, Joshua Nassari (Chadema) walitaka kufahamu jinsi Faru Ndugai alivyoweza kupewa jina la Spika.

Manongi alieleza kuwa kwanza Faru huyo alizaliwa wakati Spika Ndugai alikuwa mjumbe wa Bodi ya Mamlaka hiyo na pili kiongozi huyo wa Bunge ni mhifadhi wa kudumu nchini.

Hata hivyo, uongozi wa hifadhi ya Ngorongoro umetangaza kuwa utaratibu wa kuwapa majina Faru na wanyama wengine muhimu uko mbioni, kuandaliwa na mara utakapokamilika, basi kutakuwa na sherehe maalum ya uzinduzi.

Wajumbe hao wa Kamati ya Ardhi, Maliasili na Mazingira, akiwemo Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Meja Jenerali Gaudence Milanzi walitembelea Makumbusho makubwa ya Zamadam yaliyopo eneo la Olduvai Gorge ndani ya hifadhi hiyo ya Ngorongoro.

25 January 2018,LISSU- Kufanya mazoezi masaa manne kwa siku baada ya kutolewa kipande cha risasi jana mwilini mwake

Siku 35 baada ya Tundu Lissu kusema mwili wake bado una risasi moja baada ya kutolewa nyingine 15, jana mbunge huyo wa Singida Mashariki (Chadema) amelieleza gazeti moja hapa nchini kuwa madaktari wamemtoa kipande cha risasi kilichokuwa mwilini mwake.

Hata hivyo, mwanasheria huyo mkuu wa Chadema, ambaye alishambuliwa kwa zaidi ya risasi 30 akiwa ndani ya gari lililokuwa nje ya makazi yake mjini Dodoma Septemba 7 mwaka jana, alisema chuma hicho ni tofauti na risasi iliyonayo mwilini, ambayo alielezwa na madaktari wa Hospitali ya Nairobi, Kenya kuwa iko sehemu mbaya, lakini isipotolewa haiwezi kumdhuru.

“Leo (jana) madaktari wamenitoa kipande cha chuma katika sehemu ya makalio ambacho nilipokuwa Nairobi (Kenya) madaktari walikiona lakini kilikuwa ndani ya nyama wakashindwa kukitoa,” alisema Lissu kwa njia ya simu kutoka Ubelgiji ambako alipelekwa Januari 7 kwa ajili ya tiba ya mazoezi.

“Kipande hiki kilisogea na wamekitoa. Ni tofauti na ile risasi ambayo iko mwilini mwangu.”
Akieleza kiundani kuhusu hali yake, Lissu alisema anaendelea vizuri.

“Huu mkono wa kushoto ambao ulikuwa na tatizo, wameunyoosha na kuufanyia mazoezi kweli kweli na huu mguu wa kulia ambao ndio wenye tatizo, unaendelea vyema,” alisema.

“Huku ni mazoezi tu. Kwa siku nafanya mazoezi kwa saa nne, Naingia saa 3:00 asubuhi hadi saa 4:00 asubuhi, narudi tena saa 5:00 asubuhi hadi saa 6:00 mchana. Mwisho naingia mazoezini saa 8:00 mchana hadi saa 10:00 jioni. Hiyo ndiyo ratiba yangu kwa siku.”

Alisema katika mazoezi hayo anatumia magongo maalumu pamoja na kiti cha magurudumu.

“Mfano, huu mguu wa kulia natakiwa kuukanyagia kwa kilo 20 hadi 25 katika mzani na mimi nina kama kilo 90. Ninapoukanyagia ninaulizwa kama unauma, ikiwa sijasikia maumivu ina maana sijafanya kitu, kwa hiyo ni kazi kwelikweli,” alisema.

Kuhusu muda ambao anatakiwa kufanya mazoezi hayo mpaka atakaporejea katika hali yake ya kawaida, Lissu alisema bado hajajua.
“Ah bwana we, hapa madaktari wamegoma kunieleza hilo, lakini wameangalia katika maungio ya goti la mguu wa kulia kuna mfupa haujaunga vizuri, ni lini utaunga hilo sijajua,” alisema.

Mara baada ya kushambuliwa kwa risasi na watu ambao hadi sasa hawajajulikana, Lissu alipelekwa Hospitali ya Rufaa ya Dodoma kwa matibabu ya awali kabla ya kuhamishiwa Hospitali ya Nairobi nchini Kenya siku hiyo usiku.

Desemba 21 mwaka jana wakati akihojiwa na kituo cha televisheni cha Azam, Lissu alisema madaktari wa Nairobi walimueleza kuwa risasi iliyokuwa imesalia mwili haina madhara.

Alisema risasi saba zilitolewa na madaktari hao, jambo lililomaanisha kuwa risasi nyingine nane, zilitolewa na madaktari wa Tanzania, saa chache baada ya kushambuliwa alipofikishwa Hospitali ya Mkoa wa Dodoma.

Wednesday, January 24, 2018

24 January 2018,Jamii ya waislam wa Rohingya washambuliwa kwa kuchomewa makazi yao kwa moto

Jamii ya waislamu kutomka Myanmar Rohingya yaendelea kushambuliwa  kwa mjumba yao kuchomwa moto.
 Kumekuwa na kauli tofauti kuhusu hali halisi Rakhine kuwa wakimbizi wa jamii ya Rohingya wapo katika harakati za kurejea katika makaazi yao.
Jambo la kushangaza ni kuona kuwa majumba ya waislamu wa jamii ya Rohingya  Rakhine yanachomwa moto.
Jamii ya Rohingya ilikimbilia nchini Bangladesh kutokana na  mashambulizi ya wabuddha wakishirikina na jeshi la serikali.
Taarifa zinahakikisha kuwa mashambulizi dhidi ya Rohingya bado yanaendelea.
Zaidi ya watu 690 000 kutoka jamii ya Rohingya  walikÅŸmbilia nchini Bangladesh kunusuru maisha yao.

24 January 2018,Jamii ya waislamu wa Myanmar Rohingya waendelea kupata adha baada ya kushambuliwa makazi yao kwa kuchomwa moto

Jamii ya waislamu kutomka Myanmar Rohingya yaendelea kushambuliwa  kwa mjumba yao kuchomwa moto.
 Kumekuwa na kauli tofauti kuhusu hali halisi Rakhine kuwa wakimbizi wa jamii ya Rohingya wapo katika harakati za kurejea katika makaazi yao.
Jambo la kushangaza ni kuona kuwa majumba ya waislamu wa jamii ya Rohingya  Rakhine yanachomwa moto.
Jamii ya Rohingya ilikimbilia nchini Bangladesh kutokana na  mashambulizi ya wabuddha wakishirikina na jeshi la serikali.
Taarifa zinahakikisha kuwa mashambulizi dhidi ya Rohingya bado yanaendelea.
Zaidi ya watu 690 000 kutoka jamii ya Rohingya  walikÅŸmbilia nchini Bangladesh kunusuru maisha yao

24 January 2018,Wanafunzi wasiopungua 229 wa shule ya Msingi Mitambo Wilayami Mtwara wanasoma wakiwa chini ya miti

Wanafunzi 229 wa Shule ya Msingi Mitambo wilayani Mtwara wanasoma wakiwa chini ya miti kutokana na uhaba wa madarasa matano.

Wanafunzi wanaosoma wakiwa chini ya miti ni wa darasa la tatu, nne, tano na sita.

Akizungumza na MCL Digital, mwalimu mkuu wa shule hiyo, Rashidi Chalilo amesema wanafunzi hao ni kati ya 436 wa shule hiyo.

Chalilo amesema wanafunzi wa darasa la kwanza na la pili kutokana na kuhitaji uangalizi zaidi wanasoma darasani pamoja na wa darasa la saba wanaojiandaa kwa mitihani.

Amesema shule hiyo ilianzishwa mwaka 2009 ikiwa na wanafunzi 99 na sasa wapo 436 ikiwa na madarasa matatu pekee.

Mwalimu mkuu huyo amesema wazazi walijenga madarasa ya muda kwa kutumia miti na udongo na kuyaezeka kwa nyasi lakini baadaye yalibomolewa kwa maelekezo ya Halmashauri ya Wilaya ya Mtwara ili kupisha ujenzi wa madarasa ya kudumu.

Akizungumzia suala hilo, kaimu ofisa mtendaji wa Kijiji cha Mitambo, Ally Mselemu amesema wanasubiri kupelekewa saruji na vifaa vingine vya ujenzi.

“Wananchi tuko tayari kujitolea nguvu kazi kuboresha shule yetu, hivyo tunaiomba Serikali ituletee vifaa,” amesema Mselemu.

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mtwara, Omari Kipanga amesema wameshatenga fedha kwa ajili ya ujenzi wa madarasa matatu pamoja na nyumba ya mwalimu.

Amesema Sh156 milioni zimetengwa kutoka katika mfuko wa elimu ambazo zinatokana na mapato ya korosho.

Kipanga amesema mfuko wa P4R pia umeidhinisha Sh326 milioni kwa ajili ya kuboresha sekta ya elimu katika halmashauri hiyo.

Tuesday, January 23, 2018

23 January 2018,Kiongozi wa waasi Sudan Kusini aitaji barua kutoka Kenya ili atoe amri ya kuwaachia marubani wawili wa Kenya waliotekwa

Waasi wa Sudan Kusini wanawashikilia mateka marubani wawili wa ndege kutoka Kenya na wanasema hawatawaachilia huru hadi pale watakapotoa fidia kwa familia ya raia aliyeuawa wakati ndege yao ilipoanguka wakati wa kutua.
Ndege hiyo ilianguka katika mji wa Akobo, katika eneo la Greater Upper Nile, zaidi ya wiki mbili zilizopita, amesema Lam Paul Gabriel naibu msemaji wa waasi.
Ameongeza kuwa, wakati ndege hiyo ilipoanguka ikikaribia kutua, ilimuaa  mwanamke na mifugo kadhaa. Amesema jamaa wa mwanamke huyo na wenye mifugo wanataka walipwe fidia.
Msemaji wa waasi hao amesema, viongozi wa Kenya wanapaswa kumwandikia barua Riek Machar, kiongozi wa waasi ili atoe amri ya kuwaachili huru marubani hao.
Machar, makamu wa zamani wa Rais wa Sudan Kusini, ni kiongozi wa mrengo mkubwa zaidi wa waasi Sudan Kusini na amekuwa akiishi uhamishoni Afrika Kusini tokea mwaka 2016.
Msemaji wa Jeshi la Sudan Kusini, Brigedia Jenerali Lul Ruai Koang amethibitisha kushikiliwa mateka marubaini hao wawili Wakenya.
Sudan Kusini ilitumbukia katika vita vya ndani Disemba 2013 baada ya Rais Salva Kiir kutoka kabila la Dinka kumtuhumu makamu wake wa zamani, Riek Machar wa kabila la Nuer kwamba alihusika na jaribio la kuipindua serikali yake.

23 January 2018,Simba ,yanga kukaguliwa leseni na CAF

Shirikisho la soka Barani Afrika CAF litafanya ukaguzi wa mfumo wa leseni kwa vilabu (Club Licencing) kwenye upande wa miundo mbinu.
CAF watafanya ukaguzi huo wa kutembelea na kutazama miundo mbinu ili kuhakikisha mfumo huo unatekelezeka ipasavyo kwa kuanzia na mtazamo wa vigezo vya miundo mbinu.
Wakati wa miaka kadhaa ya kuzindua mfumo huo wa leseni kwa vilabu ni wazi changamoto kubwa kwenye Bara la Africa imekuwa ni vigezo vya miundo mbinu ambayo kwenye baadhi ya viwanja vinavyotumika wakati wa mashindano imekuwa ikitoa taswira isiyo nzuri kwa mashindano ya CAF.

Kwa mwaka huu 2018 wameandaa ukaguzi kutembelea klabu zote zitakazoshiriki hatua ya makundi kwenye mashindano ya vilabu ya CAF wakijielekeza kwenye kiwango na ubora wa viwanja vya kucheza mechi na viwanja walivyochagua kwa mazoezi.
CAF watachagua kundi la wakaguzi watakaotembelea kwenye klabu za kila mwanachama wake ili kukusanya ripoti itakayowasilishwa na moja kati ya ripoti hiyo ni miundo mbinu ya Uwanja,ripoti itakayothibitisha kama uwanja umefikia kwenye mahitaji ya juu ya kutumika kwa mechi za CAF.
Viwanja ambavyo havitakidhi mahitaji hayo ya juu hautaidhinishwa kutumika kwa mashindano na hautatumika kwa mchezo wowote wa hatua hiyo ya makundi kwa mashindano ya klabu kwa mwaka huu 2018.



23 January 2018,Kesi ya Sugu mawakili wataka ushahidi wa sauti uliopatikana usikilizwe

Kesi inayomkabili Mbunge wa Mbeya Mjini (CHADEMA) Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ na Katibu wa Kanda ya Nyassa, Emmanuel Masonga imeahirishwa baada ya kutokea mabishano makali ya Kisheria Mahakamani kutokana na ushahidi uliotolewa
Uamuzi wa kuahirisha kesi hiyo umetolewa na Hakimu Mkazi wa Mkoa wa Mbeya, Michael Mteite baada ya shahidi namba tano Afande Joramu Magova ambaye ni Mkuu wa Kitengo cha Tehama katika Ofisi ya Upelelezi ya Mkoa kutoa ushahidi wake na kumtaka Hakimu kusikiliza sauti zilizokuwa zimehifadhiwa kwenye kinasa sauti.
Aidha, baada ya kutoa kinasa sauti, kulitokea mabishano ya kisheria baina ya Mawakili wa Jamhuri na wa upande wa utetezi ambapo upande wa Jamhuri walikuwa wanataka sauti zisikilizwe na upande wa utetezi ukipinga.
Kutokana na hali hiyo Hakimu Mkazi wa Mkoa wa Mbeya, Michael Mteite ameahirisha kesi hiyo mpaka siku ya kesho ambapo atatoa uamuzi wa juu ya hilo kama utasikilizwa ushahidi huo wa sauti mbele ya Mahakama au la.
Hata hivyo, Mbunge huyo na Katibu wa CHADEMA Kanda ya Nyassa wanashikiliwa na jeshi la polisi kwa tuhuma za kuzungumza maneno ya uchochezi na yenye kuleta chuki kati ya Serikali na wananchi.





Monday, January 22, 2018

22 January 2018,Watu wasiopungua wawili wafariki,watatu kujeruhiwa kwa ajali ya gari Jijini Mwanza

Watu wawili wamefariki dunia na wengine watatu wamejeruhiwa katika ajali ya gari baada ya basi dogo la abiria kampuni ya Mkombozi kugongana uso kwa uso na basi la kampuni ya Walawi katika eneo la Kamanga jijini Mwanza.

Kamanda wa polisi mkoa wa Mwanza kamishna msaidizi Mwandamizi wa Polisi Ahmed Msangi amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kusema kuwa dereva wa basi la Mkombozi pamoja na abiria mwingine wamepoteza maisha hapo hapo.

"Ni kweli imetokea ajali hiyo na kusababisha vifo vya watu wawili akiwepo dereva la basi dogo la kampuni ya Mkombozi ambaye alifariki hapo hapo baada ya ajali pamoja na abiria mwingine, lakini pia wapo majeruhi watatu ambao wamepelekwa kwa matibabu zaidi" 

Jeshi la polisi linaendelea kufanya uchunguzi kujua chanzo za ajali hiyo 

22 January 2018,Waziri Mkuu -Wahakikishe wanatokomeza uvuvi haramu katika ziwa Victoria

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amemuagiza Mkuu wa Mkoa wa Mara, Adam Malima kwa kushirikiana na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya mkoa wahakikisha wanatokomeza uvuvi haramu katika ziwa Victoria.

Ametoa agizo hilo wakati akizungumza na viongozi wa mkoa huo katika kikao cha majumuisho ya ziara yake ya kikazi mkoani Mara.

“Kuna tatizo kubwa la uvuvi haramu katika Ziwa Viktoria. fanyeni doria za mara kwa mara na watakaobainika hatua stahiki za kisheria zichukuliwe dhidi yao.”amesema Majaliwa

Amesema viongozi hao wanatakiwa wahakikishe wanatokomeza uvuvi haramu haraka iwezekanavyo na pia wasimamie ulinzi wa rasilimali za ziwa Victoria ili ziweze kuwanufaisha wananchi wa mkoa huo na Taifa kwa ujumla.

Aidha, amesema kuwa baadhi ya wavuvi wamekua wakivua kwa kutumia nyavu zilizopigwa marufuku, kokoro pamoja na mabomu jambo ambalo haliwezi kuvumilika kwa sababu zana hizo zinaharibu uhai wa viumbe hai ndani ya ziwa Victoria.

Hata hivyo, amesema kuwa ni vema mkoa huo ukaanzisha operesheni za mara kwa mara katika ziwa Victoria kwa lengo la kuwasaka watu wote wanaojihusisha na vitendo vya uvuvi haramu na kuwachukulia hatua kali za kisheria kwa wote watakaokamatwa.

22 January 2018,Scorpion ahukumiwa kifungo cha miaka saba jela na kulipa fidia ya shilingi milioni 30

Mahakama ya Wilaya ya Ilala leo Jumatatu Januari 22, 2018 imemhukumu Salum Njwete maarufu kama ‘Scorpion’ kifungo cha miaka saba jela na kulipa fidia ya Sh30 milioni itakayotakiwa kulipwa kwa haraka.

Akisoma hukumu hiyo, Hakimu Mkazi Flora Haule amesema ameridhishwa na ushahidi uliotolewa na upande wa mashtaka, hivyo amemtia hatiani mshtakiwa chini ya kanuni ya adhabu kifungu cha 225 kama kilivyofanyiwa marekebisho mwaka 2007

Haule amesema kutokana na ushahidi uliotolewa, mahakama imejiridhisha kumtia hatiani Njwete kwa kosa la kujeruhi pamoja na wizi.

Baada ya hakimu kumaliza kupitia hoja za pande zote mbili, wakili wa Serikali Frank Tawali aliomba mahakama itoe adhabu stahiki kwa kuwa Njwete alimtoboa macho, Saidi Mrisho ambaye alikuwa akitegemewa na familia yake na Taifa.

Wakili wa mshtakiwa, Hussein Hitu aliiomba mahakama kumpunguzia mteja wake adhabu kwa kuwa ameshakaa rumande kwa muda mrefu, lakini pia ana familia inayomtegemea.

Njwete (35) alikuwa akituhumiwa kufanya unyang’anyi wa kutumia silaha na kujeruhi ikiwemo kumtoboa macho Mrisho.

Sunday, January 21, 2018

21 January 2018,Arsenal na Man United toka ni toke

Mchezaji wa kiungo cha kati wa timu ya Manchester United Henrikh Mkhitaryan amekubali kujiunga na timu ya Arsenal, huku Alexis Sanchez akitarajiwa kuhama upande wa pili.

Mkhitaryan, mwenye umri wa miaka 28,ambaye ni raia wa Armeniaatafanyia ukaguzi wa kimatibabu Leo Jumapili au kesho Jumatatu, huku Sanchez mwenye umri wa miaka 29 raia wa Chile atafanyiwa ukaguzi leo Juampili.

Muda wa mkataba wa Mkhitaryan na kitita atakachopokea kama mashahara hakijulikani.
Arsene Wenger awali alisema Sanchez atajiunga na United iwapo tu Mkhitaryan atahamia Arsenal.

Sanchez alikosa ushindi wa Arsenal wa mabao 4-1 dhidi ya Crystal Palace Jumamosi kwasababu alikuwa anasafiri kwenda Manchester.

"Huwezi kusafiri kwenda kaskazini na ucheze soka kwa wakati mmoja," alisema Wenger.

Mkufunzi wa United Jose Mourinho, wakatihuo huo amesema mkataba wa kumsajili Sanchez unakaribia kukamilika kufuatia ushindi wa timu yake wa bao 1-0 dhidi Burnley Jumamosi.

Timu hiyo ya Mashetano wekundu iliipiku Arsenal kumsajili Mkhitaryan kutoka Borussia Dortmund mnamo July 2016 kwa kima cha £ milioni 26.3.

Sanchez, amefunga mabao 80 katika mechi 166 za mashindano yote akiichezea Arsenal tangu kusajiliwa kutoka Barcelona mnamo July 2014 kwa £ milioni 35.

Raia huyo wa Chile ambaye mkataba wake na Arsenal ulitarajiwa kumalizika msimu wa joto mwaka huu alitarajiwa kusajiliwa Manchester City mwaka jana.
Imeabinika wiki hii kwamba City iliamua kutomsajili tena.

21 January 2018,Kiwanda cha Saruji cha Dangonte chapewa siku 14 kuingia mkataba na wachimbaji wadogo wa Gypsum

Naibu Waziri wa Madini, Doto Biteko ametoa siku 14 kwa uongozi wa kiwanda cha saruji cha Dangonte mkoa wa Mtwara kuingia mkataba na wachimbaji wadogo wa gypsum.

Biteko ametoa kauli hiyo leo Januari 21, 2018 baada ya kutembelea kiwanda hicho na kuzungumza na viongozi wake.

Amesema mikataba hiyo inapaswa kuwa na kipengele cha kuwalipa ndani ya siku 30 baada ya kiwanda kukusanya gypsum kutoka kwa wachimbaji hao, lengo likiwa ni kuleta ufanisi na tija katika biashara zao.

“Nimekubaliana hapa kamishna wa kanda atasimamia hili la mikataba kati ya kiwanda na wachimbaji wa gypsum. Sehemu ya malipo itakuwa ndani ya mkataba na watalipa ndani ya siku 30,” amesema.

Amesema wachimbaji hao wamekuwa wakilalamikia kucheleweshewa malipo yao baada ya kupeleka kiwandani bidhaa zao.
“Nimeambiwa wachimbaji hawa walikuwa wanalipwa baada ya miezi mitatu lakini kwa mkataba huu ambao wataingia na kiwanda sasa watakuwa wanalipwa ndani ya siku 30,” amesema Biteko.

Amesema Serikali ya Awamu ya Tano inalenga kuwasaidia wachimbaji wadogo sambamba na wawekezaji ambao wanapaswa kufanya kazi bila kusumbuliwa.

“Uwepo wa kiwanda hiki unawasaidia wachimbaji wetu waweze kupata bei nzuri pamoja na kupata soko la uhakika la kuuza bidhaa zao. Dangonte wameniahidi kwamba ndani ya muda mfupi watatekeleza agizo hili,” amesema.

Biteko amesema lengo la ziara yake ni kuwasaidia wachimbaji wa gypsum ambao hawana mikataba na kujikuta wakibanwa katika uuzaji wa bidhaa zao.

Saturday, January 20, 2018

20 January 2018,Tanzania,Kenya karibuni kudhibiti homa ya Chikungunya inaoenezwa na mbu aina ya Aedes isiokuwa na tiba wala kinga

Serikali Kenya na Tanzania ziko mbioni kudhibiti ugonjwa wa Homa ya Chikungunya ambao huambukizwa na mbu aina ya aedes na hauna tiba mahsusi wala kinga.

Nchini Kenya, harakati bado zinaendelea kudhibiti mlipuko wa homa ya Chikungunya katika mji wa pwani wa Mombasa ambako hadi sasa watu 27 kati ya 154 waliofanyiwa uchunguzi wamethibitishwa kuambukizwa ugonjwa huo.

Shirika la Afya duniani, WHO nchini humo linashirikiana na serikali kudhibiti mlipuko wa ugonjwa huo unaoenezwa na mbu ambao umekumba vitongoji vyote sita vya Mombasa ambavyo ni Mvita, Kisauni, Nyali, Changamwe, Jomvu na Likoni.

Nchini Tanzania Waziri wa Afya Ummy Ally Mwalimu ametoa tahadhari kwa umma kuhusu uwezekano wa kuenea homa hiyo ya Chikungunya baada ya kuibuka katika nchi jirani ya Kenya.

Dalili za ugonjwa huo ni pamoja na homa kali na maumivu ya viungo, misuli, kichefuchefu na uchovu.
Ripoti za awali kabisa za kuwepo ugonjwa huo wa Chikungunya zilipatikana katikati ya mwezi uliopita ambapo kilichofuatia kilikuwa ni kukusanya sampuli za damu na kuziwasilisha kwenye maabara kwa ajili ya uchunguzi.

Ugonjwa wa Chikungunya unaweza kupunguzwa kwa kuchukua hatua kadhaa kukiwemo kuhakikisha mazingira ni masafi ili kuepusha mazalia ya mbu.

20 January 2018,Tetesi za soka Ulaya michezoni leo Jumamosi

Kocha wa zamani wa Barcelona Luis Enrique ameorodheshwa miongoni mwa makocha wanaotarajiwa kumrithi Mkufunzi wa Chelsea Anonio Conte mwishoni mwa msimu huu huku aliyekuwa beki wa Cheslea Juliano Belletti akiwa mkurugenzi wa kandanda. (Star)

Na mkufunzi wa Manchester City Pep Guardiola anasakwa na klabu ya Paris St-Germain. (Mirror)

Tottenham inatarajiwa kuishinda Arsenal katika kumsajili mchezaji wa Brazil na Bordeaux mwenye umri wa miaka 20 Malcom. (Telegraph)

Huenda mkataba haujaafikiwa lakini Mkufunzi wa Manchester Pep Guardiola ameipongeza Manchester United kwa kumsajili mshambuliaji wa Arsenal na Chile Alexis Sanchez, 29. (Talksport)

Manchester City ilijiondoa katika harakati za kutaka kumsajili Alexis Sanchez kutoka Arsenal huku wakihofia kwamba hatua hiyo itaathiri vibaya udhabiti wa kifedha wa klabu hiyo.(Times - subscription required)

Kiungo wa kati wa Armenia Henrikh Mkhitaryan aliwaaga wachezaji wenzake wa Manchester United baada ya fursa ya mwisho ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28-ya kufanya mazoezi na wenzake kabla ya uhamisho wake wa kuelekea Arsenal. (Mail)

Alexis Sanchez huenda akaichezea Arsenal dhidi ya Crystal Palace siku ya Jumamosi baada ya kurudi katika mazoezi siku ya Ijumaa baada ya kufanya mazoezi na timu ya vijana.. (Mirror)

Lakini inadaiwa kulikuwa na maafikiano ya mkataba huo baadaye siku ya Ijumaa ambayo yalimlazimu Alexis Sanchez kuwaaga wachezaji wenzake wa Arsenal na kuondoka katika hoteli ya timu hiyo huku Gunners wakijiandaa kukabiliana na Crystal Palace. (Express)

Mkufunzi wa Newcastle Rafael Benitez amekataa kuhakiki hatma yake katika klabu ya Newcastle United huku akisubiri klabu hiyo kuwasajili wachezaji watatu au wanne katika kikosi chake wakati wa dirisha la uhamisho la mwezi Januari. (Guardian)

Liverpool walikuwa wanajiandaa kumnunua kipa wa Stoke Jack Butland kwa dau la £40m lakini wameambiwa kwamba mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24 hauzwi (Express)

Aliyekuwa mshambuliaji wa Manchester United Javier Hernandez hatorudi katika klabu hiyo huku Besiktas ikimnyatia kwa dau la £7.5m (8.5m euro) (Goal)

Norwich inakaribia kukamilisha usajili wa mchezaji wa klabu ya Eintracht Braunschweig's Onel Hernandez, 24. (Sun)

Everton inamtaka beki wa klabu ya Lille Adama Soumaoro, 25, lakini bado hawajawasilisha ombi la kumsajili mchezaji huyo.(Liverpool Echo)

Beki wa Rangers raia wa Ureno Bruno Alves, 36, anasakwa na klabu ya Itali Benevento. (Sky Italia - in Italian)

Mkufunzi wa Southampton Mauricio Pellegrino amesema kuwa klabu hiyo ilifanya kila kitu ili kujaribu kumnunua aliyekuwa mshambuliaji wa Arsenal Theo Walcott kabla ya mchezaji hyo kuelekea Everton (Southampton Echo)

Bournemouth ina fuaraha ya kumuuza mshambuliaji Benik Afobe mwezi huu lakini inataka kupata £10m walizolipa kwa Wolves kumsajili mchezaji huyo 24 miaka miwili iliopita . (Sun)

Crystal Palace imewasilisha ombi la kumsajili mshambuliaji wa Inter Milan na Itali Eder ,31, kwa dau la £9.75m . (Corriere dello Sport, via Croydon Advertiser)

20 January 2018,CCM yapambana na kofia za ubaguzi Manispaa ya Moshi

Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Humphrey Polepole amewataka viongozi wa chama hicho Manispaa ya Moshi, kuacha kutembea na watu mifukoni na kutengeneza kofia za ubaguzi ndani ya chama kwa kuwa hali hiyo imekuwa ikikigharimu chama wakati wa uchaguzi.

Polepole amesema chama hicho kimekuwa kikijikuta katika wakati mgumu wakati wa uchaguzi kutokana na baadhi ya viongozi ndani ya chama kupenda ubinafsi na kuweka mbele uheshimiwa badala ya utumishi.

Ametoa rai hiyo leo Jumamosi wakati akizungumza kwenye kikao cha ndani cha Halmashauri Kuu ya CCM Manispaa ya Moshi kilichofanyika mjini Moshi katika ukumbi ulioko kwenye ofisi za chama hicho mkoa ambapo amesema sasa ni wakati wa kujiimarisha ili kuweza kushika hatamu kila ngazi.

Amesema kumekuwepo na baadhi ya viongozi ndani ya chama ambao wamekuwa wakitengeneza makundi ya walionacho na wasio nacho wakati wa uchaguzi hali ambayo imekuwa ikikifanya chama kushindwa kila mwaka wa uchaguzi katika majimbo mbalimbali likiwemo jimbo la Moshi Mjini.

"Kushindwa kwa CCM katika majimbo mengi Kilimanjaro hasa hili la Moshi Mjini, kulisababishwa na viongozi, kutembea na majina yao mifukoni na kuweka uheshimiwa mbele badala ya utumishi, hali hii ilijenga makundi, sasa ni lazima tubadilike," amesema Polepole

20 January 2018,Kamati ya maadili ya viongozi yawataka Wabunge kuwasilisha taarifa za miamala ya Benki ndani ya siku 30

Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma imewaandikia barua baadhi ya wabunge, ikiwataka kuwasilisha taarifa za miamala ya benki za kuanzia Januari hadi Desemba 2017.

Sekretarieti hiyo imetaka taarifa hizo ziwe zimeifikia ndani ya siku 30 kuanzia Januari 15, 2018.

Barua iliyotumwa kwa mmoja wa wabunge na gazeti hili kuiona, inawataka wabunge hao wametakiwa kutekeleza agizo hilo ili kuthibitisha taarifa zilizomo kwenye tamko lake la alilowasilisha.

Ofisa mmoja wa taasisi hiyo ambaye hakutaka jina lake litajwe gazetini, alithibitisha kuwepo kwa barua hizo, akisema si wote walioandikiwa barua za kutakiwa kutoa taarifa hizo.

Hata hivyo, alisema wabunge walioandikiwa ni wale ambao fomu zao zinaonyesha haja ya uhakiki zaidi wa taarifa zao.

Rais wa John Pombe Magufuli ndiye alikuwa wa kwanza kuwasilisha fomu yake ya tamko kuhusu rasilimali na madeni katika ofisi ya Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma iliyopo Mtaa wa Ohio, Wilaya ya Ilala Jijini Dar es Salaam Desemba 28, 2017.

Baada ya kuwasilisha fomu hiyo, Rais aliipongeza sekretarieti hiyo kwa kazi inazofanya na kumtaka Kamishna wa Maadili Jaji Mstaafu, Harold Nsekela kutopokea fomu ya kiongozi yeyote ambaye angeshindwa kuwasilisha tamko la kabla ya Desemba31, 2017.

Kauli hiyo ya Rais iliwaamsha viongozi mbalimbali wakiwemo wabunge na viongozi wengine wa Serikali kufurika kwenye ofisi hiyo kuwasilisha matamko yao ya mali walizonazo.