Sunday, May 20, 2018

URUSI,CHINA WAITETEA IRAN

Wanadiplomasia wa Ulaya, Urusi na China watajadili makubaliano mapya ya kuipa Iran msaada wa kifedha, ili ipunguze mpango wake wa makombora na kuingilia katika masuala ya nchi jirani katika ukanda wa Mashariki ya Kati.

Kwa mujibu wa Gazeti  Welt am Sonntag nchini Ujerumani  majadiliano hayo yananuia kuyanusuru makubaliano kuhusu mpango wa nyuklia wa Iran yaliyosainiwa mwaka 2015, ambayo Marekani imeyapa kisogo.

Pia mkutano wa wanadiplomasia hao utafanyika wiki ijayo mjini Vienna, ukiongozwa na mwanadiplomasia wa Umoja wa Ulaya Helga Schmid. Ujerumani, Ufaransa, Uingereza, Urusi na China ambazo pamoja na Marekani ziliyasaini makubaliano hayo na Iran zitashiriki katika mkutano huo, lakini haijafahamika iwapo Iran itakuwa na mwakilishi.

Wanadiplomasia hao wanaamini kuwa kujumuisha makombora ya Iran na uingiliaji wake katika masuala ya kikanda, kutamshawishi Rais Donald Trump kuirejesha Marekani katika makubaliano hayo.

No comments: