Mwanamuziki wa muziki wa kizazi kipya nchini Ali Saleh Kiba (
Alikiba) ameonyesha kujali na kuthamini lugha ya kiswahili kupitia kazi zake za
sana ya muziki.
Kiba amebainisha haya hivi punde alipokuwa akizungumza na
waandishi wa habari “Lugha
yetu ni nzuri lazima tujivunie, najivunia sana kuwa mswahili na kuongea
Kiswahili na kutumia kiswahil katika kazi yangu ya kunipatia maisha, kwahiyo
kila mtanzania ni lazima ajivunie kuwa mswahili, asikwambie mtu acha uswahili,
ni lazima ujivunie sio sifa mbaya” amesema kiba
Pia amesema kwamba hata akiwa anafanya matamasha
nje ya nchi idadi kubwa ya watu wamekuwa
wakitamani kufundishwa lugha ya kiswahili.
No comments:
Post a Comment