Monday, May 7, 2018

SERIKALI YAPUNGUZA UTEGEMEZI

  Serikali imeamua kupunguza utegemezi wa Bajeti kutoka kwa wahisani kutoka nje kwa mwaka wa fedha 2018/2019 ili kuepuka adha ya kukwama kwa miradi iliyokuwa ikikwama  2017/2018

Waziri wa Maji na Umwagiliaji Isack Kamwelwe amewasilisha bajeti kwa mwaka ujao wa fedha bungeni Mjini Dodoma iliyopunguza utegemezi wa fedha za maendeleo ya sekta ya maji nchini. kutok kwa wahisani. 
Fedha za Maendeleo ya Sekta ya Maji kwa mwaka wa fedha wa 2018/2019 zimetengwa shilingi zaidi ya Bilioni 670, ambapo asilimia 66 ya fedha hizo zitakuwa fedha za ndani na asilimia 34 zitakuwa fedha za wahisani. 
Pamoja na Makadirio ya Matumizi ya fedha za maendeleo kutegemea fedha za ndani zaidi, kilio cha wabunge ni kucheleweshwa kwa utekelezaji wa miradi ya maji na wakandarasi wasio waaminifu.
Wabunge wamesema ni mara ya kwanza serikali kutenga fedha za miradi ya maendeleo ya sekta ya maji inayotegemea fedha za ndani kwa kiasi kikubwa jambo ambalo linaleta matumaini ya maendeleo kaika sekta hiyo.

No comments: