Wizara ya afya nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo idadi ya watu walioambukizwa Ebola kufikia 43 Kaskazini Magharibi mwa nchi hiyo Mbandaka.
Hadi sasa watu 17 wamepoteza maisha katika janga hili la hivi punde.
Kwa upande wake Shirika la afya duniani WHO limesema maambukizi haya bado sio tishio la Kimataifa na jitihada zinafanyika kuudhibiti.
WHO baada ya kukutana na mamlaka ya dharura ya afya imesisitiza kuwa hali ya mlipuko huo haijakidhi vigezo vya kutangazwa hali ya dharura nchini DRC.
Taarifa hiyo iliongeza kuwa serikali ya Kidemokrasia ya Congo, WHO na washirika wamekuwa na mwitiko wa haraka na wa kina kufuatia hali hiyo.
Serikali ya Kinshasa ilitangaza kuzuka kwa virusi vya ebola katika jimbo la kaskazini magharibi Equateur mnamo Mei 8
No comments:
Post a Comment