Thursday, May 10, 2018

EBORA KUINGIA KIGOMA

Kuna uwezekano mkubwa kwa ugonjwa wa Ebola kuingia Tanzania kupitia mikoa ya mpakani mwa Ziwa Tanganyika baada ya ugonjwa huo kuingia nchini jirani ya jamhuri ya kidemokrasi ya Congo hivi karibuni ambako umesababisha vifo vya watu wasipoungua 17. 

 Serikali imesema hakuna mtu yeyote  aliyeripotiwa kuugua ugonjwa huo hapa nchini, lakini uwezekano upo kwa wananchi  kuambukizwa ugonjwa huo  kutokana na muingiliano wa watu kati ya Congo na Tanzania ambao umekuwepo kwa miaka mingi.
Waziri wa Afya na Maendeleo ya Jamii,Jinsia ,Wazee na Watoto Ummy Mwalimu amesema hayo jijini Dodoma wakati akizungumza na waandishi wa habari,  ambapo amesema mikoa ambayo iko hatarini zaidi kupata maabukizi ya Ebola ni KIgoma, Rukwa na Katavi ambayo ipo mpakani mwa Ziwa Tanganika linalozitenga Congo na Tanzania.
Waziri Ummy amewataka watanzania kuwa katika tahadhari ambapo amezitaja njia ambazo zinaweza kusababisha mtu kuambukizwa Ebola kuwa ni kugusa damu au maji maji yoyote kutoka kwa mtu aliyeambukizwa ugonjwa huo na kugusa maiti ya mtu aliyekufa kwa ugonjwa huo. Njia nyingine ni kugusa baadhi ya wanyama hususan Sokwe na Swala wa msituni wenye virusi vya ugonjwa huo.

No comments: