Wednesday, May 16, 2018

MSAADA WA KIBINAADAM WAHITAJIKA SUDAN

Umoja wa Mataifa unatenga zaidi ya   dola bilioni  1 kwa msaada wa kibinadamu nchini Sudan.


Umoja huo umesema idadi ya watu walioathirika nchini  humo huongezeka kutoka milioni 5.5 hadi milioni 7.1 mwaka huu.

Mkurugenzi wa kibinadamu wa Umoja wa Mataifa, Mark Lowcock, ameihimiza  jumuiya ya kimataifa kuharakisha msaada wake.

"Ninahimiza jumuiya ya kimataifa kuendeleza usaidizi kwa mahitaji ya kibinadamu ya watu milioni 7.1 walioathirika na kuwekeza katika maendeleo ya kijamii na kiuchumi," alisema afisa wa Umoja wa Mataifa.

No comments: