Tuesday, April 17, 2018

17 APRIL 2018,MAFURIKO YAUWA SABA DAR

Watu saba  wamekufa kwa kusombwa na maji kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha katika maendeleo mbalimbali ya jiji la Dar es Salaam.
Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda amethibitisha kutokea kwa vifo hivyo na kutoa rai kwa wakazi wa jiji hilo hususan wanaoishi maeneo hatarishi kuhama ili kuepusha madhara zaidi.
Kamishna Operesheni wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Billy Mwakatage, ametembelea maeneo mbalimbali yaliyoathirika na mafuriko jijini Dar es Salaam na kujionea hali ilivyo, na kuwataka wakazi wa eneo la Vingunguti wachukue tahadhari kwa kuyahama maeneo hayo mapema kabla hawajapata madhara zaidi.
Katika ziara hiyo Kamishna Mwakatage aliwataka wananchi kutoa taarifa mapema pindi wanapoona viashiria vyovyote vya mafuriko au mtu kuzingirwa na maji kwa kupiga simu namba 114.

No comments: