Tuesday, May 1, 2018

1 MAY 2018,POLISI UGANDA WAKAMATA KUNDI JIPYA LA KIGAIDI

Jeshi la Polisi nchini Uganda limenasa kundi jingine la kigaidi linalojihusisha kutoa mafunzo kwa watoto chini ya miaka 18  katika mtaa wa kisenye kati kati mwa Kampala


polisi wameharifu kuwa  katika oparesheni  hio wameuwa  washukiwa wawili na wengine thelathini na sita kutiwa nguvuni

Kundi hilo  linalohusishwa kuwa na uhusiano na kundi ABF lililopo katika misitu ya Kongo limeweka kambi  kwenye msikiti wa soko liitwalo  usafi 

wananchi waliokataa kuanika majina yao kutokana na kuhofia usalama wameharifu kuwa  polisi  wamekuwa wakipuuzia  malalamiko yao 

mwanamke mmoja  Rahma Natumbwe ameleza kuwa mumewe Senunu  Abubakar alipotea zaidi ya miezi minne  hadi polisi ilipohujumu kambi hio ya magaidi

kwa miaka miwili sasa vitendo vya kuteka watu nyara  wa aina mbali mbali vimekithiri mjini Kampla Uganda  ambapo mateka wanateswa na kuuwawa  



No comments: