Tuesday, October 3, 2017

3 October 2017,BUGANDO yakabiliwa na uhaba wa vifaa vya matibabu na wataalamu wa Afya

Hospitali ya Rufaa ya Bugando mkoani Mwanza inakabiliwa na uhaba wa wataalam pamoja na vifaa tiba vya maradhi ya moyo na hivyo kuzorotesha utoaji wa huduma ya upasuaji wa moyo.

Mkuu wa idara ya upasuaji wa moyo na vifua kwenye hospitali hiyo Prof. William Mahalu amesema kuwa changamoto hizo zimechangia utoaji wa tiba ya maradhi ya moyo katika hospitali ya bugando kufanyika kwa kusuasua.

Akihitimisha kilele cha maadhimisho ya siku ya moyo duniani,mkuu wa wilaya nyamagana Mary Tesha amesema kuwa serikali ya awamu ya tano imejipanga kuimarisha tiba ya moyo nchini ikiwemo kwenye hospitali ya bugando.

Asilimia 50 ya watoto mia saba waliojitokeza kwenye hospitali ya rufaa ya bugando kwa ajili ya kupima maradhi ya moyo kati ya januari na septemba mwaka huu wamegundulika kuwa na maradhi hayo.

No comments: