Balozi wa Tanzania nchini Sweden Dkt. Wilbroad Slaa amesema kuwa udhaifu wa mfumo uliopo wa upitishaji wa bajeti nisababu ya mjadala wa kuonekana au kutoonekana kwa sh1.5 tilioni lililoibuka baada ya kuwasilishwa kwa Ripoti ya Mdhibiti ,Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG)
Dkt. Slaa amefafanua kuwa wabunge wamekuwa wakipitisha bajeti kabla ya fungu halisi kupatikana, ikiwa ni nadharia inayosubiri fungu hilo kupatikana kupitia kwa wafadhili au michakato mingine ya ukusanyaji.
“Kama fedha nyingi zinatumika bila kupitishwa na Bunge kwa sababu ndiyo mfumo wetu, unawezaje kuhoji fedha hizo zilitumikaje?” Dkt. Slaa anakaririwa na Mwananchi waliofanya naye mahojiano maalum.
Aliongeza kuwa kwa kawaida, huwezi kupata takwimu halisi za miradi mikubwa ya Serikali ndani ya kipindi cha mwaka wa fedha husika kwani miradi hiyo huwa katika hatua za utekelezaji.
No comments:
Post a Comment