Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Simon Sirro amesema vituo vitatu vikubwa vya polisi vilivyojengwa kwa ushirikiano uliopo kati ya jeshi la polisi na wananchi katika mapambano dhidi ya uhalifu vitazinduliwa jijini Dar es Salaam Alhamisi Mei 24 mwaka huu .
Sirro amesema Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa ndiye anatarajiwa kufungua vituo hivyo.
Pia amewaomba wananchi kujitokeza kwa wingi katika uzinduzi huo ambao utaanzia katika kituo cha Polisi Mburahati majira ya saa mbili asubuhi na kufuatiwa na kituo cha Kiluvya na mwisho kituo cha polisi Mbweni.
Uzinduzi huo utapambwa na michezo na burudani mbalimbali hivyo amewataka wananchi wa maeneo hayo na maeneo jirani kujitokeza kwa wingi
No comments:
Post a Comment