Watu zaidi ya 40 waripotiwa kufariki na wengine zaidi ya 100 kujeruhiwa katika mlipuko wa bomu uliotokea mjini Kabul nchini Afghanistan.
Bomu lililokuwa limetengwa katika gari la wagonjwa lililipuka na kusababisha maafa hayo Jumamosi mjini Kabul nchini Afghanistan.
Wanamgambo wa kundi la Taliban wamefahamisha kuhusika na shambulizi hilo.
Taarifa kutoka katika wizara ya afya zinafahamisha kuwa idadi ya watu waliofariki katika mlipuko huo itaongezeka kutokana na hali ya majeruhi.
No comments:
Post a Comment