Tuesday, April 17, 2018

17 APRIL 2018, MOURINHO AMFUNGULIA MILANGO PAUL POGBA

Mkufunzi wa Manchester United Jose Mourinho yuko tayari kumwacha kiungo wa kati aliyenunuliwa kwa kitita cha £89m Paul Pogba, 25, kuondoka klabu hiyo pamoja na mshambuliaji Anthony Martial, 22, beki wa Uholanzi Daley Blind, 28, huku beki wa Itali Matteo Darmian akitarajiwa kuuzwa. (Mail)
Darmian, 28, anasema kuwa atafanya uamuzi kuhusu ombi la uhamisho wake kutoka klabu ya Seria A Juventus mara moja. (Express)




Manchester City itampatia meneja Pep Guardiola kitita cha £200m za uhamisho baada ya kushinda taji la ligi , huku kiungo wa kati wa Napoli na Italy Jorginho, 26, pamoja na kiungo wa kati wa Shakhtar Donetsk ,24, raia wa Brazil Fred wakilengwa. (Mirror)

No comments: