Friday, December 1, 2017

1 December 2017,Serikali jitihada zifanyike ili kupunguza maambukizi ya virusi vya ukimwi kwa vijana

Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan ametaka jitihada zifanyike kupunguza maambukizi ya virusi vya ukimwi kwa vijana.

Akizungumza katika maadhimisho ya siku ya ukimwi duniani ambayo kitaifa yamefanyika mkoani Dar es salaam, Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan amesema inasikitisha kuona idadi ya waathirika wengi wa maambukizi ya virusi vya ukimwi ni wasichana wadogo.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Tume ya Kudhibiti Ukimwi Tanzania (TACAIDS), Dkt. Leonard Maboko amesema japo maambukizi yanapungua bado kuna changamoto kwa vijana

Sambamba na maadhimisho hayo yenye kauli mbiu Changia Mfuko wa Udhamini wa ukimwi okoa maisha, makamu wa Rais amezindua taarifa za maambukizi ya ukimwi ambapo mikoa ya Njombe na Iringa ina idadi kubwa ya maambukizi.

No comments: