Kwa mujibu wa shirika la haari la Anadolu, jumanne, baraza kuu la maimam nchini Ivory Coast(COSIM) limelaana unyama unaofanyiwa jamii ya Rohingyas nchini Myanmar.
Katika ujumbe wake, COSİM imesema kuwa ni baraza linalohamasisha amani na utu kama inavyofundisha Qur'ani takatifu, na ikatolea wito mataifa makubwa, umoja wa mataifa, na nchi za kiislam ili kushinikiza Myanmar ikomeshe haraka unyanyasaji, na mauaji yanaofanyiwa jamii ya waislam wa Myanmar ya Rohinga.
Tangu Agosti 25, jamii ya Rohingyas imejikuta katika hali ngumu tangu jeshi la Myanmar lianze kufanya mauaji ya kimbari dhidi ya Waislamu wa rohinga huko Rakhine, kusini magharibi mwa Myanmar.
Tangu wakati, rohinga zaidi 501,000 wamelazimika kuacha makazi yao katika jimbo la Rakhine, na kukimbilia Bangladesh.
No comments:
Post a Comment