Watu watano akiwemo mwanamke Mganga wa Jadi wilayani misungwi katika Mkoa wa Mwanza, wamefikishwa mahakamani leo kwa tuhuma ya kuua kwa kukata mapanga wazee wawili.
Mwendesha Mashtaka wa Polisi Ramsoney Sarehe akiwasomea hati ya mashitaka na kuwataka kutojibu lolote kwakuwa Mahakama hiyo ya wilayani haina mamlaka ya kusikiliza kesi hiyo mpaka Mahakama kuu.
Sarehe alisoma hati ya mashtaka April 16 (Leo) kuwa Simon Malonja (56) maarufu kwa jina la Mbuke Mkazi wa Kitongoji cha Ibongoya Kijiji 'A' Kata ya Kolomije, Kamuli Budodi (38) Mkazi wa Kijiji cha Kamyerere Kata ya Kanyerere,Charles Kasuluzu (34) Mkazi wa Kijiji cha Ibomgoya'A' Kata ya Kolomije na Kabula Nchali ambaye ni Mganga wa Jadi Mkazi wa Ibongoya'A'.
Alisema kuwa huko katika Kitongoji cha Sangila Kijiji cha Ibongoya 'A' usiku wa manane Julai 23, Mwaka 2016 kwa pamoja walivamia nyumba ya Marry Maduka (60) na kuvunja mlango kisha kumkata na kitu chenye ncha Kali na kuuawa hapo hapo, na watuhumiwa wote walikimbia na kuanza kukamatwa mmoja mmoja .
Sarehe akiwasomea shtaka jingine wote hao watano alisema kuwa huko kijiji cha kitongoji cha Nzunya Kijiji cha Ibongoya'A' Kata ya Kolomije Majira ya usiku wa saa mbili Desemba 19, Mwaka 2016 watuhumiwa wote kwa pamoja walimvamia Leticia Mlongo (67) akiwa nje na kumuua kwa kumkata kichwani na kitu chenye ncha kali kisha kutokwa na damu nyingi zilizopelekea kifo chake, watuhumiwa wote walitoweka na kukamatwa April 10 mwaka huu.
Hakimu Mkuu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya wilayani Misungwi, Russy Mkisi alisema kuwa Mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza kesi hiyo na hawapaswi kujibu lolote hadi Mahakama Kuu na kesi hiyo itaendelea kutajwa tena Mei 12, Mwaka huu na watuhumiwa wote watakwenda rumande kwa kuwa kesi hiyo haina dhamana.
No comments:
Post a Comment