Hasan Özcan mwanafunzi aliyekuwa na umri wa miaka 19 ameuawa kwa kuchomwa kisu na watu wasiojulikana nchini Uingereza.
Mwanafunzi huyo wa Kiituruki amechomwa kisu na kuuawa karibu na nyumbani kwao.
Wazazi wake wamesema kuwa hapo awali pia mtoto wao aliwahi kushambuliwa kwa kuchomwa kisu lakini washatakiwa waliachiwa kutokana na kutokuwa na ushahidi wa kutosha.
Tukio hilo limetokea katika wilaya ya Barking majira ya saa nne za usiku.
Uchunguzi unaendelea kufanyika.
No comments:
Post a Comment