Tuesday, May 22, 2018

PALESTINA YALIA NA ICC

Waziri wa mambo ya nje wa Palestina Riyad al Maliki amewasilisha ombi katika mahakama ya kimataifa inayoshughulikia kesi za uhalifu ya ICC ya kuitaka mahakama hiyo kuchungunza vitendo vya ukiukaji wa haki za binadamu vinavyohusishwa na sera za Israel za kuikalia kwa nguvu ardhi ya Wapalestina. 

Ombi hilo linakwenda mbali zaidi ya ombi la waendesha mashitaka la mwaka 2015 la kuchunguza madai ya uhalifu katika eneo hilo kati ya Israel na Palestina na hivyo huenda mchakato huo wa kisheria ukaharakisha kuanzishwa kwa uchunguzi kamili.
 Palestina imesema inataka mahakama hiyo ya ICC kuanzisha uchunguzi mara moja dhidi ya Israel.

No comments: