Waziri wa viwanda biashara na uwekekezaji Charles Mwijage amewataka Wakuu wa Mikoa na Wilaya kote nchini kupitia upya beiza viwanja ili kuwavutia wawekezaji kupata viwanja hivyo kwa gharama nafuu.
Waziri Mwijage ametoa kaulihiyo mjini Dodoma mara baada ya kuzindua kiwanda cha kutengeneza mabati kilichojengwa na kampuniya mabatiya ALAF.
Pia amewataka watanzania kulinda viwanda nchini kwa kununua na kutumia bidhaa zake ili viweze kuhimili ushindani wa soko.
Kwa upande wake Meneja mkuu wa kiwanda cha ALAFGreyson Mwakasege ametoa wito kwa watanzania kujenga tabia ya kuthamini bidhaa zinazozalishwa na viwanda vya ndaniili kuwaungamkono wawekezaji.
No comments:
Post a Comment