Saturday, February 3, 2018

3 February 2018,Tottenham kumuuza Harry Kane Real Madrid

Tottenham imejiandaa kumuuza mshambuliaji wa Uingereza Harry Kane 24 kwa Real Madrid iwapo timu hiyo hataipatia presha na kwamba watalipwa dau la £176m. (Mundo Deportivo - in Spanish)

Mkufunzi wa zamani wa Everton na Southampton Ronald Koeman atatangazwa kuwa kocha mpya wa Uholanzi Ijumaa ijayo. Koeman mwnye umri wa miaka 54 amekuwa bila kazi tangu alipofutwa kazi na Everton mnamo mwezi Oktoba. (De Telegraaf - in Dutch)

Mkufunzi wa Manchester United Jose Mourinho atamuuza kipa wa Uhispania David De Gea, 27, kwa Real Madrid iwapo kiungo wa kati wa Wales Gareth Bale, 28, atakubali kujiunga na Manchester United (Daily Express via Diario Gol)

De Gea ni mmoja wa walinda lango wanne wanaosakwa na Real Madrid. Kipa wa Chelsea 25, raia wa Ubelgiji Thibaut Courtois, yule wa Atletico Madrid na Slovenia Jan Oblak, 25, na kipa wa AC Milan 18, na Italy Gianluigi Donnarumma wanaonekana kuwa mbadala wa David De Gea. (Goal.com)

No comments: