Mashabiki wa Arsenal ulimwenguni walikua na hamu ya kufahamu atakayoyasema Wenger Kabla ya mechi, Wenger amesema: "Nilijaribu kujitolea kwa miaka mingi sana, kuwafanya watu wengi wafurahi na natumai kwamba watu wanaopenda klabu hii wataendelea kufurahi siku zijazo na kupata matamanio yao na wanayoyapenda.
"Nimekutana na watu ambao kwao mimi ndiye meneja pekee wa Arsenal wanayemfahamu, kwa hivyo sasa ni fursa nzuri kwa klabu kuwa na watu wapya na mawazo mapya ya kuendelea kusongeza mbele klabu, jambo ambalo ndilo nimejaribu kulifanya maisha yangu yote."
"Arsenal imekuwa klabu ambayo hufanikiwa kuunganisha utamaduni na kupiga hatua. Nilipofika hapa changamtoo kuu ilikuwa kupigisha hatua klabu na kuheshimu utamaduni. Nilipotua, Liverpool na Man United silikuwa ndizo klabu bora zaidi, na zilikuwa na wachezaji wazuri sana. Na hiyo ndiyo changamoto niliyokumbana nayo."
No comments:
Post a Comment